Simuhitaji sana lakini naumia kuachana naye

Simuhitaji sana lakini naumia kuachana naye

iMind

Platinum Member
Joined
Mar 27, 2011
Posts
3,229
Reaction score
5,525
Kuna huyu mdada single mother, ana watoto wawili. Nimekuwa naye for a while mwezi ujao tungefikisha miaka 2. Ukweli huyu dada nilimkuta na hali mbaya sana kiuchumi. Lakini uzuri wake uliweza kuonekana hata katika hiyo hali. Basi nikajitolea kumsaidia. Ana Degree na kazi ya kawaida, lakini alikopaga hela nyingi akaanza biashara ambayo haikumlipa ikafa. Hivyo Mshahara wake wote unakatwa. Anabaki na kama laki 3 tu kwa mwezi ambayo haimtoshi.

Basi nikawa na mlea na watoto wake. Ki ukweli toka tuanze nilikuwa nampa jumla ya tsh 1.4m kwa mwezi cash. Ikiwa ni nyumba laki 3, vicoba laki 2, matumizi laki 6, rejesho deni la vicoba laki 3. (Alikopa ada za watoto wake na some furniture).

Sasa cha ajabu huyu dada alianza kama kupoteza furaha na mimi, nikawa namuuliza nini shida anasema hakuna shida. Hali hiyo ikaendelea na akawa sasa hanitafuti wala kusalimia hadi mimi ndo nimuanze. Nikimuuliza anajibu tu kifupi kwamba hakuna shida yuko sawa, mara ya mwisho akanijibu kama unaona nimebadilika si uniache kwani umelazimishwa.

Kuanzia siku hiyo sijamtafuta wala hajanitafuta, ni mwezi sasa umepita. Ninachojiuliza huyu dada ana jeuri gani, anajiamini nini? Siamini kama ana mtu, ambaye anaweza kumuhudumia zaidi kuliko nilivyokuwa nafanya mimi. Kimsingi simuhitaji sana kwani alikuwa hana jipya zaidi ya kumzoea na kumpenda tu, ila namuonea huruma. Nimejikuta nawaza sana juu ya hatima ya maisha yake. Sijui ni kwanini. Naombeni ushauri.
 
Kuruka~ruka kwa maharage ndio kuiva kwake mkuu.

We ni mwanaume na utabaki kuwa mwanaume chukua hatua kiongozi
 
Kuna huyu mdada single mother, ana watoto wawili. Nimekuwa naye for a while mwezi ujao tungefikisha miaka 2. Ukweli huyu dada nilimkuta na hali mbaya sana kiuchumi. Lakini uzuri wake uliweza kuonekana hata katika hiyo hali. Basi nikajitolea kumsaidia. Ana Degree na kazi ya kawaida, lakini alikopaga hela nyingi akaanza biashara ambayo haikumlipa ikafa. Hivyo Mshahara wake wote unakatwa. Anabaki na kama laki 3 tu kwa mwezi ambayo haimtoshi.

Basi nikawa na mlea na watoto wake. Ki ukweli toka tuanze nilikuwa nampa jumla ya tsh 1.4m kwa mwezi cash. Ikingwa ni nyumba laki 3, vicoba laki 2, matumizi laki 6, rejesho deni la vicoba laki 3. (Alikopa ada za watoto wake na some furniture).

Sasa cha ajabu huyu dada alianza kama kupoteza furaha na mimi, nikawa namuuliza nini shida anasema hakuna shida. Hali hiyo ikaendelea na akawa sasa hanitafuti wala kusalimia hadi mimi ndo nimuanze. Nikimuuliza anajibu tu kifupi kwamba hakuna shida yuko sawa, mara ya mwisho akanijibu kama unaona nimebadilika si uniache kwani umelazimishwa.

Kuanzia siku hiyo sijamtafuta wala jahanitafuta, ni mwezi sasa umepita. Ninachojiuliza huyu dada ana jeuri gani, anajiamini nini? Siamini kama ana mtu, ambaye anaweza kumuhudumia zaidi kuliko nilivyokuwa nafanya mimi. Kimsingi simuhitaji sana kwani alikuwa hana jipya zaidi ya kumzoea na kumpenda tu, ila namuonea huruma. Nimejikuta nawaza sana juu ya hatima ya maisha yake. Sijui ni kwanini. Naombeni ushauri.
Aliye mzalisha watoto wawili atakuwa ameshajisogeza karibu mkuu baada yakumwona ananawili kwa matunzo yako!!!!
 
Achana naye huyo kiumbe tena haraka ukiona mwanamke kaanza jeuri ujue nyuma yake 90% kuna mwanaume mwenzio kakuzidi ujanja.nilikuwa na msichana wa sampo yako na mimi alinifanyia hivo hivo kama anavyokufanyia sikutaka kuhangaika naye nikapiga chiniiiii.alichokipata huko mpaka leo anasema anajutaaa na wala sikutaka kujua kimempata nn huko
 
Pengine unamla tigo Kaona isiwe shida abaki na umaskini wake
 
dah kuna watu mna roho ngumu aisee, mtu ana watoto kabisa unakomaa nae tu, limbwata hilo bila shaka
 
Back
Top Bottom