Mkuu zote zipo kamili mm nimecheza zote kuanzia fm15 ad fm 17 zote Zina majina kamili na fm 17 ipo well developed na Inataka utumie akili nying though unaweza ukafungwa mechi zote au LA sivyo kila timu utakuwa unafukuzwa, m Mara ya kwanza niliona easy kama fm16 nikaanza na timu za tz na badae nikaomba kazi timu za France nikapata kwa sabab nilikuwa na kombe LA ligi kuu ya tz, badae sikushind mech nying nikaanza kupewa warning badae nikafukuzwa na timu ya OL, sitak kuanza new game bado nakazana kuomba Kaz timu nying Lakin nying nashindwa kwa sabab unawekwa short list na watu more reputable yan
Pirate
mkuu hapo juu jamaa amezungumzia simu na sio pc.
kuhusu football manager mimi ni mzoefu kidogo huwa napenda kuanzia madaraja ya chini na kila mwaka napanda hadi kuchukua kombe kubwa la ligi na uefa.
ili uweze kuli master inabidi sana utumie tip mbali mbali online. mfano vitu kama hivi.
wonderkids
hawa ni wachezaji wadogo ambao huko baadae watakuja kuwa wachezaji wa kubwa, anaweza chukua misimu miwili hadi mitatu kuja kuwa top player, mimi hupenda kuanzia ligi ya chini sababu ya hawa ili ukipanda ligi kuu wanakuwa wamesha mature.
wanapatikana bei rahisi sana, na pia mishahara yao ni midogo hivyo hadi timu ndogo za madaraja ya chini zinawapata sema wengine wanakataa timu ndogo.
mfano wa wonderkids ni kina youri tielemans wa anderletch, julian brandt, kina pulisic, renato sanchez, ihenacho, iwobi etc sema hao wenye majina mpunga mrefu.
free players
kila game la footballer manager kunakuwa na wachezaji wa bure wenye miaka 30 na kuendelea ambao hawajaongeza mkataba kwenye timu zao wanaondoka bure, kutegemea na game ila unaweza pata mchezaji mzuri kama tevez, dani alves na wengine wakubwa waliondoka bure.
tactics na training schedule
kila game linakuwa na udhaifu kwenye match engine hivyo unakuta kuna tactics za ukweli ambazo zinaipa nguvu timu yako. mfano kuna baadhi ya FM ukicheza narrow formation bila mawinger timu yako inakuwa na nguvu zaidi, hapa inategemea na game na game.
ujue position gani inataka uwezo upi
sometime unaweza sajili striker mkali anauzwa bei ghali na asifunge magoli sababu stats zake sio za ki striker. mfano mchezaji ni namba 9 poacher halafu kwenye off ball, finishing, heading, shooting yupo mbovu ujue hatafunga hata kama anajua kukaba, ana mbio, ana maguvu, anajua kupiga cross, anarusha vizuri mipira hivyo havimsaidii striker.
kuna mambo mengi ukitulia ukicheki forums za hayo magame utapata ujuzi mkubwa na hayatakusumbua.