Simulizi: Mimi na Boss Wangu

Simulizi: Mimi na Boss Wangu

Yaani nikisoma episode mbili inakuwa kama glass ya maji ya kunywa inaisha faster.
 
SEHEMU INAYOFUATA......

Siku ya jumatatu asubuhi nilidamkia kazini huku nikipanga kwenda kumuuliza yule meneja alikuwa na maana gani kunipangia habari zangu.

Kufika ofisini , nikatulia huku nikipangilia vitu vyangu vizuri, nikaletewa taarifa kuwa nahitajika ofisini kwa meneja. nilishituka , kumbe bado anayo tu, huyu hakuna lingine analoniitia ni yake tu Sasa Leo atanijua Mimi ni nani.

Nilibisha hodi ofisini kwake nikakuta wapo watatu yeye na msaidizi wake wa kike anaye mtumaga vitu lakini pia kulikuwa na fundi wa mashine ya photocopy akiwa kaifungua yote, niliwasalimia wote wakajibu kasoro yeye tu, hasira zikanipanda.

Hebu weee Kaa hapo unaangalia Nini hapo kwani ni hicho nilichokuitia? Alisema huku akiwa bize na yule fundi.

Sasa Mimi nitajuaje uliloniitia Ukiwa hujaniambia wee vipi bwana. Nilimjibu kijeuri.

Oyaaa wewe huwezi kunijibu hivyo, Mimi nimekuita kama ndugu yangu ili nikushauri , nadhani Haina haja ya watu kusikia, ni kwamba yule uliyekaa naye pale sisi tunamuheshimu sana kama boss wetu na mke wa tajiri hivyo nimekuita ili nikuonye. Waweza kwenda, akaniruhusu.

Kwanza nilimwangalia kwa dharau Kisha nikamwambia..

Wewe nimegundua unatumia cheo chako kunyanyasa watu, kwanza una uhakika gani kama nilikuwa namtongoza madam, na pili unawezaje kuona picha tu ukaanza kuitolea maelezo bila hata upembuzi, maana pale kulikuwa na wanawake wanne akiwemo mke wangu wa ndoa , Sasa huyo mke wa boss wako nilimtongoza saa ngapi una ushahidi?

Kweli wanaokuita chogo hawakosei, nadhani unapaswa kujitafakari namna unavyomuonea wivu mwanamke akiwa na Mimi.
Kabla sijamalizia alishanivaa akitaka tupigane,akanirushia kiti na kunigonga kichwani nadhani kauli ya kusema alimuonea wivu madam ilimuudhi, pia ni mtu mwenye kichogo hivyo wakati nahamia pale nilikuta wafanyakazi wakimwita hivyo kwa Siri ili asijue maana huwa anamaindi sana.

Alitaka kunipiga lakini niliishia kumkunja motherfucker robber hakuweza kufurukuta.nilifanya vile kwasababu alikuwa anataka kunitafutia kesi,hawezi kupigana na Mimi akiwa kavaa miwani,maana ukiona mtu anaanzisha ugomvi akiwa kavaa miwani usuthubutu kupigana naye Sheria zake zitakubana sana

Yule fundi akatuamulia huku Mimi nikikimbilia ofisini kwangu.

Hasira zikiwa zimenijaa, wasiwasi na hofu ya kufukuzwa kazi navyo havikuwa mbali kwenye ubongo wangu.

Huyu chizi Mimi nikifukuzwa kazi nitamtafuta hata mtaani mjinga huyu hawezi kufuatilia mambo yangu, yaani nikipokea barua ya kusimamishwa kazi tu ajue naenda jela mpumbavu huyu. Nilisema kwa sauti huku nikigundua vishikizo viwili vya shati vimetoka kwenye Lile purukushani.

Mr Daniel, aliita Binti wa kike ambaye nipo naye ofisi moja kama anavyopenda kuniita, ni Binti mdogo nilimuona Kama mchunguzi fulani kumbe sivyo ni mambo ya utoto tu nilimgundua hasa baada ya kuwa tupo ofisi moja.

Naona unavuja damu kichwani, ona pia shati sijui limechanika kwani Nini kimetokea si umetoka hapa kwenda kwa meneja,nani kakuumiza.aliuliza

Ni meneja kaniumiza mdogo wangu, vipi nimeumia sana?
(Huku nikijipapasa sehemu panapovuja damu)

Umeumia Mr, hebu fanya mpango uende hospital, akiitaja hospital iliyo jirani na ofisi zetu huku nikimwambua ilivyo na foleni nitatibiwa mapema kweli? Sikuumia kiasi Cha kwenda hospital ila kwakuwa naamini kampuni itagharamia si kesi.

Nakupa namba za dada yangu ni daktari pale mpigie mwambie unatoka kampuni fulani atakusaidia ni dada yangu wa tumbo moja, unajua Nini wewe umepigana na meneja hivyo process za wewe kwenda hospital zitachukua muda Bora uende anakofanyia my sister utasaidiwa kirahisi.

Nilitoka nje ya ofisi nakuta taarifa zinaenea kama moto wa petrol kapigana na meneja kapigana na meneja , wengine wakiongeza kazi Hana, kazi Hana. Taarifa hazikunitisha sana.

Nikaingia kwenye gari la yule Binti baada ya kunikabidhi niwahi nalo hospital, huku nikiwa na hofu maana sikuwa na leseni japo Mara nyingi huwa natembea nayo.nikaisereresha ile Nadia mpaka hospital anakofanyia huyo dada yake, kufika pale nikapiga simu zaidi ya Mara kumi haikupokelewa ila nikiwa nimeegamia gari pale nje alikuja dada mmoja mzuri, mzuri, narudia tena ni mzuri yule dada jamani.

Alikuwa na madaktari wenzie wakishangaa ile gari.....

Jamani hili gari ni la mdogo wangu sijui kafata Nini hapa au anaumwa?
Nikagundua huyu ndiyo mwenyewe maana walikuwa wanafanana japo dada mtu ni mzuri zaidi hasa ile mianya.

Hapana doctor, nimekuja nalo Mimi kanipa mdogo wako, pia nimepiga simu Mara kadhaa hujapokea,. Nikaweka kituo.

Wale madaktari waliangaliana wakacheka huku yule dada akishindwa kuamini maneno yangu, nilionesha kidonda changu kuwa nahitaji tiba waliharakisha nikajikuta napelekwa kwa daktari bingwa kabisa nadhani wajihi wangu uliwatisha alinifunga bonge la bandeji nikaifurahia sana namna ilivyowekwa nilitaka iwe hivyo ili kila mmoja ajue nimeumia kwa kiwango Cha lami.

Baada ya Kila hatua kukamilika nikalipa kiasi fulani Cha pesa Kisha nikarejea kwenye gari huku yule daktari akija usawa wangu.

Jamani bado nipo njiapanda ningependa kukufahamu wewe ni nani. Aliuliza.

Naitwa Daniel (nikitaja full name)
Nafanyakazi kampuni ya******
anapofanyia mdogo wako na tupo ofisi moja kwahiyo baada ya Mimi kuumia akaamua kuniazima gari niwahi nalo kupata tiba.

Mmmmh haya naona tutambuana vizuri baadaye ila Mimi naitwa Dr. Rosemary ukiita Rose inatosha naona tutawasiliana. Nilimsindikiza kwa macho yule Dr.,Kisha nikawasha gari kurudi ofisini huku nikiwa natega sikio Nini nitakuta kimejadiliwa, Kuna majuto fulani yalikuwa yananijia lakini nilijikaza , kila nikiwaza jinsi nitakavyopokea barua ya kusimamishwa kazi tumbo liliunguruma huku haja kubwa isiyo ya lazima ikitaka kutoka.

Nikaliingiza gari, nikapark nikarejea huku waniko na wambea hawakuwa nyuma pole nyingi za kinafiki, nikapitiliza hadi ofisini kwangu nikamkuta yule Binti ambaye tulikuwa kama ndugu hasa baada ya kuwa nilikuwa kama mwalimu wake kwa vitu vingi na kunifanya aniheshimu sana.

Vipi Nini kimejiri hujasikia lolote, hapa niliuliza kwa shauku.
Hapana ila meneja alikuja kukuulizia nikamwambia umewahi hospital kasema ukirudi nimwite aje hapa, alisema yule dada.

Kamwite kama anataka kunimalizia nijue kabisa maana anaitaka roho yangu.

Hapana Wala Hana hizo huwezi amini kaja akiwa Mpole kweli. Aliongeza

Sikia usimwite mimi naendelea na kazi yangu, tukaendelea na kazi huku Binti akishauri ni Bora ukapumzike maana unaweza kukosa umakini. Lakini niligoma

Kuna muda nilipewa taarifa kuwa General manager anatuita kule juu ghorofani, hapa tumbo la kuharisha lilinishika , nilipandisha ngazi nikamkuta meneja niliyepigana naye, na general meneja wakiwa wanakagua vitu kwenye computer.

Nikaingia huku nikikosa kujiamini,
Nikakaribishwa

Wewe nasikia umekuwa bondia unataka haribu taswira ya kampuni vipi, unadhani nani taleta tenda kwenye kampuni iliyokosa displine, kama umechoka kufanya kazi waweza kuacha tu,. Aliongea yule msomali mwenye kiswahili kibovu huku macho yakiwa kwenye computer.

Hapana boss, niliongea Kila kitu tangu meneja chogo alivyonipigia simu hadi, alivyoniita ofisini kwake kunikanya jambo ambalo Hana uhakika nalo. Mambo yale yalimwingia sana yule msomali akaacha hata shughuli alizozifanya na kuwa bize kunisikiliza.

Sasa mbona Mimi mesikia tofauti huku akimugeukia yule meneja, wewe unasema huyu afukuzwe kazi kwa lipi labda,?

Sasa wewe nenda kaendelee na kazi maana hili jambo limemgusa mke ya boss sawa sawa ila nitakuita utakapohitajika. Akaniruhusu nikaondoka

Meneja anataka kunifukuza kazi kwasababu gani, nashukuru general kasema niendelee na kazi. Nilimwambia yule dada ambaye niko naye ofisini muombe MUNGU kaka Mimi Wala sijaona kosa lako alisema yule Binti akionesha kunihurumia

Nilifungasha vibegi vyangu nikaondoka nikiwa nimenyong'onyea kwa mawazo

Nilifika nyumbani huku kila mmoja akinishangaa kulikoni bandeji Tena,

Yaani mume wangu mwaka huu ni wako likitoka hili linaingia hili , baba, umuombe MUNGU mwenzangu utakuja kufa. Nilinyamaza , saa tatu usiku nikiwa kwenye lindi la mawazo simu ya MADAM iliingia, kwanza nilishangaa si kawaida yake kupiga simu usiku ule, nikaipokea nikaweka sikioni, tukasalimiana.

Pole sana tolu sihitaji maelezo toka kwako nimesikia Kila kitu kuhusu wewe na yule kinyamkera, yaani kunitongoza anitongoze yeye halafu akufukuzishe kazi,

Mimi yule alivyonitongoza , nilitaka kumpiga chini lakini niliwaza kuwa naye ni mwanaume aliziwasilisha hisia zake, japo alinikosea adabu unadhani mzee angesikia ingekuwaje, niliyazimazima ili tu kulinda kazi yake Sasa nasema atajuta. Ameyaamsha mwenyewe.

Wewe usijali hakuna atakaye kufukuza kazi hapo labda nikifa.vipi umeumia sana tolu nasikia nusura akuue, kabla sijajibu
Akakata simu.

Nilishusha pumzi taratibu huku nikitabasamu nikawaza Nini kilinifunga nikashindwa kumpigia simu fasta huyu boss wangu.

Mambo ni moto, ESTA kaninunia sijui kwanini, lakini Kuna Binti mrembo ambaye anaitwa Rose, huyu nitamuachaje.

Usichoke kufuatilia hii simulizi

Itaendelea....................
Rose haponi labda sio tolu ninae mjua mimi
 
SEHEMU INAYOFUATA.........

Usiku ule niliamua kutoa ule mbandeji kichwani, huku nikigundua sijaumia pakubwa na hata naweza kwenda tu kazini pasi na shaka.

Kama kawaida niliripoti kazini huku watu wengi wakinishangaa katika ofisi zile, maana walijua kabda nitasimamishwa kazi.

Aiseeeh , pole sana lakini naona kama maendeleo ni mazuri hata bandeji umetoa ? Aliongea mmoja wa wafanyakazi wenzangu huku akiwa anapark vyema gari lake.

Niliingia ofisini kwangu nikamkuta dada wa usafi akiwa kamaliza usafi mkononi ana funguo pamoja na bahasha ya khaki. Tukasalimiana

Samahani kaka hii bahasha nimepewa tangu jana na meneja wako ila nilikutafuta sikukuona ukawa umeshaondoka.
Niliipokea sikutaka kuiangalia mbele yake, nikamruhusu aende, nikachungulia nikaona kiasi Cha pesa taslimu elfu hamsini. Pamoja na karatasi yenye ujumbe fulani ambayo iliandikwa kwa mwandiko mbaya ulionipa tabu kusoma yale maneno machache yaliyosomeka hivi....

Ndugu Mr. Daniel sisi sote ni wafanyakazi kwenye kampuni ya (jina kapuni) Kila mmoja anawajibika ipasavyo kwenye eneo lake kulingana na taaluma yake. Hakuna mkubwa kwenye hii kampuni Bali ni mgawanyiko wa majukumu tu, ombi langu , naomba unisamehe na tusahau yaliyo pita. Tufanye kazi kwa nidhamu kwa ustawi wa familia zetu.

Nilisoma huku nikitabasamu sikuamini kama yule meneja katili na jeuri kaandika ujumbe ule ila huenda kashauriwa na watu, namjua ni mtu asiyejali utu wa mtu neno lake yeye ni Sheria. Nilichukua zile hela nikaziweka kwenye droo ya meza yangu huku nikiziwasha computer zote, Binti ambaye nipo naye alikuja huku naye akishangaa ujio wangu, nikagundua kuwa lile neno la Jana huenda ilitafsirika lazima kibarua kiote nyasi.

Yule Binti naye alikaa kwenye kiti Chake huku akiniangalia kwa jicho la kuibiaibia,
Kaka vipi lakini hali ya maumivu ya kichwa, aliuliza.

Kwa kweli namshukuru MUNGU Niko sawa kabisa . Nilimjibu
Siku hiyo kulikuwa na wageni wengi sana walioingia na kutoka hivyo Kila mmoja alikuwa bize huku nikiwa na kazi mbili maana baadhi ya wageni wa yule Binti alishindwa kuwatatulia shida zao kwa wakati ikabidi niwe nasolve ili mambo yawe sawa.

Baada ya muda wa lunch, tulirudi wote Kisha nikatoa ile bahasha huku nikisogea na kukaa karibu naye.

Hebu angalia humo Kuna Nini, nilisema.

Akachukua zile pesa akahesabu Kisha akaanza kusoma ule ujumbe.

Huu mwandiko si wa meneja chogo huu, aliuliza yule Binti.

Hahaha (nilicheka)we muite chogo ili ufukuzwe kazi haya. Nilitania

Kwani Hana bwanaaa, Tena na anavyonyoa upara ndiyo anafanya kichogo kionekane vizuri kama computer hiyo hapo. (Akinionesha computer za kizamani juu ya kabati la mafaili) nikacheka sana.

Sasa hii elfu hamsini ni ya Nini au ndiyo msamaha, aliuliza yule Binti.

Huenda maana maelezo yanajitosheleza. Sijui niziache nimrudishie tu.Nilijibu

Usirudishe , we kula wote hapa tunatafuta hela hivyo usirudishe kaka. Ikabidi nimpe elfu ishirini nikabaki na thelathini huku ile mada ikifa kabisa.

Aisee Jana nilivyoenda hospital nilikutana na dada yako mnafanana sana jamani. Nilimchokoza

Mmmmh Wala. Hata hatufanani nashangaaga wengi wakisema hivyo,
Alijibu,.

Dah nimemwelewa sana yule Dada yaani ni mmoja wa macute sijapata kuona , hivi anaitwa nani vile maana nakumbuka alinitajia jina na nishamsahau. Nilijifanya kusahau jina.

Haaaa kakaaa, hivi wewe utoke kumwelewa mtu halafu na jina akutajie umsahau kweli? Aliongea yule Binti akitabasamu.

Wallah nimesahau, ila nimempenda bure ni mnyenyekevu, mkarimu pia ni mzuri jamani natamani hata kuonana naye Leo tupate chakula Cha usiku ningefurahi sana. Nilizidisha upelelezi

Sawa, anaitwa Rosemary ni dada yangu ambaye tumezaliwa wawili tu na yeye kaniachia ziwa, lakini kaka wewe si una mkeo unamtaka dada yangu wa Nini?maana sipo tayari kuona ndugu yangu anaangamia maana mume wa mtu anauma na ukizingatia sisi ambao hatujaolewa hivyo tumekuwa tunarushiwa mawe kuwa tunaongoza kwa kuiba waume za watu. Aliongea yule Binti akimtetea dada yake.

Kwani huyo dada yako naye hajaolewa? Nilizidi kumchimba.

Yeah hajaolewa kwakuwa ilitokea bahati mbaya mchumba wake alifariki kwa ajali ya gari wakati wakitoka kufanya tohara huko nyanda za juu kusini. Alijibu

Kwani na huyo mchumba wake alikuwa ni daktari? Niliuliza

Ndiyo, yeye ndiye aliyemu inspire dada yangu aingie kwenye hiyo taaluma, kwanza niwe mkweli dada yangu licha ya kuchagua masomo ya Science bado alifeli, ikabidi huyo mchumba wake apambane hali na Mali ili dada atimize ndoto zake lakini lakini miezi miwili baada ya kuajiriwa umauti ukimkuta yule shemeji, Dah nitamkumbuka sana ni yeye aliyefanya nikaajiriwa hapa.aliongea huku akionesha kutonesha vidonda fulani ikabidi nimzugishe kwa kubadili mada.

Ila gari yako inaonekana inafanyiwa service sana yaani nimeipenda , Kila kitu kipo Sasa yaani. Nilijifanya kuisifia.

Yeah mjini hapa huwezi kuwa na gari ya ovyo, vile tu unavyoiona bado matraffic wanaona Ina kasoro maana wamekuwa wakisumbua Sana.

Baada ya kumzugisha kwa Yale maneno na kukuta karudi kwenye hali ya kawaida tuliendelea kuchapa kazi .

Muda fulani nilipokea simu ya madam nikaweka sikioni kuisikiliza,

Tukasalimiana.

Enhee niambie tolu maana nilitoa maagizo hapo kazini kwako kuhusu ujinga waliotaka kukufanyia, vipi Kuna usumbufu wowote, aliuliza

Hapana, nimekutana na meseji ya kutaka tuyamalize toka kwa mgomvi wangu hivyo Kila kitu kipo sawa. Nilimjibu.

Sawa, lakini Kuna suala moja tolu ulifanya sivyo Sasa saloon gani ile Tena,Haina vifaa Haina Kila kitu halafu imekaa kiswahili mno, lakini si nilikwambia kila hatua utayokwama uniambie Sasa kwanini mkafungua pale? Maana Mimi nikikupa hela ya frem utafute maeneo ya mjini , Sasa na weeeeeeeeeh...aliongea kwa sauti ya chini nikaona hizi nazo lawama.

Samahani madam mbinu niliyotumia kumshawishi ESTA ilitaka hivyo, nisingeweza kumfungulia saloon ya gharama huoni kama angeshtuka , hebu fikiria jinsi alivyonibadilikia akashindwa kupokea zile pesa huoni alikuwa mtu wa namna gani?

Na zile hela bado ninazo kama zinahitajika basi naweza kurejesha niliongea kwa mtego.

Hapana sijasema urudishe hela, hata hivyo nimefanya maboresho kwa kumuongezea vifaa vinavyohitajika ukitaka utapita pale upaone pamependeza japo kwangu sijashawishika.na pia kama Kuna kitu unahitaji nikusaidie we kuwa huru tu nitakusaidia maana umefanya kazi kubwa sana baba. Akaweka kituo.

Sawa nimekuelewa MADAM ila kuhusu kupita kwenye ile saloon sitapita maana naona kama ESTA kanichukia ghafla sijui kwanini.nilijitetea

Nalielewa hilo ila usijali hizo ni tabia za wanawake tuliowengi , yule aliniambia kwamba anaona huruma baada ya wewe kutupatanisha akahitaji akupe kiasi fulani Cha pesa
Lakini nilimwambia aache tu kwani Mimi na wewe tulishamalizana, baada ya kusikia hivyo niligundua kabadilika. Akawa anasema kama ni hivyo basi utakuwa umepiga hela nyingi hivyo chuki yake ni hiyo. Mpotezee tu ni wivu unamsumbua. Alimalizia madam

Kisha akakata simu nikawa nishapata jibu kwanini ESTA kanichukia ghafla Lakini sikujali kwani mjini shule Kila mtu anafanya kazi kwaajili ya familia hivyo ile fursa nisingeilazia damu.

Nilinukuu kauli moja toka kwa madam kwamba chochote nachohitaji nimwambie, Sasa hii ni fursa sihitaji pesa toka kwake ila nahitaji gari , maana fence yangu mafundi wanafanya kazi kwa uaminifu ipo hatua nzuri.

Sasa madam anajuana na watu wengi sana nahitaji anisaidie upatikanaji wa gari hili ni jambo linalonisumbua sana nimechoka kuaibika hata na watoto wadogo.

Muda wa kutoka ulivyokaribia, nilifungasha vitu vyangu Kisha nikatoka Huku nikihakikisha salio au muda wa maongezi kama uponwa kutosha lengo nimpigie Rose , baada ya kujiridhisha nikatoka Huku nikimpigia mke wangu kuwa Nina dharula hivyo nitachelewa kidogo, alinielewa Huku akisisitiza niwe makini.

Nilitembea kwa miguu huku nikibonyeza simu kutafuta jina la yule mrembo nilipiga Mara nyingi simu haikupokelewa, nikagundua labda Siyo yake maana hata Jana yake simu hakupokea nikakutana naye baada ya kulishitukia gari la mdogo Wake.

Nikiwa nimekata tamaa simu iliita kuangalia mpigaji ni rose. Huku nikiset set sauti yangu ya kiume kwa kukohoa kidogo ili niipokee ile simu.

Haloow naitwa Daniel, nilikuja kutibiwa Jana hapo hospital ya rufaa ulipo wewe, unanikumbuka.?

Basi salimia kwanza Mr, aliongea yule Rose

Niliona aibu kidogo baada ya kujikuta nilikurupuka, hapana my friend ningekusalimia tu ila nilitaka unitambue mapema , vipi habari za kazi, niliuliza.

Nzuri tu , vipi pole unaendeleaje na wewe na kidonda? Aliuliza

Namshukuru MUNGU Niko poa ,ila samahani Kama labda nitakuwa nimekupotezea muda wako ni kwamba , nilikuwa nahitaji mazungumzo marefu kidogo hivyo kama labda ungekuwa na muda basi tungepanga kuonana tukapata dinner? Nililipua bomu.

Ahhh samahani ulikuwa na mazungumzo gani kaka maana unanitisha?aliuliza

Ni ya kawaida tu actually ni kufahamiana tu zaidi hamna la ziada. Nilijibu

Sawa, ila samahani Leo nipo night hivyo itatuwa ngumu Lakini pia hata siku zingine itakuwa ni vigumu kukutana usiku, kwakuwa Mimi naishi kwa wazazi wangu hivyo ile heshima lazima ichukue mkondo wake najua hakuna wakunizuia ila ni heshima tu, alijibu .

Ina maana wote na yule mdogo wako mnaishi hapo kwenu, nilizidisha maswali.

Hapana yeye anaishi apartment fulani maeneo ya uzunguni alikopangiwa na mchumba wake. Vipi mbona maswali mengi Mr.

Hapana, nilitaka kujua maana aliniambia anakaa apartment Leo hii wewe unakaa kwenu nilidhanj alinidanganya, nilijitetea

Kwani invitation card hajakupa na unasema mpo ofisi moja maana harusi yake ni mwezi ujao tu. Alifafanua

Sasa muda sahihi wa wewe kuwa free ni lini, niliuliza

Ni weekend tu, ila napo ikitokea dharula ya Mimi kuhitajika hospital basi tutasitisha zoezi letu .

Nilikata simu huku nikilaumu Baadhi ya kazi kutowapa wafanyakazi wao muda wa kupumzika. Nikapita kwe baa fulani nikakiteketeza kile kielfu thelathini Cha msamaha Kisha nikashika njia ya kuelekea nyumbani.

Ambako nilikuta mafundi wakilaumu kwamba mke wangu anawasimamia mno , kwanini hawaamini.

Yaani Kila wakichana mfuko wa saruji naye yupo , tulitamani tumpe pimamaji mkeo ili aungane na sisi maana anaonekana anapenda hii kazi, aliongea kijana fulani mtata akiwa ananawa miguu usiku ule wa saa mbili .niliishia kutabasamu tu
Maana anachofanya mke wangu ni maagizo niliyompa , naijua janja janja ya mafundi.

Dr. Rosemary alipiga simu,
Huyu naye anapigaje simu kwanza si aliniambia kuwa yupo kazini, halafu Mimi mwenyewe tayari nipo nyumbani kwangu, ataniletea majanga huyu, nilitoka pembeni nikaipokea simu yake.

Usikose sehemu inayofuata.

Inaendeleaa...........
 
Huyo mwanamke,Mwanzo ulipomshirikisha kula hela za ESTA aligoma,lakin sahv anazitaka
 
SEHEMU INAYOFUATA......

Siku ya jumatatu asubuhi nilidamkia kazini huku nikipanga kwenda kumuuliza yule meneja alikuwa na maana gani kunipangia habari zangu.

Kufika ofisini , nikatulia huku nikipangilia vitu vyangu vizuri, nikaletewa taarifa kuwa nahitajika ofisini kwa meneja. nilishituka , kumbe bado anayo tu, huyu hakuna lingine analoniitia ni yake tu Sasa Leo atanijua Mimi ni nani.

Nilibisha hodi ofisini kwake nikakuta wapo watatu yeye na msaidizi wake wa kike anaye mtumaga vitu lakini pia kulikuwa na fundi wa mashine ya photocopy akiwa kaifungua yote, niliwasalimia wote wakajibu kasoro yeye tu, hasira zikanipanda.

Hebu weee Kaa hapo unaangalia Nini hapo kwani ni hicho nilichokuitia? Alisema huku akiwa bize na yule fundi.

Sasa Mimi nitajuaje uliloniitia Ukiwa hujaniambia wee vipi bwana. Nilimjibu kijeuri.

Oyaaa wewe huwezi kunijibu hivyo, Mimi nimekuita kama ndugu yangu ili nikushauri , nadhani Haina haja ya watu kusikia, ni kwamba yule uliyekaa naye pale sisi tunamuheshimu sana kama boss wetu na mke wa tajiri hivyo nimekuita ili nikuonye. Waweza kwenda, akaniruhusu.

Kwanza nilimwangalia kwa dharau Kisha nikamwambia..

Wewe nimegundua unatumia cheo chako kunyanyasa watu, kwanza una uhakika gani kama nilikuwa namtongoza madam, na pili unawezaje kuona picha tu ukaanza kuitolea maelezo bila hata upembuzi, maana pale kulikuwa na wanawake wanne akiwemo mke wangu wa ndoa , Sasa huyo mke wa boss wako nilimtongoza saa ngapi una ushahidi?

Kweli wanaokuita chogo hawakosei, nadhani unapaswa kujitafakari namna unavyomuonea wivu mwanamke akiwa na Mimi.
Kabla sijamalizia alishanivaa akitaka tupigane,akanirushia kiti na kunigonga kichwani nadhani kauli ya kusema alimuonea wivu madam ilimuudhi, pia ni mtu mwenye kichogo hivyo wakati nahamia pale nilikuta wafanyakazi wakimwita hivyo kwa Siri ili asijue maana huwa anamaindi sana.

Alitaka kunipiga lakini niliishia kumkunja motherfucker robber hakuweza kufurukuta.nilifanya vile kwasababu alikuwa anataka kunitafutia kesi,hawezi kupigana na Mimi akiwa kavaa miwani,maana ukiona mtu anaanzisha ugomvi akiwa kavaa miwani usuthubutu kupigana naye Sheria zake zitakubana sana

Yule fundi akatuamulia huku Mimi nikikimbilia ofisini kwangu.

Hasira zikiwa zimenijaa, wasiwasi na hofu ya kufukuzwa kazi navyo havikuwa mbali kwenye ubongo wangu.

Huyu chizi Mimi nikifukuzwa kazi nitamtafuta hata mtaani mjinga huyu hawezi kufuatilia mambo yangu, yaani nikipokea barua ya kusimamishwa kazi tu ajue naenda jela mpumbavu huyu. Nilisema kwa sauti huku nikigundua vishikizo viwili vya shati vimetoka kwenye Lile purukushani.

Mr Daniel, aliita Binti wa kike ambaye nipo naye ofisi moja kama anavyopenda kuniita, ni Binti mdogo nilimuona Kama mchunguzi fulani kumbe sivyo ni mambo ya utoto tu nilimgundua hasa baada ya kuwa tupo ofisi moja.

Naona unavuja damu kichwani, ona pia shati sijui limechanika kwani Nini kimetokea si umetoka hapa kwenda kwa meneja,nani kakuumiza.aliuliza

Ni meneja kaniumiza mdogo wangu, vipi nimeumia sana?
(Huku nikijipapasa sehemu panapovuja damu)

Umeumia Mr, hebu fanya mpango uende hospital, akiitaja hospital iliyo jirani na ofisi zetu huku nikimwambua ilivyo na foleni nitatibiwa mapema kweli? Sikuumia kiasi Cha kwenda hospital ila kwakuwa naamini kampuni itagharamia si kesi.

Nakupa namba za dada yangu ni daktari pale mpigie mwambie unatoka kampuni fulani atakusaidia ni dada yangu wa tumbo moja, unajua Nini wewe umepigana na meneja hivyo process za wewe kwenda hospital zitachukua muda Bora uende anakofanyia my sister utasaidiwa kirahisi.

Nilitoka nje ya ofisi nakuta taarifa zinaenea kama moto wa petrol kapigana na meneja kapigana na meneja , wengine wakiongeza kazi Hana, kazi Hana. Taarifa hazikunitisha sana.

Nikaingia kwenye gari la yule Binti baada ya kunikabidhi niwahi nalo hospital, huku nikiwa na hofu maana sikuwa na leseni japo Mara nyingi huwa natembea nayo.nikaisereresha ile Nadia mpaka hospital anakofanyia huyo dada yake, kufika pale nikapiga simu zaidi ya Mara kumi haikupokelewa ila nikiwa nimeegamia gari pale nje alikuja dada mmoja mzuri, mzuri, narudia tena ni mzuri yule dada jamani.

Alikuwa na madaktari wenzie wakishangaa ile gari.....

Jamani hili gari ni la mdogo wangu sijui kafata Nini hapa au anaumwa?
Nikagundua huyu ndiyo mwenyewe maana walikuwa wanafanana japo dada mtu ni mzuri zaidi hasa ile mianya.

Hapana doctor, nimekuja nalo Mimi kanipa mdogo wako, pia nimepiga simu Mara kadhaa hujapokea,. Nikaweka kituo.

Wale madaktari waliangaliana wakacheka huku yule dada akishindwa kuamini maneno yangu, nilionesha kidonda changu kuwa nahitaji tiba waliharakisha nikajikuta napelekwa kwa daktari bingwa kabisa nadhani wajihi wangu uliwatisha alinifunga bonge la bandeji nikaifurahia sana namna ilivyowekwa nilitaka iwe hivyo ili kila mmoja ajue nimeumia kwa kiwango Cha lami.

Baada ya Kila hatua kukamilika nikalipa kiasi fulani Cha pesa Kisha nikarejea kwenye gari huku yule daktari akija usawa wangu.

Jamani bado nipo njiapanda ningependa kukufahamu wewe ni nani. Aliuliza.

Naitwa Daniel (nikitaja full name)
Nafanyakazi kampuni ya******
anapofanyia mdogo wako na tupo ofisi moja kwahiyo baada ya Mimi kuumia akaamua kuniazima gari niwahi nalo kupata tiba.

Mmmmh haya naona tutambuana vizuri baadaye ila Mimi naitwa Dr. Rosemary ukiita Rose inatosha naona tutawasiliana. Nilimsindikiza kwa macho yule Dr.,Kisha nikawasha gari kurudi ofisini huku nikiwa natega sikio Nini nitakuta kimejadiliwa, Kuna majuto fulani yalikuwa yananijia lakini nilijikaza , kila nikiwaza jinsi nitakavyopokea barua ya kusimamishwa kazi tumbo liliunguruma huku haja kubwa isiyo ya lazima ikitaka kutoka.

Nikaliingiza gari, nikapark nikarejea huku waniko na wambea hawakuwa nyuma pole nyingi za kinafiki, nikapitiliza hadi ofisini kwangu nikamkuta yule Binti ambaye tulikuwa kama ndugu hasa baada ya kuwa nilikuwa kama mwalimu wake kwa vitu vingi na kunifanya aniheshimu sana.

Vipi Nini kimejiri hujasikia lolote, hapa niliuliza kwa shauku.
Hapana ila meneja alikuja kukuulizia nikamwambia umewahi hospital kasema ukirudi nimwite aje hapa, alisema yule dada.

Kamwite kama anataka kunimalizia nijue kabisa maana anaitaka roho yangu.

Hapana Wala Hana hizo huwezi amini kaja akiwa Mpole kweli. Aliongeza

Sikia usimwite mimi naendelea na kazi yangu, tukaendelea na kazi huku Binti akishauri ni Bora ukapumzike maana unaweza kukosa umakini. Lakini niligoma

Kuna muda nilipewa taarifa kuwa General manager anatuita kule juu ghorofani, hapa tumbo la kuharisha lilinishika , nilipandisha ngazi nikamkuta meneja niliyepigana naye, na general meneja wakiwa wanakagua vitu kwenye computer.

Nikaingia huku nikikosa kujiamini,
Nikakaribishwa

Wewe nasikia umekuwa bondia unataka haribu taswira ya kampuni vipi, unadhani nani taleta tenda kwenye kampuni iliyokosa displine, kama umechoka kufanya kazi waweza kuacha tu,. Aliongea yule msomali mwenye kiswahili kibovu huku macho yakiwa kwenye computer.

Hapana boss, niliongea Kila kitu tangu meneja chogo alivyonipigia simu hadi, alivyoniita ofisini kwake kunikanya jambo ambalo Hana uhakika nalo. Mambo yale yalimwingia sana yule msomali akaacha hata shughuli alizozifanya na kuwa bize kunisikiliza.

Sasa mbona Mimi mesikia tofauti huku akimugeukia yule meneja, wewe unasema huyu afukuzwe kazi kwa lipi labda,?

Sasa wewe nenda kaendelee na kazi maana hili jambo limemgusa mke ya boss sawa sawa ila nitakuita utakapohitajika. Akaniruhusu nikaondoka

Meneja anataka kunifukuza kazi kwasababu gani, nashukuru general kasema niendelee na kazi. Nilimwambia yule dada ambaye niko naye ofisini muombe MUNGU kaka Mimi Wala sijaona kosa lako alisema yule Binti akionesha kunihurumia

Nilifungasha vibegi vyangu nikaondoka nikiwa nimenyong'onyea kwa mawazo

Nilifika nyumbani huku kila mmoja akinishangaa kulikoni bandeji Tena,

Yaani mume wangu mwaka huu ni wako likitoka hili linaingia hili , baba, umuombe MUNGU mwenzangu utakuja kufa. Nilinyamaza , saa tatu usiku nikiwa kwenye lindi la mawazo simu ya MADAM iliingia, kwanza nilishangaa si kawaida yake kupiga simu usiku ule, nikaipokea nikaweka sikioni, tukasalimiana.

Pole sana tolu sihitaji maelezo toka kwako nimesikia Kila kitu kuhusu wewe na yule kinyamkera, yaani kunitongoza anitongoze yeye halafu akufukuzishe kazi,

Mimi yule alivyonitongoza , nilitaka kumpiga chini lakini niliwaza kuwa naye ni mwanaume aliziwasilisha hisia zake, japo alinikosea adabu unadhani mzee angesikia ingekuwaje, niliyazimazima ili tu kulinda kazi yake Sasa nasema atajuta. Ameyaamsha mwenyewe.

Wewe usijali hakuna atakaye kufukuza kazi hapo labda nikifa.vipi umeumia sana tolu nasikia nusura akuue, kabla sijajibu
Akakata simu.

Nilishusha pumzi taratibu huku nikitabasamu nikawaza Nini kilinifunga nikashindwa kumpigia simu fasta huyu boss wangu.

Mambo ni moto, ESTA kaninunia sijui kwanini, lakini Kuna Binti mrembo ambaye anaitwa Rose, huyu nitamuachaje.

Usichoke kufuatilia hii simulizi

Itaendelea....................
Mtoto rose na uwa watamu hao
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom