bayona_stories
Member
- Apr 19, 2023
- 77
- 124
- Thread starter
- #61
Nasubilia hiyo sehemu ya mwisho
Tayari zote nshaweka
Nasubilia hiyo sehemu ya mwisho
Sawa nitasomaSoma haina kusubirishana hii kaanza na kashaimaliza yote
KaribuSawa nitasoma
Asante
Nzuri! UnitahKulikuwa na kijana mmoja aliitwa Prince, alikuwa ni bodaboda aliyekuwa jirani yetu, tulikuwa tunamwamini na hata kumpa baadhi ya mizigo yetu ya msingi atupelekee mahali tulipotaka ifike.
Huu ni utaratibu wa kawaida kwa familia zetu za mjini. Kwa sababu tulimuamini, mke wangu alikuwa akimtumia sana katika safari zake, mimi kiuhalisia sikuwa nikimtumia maana mm sio mtu wa kukaa nyumbani, niko bize na kazi zangu, nilimtumia tu pale ambapo labda niko nyumbani na nahitaji kufikisha mzigo fulani mahali na mke wangu ndiye aliyekuwa akinisuggestia kuwa tumpigie Prince apeleke, ndo maana mimi nilikuwa nikimuona kama bodaboda wa mke wangu.
Basi mke wangu yeye katika safari zake zote kila alipotaka kwenda, ni kumpigia prince aje ampeleke. Karibia safari zote za mke wangu Prince alikuwa akizijua, na mimi binafsi sikuwa na wasiwasi na prince kwa sababu hiyo ni biashara kama biashara nyingine na mtu hufanya biashara na anayemuamini. Hata baada ya kuja hizi Bolt na Ubber ambazo mtu akifanya request
gharama zinakuwa chini kuliko gharama za bodaboda wa kawaida, lakini bado mke wangu yeye aliendelea kumtumia Prince kwenye safari zake ijapokuwa nilimshauri hilo, pia haikuwa shida kwangu maana niliona sio mbaya as long as prince ni mtu tunamuamini
Sasa ikafika hatua prince akawa family friend, akawa anakuja nyumbani kama siku za mechi hivii, anakuja kuangalia mechi za Ulaya tunafurahi maisha yanaendelea na mambo mengine madogo madogo tunapiga tu story kawaida.
Basi ilitokea hiyo siku moja nimesafiri nimeenda mkoani, Nipo huko usiku mida ya saa nne hivi, nilikuwa hotelini ambapo nilikuwa nimefikia na ilikuwa ni safari ya kikazi, Basi nikapokea simu kutoka kwa dada mfanyakazi wa pale nyumbani, akaniambia kaka kuna vurugu hapa ndani, Prince anagombana na dada (mke wangu) nikawa namuuliza shida ni nini?
Alikata simu maana hata kunipigia alikuwa anaongea kiuogauoga. Napiga tena akawa hapokei
Niliwaza ni nini kinachoendelea huko nikawa sielewi. Ugomvi wa mke wangu na Prince umeanzia wapi? Na Prince anatafuta nini hapo nyumbani usiku wote huo? Niliwaza sana nafanya nini nikawa sielewi.
Nilimpigia mke wangu na yeye akawa hapokei simu kabisaa, nikampigia huyo huyo Prince na yeye akawa hapokei simu. Niliwaza sanaaa, lakini sipati majibu nifanyeje. Nilimpigia rafiki yangu Amoni anisaidie kufika nyumbani aangalie kuna nini kinachoendelea.
Amoni mara ya kwanza hakupokea, nikaelewa ni kwa sababu ni usiku sana, yawezekana amelala.
Baadaye nikampigia tena, akapokea namuuliza kama yupo kwake ananiambia yupo club, halafu
sasa hiyo club ni mbali na nyumbani, nikamwambia atoke nje sehemu iliyotulia tuongee mara moja.
Akasema sawa. Nasubiria atoke nje anipigie jamaa hapigi, nikasubiria sanaa Ikabidi nimpigie tena, hapokei, nampigia mara ya pili ndo akapokea akaniambia anatoka nisubirie mara moja,
Basi ndo akawa ametoka akanipigia, kumbe ameshalewa hadi kulewa ndo sababu ya usumbufu wote
Nikamuuliza kwani uko nani akanitajia washkaji wengine aliokuwa nao nikamwambia anipe fulani niongee naye, akaingia ndani na kumcheki akamtoa nje ndo nikaongea naye, bahati nzuri yeye.
alikuwa hajalewa na nililijua hilo ndo maana nikamwambia nipe fulani, basi huyo jamaa nikamueleza kinachoendelea, nikamuomba anisaidie kufika nyumbani haraka kuangalia usalama maana hapa nimeshajaribu kila namna,. Nimecheki hadi jirani yangu mmoja hivii naona ameshalala,
Jamaa akasema sawa sawa ngoja tuelekee huko, Alimchukua Amoni na pombe zake wakaenda nyumbani kwangu njiani akawa anamueleza Amoni kinachoendelea, Sasa walienda wakafika kwangu wakakuta kuko kimya, watu wote wamelala Ikabidi wagonge mlango.
Waligonga na kugonga lakini wapi, hakuna mtu anafungua mlango wakajaribu kuita lakini wapi kuko kimya, sasa wasiwasi wao ukawa ni hawaelewi kuna watu humo ndani au hakuna mtu, walimuita sana mke wangu lakini hakuna anayeitika humo ndani, waliogopa hata kunieleza kinachoendelea ila ilibidi tu wanipigie na kuniambia kuwa waligonga mpaka kidogo wavunje mlango lakini hakuna hata mmoja anayetingishika.
Sasa hawaelewi kuna nini kinachoendelea niliwaambia, sasa fanyeni hivii, muibukieni Prince. Nendeni kwake, mfikieni mjue nini kinachoendelea Walienda kwa Prince walifika kwake wakagonga mlango ukafunguliwa, unafunguliwa anatoka rafiki yake Prince wakamuuliza prince yuko wapi, Akawajibu Prince tangu alipoondoka hapa saa mbili hajarudi mpaka saivi, Wakamuuliza kama hakuna mahali anahisi atakuwepo, akasema hapana, maana yule ni bodaboda anaweza kuwa mahali popote kulingana na wateja wake.
Wakamwambia basi fanya hivii, mpigie simu Jamaa akampigia simu Prince, simu ikaita lakini haipokelewi.
Akapiga tena haipokelewi, Alipopiga mara ya tatu simu ikawa haipatikani, ikiwa na maana Prince amezima simu Walichokaa, wakanipigia simu kunielezea yote hayo ambayo yametokea, nilichoka piaa. Wakati huo mke wangu naye simu haipatikani tena, dada wa kazi yeye hapokei.
Nini kinachoendelea hapaaa? Mke wangu na dada wa kazi wako wapi?! Zile zilikuwa ni vurugu za nini?
Prince na yeye kaenda wapi? Maswali yote haya nilijiuliza bila kuwa na majibu yake, marafiki zangu waliniomba niwaruhusu wakapumzike kwanza, kesho asubuhi na mapema wataamka na hilo iIlikuwa ngumu kuwaruhusu waende kwao kupumzika, lakini hata nikiwakatalia, wabaki waendelee kufanya nini maana huo ulikuwa ni usiku wa saa saba tayari.
Usikose sehemu ya pili ya story hii maana hayo maswali ambayo uko nayo moyoni mwako yatajibiwa yote.
Baki na mimi hapa hapaa
Hahaha ole wake aukatishe utamu siyoSa ole wako usituletee muendelezo.


Eeh yani ole wake.Hahaha ole wake aukatishe utamu siyo![]()
Sawa ccy😘😘😘Shukrani sana sis nimefika!
Asante mtani
Karibu sana mtani upunguze machungu ya kudraw kiume jana 😂Asante mtani
Sisi ni majabali ya soka 😆 😆Karibu sana mtani upunguze machungu ya kudraw kiume jana 😂
😂 simba guvu mojaSisi ni majabali ya soka 😆 😆
Aight 😘😘Thanx sisy
Bonge la story la kutisha.BODABODA WA MKE WANGU 3
( THE LAST EPISODE )
Kutokana na ukaribu wa mara kwa mara ambao mke wangu alikuwa nao na huyo Dereva wake wa bodaboda, zilianza kujengeka hisia katikati yao, zilianza kama utani, wakitaniana mambo ya kimapenzi lakini sasa ikafika
View attachment 2609156
hatua hisia zao zikawa more serious, marafiki zake Prince (huyo dereva wa bodaboda) walikuwa kila siku ni kumcheka jinsi ambavyo mtoto anaonekana kumuelewa lakini yeye anakuwa muoga. Bodaboda wenzake walimuona zuzu sana kwa sababu amekuwa na ukaribu mnoo na mke wangu mpaka wote
wanaonyeshana hisia za kupendana lakini yeye anakuwa muoga kisa mimi mume wake huyo mwanamke, walimwambia unapaswa kuhit and run, huyo ni mke wa mtu lakini anajilengesha kwako kila siku halafu wewe umezubaa.
kibaya zaidi ni kuwa huyo mke wangu alikuwa ni mzuri sanaaa, sasa na
hiyo marafiki zake wakasimama nayo kama point kumshangaa huyo Prince anavumilia vipi, na Wakamwambia hizo chance ni mara moja kwa life time, huwezi pata tena, japo pia wapo wengine ambao walimuonya asiwasikilize hao.
Kitu nilichojifunza hapa ni kuwa, hakuna jambo baya kama mke wa
mtu kuruhusu mazoea na mwanaume mwingine, hilo jambo ni hatarii mnoo japo sio mara zote litakuwa hatari, maana mke wangu na Prince walianza na uteja kama kawaida, yaani mke wangu alikuwa mteja mzuri wa Prince, safari zake anamuita Prince ampeleke, lakini ile kuwa na free time
mara kwa mara, akitaka kwenda huku yuko naye kule yuko naye, hakuna bodaboda yeyote tofauti anayemtumia mpaka sasa ikafika hatua jamaa akawa family friend anaweza kuja nyumbani muda wowote na akaondoka muda wowote, binafsi mm hata mara moja sikuwahi kuhisi kama kuna kitu kitakuja
kutokea, nilikuwa nikimuamini sana Prince na mke wangu nilimuamini pia. Kumbe mazoea yao yalikuja kuzaa mapenzi. Maana sasa prince aliona anachoshauriwa na marafiki zake ni kweli, na kwanza isitoshe yeye mwenyewe kwa muda mrefu sana amekuwa akitamani ni vile tu aliniogopa mimi
Yote hayo nilisimuliwa na rafiki yangu Amoni ile siku nimekuja kutoka safarini huko mkoani.
Wakati nipo njiani nilimpigia na kumueleza kila kitu kuhusu mazungumzo yangu na yule dada wa kazi, nikamwambia jinsi ambavyo nimegundua mke wangu kuna kitu kikubwa sanaa ananificha
Nina hasira sanaa na ninaenda kujua ni kitu gani hicho japo ninasuspect cheating hapo. Na kwa kweli moyo unaniuma mnoo, mke wangu nilimuamini sanaa. Amoni akaniambia, kabla hujafika kwako njoo upitie kwanza kwangu kuna file la mke wako ninalo.
Nilishtuka sanaa, nikamuuliza file
gani? Akaniambia straight, file la mke wako na huyo Prince.
Nilihisi kuchanganyikiwa yaani, niliendesha gari kama kichaa, mpaka ikanipelekea kusumbuana na traffic police huko njiani, lakini ni kwa sababu stress zilikuwa ni nyingi kichwani.
Nilifika kwa Amoni, Akaanza kunieleza
Kuwa baada ya kuondoka kuongea na mke wangu na akaona jinsi ambavyo kuna kitu mke wangu anaficha (kama tulivyoona sehemu iliyopita) plus na zile doubt alizokuwa nazo
Aliwaza, akaamua kumtafuta mshikaji wake ambaye alikuwa ni bodaboda wa kile kile kituo cha Prince, lakini pia na
yeye alikuwa na ukaribu na Prince, alimpigia simu akamuomba wakutane, ile wamekutana kwanza akampiga castle lite tatu, jamaa alikuwa ni mpenzi sanaa wa castle lite
Halafu ndo akamuuliza sasa anafahamu vipi kuhusu Prince na mke wangu
Inshort alimtengenezea mazingira mazuri ya yeye
kuropoka kila kitu. Ndo jamaa akamsimulia kila kitu kama nilivyozungumza hapo awali, kumbe jamaa alikuwa anawasimulia yote yanayoendelea ili kuwaonyesha yeye sio mnyonge.
Na kumbe hata ule usiku wamekuja kugonga nje mlangoni, Prince alikuwepo ndani.
Sasa ndugu msomaji
kuhusu zile vurugu zilikuwa zinahusu nini ambazo hadi dada alinipigia simu, hilo nitakuachia mwenyewe kutafsiri.
Ila ukweli ni kuwa usiku huo Prince alilala humo ndani na asubuhi na mapema akarudi kwake, akaenda kuwasimulia washikaji zake baadaye pale kijiweni
Baada ya rafiki yangu Amoni kunisimulia hayo yote. Jasho lilikuwa likinitoka na imagine sipati picha, Speed ya kwanza nilifikia kwa Prince kabla ya kwenda kwangu baada ya kutoka kwa Amoni.
Nilifika nikaambiwa Prince amehama, jana usiku kaondoka na vitu vyake.
Kumbe mke wangu alipomueleza kuwa nimejua aliona hiki ni kifo, alihama usiku huo, sijui alihamia wapi kwa haraka kiasi hicho.
Nilijaribu kuwauliza kama wanafahamu alikohamia majirani wote hakuna anayefahamu.
Ndipo Amoni akaniambia, huyo hajahamia sehemu bado ila atakuwa
kwa washikaji zake, issue ni kujua yupo kwa nani. Ilibidi tuachane naye nikadeal na mke wangu anieleze vizuri hili.
Nilienda mpaka nyumbani namkuta dada wa kazi peke yake, mke wangu hayupo.
Akaniambia dada ameondoka,
Sijui kaenda wapi, ila hakuwa sawa kabisaa Na amekataa
Kuniambia anapoenda
Wazo lililoniijia haraka haraka ni kuwa ametoroka na Prince.
Hakya Mungu nilitamani njiripue.
Nilienda kwa kila niliyemjua ni mtu wa karibu wa Prince anieleze Prince yuko wapi na mke wangu lakini wote hakuna aliyenipa jibu la Prince alipo, japo nina uhakika
Katika wote wale niliowapitia yupo mmoja ambaye alikuwa akijua Prince alipo, ni vile tu huwezi jua ni nani.
Niliamua kupiga simu nyumbani kwao mke wangu, wakasema hayupo huko, ikabidi niwaeleze kwa ufupi kinachoendelea, na wao wakaanza kuhaha huko, nikajua kabisaa huyu kaenda na
Prince kweli, kama hata kwao hawajui alipo. Baadaye kidogo nikapokea simu ya dada yangu ananiambia mke wangu yupo kwake analia tangu amekuja, ananiomba mimi msamaha na anasema nimtafute mume wake,
Ikabidi niende kwa dada nimeenda nikamkuta kumbe yupo huko, na kumbe kashamueleza
dada kila kitu, akikiri makosa yake na kuomba msamaha
Nikamueleza dada aibu hii yeye angekuwa ndio mimi angeivumilia vipi?!
Nikamwambia dada, hii aibu mimi siwezi ivumilia na huu ukatili niliotendewa na huyu mwanamke ni kama mauti.
Wakati tunaendelea kuongea, ndugu zake mke
wangu walinitafuta kujua nimefikia wapi kumpata mtoto wao, na walinipigia wakiwa kwangu kumbe na wao walikuwa wanahangaika kumtafuta tangu pale nilipowapigia kuwaeleza kupotea kwa mke wangu.
Nikawaambia njooni huku kwa dada ndio yupo huku, niliwaelekeza kwa dada ni wapi wakafika
Niliwaambia kila kitu from A to Z. Hadi wao walijiskia aibu sana kwa kile alichokifanya mtoto wao, wakamuombea msamaha maana alikuwa akilia tangu wamekuja anaomba tu msamaha.
Mimi niliwaambia ni ngumu kuuforce moyo ambao umevunjika namna hii eti uanze kumpenda mtu tena, naomba
Mchukueni mwende naye, siku nikiwa tayari kurudiana naye nitakuja kumchukua.
Na hiyo ndo ilikuwa my final say baada ya mazungumzo yote.
Waliondoka naye, hakutaka kuchukua kitu chochote nyumbani aliondoka hivo hivo, akisubiria hasira zangu ziishe.
Mpaka sasa bado nasubiria moyo
Wangu ukiwa tayari kuwa naye, ndipo nitaenda kumchukua.
Ila kwa alichonitendea, itachukua muda mrefu sana kumsamehe arudi nyumbani.
Eeh bhana sina la ziada. Mwisho wa story yetu
Hatma ya dada wa kazi je? Ameondoka au bado yupo?Ipo ya mwisho nshaweka tayari
Ngoja nitulie nisome.