Simulizi: Mtoto wa Baba Paroko

Simulizi: Mtoto wa Baba Paroko

Zipo story nyingi sana nimesoma tena zingine zikiwa na subtittle " based on true story" lakini hii ina uhalisia mwingi sana. Ukiondoa kashfa za mapadre ambazo sio wote wanafanya hivyo.lakini kikubwa ni lugha mchanganyiko iliyotumika na weledi mkubwa wa mambo kutoka kwa mwandishi ambayo kiukweli yapo. Hii story haistahili kusomwa bure hata kidogo. We need to pay for it whatever!! Asante sana mwandishi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu usiamshe hisia... Wengine hatuwezi nunua
 
Mkuu The Legend nimeona nikusaidie...
Shukran sana mkuu Ibney pamoja na mkuu mbududa Mmefanya la maana sana kuiendeleza kwa faida ya wakuu wanaoifuatilia. Kuna mambo ambayo kimsingi yalikua nje ya uwezo wangu, yaliyofanya 'nipotee' for a while. I apologize kwa wote waliokwazika kwa namna moja au nyingine

the Legend☆
 
Zipo story nyingi sana nimesoma tena zingine zikiwa na subtittle " based on true story" lakini hii ina uhalisia mwingi sana. Ukiondoa kashfa za mapadre ambazo sio wote wanafanya hivyo.lakini kikubwa ni lugha mchanganyiko iliyotumika na weledi mkubwa wa mambo kutoka kwa mwandishi ambayo kiukweli yapo. Hii story haistahili kusomwa bure hata kidogo. We need to pay for it whatever!! Asante sana mwandishi

Sent using Jamii Forums mobile app
Upo sahihi mkuu mwandishi atakua ni moja ya watu waliopitia elimu hiyo.. hata ubruda labda..
But kwann anaficha jina lake? Nimejaribu kutafuta jina lake silipati.
Niko tayariii kuilipia hii simulizi. Iko poa sna

Sent from my GT-I9300 using Tapatalk
 
Mtunzi

Lello Mmassy
+255 717 947 818
 
Jamaa anatisha sana. ..yaani anaongelea masuala ya ndani kabisa yanayo tokea RC ...tena yakiwa na undani mkubwa tu nahisi jamaa atakuwa ni padree huyu
 
Mtoto wa Baba Paroko : SEHEMU YA KUMI

Eric Afanikiwa Kusafini Kwenda Finland

“Eric, nimepokea barua kutoka Baraza la Maaskofu inayonielekeza kunisimamishwa ukuu wa Seminari na kuwa watachagua Padri mwingine mapema mwezi ujao. Ni katika hali hiyo basi nahitajika kuanza kujiandaa kuondoka na kurudi Songea.

Barua imeeleza wazi kuwa ni kwasababu ya kukaidi agizo la askofu Kengele la kukupeleka Tanga na kumdanganya kuwa umeshaondoka kumbe bado upo hapa, amezipata taarifa” Padri Mapunda alikuwa akimweleza Eric katika hali ya masikitiko makubwa.

“Padri, mbona nashindwa kuelewa? Kwa hiyo wewe sio Mkuu wa seminari tena? Na sababu ni mimi?”, Eric aliuliza huku ametoa macho.

“Ndiyo. Unajua mimi kiumri ni mtu mzima sasa na nilibaki hapa kwa sababu ya ujuzi wangu wa malezi lakini kimsingi miaka hii 65 niliyo nayo ilifaa niwe nimeanza kupumzika. Umri wa kuwa Mkuu wa seminari hizi hushauri kuwa ni kati ya miaka 45 mpaka 60. Huo ni umri mzuri kwa Mkuu wa seminari kupambana na vijana anaowakuza katika utawa lakini pia kuwapa malezi. Mimi nimeshapita umri huo.

Lakini pia nadhani taarifa zimemfikia Askofu Kengele juu ya mimi kusema umeshaelekea Tanga wakati upo hapa. Hii ni hatua ya kwanza tu nadhani nikishafika Songea nitakabiliwa na shitaka la kusema uongo. Uongo ni kosa kubwa katika utawa, nadhani tulishawafundisha hili, siyo?” Padri Mapunda alimalizia kwa swali.

“Ni kweli, lakini wamejuaje kama nipo hapa?”, Eric alihoji.

“Eric, don’t be naive. Huwezi kuficha siri za mambo kama haya. Kinachotakiwa hapa ni wewe kumtaarifu mama kuwa unelekea Dar es Salaam. Ukifika fuatilia hati ya kusafiria pale Idara ya Uhamiaji. Nitamwambia Padri Dominique atuandikie barua haraka ya wewe kuelekea Finland kumalizia masomo kule ili tuitumie kuombea VISA.

Kisha utaondoka, mimi itakuwa nimemaliza jukumu langu mwanangu.” Padri Mapunda alimalizia kwa kumwita Eric mwanangu. Alianza kujisahau, mapenzi ya ubaba yalianza kuzidi ya utawa.

“Sawa padri mimi kesho nitaanza safari. Asante sana”, Eric aliongea akionyesha uchungu ila hakuwa na la kufanya upadri aliutaka sana.

Padri Mapunda katika hali ya huzuni kubwa aliingiza mkono kwenye kabati lake la meza na kutoa kitita cha pesa shilingi milioni nne na kumkabidhi Eric. Alimweleza kuwa aende muda huo akaziweke benki na kuwa hizo ndizo pesa anazoweza kumsaidia kwa wakati ule kwa ajili ya safari yake.

Alimwambia yeye ataendelea kupambana na padri Dominique ahakikishe anafika Finland na baada ya hapo Padri Dominique kule atajua namna ya kumwingiza kwenye huduma za bure kama waseminari wengine wanaolipiwa na shirika la Waselesiani wa Don Bosco.

Eric na Padri Mapunda walikumbatiana.

“Go and be a nice priest” (Nenda ukawe mtawa mwema), Padri Mapunda alimsihi kijana wake.

“Sawa Padri. Sitarudia tena ukaidi”, Eric alijibu huku akitoa machozi.

Eric alielewa fika amemsababishia Padri Mapunda kusimamishwa ukuu wa Seminari bila ridhaa yake tena bila heshima wakati amelitumikia kanisa kwa miaka mingi bila kashfa yoyote. Mpaka wakati huo Eric hakujua kama anaongea na baba yake mzazi. Aliondoka.

Padri Mapunda alivuta pumzi nzito. Alitafakari kile wazungu wanaita ‘next move’. Aliamua kumpigia simu Padri Dominique kumuuliza amefikia wapi na suala lao maana ni siku ya tatu toka wameliongea.

“Father Domique, Praise be to Jesus Christ” (Padri Dominique, Tumsifu Yesu Kristu), Padri Mapunda alisalimia.

“Forever Amen Boniface”(Milele amina Boniface), Padri Dominique alijibu.

“Where are we with the matter. Things need to happen more quickly”(Tumefikia wapi juu ya lile suala?. Hili jambo lafaa lifanyike kwa uharaka) Padri Mapunda alihoji.

“Father Boniface, you know exactly that things in our systems do not work like that. You understand that what you asked me is against Church’s principles of good conduct and yet you are looking forward to fast tracking, how is that possible? There is a lot of people I need to consult to assist, to corrupt the procedure in place so that we can register Eric’s name without being noticed. Give sometimes Boniface”

(Padri Boniface unajua kabisa kuwa mambo kwenye utaratibu wetu hayaendi hivyo unavyotamani. Unaelewa kuwa hili jambo tunalotaka kulifanya sio halali na bado unanilazimisha lifanyike kwa uharaka, inawezekanaje sasa? Kuna watu wengi natakiwa niwasiliane nao, mifumo mingi ya kuiingilia ili tukiliingiza jina la Eric lisigundulike. Nipe muda wa kutosha Boniface), Padri Dominique alionekana kuongea kwa kuzuia hasira yake.

“I understand all that, Eric needs to move from Tanzania as soon as possible. So what I need right now is to asssist him by issuing a reception letter that he will join your Seminary for further studies. Eric will then fly to Finland, you may ask a nearby parish to receive him as an exchange program student while waiting for other procedures to be completed. What about that?

(Naelewa lakini Eric anapaswa kuondoka Tanzania haraka iwezekanavyo. Ninachohitaji usaidie ni wewe utusaidie kuandika barua ya kukubali kuja chuoni kwako kuendelea na masomo, Eric atakuja Finland na wewe utaangalia utaratibu wa kuomba Parokia iliyopo karibu impokee kama mwanafunzi aliekuja kubadilishana uwezo wakati akisubiri wewe umalizie taratibu za kumpokea rasmi hapo seminarini kwako. Unaonaje?, Padri Mapunda alishauri.

“I understand Boniface, but what if it does’nt work out? Will he fly back to Tanzania?” (Nimekuelewa Boniface lakini ipi kama nikishindwa kumwandikisha hapa seminarini? Je, atarudi Tanzania?”, Padri Dominique alihoji.

“We shall cross every bridge when we reach there. For now just do what we have agreed” (Tutalivuka kila daraja pindi tunapolifikia. Kwa sasa fanya haya tunayokubaliana) Padri Mapunda alimjibu Dominique. Walimaliza maongezi.

Padri Mapunda alidhamiria kuhakikisha Eric anafika Ufini na kuendelea na msomo yake ya seminari iwe kwa njia halali ama zisizo halali.
********************************

Eric alimpigia simu mama yake. Alimweleza kila kilichotokea kwa Padri Mapunda. MariClara, mamaye Eric alisikitika sana, hakika aliumia lakini hakuwa na la kufanya. Alimwambia Eric kuwa wakati mwingine ipo gharama katika kila jambo, kila mtu hulipa gharama kwa namna yake.

Alimweleza kuwa yeye mama yake alishalipa gharama juu yake Eric na sasa ni zamu ya Padri Mapunda kulipa gharama yake. Eric alishindwa kuelewa kwanini mama yake anatoa kauli za namna ile lakini pia alishindwa kuuliza, aliamua kubaki kimya. Walikubaliana kuwa ndani ya siku tatu angeshakuwa amefika Dar es Salaam tayari kuanza michakato ya hati ya kusafiria na kusubiria barua ya kuombea VISA.
******************************

Baada ya siku tatu ni kweli Eric alikuwa jijini Dar es Salaam ofisi za Uhamiaji, Kurasini akifuatilia hati ya kusafiria. Kwasababu yeye alijitambulisha kama mwanafunzi wa seminari na kuwa safari yake ni ya kimasomo huko Ufini na kwa kuwa kanisa Katoliki lina heshima yake nchini alisaidiwa kwa haraka.

Ndani ya siku tatu tayari alishaipata hati yake na hakika alipigiwa simu na padri Mapunda kumweleza tayari ameshamtumia barua zote zinazohitajika kuombea VISA kwa njia ya barua pepe.

Haraka Eric alianza mchakato wa kufatilia VISA ya kuelekea nchini Ufini. Kama ilivyokuwa kwa hati ya kusafiria haikumsumbua kupata VISA. Aliipata na alikuwa tayari kusafiri. Mambo yalikwenda kwa kasi sana.
***********************************

Ilikuwa ni siku ya huzuni sana iliyochanganyika na furaha, Eric alikuwa akiagana na mama yake MariaClara katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Kambarage Nyerere akielekea Ufini ambapo angetua katika uwanja wa kimataifa wa ndege wa jiji la Helsinki.

Eric alikuwa akisafiri na ndege za KLM kutokea shirika la ndege la Royal Dutch. Ilikuwa siku ya Ijumaa na kutokana na muda anaoondoka angewasili Ufini siku ya Jumamosi.

Kutokana na mipangilio ya Padri Mapunda na Padri Dominique, Eric alikuwa akashukie Parokia ya Bikira Maria iliyopo karibu na chuo Kikuu Helsinki (Helsinki University). Parokia hii ipo umbali wa kama kilometa mbili kutoka eneo la chuo, Kitivo cha Sheria.

Ni moja ya Parokia kongwe ambayo ilianzishwa mwaka 1856. Parokia hii pia huendeshwa na shirika la waselisiani wa Don Bosco hivyo Paroko wake ni rafiki mkubwa wa Padri Dominique.
Safari ya Eric ilikuwa ya salama.
********************************

“Praise be to Jesus Christ Father”, (Tumsifu Yesu Kristu Padri). Eric alimsalimia Padri Thomas Kemphus, Paroko wa Parokia ya Bikira Maria alipokuwa akiwasili parokiani.

“Forever Amen Eric, welcome to Helsinki”. (Milele amina Eric, karibu sana Helsinki), Padri Tom alimjibu Eric huku akimkumbatia.

“Here we go Tom, your new son in Christ”.(Tom mpokee mtoto wako mpya katika Kristu), Padri Dominique alieambatana na Eric alimjibu padri Tom.

“It is my pleasure Dominique. Immediately, tomorrow we shall start with him in the first mass”. (Ni furaha yangu Dominique. Haraka sana kuanzia kesho tutaanza nae ibada ya kwanza), Padri Tom alijibu huku akimpigapiga Eric mgongoni.

Padri Tom alikuwa ni mzee kidogo tena aliyependa kufuga ndefu nyingi. Alikuwa ni mcheshi mwenye kutabasamu wakati wote katika majukumu yake na watu wengine. Akiwa na Padri Domonique na Eric alikuwa akijitahidi kuwamiminia wine pale varanda walipokaa. Walijitokea mapadri wengine wawili na kuungana nao, hakika palijaa furaha.

Baada ya kukaa na kujadili mawili matatu padri Dominique aliaga ili arudi seminarini na kumwacha Eric na mapadri wa parokia ile wakiendelea na mazungumzo. Eric alikuwa ni muongeaji kidogo, aliwapa taarifa nyingi kuhusu Tanzania na jinsi kanisa linavyozidi kukua na kuimarika.

Padri Tom naye hakusita kumpa uhalisia wa kanisa la Finland. Alimwambia namna watu wanavyoikacha imani kwa kasi tofauti na miaka yake akiwa kijana mdogo. Alimweleza kuwa wana changamoto kubwa kwa sasa kwani wengi sasa wanaiacha imani yao ya zamani kabisa ambayo ni ukristo na kugeuka kuwa watu wasioamini chochote (Atheists).

Alimweleza pia kuwa masuala ya imani yamebaki kama ya sherehe (Ceremonial) na sio tena mambo ya kuogofya. Ibada hujaa wazee pekee na watu wenye asili ya Afrika ambao ni wageni waliopo kule kwa ajili ya kufanya kazi kwenye mashirika ya kimataifa au waliopo masomoni.

Padri Tom alimweleza Eric kuwa hakika umefika wakati Afrika itume watu kwenda kufufua imani bara la ulaya kama wao walivyokuja Afrika miaka iliyopita. Alimwambia kuwa kesho yake siku ya Jumapili wakati wa ibada basi atathibitisha hayo aliyomwambia kwani atajionea mahudhurio kwa macho yake. Hakika mazungumzo yalikuwa marefu siku ile na yaliyokuwa na mada nyingi mtambuka. Eric alifurahia kufika Finland.
*****************************

Ilikuwa siku ya Jumapili, siku moja tangu Eric awasili Finland alihudhuria ibada katika Parokia ile aliyofikia ya Bikira Maria pale Helsinki. Eric akiwa ameambatana na padri Tom walikuwa wakiingia kuanza ibada. Eric alishindwa kuamini idadi ya watu aliyoishuhudia pale kanisani.

Kanisa lile lilikuwa kubwa sana tena lenye nakshi nzuri. Lilijaa vito vya dhahabu, sanamu za kuvutia na taa nyingi. Jengo lake lilinyanyuka juu sana na kulikuwa na piano ambayo kwa hakika Eric hakuwahi kushuhudia mfano wake toka azaliwe. Tena kwa nyuma kulikuwa na kama ghorofa ambapo ndipo eneo la kwaya. Ilikuwa limetengenzwa vile ili kwaya inapoimba sauti zinatokea kwa juu kuja chini na kuwa kama malaika.

Kwa kutumia mtindo wa uimbaji wa kanisa katoliki ambao wao huuita ‘Gregorian chant’ sauti za kwaya huweza kusikika katika hali ya kuvutia ajabu. Eric alikuwa akiingia ibadani huku akishangaa uzuri wa kanisa lile na idadi ndogo ya watu anayoishuhudia.

Alishindwa kuelewa inakuwaje kwa uzuri wote ule watu waache kuja kanisani hata kushangaa tu. Hakujua ukizoea jambo unaliona la kawaida. Eric alikuwa akitembea huku akishuhudia mabenchi kuwa matupu ama kuwa na wazee wachache wa kizungu. Watu wenusi aliwaona ila walikuwa wachache pia. Eric na padri Tom walifika madhabahuni tayari kuanza ibada. Ibada iliendeshwa kwa lugha ya Kingereza.

“The Lord be with you all” (Bwana awe nanyi nyote), Padri Tom alianza ibada kwa mtindo wa kuimba.

“And with your spirit” (Awe rohoni mwako), Waumini wote walijibu.

Wakati waumini wakijibu Eric aliyekuwa amesimama pembeni ya Padri Tom alibaki mdomo wazi. Hakuamini alichokuwa anakishuhudia mbele yake, alitoa macho kama mtu aliyekuwa amegandishwa. Moyo wake ulijihisi kusimama kwa sekunde kadhaa, alishtuka.

Alikuwa akiingia msichana mrembo, alifika mlango wa kanisa na kuvua miwani yake iliyoonekana ya urembo. Alivaa kigauni kifupi kilichokuwa juu ya magoti na hivyo kufanya miguu yake milaini na minene kidogo kuonekana kwa uzuri. Msichana yule alichovya maji ya baraka yaliyokuwa mlangoni na kisha kuanza kujongea kuelekea kwenye dawati alilotaka kukaa.

Ajabu msichana yule nae alipoangalia vizuri waliosimama madhabahuni ghafla macho yake yaligongana na ya Eric. Alionekana na yeye kutoamini anachokitazama, alibaki ameduwaa.

Eric alijiridhisha kuwa anaemshuhudia mbele yale ni Lucia, Lucia nae alijihakikishia kuwa anaetazamana nae si mwingine bali ni Eric. Wote kwa pamoja walipandisha mikono yao na kujiziba midomo kwa mshangao.
******************************
Tumefikia Mwisho Wa Msimu Wa Kwanza Wa Simulizi Hii. Msimu Wa Pili Utaanza Mwezi Wa Machi.

the Legend☆
 
Kwa faida ya wengine huyu Lello Mmassy mtunzi wa hii simulizi ndo mtunzi pia wa ile simulizi ya 'The President and I' ambayo kuna mkuu ameileta pia huku jf

the Legend☆
Msimu wa kwanza umeisha, kitu hadi March........
 
Lucia again
 
Back
Top Bottom