the_legend
JF-Expert Member
- Jan 14, 2019
- 1,612
- 7,117
Hahahahahaa, Belinda mwenzako alikua hawapangi foleni, mpaka kutufanya tutamani kuacha vikao. Shunie Mungu anakuona ujue[emoji23]Tupo bwana weeeh
the Legend☆
Hahahahahaa, Belinda mwenzako alikua hawapangi foleni, mpaka kutufanya tutamani kuacha vikao. Shunie Mungu anakuona ujue[emoji23]Tupo bwana weeeh
Umetoa ya moyoni...Hahahahahaa, Belinda mwenzako alikua hawapangi foleni, mpaka kutufanya tutamani kuacha vikao. Shunie Mungu anakuona ujue[emoji23]
the Legend☆
Hahahahahahaha, nlijua tu utatia neno hapaUmetoa ya moyoni...
Maji yamezidi unga..nilimwambia ukaniona mie oya oya... haya sasa kula mrututu!
Sent using Jamii Forums mobile app
Umetoa ya moyoni...
Maji yamezidi unga..nilimwambia ukaniona mie oya oya... haya sasa kula mrututu!
Sent using Jamii Forums mobile app
Kivuruge kwenye ubora wakoHahahahahahaha, nlijua tu utatia neno hapa
the Legend☆
*Sehemu ya 21*
“Kijana nakuonea huruma sana lakini inabidi tu nitimize wajibu wangu wa kukuchoma sindano hii ya sumu, nisamehe sana kukuondoka duniani, haya si mapenzi yangu!” Alisema mzee nyonganyonga kabla hajamchoma sindano hiyo.
“Choma tu mzee!” Prosper alisema kwa sauti ya unyonge lakini mawazo yake yalikuwa kwa Belinda na mwanae alijua kifo chao kingekuwa cha mateso kuliko chake!
“Haya moja! Mbili….tat….!”
Prosper alilala juu ya kitanda cha chuma pembeni yake akiwa amesimama mzee Nyonganyonga ambaye kazi yake ilikuwa ni kuondoa uhai wa binadamu wenzake!
Alilipwa mshahara mkubwa kwa kazi hiyo, prosper alishangaa kuona mzee huyo hamchomi sindano ingawa alikuwa nayo mkononi mwake na muda wa yeye kuchomwa ulishafika alishindwa kuelewa ni kwanini mzee huyo alishindwa kutelekeza wajibu wake.
Prosper alitamani kufa hakutaka kuishi zaidi aliogopa sana kupambana na tatizo la ugojwa wa Ukimwi uliokuwa mbele yake, aliamini hakuwa na uwezo wa kuyastahimili matatizo yanayoambatana na ugonjwa huo!Alijilaumu kwa uamuzi wake wa kukubali kushiriki maisha ya kishoga na mfungwa mwenzake Savimbi ambaye ndiye aliyemwambukiza ugonjwa huo.
“Natamani nisife! Napenda niishi na familia yangu lakini sipo tayari kushuhudia nikikonda taratibu hadi kifo changu!”
Aliwaza prosper na aliponyanyua uso wake kumwangalia mzee nyonganyonga alishangaa kukuta sindano ikiwa imezama tumboni kwake mwenyewe.
“Nime…cho….shwa na ….kazi ya ku…..ua ….bina…damu wenza…..ngu!
Nita…..mwe..leza nini Mu….ngu ni heri nife sitaki kuitoa roho yako wa sababu huna hatia!” alisema mzee nyonganyonga akiangakua chini na mwili wake kukakamaa na ulimi kutoka nje.
“Mzee nyonganyonga umefanyua nini sasa? Kwanini umejiua wewe wakati ni mimi ninayestahili kufa?”
Aliuliza prosper huku akipiga kelele alishindwa kufanya lolote kwa sababu alibanwa na mashine mikononi na miguuni, alianza kupiga kelele kuomba msaada na muda mfupi baadaye waliingia maaskari wawili mmoja akiwa na barua mkononi.
“Vipi kimetokea nini tena?”
“Hata mimi nashangaa nilikuwa nimefumba macho nikisubiri kuchomwa sindano lakini mzee nyonganyonga hakufanya hivyo na nilipofumbua nilikuta sindano imezama tumboni mwake na akaanguka chini!”
“Kweli?”
“Ndiyo! Sasa mnafikiri ni mimi ndiye nimemchoma?”
“Hapana siyo hivyo ila….!”
“Ila nini?” ”Basi tuyaache hayo kakueleza kitu chochote kabla hajajichoma?”
“Alipaanguka chini alianza kusema maneno ingawa kwa shida!”
“Alisema maneno gani?”
“Alisema amechoshwa na kazi ya kuua binadamu wenzake na hakuwa na jambo la kumjibu Mungu!”
“Mungu wangu! Sasa kwanini asingesema tu akabadilishiwa kazi?”
Prosper alibaki ameduwaa akiwashangaa maaskari walionekana kupigwa na mshangao mkubwa na hawakujua ni nini cha kufanya, mzee nyonganyonga alikuwa amelala chini sakafuni, mikono na miguu yake ikiwa imenyooka kuelekea darini! Macho na ulimi wake yakiwa yametoka nje alitisha na picha hiyo ilimuonyesha prosper ni kifo cha aina gani ambacho angekufa.
Aliogopa kupita kiasi na kujikuta akitetemeka mwili mzima lakini kwa sababu alishaamua kufa ili kukwepa mateso ya gonjwa la Ukimwi prosper aliamua kuipuuzia picha aliyoiona sakafuni na kuwageukia maaskari waliokuwa ndani ya chumba hicho.
“Afande!” Aliita na maaskari wote waliokuwa wameinamisha nyuso zao chini wakiushangaa mwili wa mzee nyonganyonga uliolala sakafuni waligeuka kumwangalia.
“Unasemaje prosper?”Wote waliuliza kwa mpigo.
“Sasa mtafanya nini?”
“Kuhusu?” ”Mimi nataka kufa!”
“Hautakufa tena prosper bado una siku nyingi sana za kuishi!”
”Si uchukue hilo bomba la sindano uvute dawa nyingine unidunge kipi kinachokushinda kama mnaogopa basi nitoeni hapa kwenye mashine nijidunge mwenyewe!”
“Haiwezekani tena prosper serikali imeamua kusitisha hukumu ya kifo uliyopewa tena una bahati nafikiri Mungu alikuwa hajapanga ufe kwa sababu mkeo amefika hapa na barua zikiwa zimebaki sekunde ishirini tu!
Hapakuwa na njia yoyote ya kuwahi kama mzee Nyonganyonga asingejiua mwenyewe!” alisema mmoja wa maaskari.
“Ni nini mnasema nini nyinyi mbona siwaelewi?”
“Barua ni hii hapa imetoka kwa mwanasheria mkuu wa serikali hivyo haiwezekani kukuchoma sindano tena!”
“Hebu niione hiyo barua!”Alisema prosper kwa ukali kiasi kwamba maaskari walishindwa kumwelewa kwa sababu alitakiwa kufurahia kukwepa kifo akiwa juu ya kitanda cha mauti.
Askari aliyekuwa na barua hiyo mikononi alimsogezea prosper na kuifungua, prosper alianza kuipitia taratibu tangu mwanzo hadi mwisho wa barua lakini badala ya kufurahia alianza kupiga kelele.
“NATAKA KUFA!NATAKA KUFA! MIMI NATAKA KUFA SITAKI TENA KUISHI!” aliongea kwa sauti ya juu huku akijaribu kujitoa kwenye mashine iliyoshika mikono na miguu yake.
Maaskari waliamua kumfungua prosper akatoka kitandani na kusimama wima, wakiwa hawa hili wala lile maaskari walishtukia prosper anatimua mbio kulifuata bomba lililokuwa chini lengo lake likiwa ni kujichoma nalo ili afe alilifikia na kulishika lakini kabla hajalinyanyua na kutimiza azma yake mguu wa askari ulisimama juu ya kiganja chake prosper alipiga kelele sababu ya maumivu aliyoyapata.
“Kwanini unataka kufanya hivyo lakini yaani badala ya kufurahia amenusurika kifo kimiujiza unataka kufanya ujinga?”
“Braza mimi ni mtu mzima na akili zangu ukiona nataka kufanya jambo jiulize mara mbili kuna tatizo gani, hakuna mtu anayetaka kufa binadamu wote tunapenda kuishi! Kwa hiyo niache mimi nifanye ninavyotaka!”
“Haiwezekani! Afande hebu mtoe huyu chumbani mpeleke katika chumba cha washauri nasha nafikiri utakuwa na tatizo ambalo ni vyema tukalifahamu!”
Askari magereza alimshika mkono prosper ambaye wakati huo aliendelea kulia mfululizo na kutoka naye hadi nje ya chumba cha kifo mbele kidogo aliingia naye katika chumba kilichoandikwa mlangoni “Ushauri Nasaha!” ambao walimkuta mama wa makamo akiwa amekaa nyuma ya meza kubwa.
“Vipi tena?”
“Hukumu yake ya kifo imesitishwa na serikali baada ya kugundulika dakika chache kabla ya kifo kuwa hakutenda kosa lililopelekea apewe hukumu hiyo!”
“Hongera sana kijana nakushauri ukitoka hapa uwe mwema mbele za Mungu kwani amekupa nafasi nyingine ya kunyoosha njia zako unasikia?”
“Usinipe hongera mama mimi sitaki kuishi na kama kuna uwezekano wa kuniua sasa hivi fanyeni hivyo haraka kwani nitajiua mwenyewe!”
Jipu la prosper lilimshtua mtoa ushauri nasaha, aligundua prosper alikuwa na tatizo kubwa lililohitaji muda mrefu wa kuongea naye!
“Kwanza hebu tufahamiane mimi naitwa mama Mpelumbe wewe mwenzangu unaitwa nani?” Mama huyo alianzaia mbali kidogo.
“Naitwa prosper!”
“Aisee wewe ndiye prosper?”
“Ndiyo mama ni vizuri ukiniita marehemu prosper sababu tayari nimeshakufa! Mimi ni maiti inayotembea!” ”Unamaanisha nini mwanangu?”
“Yaani mama hunielewi ninaposema mimi ni maiti inayotembea!”
‘Sikuelewi hata kidogo!”
“Na si mimi tu hivi sasa vijana wengi ni maiti zinazotembea! Ndiyo maana nataka kufa kwa sababu yaliyoko mbele yangu sitaweza kuyahimili!” ”Unamaanisha nini?”
Badala ya kujibu swali prosper aliyekuwa ametulia alianza kulia machozi.
Belinda alikaa nje ya gereza na mtoto wake mgongoni akiendelea kulia machozi!Alishangaa ni kwanini maaskari walichelewa kiasi hicho kurudi kutoka ndani, alijua kwa vyovyote mume wake alikuwa amekufa! Mawazo hayo yalimzidishia huzuni aliamini asingeweza kupambana na maisha peke yake aliumia juhudi zake zote za kumuokoa prosper zilikuwa zimegonga mwamba.
*Je, nini kitaendelea?*