Simulizi: Bodaboda wa Mke wangu

Simulizi: Bodaboda wa Mke wangu

Hii story niliikuta Twitter......kama ni wewe mtunzi basi hongera kwako....ila kama umeamua kuileta huku ili kusambaza ujumbe usiisahau kutoa credit kwa mtunzi...

Ndio mm mtunzi. [mention]bayona_stories [/mention] The story writer. Nipo twitter, instagram, tiktok, YouTube na huku jamii forums kwa hii hii username.
 
BODABODA WA MKE WANGU 2

Asubuhi na mapema nampigia Amoni rafiki yangu namwambia aende nyumbani kwangu haraka, kama alivyoniahidi kuwa nimruhusu apumzike na asubuhi na mapema wataamkia kwangu kuangalia usalama.
Alienda peke yake nyumbani kwangu


IMG_7854.jpg






Alienda na kufika nyumbani kwangu alimkuta mke wangu yupo pale nyumbani, akaongea naye kuhusu ilivyokuwa jana na jinsi ambavyo waligonga mlango hakuna aliyefungua wala anayejitingisha humo ndani, akamuuliza kuna usalama wowote na nini kinachoendelea?!

Sasa kabla hajafika na kumuuliza, mimi nilikuwa nimeshampigia tena mke wangu kabla. Yaani baada ya kumpigia Amoni akaenda nyumbani kuona usalama ukoje, nilimpigia tena mke wangu ambaye tangu jana alikuwa hapatikani baada ya kumpigia mara ya kwanza asipokee, safari hii akapokea

nilishtuka kuona kapokea, atleast naweza kujua kinachoendelea.
Nikamuuliza kuna nini huko mbona tangu jana sikupati na wala simu yangu hupokei?
Akaniambia jana alichoka sanaa hivyo alilala mapema sanaa na simu yake haikuwa na chaji hivyo ilikaa on na baada ya muda ikajizima kwa

chaji kuisha.
Sasa binafsi mwanzo sikuwaza kama kunaweza kuwa na kitu cha yeye kunificha, nilikuwa nikimuamini sanaa, na hata hili la kutokumuambia kuwa nilipigiwa na dada wa kazi akaniambia kuna vurugu huku sio kwamba nilikuwa nimepanga kumficha, ila nilianza tu taratibu

kuwa mbona jana ulikuwa hupokei simu na baadaye kutokupatikana ili anielezee yeye mwenyewe tatizo, maana mimi nilichokifikiria ni kutakuwa na tatizo, japo niliwaza sana bila kupata majibu kuwa ni matatizo gani huyo jamaa anaweza kuyaleta hapo nyumbani maana ni mtu tunayemuamini

vizuri tu.
Basi aliponiambia vile halafu akawa hajanieleza chochote, ilibidi ninyamaze kwanza nisimuelezee kuwa dada wa kazi alinipigia halafu akawa hajanielezea vizuri akakata simu.
Nilimwambia sawa haina shida, tukazungumza mazungumzo mengine, ila sikuwa sawa hata kidogo

moyoni mwangu nikawa nikijiuliza ni kitu gani huyu mke wangu ananificha hapaa.

Na sasa rafiki yangu Amoni anafika kwangu na kuanza kumuelezea mke wangu kilichotokea jana, anataka afahamu shida ni nini ili akanieleze.
Mke wangu alishtushwa sanaa na kile ambacho alikiskia kutoka

kwa Amoni, akakumbuka jinsi alivyonidanganya kwenye simu kuwa hakuna shida yoyote ni simu tu haikuwa na chaji na yeye alikuwa ameshalala.
Sasa huo mshtuko Amoni ndiye aliyeuona vizuri na kunisimulia kuwa mke wako baada ya kumuelezea kuhusu kilichotuleta jana usiku na akashindwa

kufungua mlango, ameonekana kushtuka mnoo ndo mimi nikaelewa sababu ya kushtuka kwake ambayo ni kama nilivyowaeleza.
Mke wangu alimwambia Amoni kuwa yeye alikuwa amelala na alikuwa na usingizi sana, sauti aliziskia lakini hakujua ni za akina nani hivyo hakutaka kufungua kabisaa

hivyo ikabidi akae kimya.
Sasa Amoni akamuuliza kwani dada huyu (dada wa kazi) hakutufahamu kuwa ni sisi akafungua au na yeye alikuwa anausingizi kama wewe? Alimjibu kuwa, alishagamzuia kufungua mlango kwa mgeni yoyote usiku wakiwa wameshalala tayari.
Basi, akamwambia kuwa

usalama upo wala asiwe na wasiwasi, na kuhusiana na suala hilo la vurugu za yeye na Prince (yule Dereva bodaboda) asijali yeye ataongea na mume wake ila sio issue kubwa.
Na hivyo ndivyo alivyonieleza Amoni baada ya kutoka kwa mke wangu

Sasa Amoni pamoja na na kunielezea yote hayo ila ilibidi pia anielezee mtazamo wake binafsi,
Aliniambia mke wangu kwanza alishtuka nilivyoelezea kilichotuleza nyumbani usiku huo tukigonga na asifungue, jambo ambalo linatia wasiwasi, lakini pia anadanganya kusema alikuwa na

usingizi na kuwa hakujua sisi ni akina nani, kwa sababu mlango tuliugonga kwa nguvu zote lakini hakuna mtu anaitikia, na kwa sababu tulikuwa na wasiwasi kuwa kunaweza kuwa na shida ndani kama ulivyotueleza, tulitaka hadi kuuvunja huo mlango ndo baadaye tukaona tuache kwanza

tukusikilize, ndo ukatuambia twende kwa prince mwenyewe. Huyo mtu anausingizi gani huo? Hata Samaki hawalali hivo. Lakini pia anasema hakujua sisi ni akina nani, hiyo ni uongo kwa sababu tulikuwa tunaita kabisaa “shemeji, ni mimi Amoni” fungua mlango, fungua, kuna usalama huko?”

kiufupi majina yetu tuliyataja hata kama alikuwa hajui sauti kwa sababu ya usingizi basi hata majina yetu angeyaskia.
Akaniambia, mchunguze mke wako, kaka nahisi umepigwaa
Nilichokaa, na muda huo nilipaswa niwe kwenye kikao kwa ajili ya mambo ya kikazi hayo yaliyonipeleka mkoani

Nilichelewa kikao kwa muda mrefu kweli, na pia hata baada ya kuingia, akili yangu haikuwa sawa, nikiwaza mke wangu anakitu gani ananificha.
Kila nikijaribu kuwaza may be kuna cheating ananifanyia kwa huyo bodaboda, naishiwa nguvu, najilazimisha kukataa kuwa haiwezekani Kabisaa

Nilimaliza hicho kikao kwa mbinde na nilirudi hotelini nikiwaza nifanye nini, simu za mke wangu zikawa zinaingia sipokei maana nina hasira sana, kwanini anidanganye au kunificha kitu mimi mume wake, au ananicheat hapaa

Niliwaza na ndipo nilipoamua kumpigia tena dada wa kazi.
Dada alipokea nikaongea naye kitaratibu ili asiogope aweze kunielezea.
Nilimuuliza jana hizo vurugu ulizokuwa unazisema hapo nyumbani uliponipigia ni zipi? Kuna nini kinaendelea?!
Nieleze wala usiogope

Akaogopa kabisa kusema, akaniambia kaka mimi naogopa nikiongea chochote dada atanitoa roho mimi naomba tu wewe mwenyewe umpigie umuulize, ni mke wako yule, akuelezee au wewe mwenyewe fuatilia tu mwenyewe kujua kinachoendelea,
Maana mimi hapa hata sina amani, dada amejua kuwa

nilikupigia simu kukwambia kuna vurugu ndani za yeye na Prince amenigombeza tangu asubuhi ni kunisema na amesema nitarudi nyumbani kwa sababu ya huu mdomo wangu, amenipiga na kunipiga, amenikasirikia sanaa hataki hata kuniona. Naogopa sana na yeye ndo alinileta hapa kufanya kazi

Ilinibidi nikate simu.
Nikajikaza kiume kuhudhuria kikao cha kesho yake ambacho kilikuwa ni cha mwisho
Ambacho kiliisha jioni kabisaa, na hivyo kesho yake asubuhi na mapema nikaanza safari ya kurudi nyumbani, nikiwa na hasara nyingi mnooo

Ukweli unaenda kugundulika katika sehemu inayofuata.
Na tutajua hasa nini kilichokuwa kina endelea huko

Baki na mimi hapa hapa
Kwa ajili ya sehemu ya mwisho
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom