Shunie
JF-Expert Member
- Aug 14, 2016
- 157,400
- 465,166
- Thread starter
- #181
*Sehemu ya 17*
“Prosper elewa ninakupenda sana na nimekwishakukusamehe makosa yako yote na nimesikitika kujua unakufa na kuniacha mimi!” Alisema Belinda akijua hiyo ndiyo ilikuwa mara ya mwisho kuonana na Prosper kwani angenyongwa kama hukumu ilivyotolewa.
Pamoja na kujua Prosper alikuwa na virusi vya Ukimwi kama ambavyo yeye Belinda aliamini kuvipata kutoka kwake na yeye kuvipeleka kwa mtoto wao Alicia, bado Belinda hakuwa tayari kukubali Prosper anyongwe, alimpenda mno na hakutaka kumpoteza! Alitaka waishi pamoja mpaka watakapozidiwa na kufa kwa Ukimwi ikiwezekana siku moja wote watatu.
“Sipendi Prosper anyongwe na ningekuwa na uwezo wa kuliepusha hili ningefanya, siku thelathini za kukata rufaa bado zipo kama ningekuwa na pesa ningeweka wakili ili angalau afungwe kifungo cha maisha si kunyongwa!”
Alishuhudia Prosper akisukumwa na askari magereza kuingizwa gerezani, Belinda alibaki akishangaa bila kujua la kufanya na hakujua baada ya kutoka gerezani angeelekea wapi! Alitamani kurudi nyumbani kwa baba yake lakini kila alipokumbuka yaliyompata mara ya mwisho alipokwenda alishindwa kufikia uamuzi huo.
“Mdogo wangu unaweza kuja Jumamosi au Jumapili, ndiyo siku ya kuona wafungwa!” Alisema askari magereza baada ya kurudi na kumkuta Belinda.
“Ahsante sana dada kwa kweli ninakushukuru mno kwa msaada wako Mungu atakulipa!”
“Huyo ndiye mumeo?”
“Ndiyo na ndiye baba wa mtoto huyu!”
“Ulisema wewe ni mtoto wa mzee Thomson Komba?”
“Ndiyo!”
“Mama yako ni yupi?”
“Mke wake wa kwanza achana na huyu aliyepo hivi sasa ambaye ni mama wa David na John!”
“Kwa hiyo wewe mama yako ni aliyefariki?”
“Ndiyo!”
“Sasa kwanini usirudi ukae nyumbani kwa baba yako kama mumeo amehukumiwa kunyongwa?”
“Dada…wee acha tu!” Belinda aliongea kwa masikitiko.
“Kwanini unasema hivyo?”
“Huwezi kuamini baba yangu hataki hata kuniona, alinifukuza kama mbwa kila ninapokwenda nyumbani hunifukuza!”
“Kwanini?”
“Eti kwa sababu nilipata mimba ya huyu mtoto hawakutaka iwe hivyo nimetengwa kabisa na familia yangu!”
“Pole sana, sasa ukitoka hapa utakwenda wapi?”
“Kwa kweli sijui ila Mungu mwenyewe anaelewa, najua hawezi kuniacha!”
“Ningeweza kukuchukua ukae nyumbani kwangu lakini nina chumba kimoja tu na nina familia kubwa, ninakuhurumia lakini sina la kufanya kukusaidia!”
“Hakuna shida Mungu anafahamu yote!”
*************
Baada ya kuondoka gerezani Belinda alianza kutembea kuelekea kituo cha mabasi cha Segerea, akiwa njiani mvua kubwa ilianza kunyesha na kuwalowanisha yeye na mtoto wake.
Alihofia mtoto wake kupata kichomi lakini hakuwa na la kufanya ilibidi aendelee na safari yake hadi kituoni ambako alisimama peke yake akisubiri magari lakini halikupita gari lolote kuelekea mjini, alisongea pembeni na kujikinga mvua chini ya mti na kuendelea kusubiri gari ambalo lingepita.
Akiwa katika dimbwi la mawazo ghafla alishtukia gari moja likipita kwa kasi kubwa na mbele kidogo lilisimama na kuanza kurudi kinyumenyume, Belinda alipoliona alijua ni msamaria mwema amemwona yeye na mtoto wake akawahurumia na kuamua kuwapa msaada wa usafiri.
Alianza kukimbia kulifuata gari hilo wakati likirudi nyuma, alipolifikia alizunguka upande wa dereva na kuinamisha kichwa chake ili aongee naye lakini dirisha liliendelea kufungwa ilionekana watu waliokuwa ndani walikula kiyoyozi cha kasi, dakika moja baadaye Belinda akiendelea kulowa dirisha lilianza kufunguliwa taratibu.
Hakuyaamini macho yake kwa alichokiona ndani ya gari hilo, kulikuwa na watu wanne na kila mmoja wao alikuwa ameshika chupa ya bia mkononi mwake! Walionekana ni watu waliolewa na waliongea kwa sauti ya juu kupita kiasi!
“Wee kuku unakipeleka wapi hicho kifaranga chako?”
Ilikuwa ni sauti ya dereva na sauti hiyo haikuwa ngeni kabisa masikioni pa Belinda ingawa dereva mwenyewe alivaa kofia kubwa iliyofunika uso wake na aliongea akiwa ameinamisha kichwa sababu ya kulewa!
Wasichana wote ndani ya gari hilo walicheka kusikia mwanamke mwenzao anaitwa kuku!
Dereva alivua kofia yake ndipo Belinda alipotambua alikuwa ni David kaka yake wa kambo! Nyuma alikaa mdogo wake John naye akiwa amekumbatiwa na msichana mrembo kupita kiasi! Kila mtu alikuwa na chupa ya bia mkononi mwake.
“Ingia kwenye buti tukupe lifti kifaranga chako kitapata kichomi!” Lilikuwa ni tusi jingine tena kwa Belinda kutoka kwa mtu waliyechangia naye baba, roho ilimuuma sana Belinda ukizingatia mali zilizowatia kiburi zilikuwa ni za baba yao wote.
“Mpenzi ondoa gari bwana nini achana na kichaa huyo!” mrembo aliyekaa pembeni kwa David alisema na gari lilianza kuondoka kwa kasi likimmwagia Belinda matope mengi! Alisikia kitu kama miba kikimchoma moyoni mwake yalikuwa ni maumivu ya moyo! Akajikuta amekaa chini kuanza kulia.
Belinda aliona dunia kwake ni kama jehanamu, alikuwa akiadhibiwa kwa kosa ambalo hakulielewa, kila upande ulikuwa umemgeukia yeye hakuwa tena na mahali pa kukimbilia, alijihisi kuwa na mkosi.
“Ee Mungu kwanini mimi tu?”Belinda alijiuliza huku akilia machozi.
Sekunde chache baadaye akiwa amekaa chini mvua ikiendelea kumnyeshea, alisikia honi nyuma yake, kumbe alikuwa katikati ya barabara bila kufahamu, gari hilo lilikuwa ni daladala!
“Huyu sijui chizi?” Dereva aliwaambia abiria waliokuwa ndani ya gari.
“Inawezekana ni chizi kweli?” ”Piiiii!Piiiiii!Piiiii!” Dereva alizidi kupiga honi.
Belinda alijinyanyua taratibu kutoka katikati ya barabara huku akipunga mkono kumwomba dereva asimamishe gari ili apande lakini dereva aliondoa gari bila kujali, alisimama aliposikia kelele za abiria zikimwomba asimame na kumsaidia Belinda na mtoto wake.
“Simama bwana umsaidie hata kama ni chizi ana mtoto mdogo anayelowa na mvua!” Mama mmoja aling’aka ndani ya gari.
Gari lilisimama na Belinda alikimbia mbio na kupanda ndani ya gari, nguo zake zilidondosha maji kiasi cha kuwalowanisha abiria wengine ndani ya daladala hilo! Wengi walifoka na watu wote waliokuwa karibu yake walilalamika vibaya, kabla hajakaa vizuri kitini dereva alisikika akipiga kelele kwa sauti ya juu!
“Jamani ajali!Gari linadumbukia darajani!”
Kufuatia sauti hiyo abiria wote walitupa macho yao mbele kuangalia ni kitu gani kilikuwa kimetokea, Belinda alikuwa miongoni mwa watu waliofanya jambo hilo kweli gari lilikuwa darajani tena ndani ya maji ya mto uliokwenda kwa kasi ni sehemu ya juu tu iliyoonekana.
Dereva alipolifikia daraja alilisimamisha gari pembeni na watu wote walishuka na kukimbia darajani kwenda kuona kilichotokea hata Belinda alifuata nyuma akiwa na mtoto wake mgongoni mvua ilikuwa bado ikinyesha!
“John tuna kamba kwenye gari?” Dereva alimuuliza konda.
“Ndiyo!”
“Itoe ili tujaribu kuvuta hii gari tuone itakuwaje inawezekana kuna watu ndani!”
“Poa Suka!”
Dereva na utingo wake walikimbia kwenda mahali lilipokuwa gari na dereva aliligeuza na kuanza kulirudisha kinyumenyume kuelekea darajani, mita kama kumi hivi alilisimamisha na likafungwa kwa kamba na kuanza kuvutwa!
*Je, nini kitaendelea?*