Simuhitaji sana lakini naumia kuachana naye

Simuhitaji sana lakini naumia kuachana naye

Kimsingi, kumsaidia huyo mwanamama kulikufanya ujisikie vizuri kwa namna moja ama nyingine, na sasa hakuhitaji tena so unahisi umepoteza kitu. Tafuta sehemu nyingine tu wanapohitaji msaada wako, halafu uone.
 
Kuna huyu mdada single mother, ana watoto wawili. Nimekuwa naye for a while mwezi ujao tungefikisha miaka 2. Ukweli huyu dada nilimkuta na hali mbaya sana kiuchumi. Lakini uzuri wake uliweza kuonekana hata katika hiyo hali. Basi nikajitolea kumsaidia. Ana Degree na kazi ya kawaida, lakini alikopaga hela nyingi akaanza biashara ambayo haikumlipa ikafa. Hivyo Mshahara wake wote unakatwa. Anabaki na kama laki 3 tu kwa mwezi ambayo haimtoshi.

Basi nikawa na mlea na watoto wake. Ki ukweli toka tuanze nilikuwa nampa jumla ya tsh 1.4m kwa mwezi cash. Ikiwa ni nyumba laki 3, vicoba laki 2, matumizi laki 6, rejesho deni la vicoba laki 3. (Alikopa ada za watoto wake na some furniture).

Sasa cha ajabu huyu dada alianza kama kupoteza furaha na mimi, nikawa namuuliza nini shida anasema hakuna shida. Hali hiyo ikaendelea na akawa sasa hanitafuti wala kusalimia hadi mimi ndo nimuanze. Nikimuuliza anajibu tu kifupi kwamba hakuna shida yuko sawa, mara ya mwisho akanijibu kama unaona nimebadilika si uniache kwani umelazimishwa.

Kuanzia siku hiyo sijamtafuta wala hajanitafuta, ni mwezi sasa umepita. Ninachojiuliza huyu dada ana jeuri gani, anajiamini nini? Siamini kama ana mtu, ambaye anaweza kumuhudumia zaidi kuliko nilivyokuwa nafanya mimi. Kimsingi simuhitaji sana kwani alikuwa hana jipya zaidi ya kumzoea na kumpenda tu, ila namuonea huruma. Nimejikuta nawaza sana juu ya hatima ya maisha yake. Sijui ni kwanini. Naombeni ushauri.
Unamuhitaji sana, kiasi cha kumuanzishia thread.

Kubali hilo kwanza kabla ya mjadala zaidi.
 
Kinachonishangaza ' hanipigii hadi nipige' unakuta tangu asubuhi hadi week inaisha hamjatafutana lakini mwanaume anaanza kulaumu huyu mwanamke ana jeuri we si upige??

Hayo mengine angalia moyo wako kama wamtaka ama humtaki. Issue ya watoto sio kigezo cha tabia mbaya kuna watubwana mahusiano na wasichana hawana watoto lakini wana changamoto zaidi ya huyo, wajeuri wavivu n. K tabia ni tabia tu. Pia mahusiano ya biandamu hayawezi kuwa na furaha mda wote kuna nyakati za kuvumiliana.
 
Million 1.5 kwa mwezi kwa mwanamke umemshinda hata Dimond kwa hamisa mobetto
 
Hapa kuna mambo matatu.
Mos, kuna muwekezaji mpya kapatikana mwenye maslahi bora kuliko wewe.
Pili, historia inajieleza ni mwanamke aliepitia mengi, ktk uzoefu hue basi wewe unaonekana unacheza chini ya kiwango kunako 6×6. Asikudanganye mtu, mwanamke hata uwe na pesa kiasi gani kama humkuni kipande hiki wewe siikitu siichochote kwake.
Tatu, huenda keshajiweza mwenyewe kiuchumi so anataka uhuru wa kujiamulia na kuishi maisha apendayo na wanawe.
 
Inasikitisha sana pale unapomuonea huruma mtu ambaye hana hata mawazo kwamba unamuonea huruma.

Mpaka kafikia hvyo huenda ikawa yupo ambaye anampa kiburi au hata kama hana basi anajiona naweza kumudu maisha bila wewe.

Pole sana kwa kudhani umepata kumbe umepatikana.
 
Kuna huyu mdada single mother, ana watoto wawili. Nimekuwa naye for a while mwezi ujao tungefikisha miaka 2. Ukweli huyu dada nilimkuta na hali mbaya sana kiuchumi. Lakini uzuri wake uliweza kuonekana hata katika hiyo hali. Basi nikajitolea kumsaidia. Ana Degree na kazi ya kawaida, lakini alikopaga hela nyingi akaanza biashara ambayo haikumlipa ikafa. Hivyo Mshahara wake wote unakatwa. Anabaki na kama laki 3 tu kwa mwezi ambayo haimtoshi.

Basi nikawa na mlea na watoto wake. Ki ukweli toka tuanze nilikuwa nampa jumla ya tsh 1.4m kwa mwezi cash. Ikiwa ni nyumba laki 3, vicoba laki 2, matumizi laki 6, rejesho deni la vicoba laki 3. (Alikopa ada za watoto wake na some furniture).

Sasa cha ajabu huyu dada alianza kama kupoteza furaha na mimi, nikawa namuuliza nini shida anasema hakuna shida. Hali hiyo ikaendelea na akawa sasa hanitafuti wala kusalimia hadi mimi ndo nimuanze. Nikimuuliza anajibu tu kifupi kwamba hakuna shida yuko sawa, mara ya mwisho akanijibu kama unaona nimebadilika si uniache kwani umelazimishwa.

Kuanzia siku hiyo sijamtafuta wala hajanitafuta, ni mwezi sasa umepita. Ninachojiuliza huyu dada ana jeuri gani, anajiamini nini? Siamini kama ana mtu, ambaye anaweza kumuhudumia zaidi kuliko nilivyokuwa nafanya mimi. Kimsingi simuhitaji sana kwani alikuwa hana jipya zaidi ya kumzoea na kumpenda tu, ila namuonea huruma. Nimejikuta nawaza sana juu ya hatima ya maisha yake. Sijui ni kwanini. Naombeni ushauri.
Nani aliyekufundisha mapenzi ni pesa tu,huenda ulikua unamnyanyasa au unamtreat ndivyo sivyo kachoka kaamua kukupotezea na vihela vyako
 
Jifunze kwa Ruge kuna watu wanaitwa Zamaradi...
You only know you love her when you let her go..
 
Hehehehe milion 1 na laki 4 ukizidisha kwa miaka miwili unapata sh ngap?!


Halaf umpe mtu ambaye humpendi


Jf bwana.
Halafu utakuta jamii yake inaishi maisha ya kuunga unga halafu anahonga huku 1.4M kwa mwezi,ungekua mdogo wangu ungekula vitasa vya kutosha kurestore akili yake
 
Ameamua kuishi maisha yake smart ya kimaskini.amegundua wewe unamsimanga sana.anataka kukuonyesha anaeweza kuishi bila wewe .sababu ulimkuta pia katika maisha hayo
 
Nani aliyekufundisha mapenzi ni pesa tu,huenda ulikua unamnyanyasa au unamtreat ndivyo sivyo kachoka kaamua kukupotezea na vihela vyako
Kwa alivyoandika inaonekana alifikiri mwanamme akitoa pesa ana haki ya kummiliki mwanamke kama kitu unachonunua.

Ni mentality fulani ya kifukara sana.
 
Unaonekana unalazimisha kupenda usipo pendwa.
Na unaonekana kama umetanguliza sana pesa ulizokua ukimpatia kuliko kitu chochote kwenye hayo mahusiano yenu
 
Kumbe bado Kuna wanaume wenye akili kama zako...
Mkuu badilika bora ufadhiri mbuzi utakula hata miguu...
Alafu nawaza hapa kuwa ulikuwa unampatia 1.4 kwa mwez ..
Je una family? Means wazaz au nduguzo au watoto ? Dah u have done very worse mkuu
 
Block hiyo kitu ni hatari kwa afya yako, amekuona ng'ombe huyo, kodi ukifika atakutafuta tu, alafu wewe mrushie buku tu..Kama vipi c utafute kisu kipya mzee uwekeze ktk ndoa tu? Huyo kunguru watoto wa2 alafu jeuri
 
Mara nyingi wazee wa kuhonga ugeuka kuwa wahasibu haraka sana baada ya kutengana na kujutia kila shilingi waliyoitumia kwa mwanamke. Pole sana mkuu
 
Achana naye huyo kiumbe tena haraka ukiona mwanamke kaanza jeuri ujue nyuma yake 90% kuna mwanaume mwenzio kakuzidi ujanja.nilikuwa na msichana wa sampo yako na mimi alinifanyia hivo hivo kama anavyokufanyia sikutaka kuhangaika naye nikapiga chiniiiii.alichokipata huko mpaka leo anasema anajutaaa na wala sikutaka kujua kimempata nn huko
ebu simulia mkuu
 
Kiukweli, Ni ngumu kumeza. Mtu unamgharamikia kiasi hicho kisha anaanza kubadilika!
Najua unajutia msaada wako kwake.
Hapo amesababisha hata demu utakayempata uwe na mashaka naye. Maana utakuwa unakumbuka roho inauma sana.
Pole sana, inauma sana lakini huo ndiyo ukubwa.
Wanaume tumeumbwa mateso....
 
Back
Top Bottom