Simulizi: Kiu ya talaka

Simulizi: Kiu ya talaka

SEHEMU YA MWISHO:

Ndugu zanguni baada ya kupoteza muda wenu kufuatilia simulizi yangu ambayo nina imani kuna kitu mmepata. Mazuri yachukueni udhaifu wako uacheni kwa vile tunajifunza kutokana na makosa ya wenzetu.

Basi hapa ndipa ndiyo namalizia mkasa wangu Mungu awalipe kwa kupoteza muda wenu kusoma mkasa huu. Namalizia kwa kuowaomba wazazi wote hasa wa kike na watoto wao wa kike wajiepushe kuingilia ndoa za watoto wao au kaka zao.

Kila mtu ana haki ya kuiongoza nyumba yake mzazi au wifi ni mshauri na si mwenye mamlaka bali wana ndoa wenyewe. Tujiepeshe kuwa chanzo cha migogoro ya familia za wenzetu.

Mwisho kabisa nataka niseme, mtoto ni zawadi toka kwa Mungu, kwa vile mtoto ni mtoto awe wa kiume au wa kike. Mtoto yeyote anaweza kuwa mrithi wa mali za wazazi kwa vile wapo viongozi wa kike mwenye madaraka makubwa dunia na wameongoza vyema.

Kumbagua mtoto wa kike ni sawa na kuingilia kazi ya Mungu na kuona alimuumba mwanamke kimakosa. Napenda kusema nawapenda wote, namuomba mwenyezi Mungu awatangulie kwa kila jambo pia msichoke kumuomba yeye kwa vile ni kila kitu kwetu, asanteni sana.

Ni mimi, Eliza Elias.
Mwisho.

Simulizi inahuzunisha sana...

Inafundisha sana... hujafa hujaumbika...

Chapter closed...



Cc: mahondaw
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] Mshana Jr ukuye pande hii puliiizi
Aaaiseeee. Natamani kujua upande wa pili pale mtu anapokuwa amefariki roho inapotengana na mwili huwa anajisikiaje anafanya Nini au anaenda wapi plus kuona na kusikia nini,. Je wanaomlilia anawaona? Wanaomzika anawaona, au roho inazikwa na mwili?

Mnisaidie kumtag mchawi wa jf mshana Jr tafadhari.
 
Ahsante sana mkuu Shunie. Kuna funzo nimelipata hapa [emoji120][emoji120][emoji120][emoji120][emoji120][emoji120]
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom