Simulizi: Bodaboda wa Mke wangu

Bwana prince na wife wako sasa
IMG-20230502-WA0010.jpg
 
BODABODA WA MKE WANGU 3
( THE LAST EPISODE )

Kutokana na ukaribu wa mara kwa mara ambao mke wangu alikuwa nao na huyo Dereva wake wa bodaboda, zilianza kujengeka hisia katikati yao, zilianza kama utani, wakitaniana mambo ya kimapenzi lakini sasa ikafika



View attachment 2609156




hatua hisia zao zikawa more serious, marafiki zake Prince (huyo dereva wa bodaboda) walikuwa kila siku ni kumcheka jinsi ambavyo mtoto anaonekana kumuelewa lakini yeye anakuwa muoga. Bodaboda wenzake walimuona zuzu sana kwa sababu amekuwa na ukaribu mnoo na mke wangu mpaka wote

wanaonyeshana hisia za kupendana lakini yeye anakuwa muoga kisa mimi mume wake huyo mwanamke, walimwambia unapaswa kuhit and run, huyo ni mke wa mtu lakini anajilengesha kwako kila siku halafu wewe umezubaa.
kibaya zaidi ni kuwa huyo mke wangu alikuwa ni mzuri sanaaa, sasa na

hiyo marafiki zake wakasimama nayo kama point kumshangaa huyo Prince anavumilia vipi, na Wakamwambia hizo chance ni mara moja kwa life time, huwezi pata tena, japo pia wapo wengine ambao walimuonya asiwasikilize hao.
Kitu nilichojifunza hapa ni kuwa, hakuna jambo baya kama mke wa

mtu kuruhusu mazoea na mwanaume mwingine, hilo jambo ni hatarii mnoo japo sio mara zote litakuwa hatari, maana mke wangu na Prince walianza na uteja kama kawaida, yaani mke wangu alikuwa mteja mzuri wa Prince, safari zake anamuita Prince ampeleke, lakini ile kuwa na free time

mara kwa mara, akitaka kwenda huku yuko naye kule yuko naye, hakuna bodaboda yeyote tofauti anayemtumia mpaka sasa ikafika hatua jamaa akawa family friend anaweza kuja nyumbani muda wowote na akaondoka muda wowote, binafsi mm hata mara moja sikuwahi kuhisi kama kuna kitu kitakuja

kutokea, nilikuwa nikimuamini sana Prince na mke wangu nilimuamini pia. Kumbe mazoea yao yalikuja kuzaa mapenzi. Maana sasa prince aliona anachoshauriwa na marafiki zake ni kweli, na kwanza isitoshe yeye mwenyewe kwa muda mrefu sana amekuwa akitamani ni vile tu aliniogopa mimi

Yote hayo nilisimuliwa na rafiki yangu Amoni ile siku nimekuja kutoka safarini huko mkoani.
Wakati nipo njiani nilimpigia na kumueleza kila kitu kuhusu mazungumzo yangu na yule dada wa kazi, nikamwambia jinsi ambavyo nimegundua mke wangu kuna kitu kikubwa sanaa ananificha

Nina hasira sanaa na ninaenda kujua ni kitu gani hicho japo ninasuspect cheating hapo. Na kwa kweli moyo unaniuma mnoo, mke wangu nilimuamini sanaa. Amoni akaniambia, kabla hujafika kwako njoo upitie kwanza kwangu kuna file la mke wako ninalo.
Nilishtuka sanaa, nikamuuliza file

gani? Akaniambia straight, file la mke wako na huyo Prince.
Nilihisi kuchanganyikiwa yaani, niliendesha gari kama kichaa, mpaka ikanipelekea kusumbuana na traffic police huko njiani, lakini ni kwa sababu stress zilikuwa ni nyingi kichwani.
Nilifika kwa Amoni, Akaanza kunieleza

Kuwa baada ya kuondoka kuongea na mke wangu na akaona jinsi ambavyo kuna kitu mke wangu anaficha (kama tulivyoona sehemu iliyopita) plus na zile doubt alizokuwa nazo
Aliwaza, akaamua kumtafuta mshikaji wake ambaye alikuwa ni bodaboda wa kile kile kituo cha Prince, lakini pia na

yeye alikuwa na ukaribu na Prince, alimpigia simu akamuomba wakutane, ile wamekutana kwanza akampiga castle lite tatu, jamaa alikuwa ni mpenzi sanaa wa castle lite
Halafu ndo akamuuliza sasa anafahamu vipi kuhusu Prince na mke wangu
Inshort alimtengenezea mazingira mazuri ya yeye

kuropoka kila kitu. Ndo jamaa akamsimulia kila kitu kama nilivyozungumza hapo awali, kumbe jamaa alikuwa anawasimulia yote yanayoendelea ili kuwaonyesha yeye sio mnyonge.
Na kumbe hata ule usiku wamekuja kugonga nje mlangoni, Prince alikuwepo ndani.
Sasa ndugu msomaji

kuhusu zile vurugu zilikuwa zinahusu nini ambazo hadi dada alinipigia simu, hilo nitakuachia mwenyewe kutafsiri.
Ila ukweli ni kuwa usiku huo Prince alilala humo ndani na asubuhi na mapema akarudi kwake, akaenda kuwasimulia washikaji zake baadaye pale kijiweni

Baada ya rafiki yangu Amoni kunisimulia hayo yote. Jasho lilikuwa likinitoka na imagine sipati picha, Speed ya kwanza nilifikia kwa Prince kabla ya kwenda kwangu baada ya kutoka kwa Amoni.
Nilifika nikaambiwa Prince amehama, jana usiku kaondoka na vitu vyake.

Kumbe mke wangu alipomueleza kuwa nimejua aliona hiki ni kifo, alihama usiku huo, sijui alihamia wapi kwa haraka kiasi hicho.

Nilijaribu kuwauliza kama wanafahamu alikohamia majirani wote hakuna anayefahamu.

Ndipo Amoni akaniambia, huyo hajahamia sehemu bado ila atakuwa

kwa washikaji zake, issue ni kujua yupo kwa nani. Ilibidi tuachane naye nikadeal na mke wangu anieleze vizuri hili.
Nilienda mpaka nyumbani namkuta dada wa kazi peke yake, mke wangu hayupo.
Akaniambia dada ameondoka,
Sijui kaenda wapi, ila hakuwa sawa kabisaa Na amekataa

Kuniambia anapoenda
Wazo lililoniijia haraka haraka ni kuwa ametoroka na Prince.
Hakya Mungu nilitamani njiripue.
Nilienda kwa kila niliyemjua ni mtu wa karibu wa Prince anieleze Prince yuko wapi na mke wangu lakini wote hakuna aliyenipa jibu la Prince alipo, japo nina uhakika

Katika wote wale niliowapitia yupo mmoja ambaye alikuwa akijua Prince alipo, ni vile tu huwezi jua ni nani.
Niliamua kupiga simu nyumbani kwao mke wangu, wakasema hayupo huko, ikabidi niwaeleze kwa ufupi kinachoendelea, na wao wakaanza kuhaha huko, nikajua kabisaa huyu kaenda na

Prince kweli, kama hata kwao hawajui alipo. Baadaye kidogo nikapokea simu ya dada yangu ananiambia mke wangu yupo kwake analia tangu amekuja, ananiomba mimi msamaha na anasema nimtafute mume wake,
Ikabidi niende kwa dada nimeenda nikamkuta kumbe yupo huko, na kumbe kashamueleza

dada kila kitu, akikiri makosa yake na kuomba msamaha
Nikamueleza dada aibu hii yeye angekuwa ndio mimi angeivumilia vipi?!
Nikamwambia dada, hii aibu mimi siwezi ivumilia na huu ukatili niliotendewa na huyu mwanamke ni kama mauti.

Wakati tunaendelea kuongea, ndugu zake mke

wangu walinitafuta kujua nimefikia wapi kumpata mtoto wao, na walinipigia wakiwa kwangu kumbe na wao walikuwa wanahangaika kumtafuta tangu pale nilipowapigia kuwaeleza kupotea kwa mke wangu.
Nikawaambia njooni huku kwa dada ndio yupo huku, niliwaelekeza kwa dada ni wapi wakafika

Niliwaambia kila kitu from A to Z. Hadi wao walijiskia aibu sana kwa kile alichokifanya mtoto wao, wakamuombea msamaha maana alikuwa akilia tangu wamekuja anaomba tu msamaha.
Mimi niliwaambia ni ngumu kuuforce moyo ambao umevunjika namna hii eti uanze kumpenda mtu tena, naomba

Mchukueni mwende naye, siku nikiwa tayari kurudiana naye nitakuja kumchukua.
Na hiyo ndo ilikuwa my final say baada ya mazungumzo yote.
Waliondoka naye, hakutaka kuchukua kitu chochote nyumbani aliondoka hivo hivo, akisubiria hasira zangu ziishe.
Mpaka sasa bado nasubiria moyo

Wangu ukiwa tayari kuwa naye, ndipo nitaenda kumchukua.
Ila kwa alichonitendea, itachukua muda mrefu sana kumsamehe arudi nyumbani.

Eeh bhana sina la ziada. Mwisho wa story yetu
Chief hakikisha house girl wako anarudi kwao, ila asirudi kinyonge mtafutie mtaji wa chochote atataka, mpka hapo ame risk sana kazi yake kwa ajili yako, sio rahisi kwa nyumba nyingi house girl kumpigia baba, huo ni ujasiri mkubwa sana huyo binti ameufanya na amekuheshimisha
 
Chief hakikisha house girl wako anarudi kwao, ila asirudi kinyonge mtafutie mtaji wa chochote atataka, mpka hapo ame risk sana kazi yake kwa ajili yako, sio rahisi kwa nyumba nyingi house girl kumpigia baba, huo ni ujasiri mkubwa sana huyo binti ameufanya na amekuheshimisha

Kabisaaaaa
 
Kaka wakina prinxe wajanja sana mimi mwenyewe kuna prince aliniibia simu nikamdaka ila mimi nilimshushia kipigo cha ajabu nashangaa wewe braza na songombingo lote ilo!!
 
Siku moja nilimwomba wife aniitie bodaboda mambo ikawa hivi "Dulla njoo nyumbani mpenzi"

Sikuamini masikio yangu, na yeye akabaki ameduwaa maana alijua kesha haribu.

Kilichoendelea baad ya hapo we acha tu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom