Simulizi: Kazi ya Kutengeneza Majeneza

Simulizi: Kazi ya Kutengeneza Majeneza

Sehemu ya 20.

"Vipi biashara?"
"Biashara nzuri tu," nilimjibu.
Alinijibu kana kwamba hanijali lakini ukweli alikuwa ananijali, tena sana.

Akiwa bado amesimama aliniambia kuwa yeye anazo dawa za kuvuta wateja kwenye biashara yangu.

"Wateja mbona wapo kibao tu," nilimjibu huku nikimwangalia.

"Sawa bwana," naye alinijibu huku akianza kuondoka mahali pale.

Wakati anaondoka nilikuwa nikimkazia macho ya kumsindikiza mpaka alipopotea machoni mwangu. Wakati narudisha macho katika kazi niliokuwa naifanya pembeni yangu alisimama mwanamke mmoja ambapo tulipokutana macho tu alinisalimia.

"Hujambo kijana?"
"Sijambo, shikamoo."
"Marahaba eti nimemkuta mzee Jumaa?"
"Simfahamu halafu sitaki kusikia habari za huyo mzee," nilimjibu huyo mwanamke.

Je, nini kitaendelea?
 
Wek vitu bonge moja ya story tuusindikize usiku huu
 
Sehemu ya 21.

Wakati narudisha macho katika kazi niliokuwa naifanya pembeni yangu alisimama mwanamke mmoja ambapo tulipokutana macho tu alinisalimia.
"Hujambo kijana?"
"Sijambo, shikamoo."

"Marahaba eti nimemkuta mzee Jumaa?"
"Simfahamu halafu sitaki kusikia habari za huyo mzee," nilimjibu huyo mwanamke.
"Sasa sikuelewi hunijibu au hutaki kusikia habari zake?" yule mwanamke aliniuliza.
"Simfahamu," nilimjibu.

"Mbona nimesikia kaja hapa kwako muda si mrefu?" aliniuliza.

"Aliyekuelekeza amekosea," nilimjibu tena.
"Sawa kazi njema," mara nyuma yangu nikasikia sauti ikisema "Jitahidi uwe muungwana."

Niligeuka nyuma hamna kitu zaidi ya kuku mmoja na vifaranga vyake aliyekuwa hapo kwa muda mrefu.

Wakati huo yule mwanamke alishaondoka kibandani kwangu kwa muda mrefu na pia sauti yenyewe ilikuwa ya mwanaume.
Hilo halikunitia wasiwasi kwani kule nyuma yangu ilipotokea sauti hiyo kulikuwa na njia moja kwenda nyingine. Kwa hiyo huenda kuna watu walikuwa na hamsini zao.

Saa kumi na moja jioni nilikuwa nimeshamaliza kulitengeneza lile jeneza. Na wale wanajeshi walitokea muda huo na wakati wanafika jeneza lao lilikuwa ndani kwa sababu hali hewa siku hiyo ilikuwa ni ya mvua.

Niliwaacha nje na mimi niliingia ndani kulitoa. Mara zote majeneza nilikuwa nayatoa nje kwa kuvuta kwa kamba juu ya mbao mpaka nje. Kwa hiyo hata kwa peke yangu niliweza kutoa.
Kabla sijazungusha kamba ya kuvutia, nilifunua mfuniko wa juu ili kuhakikisha usafi ndani yake.

"Mama," nilisema kwa sauti.
Lakini cha kushangaza ni kwamba, wale watu waliokuwa wakisubiria jeneza lao hakuna aliyesikia kama nilipiga kelele za hamaki.

Ndani ya lile jeneza niliona mwili wa binadamu ukiwa umelala kama maiti. Nikiwa nimesimama huku nikitetemeka kwa hofu niliyoiona, mara ule mwili ulitoweka na jeneza likabaki tupu kama nilivyokwishalitengeneza.

Itaendelea...
 
Sehemu ya 22.

Ndani ya lile jeneza niliona mwili wa binadamu ukiwa umelala kama maiti. Nikiwa nimesimama huku nikitetemeka kwa hofu niliyoiona, mara ule mwili ulitoweka na jeneza likabaki tupu kama nilivyokwishalitengeneza.
Nililizungushia kamba na kuliburuza mpaka nje.

"Haya shika huko," alisema mmoja kati yao wale watu akiwaambia wenzake ili walibebe jeneza.

Walilibeba na kulipakia kwenye gari lao la kijeshi huku wakisema kuwa, wamepata sehemu ambayo kila watakapokuwa wakitaka jeneza wanakuja.

Sikujua walikuwa na maana gani. Kwamba sehemu nyingine ambazo majeneza yanatengenezwa kabisa hawayapendi au vipi.

Nje ya kibanda changu kulikuwa kuna meza kubwa ambayo ndiyo nilikuwa naitumia kufanyia kazi zote zile.

Nilirukia juu ya meza na kukaa hapo. Nikajishika kifua kujipima kwa jinsi nilivyokuwa nikihema kwa hofu ya tukio nililoliona kwa macho yangu.

Mapigo ya moyo yalikuwa yakienda kwa kasi sana. Nilihema kiasi kwamba hata kifua kilikuwa kikionekana kupanda juu na kushuka kwa haraka sana.

Picha ya ile maiti niliyoiona ndani ya lile jeneza ilinijia kila baada ya kama sekunde kadhaa hivi. Na kila iliponijia nilishtuka na kuangalia ndani ya kibanda.

Mwili ulikwisha nguvu nikawa kama naumwa. Kati ya maajabu niliyokwishayaona likiwemo lile la kuona paka, hili la mwisho niliona kama limenielemea kiakili.

Ukweli lilikuwa zito la na ajabu zaidi kwangu kuliko yote yaliyowahi kunitokea.
"Hapa nitakuja kufa licha ya kwamba pana biashara," nilijiambia moyoni huku nikitema mate ya uchungu fulani.

Lakini wakati nawaza hivyo, kuna wazo lilikuwa likinisogelea kwa mbali kwamba itakuwa vizuri sana kama nitakuwa nikitengeneza majeneza kama matatu au manne kisha yanakaa tayari, wafiwa wakifika kuhitaji, wanachagua katika hayo yaliyokuwa tayari.

Nikiwa naendelea kuwaza, yule mama jirani alitokea.
"Mwanangu toka juzi nina wazo lakini nilikuwa nasita kukwambia," alisema yule mama.

"Wazo lipi mama, nipo tayari kupokea mawazo mbalimbali," nilimjibu nikiwa nimeshuka kutoka juu ya meza niliyokuwa nimekalia.

"Naona kama una wateja kidogo. Sasa kwanini usinunue mbao kwa wingi na kutengeneza majeneza mengi ili iwe rahisi wateja wakifika tu wanachagua wanayotaka na kuondoka.

Itaendelea....
 
Sehemu ya 23.

Maana kwa hivi unavyofanya naona kama unajipa tabu. Unakuwa juu kila wakati."
Nilimkazia macho yule mama nikifikiria ni jinsi gani alivyoingia mawazoni mwangu. Nikafikiria kwamba alikuwa sahihi kimawazo kama nilivyokuwa nimewaza mimi au kuna kitu zaidi hapo.

"Lakini ni mawazo yangu tu kijana wangu, si lazima uyafanyie kazi," aliendelea kusema. Nadhani ni baada ya kuhisi kuwa, alivyoniambia hivyo yalionekana kama yamenishangaza kwa jinsi nilivyokuwa nimemkazia macho.

"Sawa mama naona kama ni kweli kabisa. Ila sema mtaji, kidogo ndiyo unasumbua. Kama ningekuwa na mtaji mkubwa, hata kesho ningetengeneza," nilimjibu.

"Mungu atakusaidia mwanangu. Kuanzia leo utakuwa unapata kazi nyingi tu, kikubwa wewe weka akiba, usitumie sana pesa," aliniambia.

Na mimi nilimjibu kuhusu kuweka akiba naweza sana, na ni kweli naweza.
Alipomaliza kusema aligeuka na kuanza kuondoka kurudi kwake. Nilimkazia macho kwa nyuma. Mpaka anapanda ngazi za kuingia ndani kwake, nilikuwa bado namkazia macho.

Wakati anamalizia kuingia ndani aligeuka kuniangalia, tukakutana macho lakini yeye akarudisha uso mbele kwa haraka wakati mimi sikuona haya kuendelea kumwangalia.
Mawazo yalijaa mengi kichwani. Nilianza kumuwaza huyu mama sasa. Je, ni mshauri mzuri ama ni mzushi tu.

Kwa nini anishauri kitu ambacho na mimi nilikuwa nikiwaza?
Kuna usalama kweli? Halafu mbona kama simwamini amini siku mbili hizi?

Hayo yote ni mawazo yaliyokuwa yakivinjari ndani ya ubongo wangu kuhusu huyu mama. Ilibaki kidogo tu nianze kumuunganisha na yule babu.

Niliachana na mawazo hayo baada ya kijana mmoja kufika na kuniuliza bei ya kitanda, kama mbao zangu.

Nilimuuliza aina ya kitanda, mti anaoutaka kuutumia na upana wake.
Alipomaliza kuniambia nilimtajia bei baada ya kupiga mahesabu yangu.


Siyo siri, alinilipa kiasi cha pesa za kutangulizia ili nianze kazi. Akaniuliza siku ya kuja kukichukua kitanda chake nikamtajia. Akaaga na kuondoka.

Alielekea njia inayokwenda nyumbani kwa yule mama, na mimi nikawa naendelea kupiga piga hesabu fulani ili kudhibiti mahesabu yangu.
Lakini nilikumbuka kitu kimoja ambacho sikumuuliza, nikageuka ili kumwita nimuulize, sikumuona!
"Khaaa!" nilishangaa.

Itaendelea...
 
Sehemu ya 24.

Kwani kwa ile njia aliyokuwa akielekea haikuwa rahisi awe alishazama uchochoroni.
Hapo ilikuwa kwamba, lazima awe ameingia nyumbani kwa yule mama au awe jini hivyo awe ameyeyuka ghafla, lakini kwamba aliingia uchochoroni nilikataa akilini, nilikataa kabisa.

Lakini wakati huo huo kichwani nilisikia sauti ya yule mama jirani ikiniambia.
"Mungu atakusaidia mwanangu. Kuanzia leo utakuwa unapata kazi nyingi tu, kikubwa wewe weka akiba, usitumie sana pesa."
"Mh!" nilijikuta nikiguna mwenyewe tena kwa sauti ya juu huku nikitingisha kichwa kusikitikia hali ile.

Itaendelea??
 
Sehemu ya 25.

Mawazo tele yalizidi kunijia kichwani kuhusu tukio hili la mara ya pili. Kwamba yule kijana alitowekea wapi katika kuondoka zake baada ya kutoka kwangu. Nilikosa jibu la haraka na nikaendelea kusumbuka san kichwani mwangu.

Ili kupata ukweli wa tukio lile niliamua kuendelea na kazi kama vile hakuna cha ajabu kilichotokea kwangu. Nilijua siku ya siku niliyomwahidi yule kijana si angekuja kuchukua kitanda chake, ningembana hapo hapo kujua alipitia wapi na kwa muda gani?
Ulipofika wakati wa kula mchana sikutoka siku hiyo.

Nilimwita mtoto mmoja aliyekuwa akicheza cheza nikamtuma akaniitie mama ntilie mmoja ambaye alikuwa akiuza chakula nyuma tu ya kibanda changu.

Niliagizia ugali kwa maharage niletewe kibandani kwangu. Ukweli ni kuwa, ilifika mahali sasa nikawa naogopa hata kutoka pale kibandani kwangu. Nilikuwa nikiamini kuwa ningetoka tu, nyuma kungekuja mambo mengine mabaya ambayo yangenifanya nipate tabu zaidi kichwani mwangu.

Nikiwa naendelea na kazi, mzee mmoja alikuja na kuomba misumari mitano, hata kama iliyokuwa imetumika. Alitaka kwenda kugongea kwenye kabati lake la vyombo nyumbani kwake.

Ni mzee mwenye umri kama yule babu mbaya wangu. Nilimwangalia kwanza usoni ili kumvutia kumbukumbu kama namfahamu, lakini sikukumbuka kama nilishawahi kumwona kabla ya siku hiyo aliyokuja kuomba misumari. Lakini wakati akigeuka kuondoka akaniuliza.

"Uko safi wewe kijana?"
"Kivipi mwili au damu?" nami nilimjibu kwa swali.
"Nina maana kwa kila mtu," alinijibu akikunja sura kama anayenishangaa kwa kutomuelewa.

"Ndiyo niko safi," nilimjibu kwa kujiamini lakini ghafla! Mapigo ya moyo wangu yalianza kwenda mbio bila kukusudia wala kuwepo kitu cha kunishtua ingawa ujio wa mzee huyu kwa namna moja ama nyingine ulinishtua.

"Aa, na mimi naona. Maana bwana," alisema yule mzee huku akiwa anaondoka. Lakini nilimsimamisha.
"Mzee unajua sikuelewi kauli yako," nilimwambia akiwa amesimama.

Je nini kitaendelea...
 
Sehemu ya 25.

Mawazo tele yalizidi kunijia kichwani kuhusu tukio hili la mara ya pili. Kwamba yule kijana alitowekea wapi katika kuondoka zake baada ya kutoka kwangu. Nilikosa jibu la haraka na nikaendelea kusumbuka san kichwani mwangu.

Ili kupata ukweli wa tukio lile niliamua kuendelea na kazi kama vile hakuna cha ajabu kilichotokea kwangu. Nilijua siku ya siku niliyomwahidi yule kijana si angekuja kuchukua kitanda chake, ningembana hapo hapo kujua alipitia wapi na kwa muda gani?
Ulipofika wakati wa kula mchana sikutoka siku hiyo.

Nilimwita mtoto mmoja aliyekuwa akicheza cheza nikamtuma akaniitie mama ntilie mmoja ambaye alikuwa akiuza chakula nyuma tu ya kibanda changu.

Niliagizia ugali kwa maharage niletewe kibandani kwangu. Ukweli ni kuwa, ilifika mahali sasa nikawa naogopa hata kutoka pale kibandani kwangu. Nilikuwa nikiamini kuwa ningetoka tu, nyuma kungekuja mambo mengine mabaya ambayo yangenifanya nipate tabu zaidi kichwani mwangu.

Nikiwa naendelea na kazi, mzee mmoja alikuja na kuomba misumari mitano, hata kama iliyokuwa imetumika. Alitaka kwenda kugongea kwenye kabati lake la vyombo nyumbani kwake.

Ni mzee mwenye umri kama yule babu mbaya wangu. Nilimwangalia kwanza usoni ili kumvutia kumbukumbu kama namfahamu, lakini sikukumbuka kama nilishawahi kumwona kabla ya siku hiyo aliyokuja kuomba misumari. Lakini wakati akigeuka kuondoka akaniuliza.

"Uko safi wewe kijana?"
"Kivipi mwili au damu?" nami nilimjibu kwa swali.
"Nina maana kwa kila mtu," alinijibu akikunja sura kama anayenishangaa kwa kutomuelewa.

"Ndiyo niko safi," nilimjibu kwa kujiamini lakini ghafla! Mapigo ya moyo wangu yalianza kwenda mbio bila kukusudia wala kuwepo kitu cha kunishtua ingawa ujio wa mzee huyu kwa namna moja ama nyingine ulinishtua.

"Aa, na mimi naona. Maana bwana," alisema yule mzee huku akiwa anaondoka. Lakini nilimsimamisha.
"Mzee unajua sikuelewi kauli yako," nilimwambia akiwa amesimama.

Je nini kitaendelea...
Eer tukoge eb hatari,
 
Sehemu ya 26.

"Hujanielewa katika upande gani?" aliniuliza.
"Nilivyokujibu kwamba nipo safi kivyote ukasema hata wewe unaona maana...ulikuwa na maana gani mzee wangu?" nilimuuliza huku nikiwa nimesimama nimeshika msumeno niliotaka kukatia mbao.

"Unajua kijana kuchonga majeneza sehemu kama hii yenye kusifika kwa uchawi si jambo la kawaida," aliniambia yule mzee akigeuka kuangalia nyumba ya yule mama jirani yangu. Hapo nikawa kama nimehisi kitu kipya kufuatia kauli ya huyu mzee.

"Wachawi kama akina nani?" nilimuuliza kwa sauti ya chini. Lakini kabla hajanijibu, yule mama jirani alitokea huku akiwa anasema kwa sauti.

"Mmemuona kijana wa watu kafungua sehemu ya kupata riziki zake basi kila dakika mnataka kuja kwake, atafanya kazi saa ngapi?"

Yule mzee aliniangalia mimi wakati aliyesema ni mtu mwingine.
Akaondoka bila kuaga huku akinishukuru kwa misumari niliyompatia.
Wakazi yule mzee anazama kichochoroni, yule mama alikuwa amefika kibandani kwangu.

"Huyu mzee ni mchawi, mchawi hapa mtaani. Muulize hata mtoto mdogo wa hapa mtaani. Acha kumruhusu kufika kwako, atakuharibia kazi," yule mama aliniambia huku akiwa amejishika kiuno.

Je nini kitaendelea....
 
Sehemu ya 27.

"Nimekuelewa mama, nitafanya hivyo," nilimjibu kwa sauti ya upole sana.
Alipoondoka nyuma nilijiuliza maswali mawili makuu. Kati ya huyu mama anayesema yule mzee mtaani anasifika kwa uchawi na yule mzee aliyesema mimi niko safi kiasi gani mpaka niamue kufungua kibanda cha kuchongesha mbao pale, nani mkweli?


Nikiangalia kwa upande wa yule mama, huenda ni kweli kwani kuna matukio mengi yalikuwa yakimuunganisha yeye. Mfano, tukio la yule kijana kufutika ghafla! Mbele ya macho yangu akiwa ameelekea njia inayopita nje ya yule mama.

Au kitendo cha yule mama kuniambia Mungu atanipa wateja wengi ili mambo yangu yaende vizuri na wakati huo huo anatokea mteja ambaye ndiye yule kijana.

Kwa upande wa yule mzee, kitu gani kilimfanya aniambie vile wakati hatujazoeana kabisa.

Ndiyo siku ya kwanza kuonana. Anajua mimi nikoje?
Je, ni misumari tu kweli ndiyo iliyomleta kazini kwangu? Hayo yote nilijiuliza kichwani mwangu huku nikiwa nimesimama kwa mshangao wa mambo yote yale.
Kazi za siku hiyo nilipozimaliza zote nilibaki nimekaa tu.

Kwa kazi zile ambazo zilikuwa hazina sababu ya kuzimaliza siku hiyo niliziingiza ndani kabisa ili nitakapoamua kufunga geti kuondoka isiwe tabu sana.
Lakini nikiwa nimekaa nje juu ya benchi kubwa, alitokea mzee mmoja akanisalimia.
"Salama mzee wangu, shikamoo," nilimwitika nikamsalimia.

"Marahaba bwana, nawangoja wenzangu hapa tunataka kutengenezewa jeneza au umeshafunga hupokei kazi za watu?" alisema yule mzee huku akiniangalia kwa umakini.

"Hata kazi ni kazi tu. Nipo, karibuni sana," nilisema nikiwa nashuka kutoka juu ya lile benchi nililokalia.

Mara walitokea watu wazima watatu akiwemo na kijana mmoja mdogo wa kiume.
"Hawa hapa," yule mzee aliyekuwa amevaa kofia maarufu kwa jina la baraghashia alisema akiniangalia.

Wote walisimama mbele yangu na kuomba kutengenezewa jeneza. Walitoa kipimo kisha wakanilipa pesa zote.

Hii nayo ilikuwa ajabu kubwa sana kwangu. Kwani kila mteja aliyekuja kuchonga jeneza kwangu lazima alilipa pesa kiasi chote au kwa sehemu.

Hakuna hata mmoja aliyesema atalipa akija kuchukua ingawa ningekuwa tayari kwa hilo.


Je, nini kitaendelea?
 
Sehemu ya 28.

Walisema watalitaka saa nne asubuhi ya siku inayofuata. Niliwakubalia kwamba watakuta kila kitu tayari. Walipoondoka tu, nilikagua mbao na kugundua ziko za kutosha sana kwa kazi ile tena zilizokwisharandwa na kupasuliwa tayari kwa kazi. Sikukumbuka ni wakati gani nilizipasua, lakini zilipasuliwa tayari.

Ilikuwa jioni ya saa kumi na moja na nusu hivi. Sikuona umuhimu wa kusema nijihimu kesho yake asubuhi ndipo nianze kazi wakati muda uliruhusu na jua lilikuwa bado kuzama.

Hivyo nilianza kazi chapchap kwa kutoa baadhi ya mbao na kuanza kuzifanyia kazi kwa kufuatia kipimo nilichoachiwa na wateja wale. Mpaka saa kumi na mbili na nusu jioni, jua likiwa limezama, nilikuwa nimeshamaliza sehemu kubwa sana ya kazi.

Ilikuwa bado kuunga na kupigilia misumari, kazi ambayo niliamini kama ningejihimu alfajiri ya siku ya pili, ningemaliza kwa muda unaostahili kuwapatia jeneza lao wateja wangu.

Wakati naingiza vifaa vya kazi pamoja na mbao za kuunganishia jeneza. Kwa mara ya pili, ndani ya kibanda ilikuwa giza totoro. Kumbe balbu ilikuwa imeungua. Na giza lile la ndani lilisababishwa na hali ya nje. Kwani pia kigiza kilishaanza kuingia.

Ghafla! Nikasikia mlio wa kama vitu vinavyoanguka baada ya kupangwa vibaya. Nikaruka na kutoka nje. Nikasimama mlangoni nikiangalia ndani kwa kuchungulia. Nilisikia mlio wa paka akilia kwa unyonge sana.

Je nini kitaendelea?
 
Sehemu ya 29.

Ghafla! Nikasikia mlio wa kama vitu vinavyoanguka baada ya kupangwa vibaya. Nikaruka na kutoka nje. Nikasimama mlangoni nikiangalia ndani kwa kuchungulia. Nilisikia mlio wa paka akilia kwa unyonge sana.

"Shetani mkubwa wewe, tokaa," nilisema lakini nikiwa naogopa sana na mwili ukitetemeka.

Kwa juu unapomalizika ukuta kulikuwa na nafasi ya kuweza kumwingiza panya, kwa hiyo mawazo mengine yalinijia kichwani kwamba huenda yule paka aliingia ndani kwa kutumia nafasi ile kwani ni kubwa ya kuweza kupenya mnyama kama mbwa.

Niliposema shetani mkubwa toka, nikasikia kimyaaa. Yaani kama ni paka kweli, maana nilikuwa sijamuona zaidi ya kusikia mlio, alikuwa amebana mahali.

Lakini kila kitu kilikuwa kiko ndani kwa hiyo nilikuwa na uwezo wa kufunga geti kubwa bila kuingia.

Na kama yule paka aliingia kwa kupitia mlango ina maana asingeweza kutoka mpaka kesho yake au atumie ule mwanya wa juu kwenye bati.

Nikiwa nawaza hivyo, alilia tena, safari hii sauti ilinikaribia mlangoni nilipokuwa nimesimama, nikakimbia mpaka mbali kabisa tena jirani na kwa yule mama wa jirani.

Niliposimama nilikuwa nikihema kwa nguvu kiasi kwamba, kila mtu ambaye angeniona angeniuliza ni kipi kiliniletea tabu.
Hata hivyo nilijikaza kiume na kurudi tena pale ili kufunga kabisa lile geti kubwa.

Nilifanikiwa kulifunga bila kusikia sauti ya paka wala tishio lingine lolote.

Nilipomaliza kufunga geti niliondoka zangu bila kumsimulia mtu yeyoye wa jirani, akiwemo yule mama ambaye sasa na yeye nilikuwa simuelewi.

Nilifika nyumbani majira ya saa moja na nusu usiku. Niliingia ndani kwangu kisha nikatoka. Sikujua nilikuwa nakwenda wapi, lakini nilichogundua ni kuwa ni kuwa, sikuwa na mahali ninakokwenda ila ilikuwa ni kuchanganyikiwa tu.

Nje ya nyumba nilikutana na mama mwenye nyumba ambaye ni mzee sana, lakini alikuwa anaona na kusikia kila kitu.
"Shikamoo bibi," nilimsalimia. Aligeuka kuangalia niliko kisha akaitikia.

Je nini kitaendelea?
 
Sehemu ya 30.

"Vipi mbona unaingia na kutoka kuna tatizo?" aliniuliza.
"Hapana bibi, nakwenda kufuata chakula cha usiku," nilimjibu.

"Hayo matatizo unayataka mwenyewe bwana. We sasa hivi u unatakiwa uwe na mke lakini unasema bado bado. Bado bado utakuja kuta mtoto si wako," alinitania.

"Bibi nataka nikioa nioe mwanamke ambaye atakuwa tayari kukuwekea maji ya kuoa wewe bibi yake. Sio unaoa mwanamke ukimwambia kamuwekee maji bibi anakwambia sijaolewa na wanaume wawili," nami nilimtania, akacheka kwa sauti nzito lakini akasema.

"Lakini sasa mjukuu wangu siku hizi maisha ni wawili wawili, kuna magonjwa ya ghafla usiku, kuna mambo mengi usiku ukiwa peke yako si vizuri. Je, ukienda kazini ukikumbwa na mambo mabaya sisi tutajuaje kama huna mke? Maana mkeo usiporudi ndiyo atakuwa wa kwanza kujua, halafu atatujuza na sisi majirani."

Ushauri huo wa bibi ulinikumbusha matukio yangu ya ajabu, nikabaini ni kweli alichoongea. Nilimsogelea nikakaa nikajifikiria nimweleze matatizo yangu au nisimweleze.

Je nini kitaendelea?
 
Sehemu ya 24.

Kwani kwa ile njia aliyokuwa akielekea haikuwa rahisi awe alishazama uchochoroni.
Hapo ilikuwa kwamba, lazima awe ameingia nyumbani kwa yule mama au awe jini hivyo awe ameyeyuka ghafla, lakini kwamba aliingia uchochoroni nilikataa akilini, nilikataa kabisa.

Lakini wakati huo huo kichwani nilisikia sauti ya yule mama jirani ikiniambia.
"Mungu atakusaidia mwanangu. Kuanzia leo utakuwa unapata kazi nyingi tu, kikubwa wewe weka akiba, usitumie sana pesa."
"Mh!" nilijikuta nikiguna mwenyewe tena kwa sauti ya juu huku nikitingisha kichwa kusikitikia hali ile.

Itaendelea??

Sehemu ya 24 imekaa kishambenga sana
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom