Simulizi: Basi la shetani

Simulizi: Basi la shetani

Ahsante sana The_ Legend kwa kuimaliza simulizi hii kwa wakati
Karibu tena mkuu. Kimsingi ilikua rahisi kuiweka yote kwa mda mfupi sababu ilishatumwa yote whatsapp, so tayari nlikua nayo mwanzo mpaka mwisho

the Legend☆
 
Hahahaha!! Tokea nimejiunga JF kama siyo 2009 ni 2010 sijawahi kusoma riwaya humu jamvini lakini hii nimesoma na kuimaliza......Nachangia wapi hata maji ya kunywa kwa mtunzi au mhusika?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hahahaha!! Tokea nimejiunga JF kama siyo 2009 ni 2010 sijawahi kusoma riwaya humu jamvini lakini hii nimesoma na kuimaliza......Nachangia wapi hata maji ya kunywa kwa mtunzi au mhusika?

Sent using Jamii Forums mobile app
0653195298 (namba imesajiliwa kwa jina Deogratius Tarimo) Hiyo ni namba ya Deo mwenyewe, ambae ndio mtunzi wa hii simulizi. Unaeza cheki nae mkuu

the Legend☆
 
BASI LA SHETANI: SEHEMU YA-32

Mtunzi: DEO MASSAWE

Mpiganaji wa Martin aliykua amevaa gauni alichomoa bunguki aina ya SMG, aliinyoosha kwa Mazengo na kufyatua lakini watu wote walishangaa kumuona Mazengo akiidaka risasi. Kelele zilitawala kwa kitendo kile mashambulizi yalianza vikosi vyote vilivyotaka Mazengo auwawe vilikua vikimshambulia kwa risasi ambazo zilikua zikidunda mwilini mwake, alimshikilia mkewe kwa uangalifu huku Mainda akipiga kelele, watu wote waliamini ni ndoto, lakini ukweli ulikua huo, kuwa Mazengo alikua amerudi katika uso wa dunia akiwa mtu mwingine akiwa na nguvu zingine.
Baada ya mapigano kudumu kwa dakika ishirini pasipo kumuweza vikosi vyote vilipigwa na butwaa, taarifa zilisambaa dunia nzima. Zoezi la kutoa dawa likawa linaendelea.
Mataifa makubwa kama China, Finland, Singapore,Russia walianza kumsaka Mazengo ili akapewe uraia katika nchi hizo lakini katu hakutaka kutoka Tanzania, alitengeneza Hospital kuba kila tarafa nchini Tanzania, pamoja na kuanzisha shule za watoto wanaoishi katika mazingira magumu kote duniani. Mke wake alirudiwa na afya yake baada ya kupata dawa, maisha yakawa mapya wakiwa na Mainda,
Mazengo alikua anafanya safari za mara kwa mara kuenda katika msitu wa Amazon kwa ajili ya kuchukua mizizi ya kutengenezea dawa, dunia nzima ilimjua kwani pia alikua anasafiri katika nchi mbalimbali kufundisha wanajeshi na makomando.
***
Baada ya mwezi mmoja Mazengo aliongoza jeshi la polisi kuwakamata wauzaji na wasambazaji wote wa dawa za kulevya na kuwaweka ndani akiwemo Martin, huku watumiaji wote waliokua wamethirika na madawa hayo wakiwekwa sehemu maalumu kwa ajili ya matibabu
Pamoja na kuwa na furaha juu ya kukutana na mkewe bado mtoto wake wa pekee Winny alimnyima usingizi, hakujua ni mzima au amekufa lakini siku moja katika hali ya kushangaza alisikia taarifa za kuokotwa kwa msichana aliyedhoofika kupita kiasi, hapo alienda hadi hospital kuu ya Lugalo na ndipo alimkuta Winny, hakika alipata furaha ya ajabu, alimchukua na kumtibu.
“Baba, mama, Mainda naombeni mnisamahe kwa yote niliyowahi kukosea, hakika nilikua katika hatua za mwisho kufa, nilikua katika mateso makali, nilitumika vibaya kwa ujinga wangu, namshukuru Mungu alinipigania, Baba nakushukuru sana hakika anilikua siamini kama ni wewe umeniponya na jinsi nilivyokudharau hadi nikawa sikusikilizi, nakupenda sana baba yangu,Mama nakuomba nisamehe, najua ni jinsi gani ulikua unanipenda lakini nikaamua kukusaliti mama please nisamehe bure nina furaha sana kukutana na nyie tena, Mainda mdogo wangu nisamehe kwa haya yote yaliyotokea” Winny alikua akitamka hayo huku akitokwa na machozi aliinama na kuwalamba miguu wazazi wake kama ishara ya kuomba msamaha na kutubu.Wote walisimama na kushikana mikono.
“Tumeanza maisha mapya hakika tulikua tumepanda BASI LA SHETANI LAKINI TUMEFANIKIWA KUSHUKA KWA UWEZO WA MUNGU” alitamka Mazengo kwa uchungu huku akitoa dawa ambayo aliamini ni ya kurudisha umri nyuma wote waliinywa na kuamka asubuhi wakajikuta wamebadilika, Winny na Mainda walirudi na kuwa na miaka 3 huku mazengo na mkewe wakiwa na miaka 25, hakika ilikua dawa ya maajabu iliyoishangaza dunia nzima. Mainda na Winny walianza shule huku Mazengo na mkewe wakisimamia miradi yao, dunia nzima jina la Mazengo lilitawala.
***

MWISHO..

the Legend☆
Safi sana story nzuri sana...

Winny anapenda sana kuchokonolewa hahahaha...

Mahinda ni mwanamke mwenye msimamo sana, safi...

Ila imeisha kivichekesho chekesho...


Chapter closed...


Cc: mahondaw
 
nimeisoma kwa siku mbili ! kwa hakika ilikuwa ni hadithi nzuri especialy kwa sie tuishio porini sometime simulizi kama hizi zinatupa kampani fulani baada ya kazi na mihangaiko yetu... big up mtunzi hope utakuwa na kitu kipya tena
 
nimeisoma kwa siku mbili ! kwa hakika ilikuwa ni hadithi nzuri especialy kwa sie tuishio porini sometime simulizi kama hizi zinatupa kampani fulani baada ya kazi na mihangaiko yetu... big up mtunzi hope utakuwa na kitu kipya tena
Nakushkuru kwa niaba ya mtunzi. Vitu vingine vipo mkuu, ukicheki kwenye threads zangu utazikuta

the Legend☆
 
Mambo ni Sawa
BASI LA SHETANI: SEHEMU YA-15

Licha ya mvua kuendelea kunyesha Winny alikua akitokwa na jasho kutokana na mbu waliomfanya ajipige pige mara kwa mara kuwafukuza, kwa kupitia upenyo nyumba hiyo alifanikiwa kuona wanyama wakali pale radi ilipomulika, alitetemeka kwa hofu hasa pale aliposikia mingurumo ya simba na chui.
Alimuomba Mungu aweze kumsaidia pakuche salama ili aweze kutafuta msaada wa kutoka mahali pale,
“Kwanza huku ni wapi?” ni swali Winny alilojiuliza bila kupata jibu, hakujua kama bado yupo Zambia au yupo wapi, ingawa alijua dhahiri hayupo Tanzania kutokana na lugha aliyosikia vijana wale wakiongea wakati akifukiwa shimoni.
***
Pamoja na kufundishwa kupigana pia Mazengo alifundishwa kumsoma mtu saikolojia , alifundishwa kusoma hisia za mtu, umri wa miaka arobaini haukumfanya mwalimu wake Vajiralong kushindwa kumpasua msamba, japo ilikua shida kwa Mazengo lakini kutokana na hasira ya kupewa taarifa ya mkewe kuuwawa ilimfanya ajitoe ufahamu na kuapa kujifunza kwa bidii ili siku moja aweze kulipa kisasi kwa wauwaji wote.
***
Baada ya Winny kuvumilia usiku mrefu aliweza kuona jua likichomoza kwa mbali, kichwani mwake hakuwaza kitu zaidi ya kutoka mahali pale, hakujua angeelekea wapi kwani alishaamini Martin sio mtu mzuri kwake,
“Kama Martin ndiye ametuma watu waje kunizika nikiwa mzima basi ana nia ya kuniuwa” alijisema Winny huku akijifunga shuka lililokua ndani hapo, alitoka na kusimama nje, hakujua njia ilipo, hakujua aelekee wapi ,
“Ngoja nichukue kisu hapa ndani”, alijisemea Winny na kurudi ndani, alichukua kisu kilichokua ndani hapo na kutoka nacho kama silaha, baada ya kuwaza kwa dakika tatu aliamua kuelekea upande wa kulia ambao aliamini ndio upande wa kuume tena wenye nguvu,alitembea kwenye tope, lililomsababishia kuanguka mara kwa mara, hakujua kama yupo eneo la hifadhi ya taifa, na katika upande wa kulia aliokua akielekea ulikua ndio upande wa kuingiza zaidi ndani ya hifadhi.
“Mungu nisaidie” alijisemea Winny baada ya kuona gari aina ya Land Rover, ambazo mara nyingi zilitumiwa na walinzi wa hifadhi za wanyama, gari hilo iliendeshwa taratibu kutokana na hali ya hewa, walikua ni askari wa msitu waliokua wakifanaya doria katika msitu huo, Winny akajiwa na wazo la kulala chini, hapo alipolala alikipachika chini kisu alichokua ameshikilia, alizidi kuingiwa na hofu hasa baada ya kuona gari ikielekea mahali alipolala,
“Najifanya nimekufa” alijisemea Winny moyoni baada ya kuona askari mmoja akishuka garini na kumsogelea, alimpekua Winny kwa haraka na kumuita mwenzake aliyekua ndani ya gari, walizungumza kingereza wakijiuliza kuhusu mwanamke huyo,
Winny hakuzungumza chochote, zaidi alizidi kujibana pumzi yake, walimgeuza geuza pale chini, hadi shuka alilokua amejifunika nalo likamtoka mwilini,
“Maaskari wote walipagawa baada ya kuona mwili wa Winny, hakika wote walijikuta wakimeza mate, askari mmoja alijikuta akipenyeza kidole cha kati ndani ya uke wa Winny, huku akisema ,
“Ooooh yeaaaaahs” Winny alijitahidi kuvumilia, alijiua ni dhahiri kuwa kuna uwezekano wa kubakwa,katika yale mazingira, baaada ya dakika tano, walichukua shuka lake na kumfunika, hapo bila askari hao kuona alikichomoa kile kisu ardhini na kukishikilia kwapani, alijikuta akiomba Mungu asishikwe vibaya kusudi kisimchome. Baada ya hapo alibebwa na kutupwa ndani ya gari, kisha gari kuanza safari.
Maamuzi ya kumbeba na kuondoka naye yalikua ni kumpeleka mochwari, kwani askari hao waliona kama ameshakufa napengine waliamini amekufa kwa maji usiku wa kuamkia siku hiyo.
Winny alipoachwa mwenyewe nyuma ya gari aliendelea kupumua kama kawaida, kila alipowaza kuruka alijikuta akitamani kuruka pale atakapoona amefika sehemu zenye watu wengi ili aweze kupata msaada wa kufika nchini Tanzania kumkwepa Martin ambaye aliamini kama atamuona ataweza kumuuwa.
***
Mainda akiwa na mama Winny walihifadhiwa katika chumba cha siri nyumbani kwa mchungaji mmoja, jijini Dar es salam, alifanyiwa matibabu kwa siri hasa baada ya kutokea vifo vya mara kwa mara, Mainda alikua akiomba Mungu usiku na mchana, kusudi mama Winny aweze kuwa mzima wa afya kwani kitendo cha kumshuhudia mumewe akiuwawa kilizidi kumtia machungu, Mainda alifanya kazi ya ziada kumbembeleza na kuzidi kumpa matumaini kwamba siku moja wangekutana mbinguni.
***
Baada ya dakika arobaini na tano gari iliyombeba Winny ilifunga breki nje ya geti la Lusaka Trust Hospital (LTH) ,Winny aliona huo ndio wakati muafaka wa kutoka ndani ya gari, alichungulia pande zote na hapo aliona gari la takataka likipakia taka eneo hilo, bila kupoteza mda alipoona askari wameshuka na kuingia katika mapokezi ya hospital hiyo naye alitoka na kukikamata kichochoro cha kulekea barabara kuu ya Independence Ave, alipiga kama hatua mia mbili ndipo alipoweza kukutana na barabara kubwa iliyo katikati ya mji, kila mtu alikuwa akihangaika na shughuli zake, hali ya hewa ya manyunyu ilimfanya kila mtu awe busy na kazi yake,
“Nitaanzia wapi Mungu wangu” alijisemea maneno hayo baada ya kubanwa na mkojo hakuwa na lakufanya zaidi ya kuachilia kidogo kidogo, kila alipofika mahali palipotwama maji basi aliachilia kidogo kwani alimini hakuna atakayemgundua.
Madaktari wakiwa na machela walifika ilikoegeshwa Land Rover ya askari, walishangaa sana baada ya kutoona mwili uliotakiwa kwenda kufanyiwa uchunguzi,wote walishangaa hasa baada ya watu waliokuja karibu kusema wameona msichana akishuka garini, waliona kama maaajabu, huku wakihisi wamebeba mzimu.
***
“Winny alitembea kama kilomita tatu, ndipo alikutana na wanafunzi wa chuo cha David Kaunda Technical , walikua wamevaa sare nzuri, Winny alijaribu kuwasalimi kwa kingereza cha kuungaunga, moja kwa moja wakajua ni mtu anayehitaji msaada, walimwamuru kuongozana nao hadi walipokua wakiishi.
“Kweli hawa wanafunzi wa Zambia ni waelewa na wenye upendo wa dhati, ingekua ni wa pale chuo cha IFM ningeshakula misonyo ya maana” alijisemea Winny wakiendelea kupiga hatua za haraka haraka, alimshukuru Mungu kwani aliamini kuwa atakua salama na ataweza kufika Tanzania bila matatizo yoyote.
Wanafunzi hao waliokubali kumsaidia Winny walikua wakimwangalia Winny kutoka juu hadi chini kila mmoja alipendezwa naye, kila mmoja aliamini Winny atafaa sana katika kazi yao ambayo waliifanya kwa siri.
***
Edson alianza kwa kujaribu kuuza madawa ya kulevya katika mitaa ya magomeni, Mwananyamala na Kinondoni, yote hayo ili kujifunza biashara hiyo kabla ya kuwekeza mtaji mkubwa, alitamani sana kukutana na msambazaji mkubwa wa madawa hayo ili aweze kuzungumza naye na kumpa mfululizo mzima wa namna ya kusafiri na namna ya kujua madawa yenye ubora na madawa bandia.
“Kuna mtu anaitwa Martin, ukiweza kumpata huyo ndio atakupa utaratibu mzima” maneno hayo kutoka kwa muuzaji mdogo yalimfanya Edson kumtafuta huyo Martin usiku na mchana,
“Sio rahisi kukutana na Martin ovyo ovyo, na ukae makini maana akijua unamfuatilia unauwawa mara moja” yalikua maneno yaliyozidi kumkatisha Edson tamaa ya kukutana na Martin,
“Kama kweli unataka mfanye biashara basi namba zake hizo mpigie simu” kijana aitwaye Shedrack alimkabidhi Edson namba za Martin na ilikua baada ya Martin kupokea ujumbe wa kazi , Edson alitoa simu yake ya mkononi na kuipiga namba ya Martin.,

INAENDELEA

the Legend☆

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hili basi la sheitwan kweli hajulikani konda wala dereva achilia mbali abiria
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom