the_legend
JF-Expert Member
- Jan 14, 2019
- 1,612
- 7,112
- Thread starter
- #21
BASI LA SHETANI: SEHEMU YA-12
Mazengo aliinua uso na kumtazama aliyekua anahesabu, aligeuka upande wa pili na kuwaangalia waandishi wa habari waliokua wamejipanga pale,
“Moja, mbili,tatuu” baada ya maneno hayo kilio kilitanda kwa watu wote waliokua wanaangalia tukio lile, mkewe ndiye hakuamini alijikuta akipoteza fahamu baada ya kuona mmewe amesukumwa na kudumbukia shimoni, tena shimo ambalo ingekua vigumu kwa mtu kupona kutokana na miamba iliyokua chini.
Winny ndiye hakuamini kilichotokea, Martin alizidi kumbembeleza bila mafanikio,
“Mpenzi wangu hata kama baba amekufa amini bado nipo na wewe” Martin aliongea maneno ambayo yalimpa Winny hasira,
“Kwani wewe ni nani kwangu, mimi nipo na wewe kukuchuna tu huna maana zaidi ya baba yangu”Winny alitamka baada ya kutolewa gundi mdomoni, Martin alipoona Winny hataki kutulia aliamua kumchoma sindano ya usingizi.
***
Katika eneo hilo la Hong Kong mita chache kutoka eneo yalipokua makao makuu ya tume ya kuthibiti madawa ya kulevya palikua na msitu mnene, msitu huo ulikua na wanyama wakali kitu kilichopelekea serikali ya China kupiga marufuku watu kuingia msituni hapo, pia katika ardhi ya msitu huo kulidaiwa kuwa na madini ya dhahabu, hivyo kukawa na kikundi kimoja kilichoamua kuingia msituni hapo kisirisiri na kuanza kuchimba, kilikua kikundi cha vijana zaidi ya mia moja, walijipanga msituni hapo wakichimba kwa kupokezana, walikua na mitungi ya hewa, walijipanga kuanzia mwanzo wa shimo hivyo walipokezana kutoa udongo kwa mtindo wa kumsogezea mwenzako ndoo hadi nje, na chakula kilitoka nje kwa mtindo wa kumsogezea mwenzako hadi shimo lilipokua limefikia, vijana hao walitoka sehemu mbalimbali kama Wuhan, Shanghai, Quanzhou, na hadi wengine walitoka katika kisiwa cha Taiwan, na Taipei,baada ya miaka mitatu wakiwa wanachimba bila mafanikio siku moja aliyekua ameshika jembe kwa mbele alishtuka kukutana na shimo, alipotazama juu alishtuka kuona mwanga kwa mbali haraka alitoa taarifa kwa mwenzake aliyekua nyuma yake hivyo hivyo hadi kwa kiongozi wao aliyekua nje kabisa,baada ya taarifa kufika kwa kiongozi kiongozi alitoa amri ya kazi kuendelea, hivyo kijana huyo akalazimika kuendelea kuchimba, miamba iliyochongoka mwisho wa shimo hilo ilimpasa afanye kazi pale kwa umakini aweze kufukia miamba hivyo kusudi isimkate mtu, Kwa hali isiyo ya kawaida walishtuka kishindo cha mzigo uliodondoka kutoka juu, wote walishtuka, hawakujua lile shimo lilikua na kazi gani, walitetemeka kwa hofu na ndipo mmoja aliposogea karibu na kuona binadamu aliyewekwa ndani ya kiroba huku kichwa kikiwa nje, taarifa ilienda moja kwa moja kwa kiongozi wao na kiongozi akaamuru mtu huyo atolewe nje, hivyo kwa kupokezana walianza kumtoa nje huku akiwa hana fahamu, walimtoa nje ya kiroba, baada ya mita kumi tokea alipodondokea alirudiwa na fahamu na kuanza kupige kelele, hakujua mahali alipo, aliamini pale ndipo anabebwa aidha na malaika kwenda mbinguni au au mashetani kwenda motoni, hakuamini kama angekua hai tena,
“Ni mimi kweli nimesukumiwa ndani ya shimo, na niko hai hadi sahivi? siamini” alijisemea Mazengo, mikwaruzo aliyoipata kichwani hakuisikia zaidi alishindwa kujua ameokokaje, pia alishindwa kujua hao wanaombeba wametoka wapi na ni akina nani na nini kitatokea akifika huko anakopelekwa, ghafla wazo likamjia kichwani, akawa mbishi kubebwa, alikataa katu katu, alipiga kelele hadi vijana wa kichina wakaamua kuchimba shimo pembeni ili wamfiche na waweze kuendelea na kazi, walichimba shimo kwa haraka lakini bila kutarajia walishtuka kuona vitu vinavyongaa, kuangalai vizuri walikuta ni dhahabu zenye zaidi ya kilogramu kumi, hawakuamini macho yao taarifa ilifika kwa kiongozi wao huku wakieleza jinsi walivyokua wanachimba shimo kwa ajili ya kumhifadhi huyo mtu aliyedondoka na ndipo wakapata dhahabu, huku wakiendelea kushangilia walishtuka moto ukishuka kutoka juu na kutua sehemu ambayo mwili wa Mazengo ulipodondokea, hapo moja kwa moja wakagundua Mazengo ilibidi auwawe wakamuokoa.
Hawakupoteza muda walitoka na mazengo hadi msituni, walikua wakiongea kwa matendo, kutokana na njaa Mazengo aliyokua nayo alijikuta akila nyoka aliyechomwa. Lakini hakutaka kabisa kutoka msoituni hapo kwani alimini atauwawa pale atakapogundulika na maadui zake.
***
Kilio kilizidi baada ya mkaa kushushwa shimoni, watu walivuta picha na kuona jinsi mwili wa mazengo unavyoungua, Martin ndiye alikua na furaha kupita kiasi kuona kesi yake imefutika, mke wa Mazengo alikua akizinduka na kupoteza fahamu mara kwa mara, bado tukio hilo la kuchomwa moto lilikua likiendelea kurushwa katika vituo vya televisheni, askari wa kichina walionekana kuongeza mkaa kwa wingi shimoni kisha kulifunika kwa juu ili aungue na kuteketea moja kwa moja, ingekua vigumu kwa mtu yeyote aliyekua anaona tukio hilo kuamini kama Mazengo bado yupo hai.
***
Haraka kiongozi wa waliokuya wakichimba madini, aliwaacha vijana wake msituni na kusafiri hadi New Delh nchini India kwa ajili ya kuuza madini, vijana wake walibaki na Mazengo msituni wakimwabudu kama Mungu aliyewapa utajiri, kwani bila yeye wasingepata madini kirahisi,kila asubuhi wote walikua wakimsalimia kwa heshima japo hawakuweza kuwasiliana kwa lugha zaidi ya matendo.
“Ama kweli ukimtumaini Mungu hakuna linaloshindikana, sipati picha dunia nzima itakaponiona nikiwa hai tena” alijisemea Mazengo huku akiwaza kwa jinsi gani angeonana na mkewe tena.
***
Baada ya Martin kuamini amekamilisha zoezi la kumuua Mazengo haraka alipanga mbinu za kumuua mkewe kisha aweze kumuua Winny, ili siri isiweze kugundulika. Alifanya mawasilino na daktari mmoja wa Muhimbili na kumhonga kiasi kikubwa cha pesa kusudi aweze kumuweka mke wa Mazengo chumba cha pekee cha wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalumu, Mainda ndiye alikua anamuuguza, alisitisha masomo yake akawa anashinda nae hospital. Haraka mipango ya kumhamishia katika chumba maalumu ilifanyika, alipewa chumba cha peke yake ambacho hata Mainda hakuruhusiwa kuingia katika chumba hicho hivyo alilazimika kukaa mlangoni mda wote, daktari mmoja tu ndiye alikua akimhudumia mama Winny siku zote, presha ilimpanda kwa kiasi kikubwa , yote kutokana kushuhudia tukio la kuuwawa kwa mumewe.
Katika hali ya kawaida ambayo ilikua ikitokea katika nyingi ya hospital pale anapotokea mgonjwa mwenye hela basi mara nyingi huweza kuhamisha mgonjwa asiye na pesa ili kupisha mwenye hela atibiwe kwanza, kwa bahati mbaya au nzuri asubuhi moja ya siku ya jumamosi kuliletwa mgonjwa mmoja mwanamke aliyekua katika hali mbaya, hivyo alilazimika kuwekwa katika chumba maalumu, na hapo ndipo mme wake aliweza kuhonga pesa nyingi na kumuondoa mke wa Mazengo katika chumba hicho, mke wa mazengo alihamishiwa katika chumba cha wagonjwa wa kawaida, bila Mainda kujua hivyo Mainda aliendelea kukaa mlangoni akiamini mama Winny ndiye yupo ndani, akiwa ameinamisha kichwa chini aliona daktari mmoja aliyevaa gauni lakini hakutembea kama mwanamke, kitendo hicho kilimpa wasiwasi hasa baada ya daktari huyo kufungua mlango ambao Mainda aliamini mama Winny ndiye aliye ndani.
Itaendelea
the Legend☆