SIMULIZI: Mama mkwe

SIMULIZI: Mama mkwe

SEHEMU YA KUMI NA MOJA:

Nilikuja kuamka siku tano mbele baada ya kuutambua mwili wa Lameck. Mazishi ilibidi yafanyike bila ya uwepo wangu wala wa mama angu mpenzi. Baba ,mume wangu, ndugu wengine jamaa na marafiki walishirikiana kumuhifadhi mwanangu mpenzi. Mamangu mkwe na mawifi zangu nao walikuja msibani, cha ajabu ma mkwe hakushughulika chochote, ni kama alikuja kutusanifu kua mnaendelea na vita au mtatii masharti.

Baada ya kupata nguvu ilibidi tusafiri kama familia kwenda mkoani Iringa ambako ndio chimbuko la asili ya mume wangu. Mume wangu ni mkinga , kwahiyo kwa mila za kwao yeye akiwa kama mkubwa alitakiwa kuendeleza matambiko yote kwa usalama wa familia yao. Dominic alikua akijitahidi kufanya kila anachoambiwa, ambacho kilimshinda ni kafara za kutoa uhai wa binadamu na ndio maana akaamua kua atatoa dume la ng'ombe mweusi kila inapofika siku ya kuzaliwa ya mwanafamilia wake, huo mwaka ambao ulitokea ajali ya mtoto, hakumudu kufanya na ndio mama mkwe alipopata nafasi ya kutupa kombora lake.

Dommy alinieleza hayo siku mbili kabla hatujasafiri kua inabidi tukawekewe kinga maalumu maana mambo yanamzidi nguvu, na kua anaelekea kushindwa. Akanambia sitakiwi kumwambia yeyote hasa mama angu mzazi maana mama haamini katika mizimu, na kua sio kama haamini kua Mungu yupo lakini vita tuliyonayo ni kubwa mnooo, lazima apambane kila Kona, akaapiza kutulinda hata kama atatakiwa kutoa uhai wake sisi tuishi.

Tukiwa njiani, nilipokea simu kupitia namba ngeni, kupokea sauti ilikua ya mama mkwe wangu, akanambia nawatakia safari njema...umemchukua mwanangu nami mechukua wako, utakua umeelewa sasa inavyouma kubebewa mtoto...Nilibaki na mshangao wa mwaka, kumbe tupo vitani eeeh ?mume wangu akaniuliza unaongea na nani? Sikutaka kumficha nikamwambia kua mama mkwe amepiga simu anatutakia safari njema . Tulikua nanenane , kilomita chache kabla hujafika Morogoro mjini, Dominic akashauri hatuwezi kuendelea na safari maana kauli ya mamake anajua ni kebehi, hatutofika tunapoenda, nilikua kwenye gari, mimi, Dommy na mwanangu wa pili Mathew.

Safari ikabidi iishie Morogoro mjini baada ya kukoswakoswa na fuso lililokua linatokea njia ya dodoma wakati tunakunja tuingie barabara hiyo , ni kama akili ilisimama ghafla, nilisali Sala zote ninazozifahamu na ambazo sizifahamu, sikuwahi jua kua nafahamu kunena kwa lugha, ile siku nilinena. Dominic alipambana kukwepesha gari tukajikuta tumeenda kugonga nguzo ya umeme.Nadhani siku zetu zilikua bado hazijafika maana hadi tunatoka ndani ya ile gari hakuna alieamini kua tumenusurika.

Dominic akafanikiwa kunituliza na kukusanya vitu vyetu muhimu, wakaja trafiki wakapima na gari ikachukuliwa kupelekwa sehemu husika, sisi ikabidi tutafute hotel kupumzika, ndipo nilipopata wasaa wa kumpigia mama mkwe na kumuuliza kwa nini yote haya mama...sisi ni wanao...kwa Nini unatuumiza? Kwanini umeniondolea Lameck wangu? Kwanini umekatili maisha ya vijana wadogo 40, dereva na mwalimu wao. Kwanini mama, kwanini?

Akanijibu jibu rahisi sana, nirudishie mwanangu nami nitakuachia huyo kifaranga wako aliebaki...akakata simu. Dominic alikua anaongea na simu nje , aliporudi akanambia tunaondoka jioni na lory, ila tutapitia njia ya dodoma hadi tutokee Iringa nimeambiwa nikipitia njia ya Mikumi hatutofika....jiandaeni

Nilimpigia simu mamangu kipenzi na kumwambia kua aingie kwenye maombi , kuanzia huo mda hadi tutakapofika iringa kijijini Lupembe. Mama akaniuliza upo safarini? Kumbuka dommy alinambia nisimuage yoyote hata dada wa kazi tulimpa likizo kabla hatujasafiri maana hatukutaka ajue tunapoelekea, nikamwambia mama sina muda wa kukuelezea lakini nakuhitaji kuliko wakati wowote ule.

Safari ilianza jioni yake kwa kupitia njia ya Dodoma ,tulivikata vijiji na vitongoji kwa shida maana mwendo wa lori yataka moyo...tulifika kibaigwa usiku wa saa saba, Lori lilikua linaingia vijijini mbali na hapo, ikabidi safari yetu iishie pale. Dereva wa lori alitushusha karibia na gesti iliyokua njiani , uchovu, baridi, njaa na maumivu ya msiba bado havikutuacha salama.

Ilikua ni mara ya kwanza kulala katika chumba chenye hali duni namna ile, sio kama hatukua na pesa ya kutafuta hotel, ila matatizo yasikie kwa mwenzio, hata hamu ya kutafuta sehemu nzuri ya kulala haikuwepo, tulichokua tunaomba ni pakuche tusonge mbele. Niliamua kuingia vitani rasmi na mama mkwe wangu maana niliona ukimya wangu unazidi kuniumiza. Acha iwe anavyotaka iwe, ila nitapambana kumlinda mwanangu kwa gharama yoyote ile, ikibidi kutoa uhai wangu ili Mathew aishi nilikua radhi.

Hatimaye palikucha, watoto ni malaika jamani, na madhira yote yale mwanangu anakoroma kama chura, nilijikuta nacheka tuuuu, dommy akashtuka na kuniuliza hujalala ma Lameck, bado ananiita ma Lameck , sijui kama jina litakuja kusahaulika walahi, nikamwambia sijalala nawalinda, akaniangalia kwa upendo akanambia ahsante kwa kua mke wangu...Nakupenda we mwanamke, ahsante kwa kua jasiri...

Kulikucha na safari ikaendelea ,tulifika Dodoma mjini mapema tu, maana tulidamka saa kumi na moja na kupata private car iliyotusogeza hadi mjini. Tulifanikiwa kupata usafiri baada ya kupata kifungua kinywa na safari ikaanza mapema tu kuelekea Iringa. Mungu alikua upande wetu kwani licha ya mvua kubwa iliyokua inanyesha tulifanikiwa kuingia salama kijijini Lupembe usiku wa hiyo siku...kijijini ni kijijini tuuu, huduma mbovu , barabara mbovu, chakula cha utofauti, lakini nilipata amani mara mia ya ninayoipata ninapokua dar, kua mbali na mama mkwe wangu ilikua inanipa amani sana.

Tulifanyiwa tiba mbalimbali pamoja na kupewa kinga , baada ya siku saba za kulala kaburini kwa marehemu baba mkwe ,kutambika na kusoma dua tuliruhusiwa kurudi dar...safari hii tukitumia njia ya kawaida ya iringa kupitia Mikumi hadi Morogoro ,tuliingia salama salimini dar, jioni ya siku ya safari, mume wangu alishafanya utaratibu kupitia connections zake gari ikarekebishwa, na kurudishwa dar.

Maisha baada ya hapo yalikua mazuri na kutufanya kusahau madhira ya mama mkwe kwa mda....miaka kadhaa ikapita, mama mkwe akatupigia simu kuomba kikao cha familia. Mume wangu alirudi akanipa taarifa hiyo na kuniambia moyo wake mzito ,lakini mwisho wa siku yule anabaki kua mama ake, kama ametambua kosa lake yeye binafsi anamshukuru Mungu kwa huo muujiza. Nilichagua kua Thomaso katika hili, kuwaamini watu kumeniletea maumivu sana, nikampigia babu wa Lupembe na kumueleza kila kitu, babu akanisikiliza akanambia siku ya kikao niwasiliane nae.

Hatimaye siku ya kikao ikafika, tukatoka Mimi na mume wangu, mtoto wangu nikampeleka kwa mama, bado sikua na imani nao. Nikampigia babu akanambia chukua chumvi ya mawe changanya na karafuu vifunge kwenye mfuko wa nailoni, weka kwenye mkoba wako...na pia ukifika getini kwa mama mkwe wako kabla hujaingia tazama magharibi mara nne, nuia maneno yafutayo kila unavyotazama magharibi...' Wakuu naomba mtulinde' Wakuu naomba mtulinde' ....Mungu awatangulie.

Tulifika kikaoni, nikamuomba mume wangu atangulie mimi naongea na simu na mama nakuja, alipoingia tu ndani nikaanza kufanya kama nilivyoelekezwa...Kisha nikaingia ndani nikasamilia na kukaa kusubiria kikao..Mama mkwe alitoka baada ya kama nusu saaa hivi, mda wote tulikua na wifi zangu , walifurahi kutuona na unaona kabisa yanayoendelea hawapendezwi nayo lakini hawana namna, mama mkwe alikuja akatusalimia kwa kutukumbatia, alipofikia kwangu akanambia najua ulichofanya.

Asikwambie mtu sikuelewa kilichoendelea pale kwenye kikao, nachokumbuka ni wifi angu alinishika akanambia wifi kunywa juice inazidi kupoa , ndipo nilipogundua kua kumbe nimewekewa juice...sikumudu kunywa nikawaambia kua sijisikii vizuri ,tumbo linanisumbua. Ma mkwe akanambia kunywa Grace ningetaka kukuua hata hapa usingefika, Sina shida na wewe....nataka damu yangu tuuuu.

Tumbo la uzazi liliunguruma, nikajikaza nikanywa juice, mme wangu akamwambia mama hayo sio maneno ya kumwambia mkweo, tumeshayapita hayo...kikao kiliisha ,tukaaga na kuondoka salama. Mume wangu akawa anaenda kwao mara kwa mara na mtoto Mimi sikuwahi kanyaga tena. Wifi zangu wakaanza kuja kwangu, kawifi kangu ka mwisho kakaomba kuja kuishi na sisi, sikuona shida tukamkaribisha .
 
SEHEMU YA KUMI NA MBILI:

Mathew alikua sasa, taratibu za kumpeleka kwa bibi ake kwa ajili ya birthday zilirudi tena kwa Kasi...nikaona kama birthday ndio gharama ya maisha ya mwanangu acha tu afanyiwe...sikutaka tena ligi, ili mradi amani ilikuwepo basi sikutaka tena maugomvi, swala tu wasiniumize mimi wala mwanangu kihisia wala kimwili.

Mathew alipofikisha miaka mitano alianza kupata ugonjwa wa ajabu, alikua anaanguka kila ifikapo tarehe 20 ya kila mwezi....na ndio tarehe aliyofariki marehemu baba yangu mkwe. Mara ya kwanza nilijua ni masikhara lakini mda ulipozidi kwenda nikaona hii Sasa sio kawaida...kila tarehe 20 mtoto anaanguka kwa miezi mitatu mfululizo, nikaanza kupambana na hospitali, nilizungumka kwa specialist wote hapa dar bila mafanikio, tukaomba transfer tukaenda aghakhan Nairobi, bado mtoto hakua na nafuu, tena akawa anazidi, akawa anaanguka anakaa hata masaa matano badala ya lisaa limoja kama awali.

Mme wangu ikabidi amuangukie mama ake kua naomba unisaidie mwanangu apone, mama mkwe akamwambia mme wangu , sio wewe wa kuja kupiga magoti nataka aje mkeo..Muulize mkeo alichokifanya siku amekuja kwenye kikao miaka kadhaa nyuma, mwambie yale matusi ndio gharama yake hii, rudini tena Lupembe. Dominic alirudi nyumbani akiwa amekasirika isiyo kifani, akanambia napambana kwa ajili yenu na bado unafanya mambo kinyume na makubaliano? Ile siku nilisema sitoweza tena? Kama gharama nayotakiwa ni kwenda kutendewa tena unyama na mamake kama kikao cha kwanza, sitomudu....nilipiga magoti nikamtafuta Mungu kwa bidii...nilitubu kukubali kutumika na miungu kwa miaka yote hiyo, nilisali na kufunga kwa kumaanisha sana. Dominic hakua akirudi nyumbani, nilhamisha makazi pia pamoja na mwanangu ile nyumba nilipangisha.

Nikiri tu maisha hayakua rahisi lakini Mungu ni mwema alinipigania, nilipambana na maombi pamoja na matibabu ya hospitali hadi mwanangu alikaa sawa . Nilikuja kusikia kua Dominic alioa tena mwanamke alietafutiwa na mamake, sikutaka kujihusisha na ile familia tena.Miaka mingi mbele kijana wangu akiwa mkubwa wa kwenda secondary nakuja kuonana na Dominic akiwa amedhoofu mnooo...akaomba radhi na akaomba wasaa wa kuongea nami, nilimruhusu tukatafuta mahala tukaongea, akanambia kua mama alifariki miaka mingi na pia alioa lakini watoto walikua wanafariki kila mwaka...

Akanambia anajutia kwa kushindwa kua baba bora kwa wanangu...na akaomba radhi kwa yote aliyonipitisha, akanambia alipambana lakini amekubali kushindwa, na hapo alipo anapambana na maradhi mbalimbali maana majini yaliyoachwa na mamake yanamshinda kwaio yametafuna watoto wake, wadogo zake wamefariki kwenye ajali mfululizo na yeye yamempa maradhi ya kudumu...ananambia mimi ni kitu bora kuwahi kutokea kwake, na kua hakunistahili...alinambia atakuja wakili kuniletea documents za kusaini kuhusu mali anazomiliki na alivyofanikiwa kuchuma maana hana familia nyingine zaidi yangu, alinipa hongera kwa kua jasiri na kusimamia msimamo wangu katika imani...

Aliomba japo amuone Mathew kwa picha, nikamwambia next Friday ni graduation yake karibu sana....hakuamini kua hatimaye Mathew anamaliza form four...Alikuja kwa graduation na akajitambulisha kwa Mathew maana ni miaka mingi ilikua imepita, tukapata wasaa wa kuishi na Dominic kwa miaka mitano mingine, alikuja kufariki katika ajali mbaya ya gari iliyoondoa na maisha ya watu wengine nane....Mungu ampumzishe mahala pema Dominic wangu, who am I to judge him....nilimpenda sana ila alichagua fungu lingine ....

Mwisho:

Ahsanteni...Nawapenda mnooo..


Just Nana...
 
SEHEMU YA KUMI:

Yalipita mawiki kadhaa, ilikua asubuhi najiandaa kutoka kwenda kwenye biashara zangu, school bus inayombeba Lameck ilikua imeshaondoka kama nusu saa hivi, dada alikuja mbio akanambia mama baba amenipigia simu anasema pokea simu yako.
Nilikua metoka bafuni kuoga, kwhiyo simu itakua ilipigwa wakati nipo bafuni...

Nikakuta missed calls kama nne za mme wangu, sio kawaida yake, niseme tu nilipatwa na mshtuko ila nikajikaza...mme wangu akapiga tena wakati najiandaa kununua salio nimpigie, nikaipokea kwa kihoro...dommy akaniuliza kama nimeshatoka nyumbani, nikamwambia hapana...nipo najiandaa, akanambia usitoke nakuja...nikamuuliza dommy mbona hivyo kuna nini? Akanambia naomba tu nisikilize mke wangu, usitoke nyumbani...

Nikakaa katika msongo wa mawazo, nikamuita dada na kumuuliza baba alipokupigia alisemaje? Dada akanambia alinambia nikwambie upokee simu...nikasema sawa hamna tatizo, nikaamua kutumia huo mda kumsaidia dada kumuogesha mwanangu wa pili, huku nikimsubiria dommy arudi, baada ya kama lisaa na nusu dommy akafika, nadhani foleni ilimchelewesha, dommy akanambia chukua mkoba na vitenge kuna mahala tunaenda, nikamwambia vitenge? vya nini tena? akanambia nitakueleza wife...hebu fanya nachokwambia .

Nikawaza tugombane kisa vitenge tu jamani, nikaingia ndani nikatoka na vitenge viwili, hao tukaingia kwenye gari na safari ikaanza...dommy hakua yule niliyemzoea , muongeaji na mcheshi, akaendesha gari kwa umakini sana hadi Amana hospitali, nikaona nivunje ukimya ....honey hospitali asubuhi yote hii tunakuja kumuona nani? mbona hunielezi vizuri...mme wangu akainama aliponyanyuka alikua ameloana machozi, akanambia nisamehe grace...nimeshindwa kwa mara nyingine kuwalinda, nikiwa katika sintofahamu nikaona gari ya nyumbani kwetu inaingia pale hospitali, baba na mamangu walishuka wakiwa wameongozana na wadogo zangu wote wawili...

Nikaona kama wananichanganya, nikataka kushuka, kwa Kasi Dominic akaniwahi nisifungue mlango, mama na baba wakaja pale tulipopaki gari, baba akafungua mlango na kuniambia grace ....pole mwanangu kipenzi...mama akanichukua hadi nyuma ya gari, akanifunga vile vitenge style ya kinyakyusa, kitenge kikakazwa tumboni...mama akanambia nisamehe grace...sikusimama vema katika kuombea ndoa yako kabla hujaolewa, nisamehe mwanangu...

Nikamwambia mama, wewe ni mamangu mpenzi, naomba uniambiae nini kimetokea....mama hakujibu kitu akanikumbatia kwa upendo akanambia atakwambia mmeo...dommy akaja akanambia twende tukamuone mtoto...
Nikapatwa na kama mshtuko wa ghafla, mwanangu ameondoka asubuhi na school bus, mwingine memuacha na dada , huyu naekuja kumuona Amana ni yupi? Baba na mama wakazidi kuniambia nijikaze...

Tukaingia ndani hospitali, badala ya kuelekea wodini tukaelekea upande wa mochwari, nikasimama kwanza, nikawaambia ...hata kama mwanangu yupo hapa, ndio awe huku? hebu acheni masikhara jamani..
Nikaanza kuita jina la Lameck kama mtu aliechanganyikiwa, baba na mme wangu wakashauri nirudishwe kwenye gari, nikarudi pamoja na mama, sikua na nguvu nikakaa chini kwanza.

Nikamwambia mama, mnanikosea ....naomba uniambie kilichotokea, mama akanambia niahidi utakua mtulivu grace, nikamwambia naahidi mama...akanambia gari ya shule aliyopanda Lameck imetumbukia mto msimbazi, watoto kumi kati ya 40 waliokuwepo wamefariki hapohapo kwa kunywa maji, watoto wengine wamesombwa na maji...tupo hapa kuweza kutambua mwili wa Lameck...wewe ni mama unamjua vema mwanao katika hali zote, maiti zimevimba sababu ya majeraha na kunywa maji mengi...jikaze uweze kumtambua mwanao....

Huwezi amini sikuweza hata kulia, nilimuangalia mama nikamwambia twende huko kwenye utambuzi , mama akiwa bado hajaamini kama natumia akili yangu ya kawaida au wazimu umenirudia , akashangaa nimeshanyanyuka na kuelekea walipoelekea baba na Dommy.

Mtoto wako uliemuweka miezi tisa tumboni ni wako jamani...ile bond ni ya ajabu sana, nilizipiga hatua kama kichaa, mama alikua anafanya kazi ya kunikimbiza, mamangu ana mwili kiasi, nilimtesa sana ile siku...
Nikafika huko mochuari , mlangoni nakutana na baba na Dommy, wananishangaa nimefikaje pale,.mara wakamuona mama anakuja mbiombio, mama akafikia kukaa kwanza...

Nikamwambia dommy nipeleke nikamuone mwanangu,dommy akanambia hawajamuona labda atakua katika wale waliondoka na maji, nikamwambia mwanangu yupo hapa nipeleke ...baba akamwambia sawa acha aingie na yeye akaangalie...niliingia ndani, masikini vitoto vyote kumi vilikua vimehifadhiwa sakafuni...vimefunikwa na mashuka ya hospitali, wakasema wameshindwa kuwaweka kwa majokofu ili kurahisisha zoezi la utambuzi, nikapiga jicho moja tu, nikagundua alama ya weusi kwa mbali chini ya jicho la Lameck..mwanangu mpenzi alikua amelala pale chini, mwanangu, malaika wangu alikua amelala pale chini bila uhai...oh dear Lord...
Aisee hapa nimepata uchungu
 
SEHEMU YA KUMI NA MBILI:

Mathew alikua sasa, taratibu za kumpeleka kwa bibi ake kwa ajili ya birthday zilirudi tena kwa Kasi...nikaona kama birthday ndio gharama ya maisha ya mwanangu acha tu afanyiwe...sikutaka tena ligi, ili mradi amani ilikuwepo basi sikutaka tena maugomvi, swala tu wasiniumize mimi wala mwanangu kihisia wala kimwili.

Mathew alipofikisha miaka mitano alianza kupata ugonjwa wa ajabu, alikua anaangula kila ifikapo tarehe 20 ya kila mwezi....na ndio tarehe aliyofariki marehemu baba yangu mkwe. Mara ya kwanza nilijua ni masikhara lakini mda ulipozidi kwenda nikaona hii Sasa sio kawaida...kila tarehe 20 mtoto anaangula kwa miezi mitatu mfululizo, nikaanza kupambana na hospitali, nilizungumka kwa specialist wote hapa dar bila mafanikio, tukaomba transfer tukaenda aghakhan Nairobi, bado mtoto hakua na nafuu, tena akawa anazidi, akawa anaangula anakaa hata masaa matano badala ya lisaa limoja kama awali.

Mme wangu ikabidi amuangukie mama ake kua naomba unisaidie mwanangu apone, mama mkwe akamwambia mme wangu , sio wewe wa kuja kupiga magoti nataka aje mkeo..Muulize mkeo alichokifanya siku amekuja kwenye kikao miaka kadhaa nyuma, mwambie yale matusi ndio gharama yake hii, rudini tena Lupembe. Dominic alirudi nyumbani akiwa amekasirika isiyo kifani, akanambia napambana kwa ajili yenu na bado unafanya mambo kinyume na makubaliano? Ile siku nilisema sitoweza tena? Kama gharama nayotakiwa ni kwenda kutendewa tena unyama na mamake kama kikao cha kwanza, sitomudu....nilipiga magoti nikamtafuta Mungu kwa bidii...nilitubu kukubali kutumika na miungu kwa miaka yote hiyo, nilisali na kufunga kwa kumaanisha sana. Dominic hakua akirudi nyumbani, nilhamisha makazi pia pamoja na mwanangu ile nyumba nilipangisha.

Nikiri tu maisha hayakua rahisi lakini Mungu ni mwema alinipigania, nilipambana na maombi pamoja na matibabu ya hospitali hadi mwanangu alikaa sawa . Nilikuja kusikia kua Dominic alioa tena mwanamke alietafutiwa na mamake, sikutaka kujihusisha na ile familia tena.Miaka mingi mbele kijana wangu akiwa mkubwa wa kwenda secondary nakuja kuonana na Dominic akiwa amedhoofu mnooo...akaomba radhi na akaomba wasaa wa kuongea nami, nilimruhusu tukatafuta mahala tukaongea, akanambia kua mama alifariki miaka mingi na pia alioa lakini watoto walikua wanafariki kila mwaka...

Akanambia anajutia kwa kushindwa kua baba bora kwa wanangu...na akaomba radhi kwa yote aliyonipitisha, akanambia alipambana lakini amekubali kushindwa, na hapo alipo anapambana na maradhi mbalimbali maana majini yaliyoachwa na mamake yanamshinda kwaio yametafuna watoto wake, wadogo zake wamefariki kwenye ajali mfululizo na yeye yamempa maradhi ya kudumu...ananambia mimi ni kitu bora kuwahi kutokea kwake, na kua hakunistahili...alinambia atakuja wakili kuniletea documents za kusaini kuhusu mali anazomiliki na alivyofanikiwa kuchuma maana hana familia nyingine zaidi yangu, alinipa hongera kwa kua jasiri na kusimamia msimamo wangu katika imani...

Aliomba japo amuone Mathew kwa picha, nikamwambia next Friday ni graduation yake karibu sana....hakuamini kua hatimaye Mathew anamaliza form four...Alikuja kwa graduation na akajitambulisha kwa Mathew maana ni miaka mingi ilikua imepita, tukapata wasaa wa kuishi na Dominic kwa miaka mitano mingine, alikuja kufariki katika ajali mbaya ya gari iliyoondoa na maisha ya watu wengine nane....Mungu ampumzishe mahala pema Dominic wangu, who am I to judge him....nilimpenda sana ila alichagua fungu lingine ....

Mwisho:

Ahsanteni...Nawapenda mnooo..


Just Nana...
daah asante Nana japo umenitoa machozi
 
ulivotaja lupembe ni kwetu huko ila mimi nipo mufindi kwenda lupembe napandisha milima nikajua ni tukio la kweli coz uchawi huko lupembe upo kwa sanaaa
Nimewahi sikia story kuhusu uchawi na maeneo hayo, nikaona nikiiweka kwa story itanoga, ila naamini ushirikina upo kila sehemu my dear ingawa baadhi ya maeneo ni vinara kama usukumani, Tanga, kigoma na Sumbawanga...it's just a story ,enjoy...nothing personal
 
Nimewahi sikia story kuhusu uchawi na maeneo hayo, nikaona nikiiweka kwa story itanoga, ila naamini ushirikina upo kila sehemu my dear ingawa baadhi ya maeneo ni vinara kama usukumani, Tanga, kigoma na Sumbawanga...it's just a story ,enjoy...nothing personal
ni story nzuri sana mpenzi
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom