Hakuna kuchoka humuSEHEMU INAYOFUATA..........
Jambo ambalo lilikwamisha mpango wa Mimi na ESTA kuhusu biashara ya saloon,ni baada ya madam kusafiri kwa muda wa wiki nzima huku akiniahidi akirudi mipango itakuwa kama kawaida.
Matukio ya kununiana bila sababu ndani ya nyumba, mashtaka mbalimbali yalijitokeza ila ilikuwa ni kama kawaida tu kwakuwa wanawake ndivyo walivyo,
Kuna siku nikiwa ofisini nilipokea taarifa ya watu kuumizana Kati ya Dada yangu wa tumbo moja na ESTA , wakipigana kwa sababu zisizoelezeka huku mke wangu akiwa upande wa ndugu yangu.
Nilifikiria kuhusu ESTA, nikagundua wamepanga kumuhamisha kwa nguvu, lakini madam si atarudi siku si nyingi? nilijiuliza
Nikarudi nyumbani,nakumbuka dada yangu na mke wangu walichachamaa huku wote wakidai,Bora wote
Wote tuondoke mkoani ili wewe ukae na ESTA
Mtu gani Kila tukimwambia hatumtaki anang'ang'ania tu , mtoe nakwambia muondoe huyo malaya wako, alizungumza mke wangu,
Huku nikimtazama nikikumbuka urafiki wao wa siku ya kwanza namna walivyokuwa wanakaribishana.
Wakati hayo yakiendelea ESTA alikuwa kashika mkoba mdogo wa kike mkononi huku akiwa na begi dogo la mgongoni,
Leta begi hilo, la kwako ? Yaani mchana kweupe unaniibia,
Ni maneno toka kwa dada yangu wa tumbo moja ambaye alishindwa kuwa na hekima ni kwasababu tu yalifanana, ESTA akarudisha like begi ndani akachukua la kwake,
Muda huu anaenda wapi huyu ,lazima nisimame kama mwanaume huku nikihakikisha , Kila mmoja namdhibiti , sikuwa na maneno na dada yangu, jicho nililomwangalia lilitosha kumfanya akimbilie chumbani kwake , huku nikitoa ukali na msimamo wenye kutaka Kila mmoja aingie ndani si ESTA Wala na nani , niliingia chumbani huku mke wangu akiwa Hana hata neno la kuniambia ikabidi atoke aingie kwenye chumba Chake anacholala na mtoto kwa kipindi hicho.
Nakumbuka nililala bila kula, saa kumi alfajiri niliamka nikajiandaa fresh, Kisha nikawaamsha wote,
Nikasema yafuatayo,
Hii nyumba kiongozi ni nani? Niliuliza
Wote wakajibu ni wewe.
Sasa kuanzia Leo naomba ESTA tafuta pa kwenda sitaki migogoro na malumbano yasiyo ya lazima ndani kwangu, lakini pia wewe mke wangu na dada yangu naomba mniandalie majibu mazuri ni kwanini mmekosa heshima na adabu kwa Sasa, au kwakuwa mama kaondoka ?
Nawapa kutwa nzima Kila mmoja awe na majibu, niliongea huku nikionesha sura ambayo hakuna aliyenijibu,
Sasa shemeji namimi nikupe jibu gani maana Mimi sijui chochote, aliongeza dada wa kazi akijitetea
Wewe haupo naongea na Hawa, nikainuka kuwahi kazini kwangu, kama kawaida shughuli ziliendelea huku uzoefu ukiongezeka, kiasi Cha baadhi ya wafanyakazi kuwa wanajiuliza vitu vingi kwangu ilinipa heshima kubwa kwenye kampuni.
Kama kawaida Kuna mdada ana kiherehere sana pale ofisini, aliingia huku akiwa na taarifa mpya, ambayo kwangu ilinistua,
Mr Daniel, Kuna tetesi nazisikia kuwa yule mke mdogo wa boss atakuja kampuni hii, na hapa tunapoongea yupo South Africa kwa mumewe . Ambako yametokea mabadiliko kwamba mtoto wa boss hatahusika Tena hapa Bali atashughulikia habari zake za ufuatiliaji wa mizigo toka nchi za nje na kuiingiza humu,
Ni kazi ambayo alikuwa nayo zamani kabla hajapandishwa cheo, Sasa sijui yule mwanamke akija hapa itakuwaje maana ni ana majungu sijapata kuona Tena ni mchawi sana yule yaani huwa simpendi basi tu.
Japokuwa haijawekwa wazi kuwa hapa atakuwa nani,
Alimalizia yule dada.
Haina shida Mimi naona Mimi na wewe haituhusu kwasababu atakuja kukaa kwenye nafasi yake na sisi tutampa heshima anayostahili,
Nilijibu kwa kujikaza.
Niliwaza sana kama yule atakuja pale ofisini kwetu maana kiukweli ni mtu mzuri mkiwasiliana mkiwa mbalimbali lakini hayuko poa mkiwa sehemu moja.
Anyway hayanihusu haya nitaongeza tu umakini.
Kuja kushtuka kumbe simu kutoka kwa ESTA iliita sana , ikabidi nimpigie ESTA mtu ambaye hajui kususa maana Mimi nilidhanj pengine hatonitafuta Tena huyu mwanamama.
Samahani shemu Mimi nipo sehemu tu kwa mjumbe wa mtaa huu hapa kwako, lengo la kukupigia simu ni kuulizia ule mpango vipi, maana hata eneo na frem nimeshapata siku nyingi sana kwahiyo nakusikiliza.
Alimalizia.
Subiri nitakuja hapohapo ulipo baadae usitoke.
Nikakata simu,
Nikakumbuka ninavyotoka asubuhi nyumbani nilichimba mkwara ambao lengo nikuwatuliza tu wale ili wasinipande kichwani, nikampigia simu mke wangu ambaye alikuwa mpole sana mithili ya kuniogopa, ila nikamtuliza tu.
Nikapanga lazima niende kwa ESTA kwasababu ya ule mpango wangu, isingekuwa huu mpango pengine ningemuacha apambane na hali yake.Japokuwa huu mpango ni kama hauna uhakika sana kwasababu nilizokuwa naziona ila bado nilikuwa na IMANI, nilitoka kazini nikitembea maeneo ya city centre huku nikiangalia maduka mazuri yanayouzwa nguo za kike,
Nikanunua nguo fulani za mke wangu( jina kapuni)
Bangili na urembo urembo nikaweka kwenye pocket huyooo kutafuta daladala zinazoelekea nje ya jiji.
Nikashuka kwenye daladala huku nikielekea kwa mama mmoja mjane ambaye ndiye mjumbe wetu aliyempokea ESTA.
Nilifika tukasalimiana maongezi yakawaanza
Kwanza baba nikushukuru kwa ukarimu wako wa kumpokea huyu ukakaa naye sikuzote hizo, japo ulifanya kosa kutokuziona mamlaka ili wajue kuwa unahifadhi mgeni,
Huyu ni binadamu angekufa ungefanyaje,?
Nikakiri kosa hasa ukizingatia hata mama yangu mzazi alishasema kipindi fulani nikapuuzia.
Akaendelea yule mjumbe..
Sasa naweza kuwaacha mkaongea wenyewe maana kaniambia wewe ndiye anakutegemea kwa vitu vingi kwa sasa.
Akatupisha,
Nilizungumza mengi na ESTA alishauri angepanga chumba, nilifikiria kidogo nikaona ni wazo zuri Bora apange, lengo awe kwenye himaya yangu mpaka nitakapopiga hela kwa madam, nikashauri atafute chumba kesho yake.
Huku nikimuita yule mama mjumbe.
Kwanza mama Mimi nikushukuru kwa kumpokea huyu ndugu yangu ni kwamba si Mimi niliyemfukuza Bali kalazimika kutoka, nilijitetea
Wewe mwananguu (akiongea kwa sauti ya chini ESTA asisikie)
Mwanamke mzuri Kama huyu unampotezaje? Yaani ningekuwa na mtoto wa kiume ningemwambia amuoe kabisa mtoto kaumbika mtoto mashallah, hebu mpangie chumba basi na wewe hutaki kuwa na wanawake wawili?
Maana kutwa nzima nilimuhoji ananiambia hujawahi hata kutembea naye mwanangu,? Acha uzembe bwanaaa, unaniangusha.aliongea bila breki yule mama mjumbe mswahili kupitiliza mwenye kabila fulani maarufu mwambao wa bahari ya hindi
Sikumjibu neno zaidi ya kucheka tu, nikiwaza jinsi watu tulivyokuwa nyuma kwenye mambo mengi,
Kweli Elimu ni muhimu, yaani kusoma si lazima upate kazi kwanza unaongeza ufahamu, hebu fikiria mtu anafahamiana na mwanamke kwa Mara ya kwanza tayari anawaza angekuwa na mtoto wa kiume amuoe. Hawazi kuhusu magonjwa ya zinaa na ukimwi. Yaani waswahili tunarahisisha sana mambo.
Na ndiko magonjwa mengi ya ngono yaliko,niliwaza sana.
Sasa baba yanguuu nisikufiche niwe mkweli Sina kitu humu ñdani, unaniachaje?
Aliongea yule mama ambaye huenda kwenye ujana wake alikuwa shangingi na sijui, ujumbe aliupataje
Ikabidi nimpe Msimbazi mmoja.
Huku nikiwaza kweli wanaume tumeumbwa mateso,
Yaani muda wote lazima uwe na hela japo do lazima kutoa, lakini Kuna ile kujiepusha na lawama ndogo ndogo.
Tukaagana huku nikisisitiza ESTA atafute chumba. Najua ule mpango wa Mimi na madam Sina uhakika ila ESTA simwachi lazima nibeti hebu fikiria unaipata milioni tano kwa pamoja bila kutumia nguvu nyingi.
Weeee ESTA ninaye , nilijisemea
Nikafika nyumbani kila huku Kila akiwa mtu mnyonge mnyonge, nikamuita mke wangu nikambembeleza plus uongo mwingi huyoo kalainika, niwanawake tu Hawa wametoka kwenye mbavu zetu. Kama huwezi kubembeleza mwanamke basi utapata tabu sana kwenye ndoa yako, watu wengi wameshindwa kukaa na wake au wapenzi kwa kujitia misimamo ambayo baadaye iligeuka Majuto.
Lazima muda mwingine umpe ushindi hata asiostahili kwa ustawi wa penzi au NDOA.
Tuliendelea kutaniana na mke wangu Huku nikiwa namsoma vitu Fulani Mara tukaitwa na dada wa kazi, natoka nje nakutana na mke wa Shedy akiwa kama kakasirika hivi,.
MADAM nasikia tetesi kuwa huenda tukawa sehemu moja, Haina shida je mpango wangu kwa ESTA utafanikiwa? Na ESTA simuachi
Mke wa Shedy anatafuta Nini huyu maan anajua wazi Hawa hatuna uhusiano nao mzuri.
Sehemu ijayo Ina majibu.usichoke
Inaendeleaa.......
Patamu kma Asalina kulia Kisha wakanyamaza huku wakikumbatiana Mara kadhaa hasa madam na ESTA, hata baada ya dereva wa madam kusogea pale alikataliwa akiambiwa Kuna amani tu, akaja kwangu huku akijichekesha chekesha , akitaka kujua kwani Nini kimetokea pale lakini nilimwambia Mimi mwenyewe sijui,
Hata baadhi ya wateja na wafanyakazi wa mgahawa ule walianza kutawanyika huku walikosa majibu, huku kila mmoja aliniangalia Mimi pengine walitamani kuniuliza lakini nilikuwa bize na simu yangu.
Wote wanne walipiga stori pale Kisha wakaniita,
Ahsante sana tolu, lakini pole kwa baadhi ya mitihani iliyokukuta yote kwa yote tumshukuru MUNGU kwa kulimaliza hili jambo salama , dada yangu (akimaanisha mke wangu) hongera sana umepata mume. Nawaombea muishi maisha marefu ikiwezekana mzeeke pamoja. Aliongea madam na kufanya watu wacheke.
Hata Mimi nashukuru hata hivyo najiona nimefunguliwa nimekuwa huru ,nakushukuru sana shemeji yangu. Alisema ESTA.
Sasa tolu hapa hakuna la ziada nadhani ni muda wa kwenda mkapeane hizo hela maana kilichokuwa kinakwamisha kimeshapatiwa ufumbuzi, aliongea madam.
Hapana madam si wapi Wala wapi hizi hela zilishakuwa mzigo kwangu hivyo nilikuja nazo kama kupewa apewe tu mzigo wake, nilishauri.
Sawa, ni kheri zaidi japo muende kule nilikopark gari ndiko kwenye usalama zaidi naomba niletewe PC(personal computer) maana Nina kazi ya kufanya humo, aliongea Madam akimuelekeza dereva atupeleke kwenye gari.
Ndani ya gari, tukiwa watu wanne Mimi, mke wangu, ESTA na yule mama yake wa hiari, nikatoa zile PESA na kumkabidhi ESTA, ambaye alikuwa anatabasamu huku akishindwa Cha kufanya akawa kaziweka hela mapajani mwake.
Sasa shemu, umefanya kazi kubwa sana nadhani hizi hela tunastahili kugawana , alivunja ukimya ESTA.
Hapana shemu we kwanza hesabu mzigo umetimia? Mengine yatafuata, akabaki kaduwaa tu huku akiziangalia mke wangu na mama mchungaji wakaanza kuzihesabu kwa zamu zile pesa nyingi kwao, maana walitumia muda mwingi .
Ni sawa zipo milioni kumi taslimu,walisema kwa pamoja mke wangu na mama mchungaji.
Sawa,Hilo halina shida nilijua shem hawezi kuleta ubabaishaji na ningekuwa Mimi pekee yangu hata nisinge hesabu, je shem tunagawanaje?alizungumza ESTA.
Shemu Mimi nipo na wewe siku nyingi tangu nilivyotambulishwa na mke wangu huyu, hata hivyo ulieleza masahibu yako, pamoja na kumuweka wazi huyo mtu aliyekufanyia ubaya, lakini jinsi MUNGU alivyo mwema hata yeye alikiri makosa yake, kama mlivyoona mwenyewe akiongea muda mfupi ulopita (wote wakatikisa vichwa kukubaliana na Mimi)
Kwahiyo kwanza shida siyo pesa, hatujapatana hapa kwa lengo la kutaka PESA, hata yeye hajatoa pesa kwa lengo la kusamehewa hapana, maana itaonekana kama kanunua msamaha.
Mmesameheana ili kuipa amani mioyo yenu, ukimkosea mtu una kuwa na deni nafsini mwako ambalo linaweza kukutesa kisaikolojia hasa kama hujazoea kumkwaza mtu
Lakini pia kwa aliyefanyiwa kosa anapaswa kusamehe ili kuondoa deni, laana na mikosi ambayo siyo ya lazima, hivyo ukisamehe kwa moyo wa dhati kabisa unakuwa huru kiroho na kimwili.
Kuhusu vijizawadi vya pesa kama hivi unaweza sema havina ulazima, lakini ni kwamba, kwanza aliyetoa hii takrima kwa hiari yake, kaamua kuomba msamaha wa dhati.
Lakini pili atakayepokea ambaye kwa Sasa ni wewe shem tunaamini umesamehe kidhati. Hivyo hizo pesa ni zako shemu. Nilikataa
Umeongea mengi sana baba, lakini kwa mtazamo wangu naona Bora ungepokea hata kiasi kidogo, maana masumbuko uliyopata Mara utake kupelekwa kituo Cha polisi, na mengine mengi hivyo Mimi kwa mtazamo wangu naona unasitahili kuwa sehemu ya huu mgao. Aliongea mama mchungaji.
Lakini nilikataa katakata .
Halafu mume wangu sijui upoje, hujaomba, Bali watu ambao umewasaidia wanakwambia wakupe hela bado unakataa?
Siyo bure jamani khaaah, ukute eti unaona aibu, utakuja kufa masikini wewe.
Aliongea kwa jazba mke wangu akihoji kwanini nakataa hela, alikuwa sahihi kwa sababu hajui mapatano yetu na MADAM aliyenituma hii kazi ambayo nishaifanikisha tayari
Licha ya wale wanawake kumshawishi mke wangu kuwa kama Mimi nimegoma basi achukue yeye bado nilikataa.
Nilikataa kwasababu muda si mrefu mke wangu nitamuonesha kiasi kama kile tukiwa nyumbani sikutaka ajue tukiwa pale, pia kama madam akisikia Kuna chochote kitu nilichukua kwa ESTA ataniona Sina maana, kubwa zaidi madam aliniahidi makubwa kama nitafanikisha zoezi lile, Sasa haraka ya Nini?
ESTA akazisunda hela zote kwenye mkoba wake wa kike, Kisha wote tukatoka kuelekea alipo madam.
Watu walikumbatiana huku wakibadilishana namba za simu, mtu pekee aliyekuwa kakosa amani ni mke wangu, maana muda wote alikuwa ananiangalia jicho baya akiniona kama mzembe Fulani hivi.
Madam aliniita tuongee pembeni tukiwa wawilibtu
Sasa tulo Mimi naona wewe tutaongea zaidi maana Leo nimekuja tu kwakuwa ulinilazimisha ukihofia usalama wako,.
Ujue madam Kuna siku ungesikia nipo ndani maana tayari nilishaonekana kama Nina njama za kutaka kumuua,
Kisa nini umuue, aliuliza madam.
Ni kwasababu nilimpa hela nyingi kiasi Cha kumtisha huyo dada yako sijui mdogo wako,
Achana naye mshamba tu huyo angekuwa mtu mwingine si angekula zile hela, Tena nikwambie tolu huu mpango wa kutaka kupatanishwa na ESTA nilianza siku nyingi tu, nilimtuma mtu nikampa pesa amshawishi huyu ESTA ili tupatane lakini Cha ajabu yule yule mtu aliishia kumtongoza tu ESTA akatembea naye, na Akala hela zangu.
Alisema madam kwa masikitiko .
Nikawaza kumbe Kuna majamaa hawana woga na kitu Cha mtu.
Tuliagana huku madam akiondoka na ESTA na yule mama yake, na Mimi na mke wangu tukatafuta kituo Cha Dala dala. Wakati tukatembea taratibu huku mke wangu akionesha kutokuwa namimi hata kistori tu.
Dah hii adha ya daladala hii, ya ipo siku tu lazima tununue gari yetu mke wangu maana hebu ona watu wanavyogombania mlangoni, Sasa wewe unawezaje Ukiwa na mtoto mdogo, Bora tuite Taxi tu.
Nani wa kununua gari, wewe mume wangu Huyu huyu, ambaye unafanya kazi kuuubwa isiyokuwa na malipo, mbaya zaidi wanakubembeleza chukua basi hata kidogo hutaki wakataka kunipa Mimi umekataa,
Yaani unajifanya mtume mwaminifu kwamba unapatanisha watu bure bila malipo, kwanza ngoja tufike nyumbani utanieleza vizuri we ni mtu wa aina gani ambaye unafanya mambo makubwa bila kunishirikisha na hadi Sasa nashindwa kuelewa uliwezaje kujitesa mwanaume mzima kujaa unafiki wa kupatanisha watu bila maslahi,
Sasa pale hata kama ungesema wakupe milioni moja , kwa kazi uliyofanya nani angeguna unafikiri Cha ajabu eti hutaki hela, pole sana mume wangu nadhani kwako Kuna kitu hakipo sawa,. Aliweka kituo baada ya dereva taxi kuwa amefika tukaingia ndani.
Malalamiko ya mke wangu niliyavumilia baada ya kukuta ni mropokaji asiyekuwa na subira hata hivyo siyo kosa lake maana sikumwelewesha mapema lakini nitamfanyia surprise tukifika nyumbani.
Tulifika nyumbani huku mke wangu akiwa bado kakasirika sana, akawa mkali mkali fulani, Kabla sijamuonesha ule mpango mzima nilipokea simu toka kwa meneja wa kazini kwangu,
Huyu naye anataka Nini kwenye hii wikiendi , nikaweka simu sikioni.
Daniel, nimekuona na mke wa boss mida fulani hapo vipi man kikao gani?
Aliuliza bila hata salamu.
Sasa meneja pale ni mgahawani, Mimi nilienda kivyangu na yeye alikuwa kivyake Sasa kwakuwa ananifahamu ikabidi tujumuike kwenye meza moja vipi Kuna tatizo?
Tatizo lipo, Tena unatafuta kufukuzwa kazi. Akakata simu
Itaendelea..............
Balaa lingnena kulia Kisha wakanyamaza huku wakikumbatiana Mara kadhaa hasa madam na ESTA, hata baada ya dereva wa madam kusogea pale alikataliwa akiambiwa Kuna amani tu, akaja kwangu huku akijichekesha chekesha , akitaka kujua kwani Nini kimetokea pale lakini nilimwambia Mimi mwenyewe sijui,

Niko apa,nasogea kwa kasi sana,kaz nzur mwandishi keep it goingSEHEMU INAYOFUATA....
Usiku wa siku hiyo, nilikuwa na mawazo kiasi,
Huyu Madam, anataka nini kwangu, ana watu maarufu wakubwa wakubwa anafahamiana nao, amekosa wasiri wake kuwaeleza juu ya shida yake.
Kwanini Mimi,
Anadhani Mimi mtoto wakiume nitamsaidia Nini.
Halafu kumbe namheshimu bure tu hata Elimu hana ya kutosha yaani ndumba na uchawi vilimbeba,
Ila huyu stori zake zinatisha, yaani kile mwanaume anaye mpata rafiki yake alimpora, na kumroga kabisa, dah mdada ana roho mbaya sana huyu, Tena Sasa hivi sipaswi kujenga naye mazoea kuonekana naye kwa jinsi alivyo anaweza kukuchoma na kukuachisha kazi.
Ila anaonekana kakitembeza sana, maana Kuna Mwajuma wa uwanja wa fisi huwa wanamsifu kuwa aliitendea haki kazi yake ya kujiuza kiasi Cha kupata kibanda Cha vyumba vinne, lakini huyu Madam kiboko, kutoka huko mkoani Hadi kuwateka mtu na baba yake mbaya zaidi bado akapata utajiri wa kutosha. Kweli uchawi upo, na kama anatoka kweli huo mkoa alionitajia, Sina pingamizi kuhusu uchawi,niliwaza sana.
Mke wangu,
Akaitika.
Hivi yule kijana mnaye sali naye ambaye ni fundi ujenzi ana jicho chongo hivi bado yupo? Niliuliza
Ndiyo yupo, huwa anapiga kinanda kanisani? Alijibu
Sawa nataka namba zake au kesho ukimuona mwambie aje hapa nyumbani, nataka aje anipe ramani fulani jinsi fence yangu itakavyokaa,
Heeee mume wangu hivi naye yule ni fundi, mbona kama ni kilema?
Hapana, ni bonge moja la architecture kama hujui, nikamtajia baadhi ya majengo aliyosimamia na yakawa poa,
Na hata lile jicho aliumia kazini hajazaliwa nalo vile. Niliongeza
Haya, naona safari hii hutaki masihara baba, aliongea huku alitoa kicheko flani Cha sanifu.
Mke wangu , hata Kama huku ni uswahilini lakini, lazima nyumba yangu iheshimike hebu fikiria kesho unasema Kuna wageni watakuja naamini tutalazimika kukaa hapo nje kwenye mti huku wapita njia wakiona kila kinachoendelea. Yaani siyo sawa.
Ila nikweli, alijibu.
Halafu mke wangu, hivi umeniambia na ESTA anakuja hapa,?
Ndiyo atakuja, kwanini umeuliza hivyo mume wangu.
Ni kwasababu yeye ana sali kwenye makanisa mengine, kumbuka wanaokuja hapa ni sehemu ya jumuiya yetu.
Nilimjibu hivyo kwa kumpoteza ila nilitaka kuhakikisha ujio wake kwakuwa nilitamani kujua historia fulani ya maisha yake.
Ujue Nini mume wangu, yule ESTA anapenda sana kuwa karibu na Mimi na pia namfariji kwa namna moja au nyingine, unakumbuka siku ambayo ulitoka mkoani Kisha nikakwambia nitampeleka sehemu?
Ndiyo nakumbuka,
Nilimjibu
Basi kibao kilibadilika, baada ya Mimi kumpeleka, akanipeleka Mimi, kama unavyojua nilikuwa nimeishiwa nguvu kwahiyo akataka kunisaidia, Cha kushangaza baada ya kugundua kuwa ofisini kwako ni pale , nilimuona akinyongea sana yule shoga yangu,
Hata baada ya kutoka eneo lile bado hakuwa na amani kama mwanzo alivyokuwa akinifariji kuwa wewe utatoka tu, badala yake akawa yeye ndiyo mwenye mawazo zaidi, huku akiwa anaongea peke yake, siku zingatia mambo yake kwa kuwa nilikuwa nakuwaza wewe. Aliweka kituo
Nilimwelewa sana mke wangu Tena sana kwakuwa tayari nilijua kitu,.
Halafu mume wangu nasikia kumbe ESTA alikuwa malaya balaa, na kachezea maisha sana.
Wewe umemsikia nani? Niliuliza
Dunia Ina Siri baba, eheeeeh kila kitu kipo wazi mbona, wamechezea maisha huko halafu wanakuja kuishi maisha mabaya kiasi hiki, yaani ana maisha magumu yule dada wewe acha , Tena mzuri masikini, kweli uzuri siyo ndiyo kila kitu, Tena pale alipo Hana hata mtoto, sijui atapata lini maskini, wameharibu mimba weeeee Sasa hivi wanahaha,
Aliongea kwa kulaumu
Dunia Ina mapito mengi mke wangu huwezi jua, niliongea kwa utulivu huku huruma ikiniingia kulingana na nikichosikia mchana wa siku ile .
Sikutaka kumsimulia mke wangu, maana nawajua wanawake zetu hawa.
Lakini nikafikiria kama ESTA atakuja nitatumia nafasi hiyo kuongea naye mambo fulani ili nipate kuwianisha vitu, japo sikutaka kumwambia Yale aliyonituma Madam,
Kwanza ningeanzaje, mwanaume nakuwaje hivyo, niliwaza kumsaidia ESTA
Mume wangu ni saa sita hii tayari jumapili ishaingia tulale bwana tupunguze usingizi naona unawaza, unamuwaza huyo ESTA au,
Weweeee Mimi Nina mawazo yangu mke wangu kama tumeishiwa stori tulale, nilimjibu.
Asubuhi ilifika maandalizi ya kanisani yalipamba moto, Mama mzazi akanifuata,
Dani mwanangu Leo unaenda kanisani, kumbuka tangu nifike hapa sijawahi kuona ukijishughulisha na mambo ya kanisani vipi, na kesho kutwa jumanne nasafiri sitaki niondoke bila kuona ukienda kanisani, Sasa Leo lazima utaenda.
Nikaona ishakuwa kesi hii nikajiandaa nikaenda na Mimi ,
Huku nikijifichaficha baada ya Misa kuisha nikawa wa kwanza kutoka na kurudi nyumbani huku nikiwaza sana
MUNGU atusamehe sana , hivi Leo kifuani Nina chale,Tena mbichi kabisa Leo nimeenda kanisani, Yesu mwenye alikataa mtu kuwa wa vuguvugu , leo hii sijulikani wamoto au wa baridi, MUNGU nahitaji huruma yako, nafika nyumbani nilimkuta ESTA kajaa tele anatusubiri,
Shemu huyoooo, alinikaribisha ESTA
Najua kama nimewahi sana ila kwakuwa Sina simu nikaona ni vyema kuwahi, aliongea.
Ina maana huna simu ya mkononi . Niliuliza kwa mshangao.
Ndiyo Nini Cha ajabu nimeamua kuiuza kwakuwa maisha ni magumu Tena na maisha magumu we Daniel acha tu, sijui kwanini MUNGU hanichukui nikapumzike Mimi.
Aliongea kwa uchungu sana.
Hayo siyo maneno Dada yangu,kikubwa ni kuendelea kumuomba MUNGU mbona kila kitu kitakuwa sawa tu,nilimfariji.
Hapana Dani siyo kwangu,Sina makazi maalum Sina familia,kama nyie wenzangu ama kweli ujanja mwingi mbele kiza,naishije mjini Daniel, aliongeza.
Dah,kwani kwa Sasa una kazi gani ya kujiongezea kipato? Nikiuliza
Niwe na kazi gani mwenzangu,Mimi naishi kama omba omba tu.
Nikaingia ndani nikawaza sana
Yule madam anaonekana anajuta kwa kile alichomfanyia mwenzake miaka hiyo na yupo tayari kumsaidia kama kumlipa kwa mabaya aliyomfanyia.
Mmmmh hili ni balaa,na Mimi sitaki kujiingiza kwenye huu upumbavu,kwanini asitafute wanawake wenzie wawaunganishe ,halafu hivi anashindwa kabisa kumsaka huyu akamface mwenyewe,
Natamanj nimwambie kuwa Kuna mtu Ana shida na wewe lakini siwezi,au nimuunganishe yule madam na mke wangu ili ujumbe umfikie ESTA?
Haaaa siwezi kwanza nitamtesa mke wangu na tumbo lake siwezi.
Japo kuwa lazima nitakaa na ESTA ili anipe background ya maisha yake ili lazima nitakaa naye.
Nikachukua kiasi fulani Cha pesa nikampatia huku nikimuahidi kumsaidia na pia nikisisitiza ananunue simu,
Alifurahi na kunishukuru sana.
ESTA mwanamke wa mjini kipindi hicho niliwahigi kumfuatilia sana lakini alinifungia vioo,sikuwa saizi yake
Lakini siku si nyingi nilimtongoza huyu, Kabla hatujakutana tayari nikapata taarifa juu ya shida yake.
Ni mzuri,mrefu kaenda hewani mweupe umbo ni kama madamu yaani wanafanana vitu vingi tofauti yao ni kwamba Madam ana weusi kidogo,wanaita chocolate colour.
Ila madam ana ngozi ya hela, huyu ESTA ukute anaogea mpaka sabuni ya magadi,wakati nafikiria haya nilisikia sauti za watu wengi wakija nyumbani kwangu.
Huku wakiwa wameongoza na mke wangu,
Mke wangu naye yaani kawatoa watu kanisani anawaleta huku wamekula kweli Hawa,haya si mambo ya kuharibu bajeti haya.niliwaza
Mume wangu wakati ibada fupi ikiendelea hapa itabidi ,itabidi tuandae Chakula kwaajili ya ugeni,
Haaaa uandae saizi kwanini usingewahi? niliuliza
Sikujua kuwa tukitoka tu kanisani watakuja moja kwa moja na huu siyo muda wa kubishana, najua ulitoa hela ya vinywaji,ila Leo bajeti zimeongezeka, aliongeza
sikuwa na jinsi ikabidi nifanye nilichoambiwa si wanasema wageni ni BARAKA,
Halafu njoo huku nje haiwezekani watu wanakuja wewe upo ndani tabia yako sijapenda mtu naangaza macho kule kanisani kumbe wewe umetangulia huku
Itaendelea............
Nisingefanya hivyo,Hongera tolu kwa upatanisho ulioufanikisha. Above all ni kwasababu kulikuwa na maslahi, je ingekuwa bila maslahi binafsi ungejitosa hata kufikia kuhatarisha ndoa yako?
Haya mkuu tuendelee na simulizi yetu. On this, kuna mengi ya kujifunza kuhusu maisha, mambo ya kazini, mahusiano na social wellfare kiujumla.Nisingefanya hivyo,
Ila pesa ni mwanaharamu