Simuhitaji sana lakini naumia kuachana naye

Simuhitaji sana lakini naumia kuachana naye

WTF...unampa mwanamke 1.4m cash kwa mwezi mama yako unampaga shilingi ngapi,je huna ndugu wa kumsaidia japo kumsomeshea watoto?next time usiandike ujinga huu mbele ya wanaume wanaojielewa!
Mimi nafikirimleta mada anatafuta kiki ya kupata PMs humu kutoka kwa wadada mahuju!!!!
 
Hii mitandao imetupunguazia kabisa hata uwezo wa kutatua matatizo madogo madogo kama haya,jambo dogo kama hili mpk uombe ushauri.
 
Kumbe baadhi ya Single Mothers wana tabia za ajabu...duuh...
Mkuu achana nae japo inauma..inaonesha amepata mfadhili mpya
 
Mimi nafikirimleta mada anatafuta kiki ya kupata PMs humu kutoka kwa wadada mahuju!!!!
Umewaza kwa akili kubwa sana mkuu,haingii akilini hii hata kama fisadi kiasi gani hakuna mtu atahonga kwa kiwango hiki!
 
wahenga walisema umasikini ni mbegu kila ukavyojitahidi mahindi ya njano Kuwa meupe ndivyo kadri utakavyo sumbua moyo wako
 
WTF...unampa mwanamke 1.4m cash kwa mwezi mama yako unampaga shilingi ngapi,je huna ndugu wa kumsaidia japo kumsomeshea watoto?next time usiandike ujinga huu mbele ya wanaume wanaojielewa!
Mama si ana mume wake anaempa
 
Umewaza kwa akili kubwa sana mkuu,haingii akilini hii hata kama fisadi kiasi gani hakuna mtu atahonga kwa kiwango hiki!
Mimi siiti kuhonga, bali kusaidia. Kiwango unachoweza kumsaidia demu wako inatokana na kiwango cha fedha unazopata na moyo wa kutoa. Mimi sina hela nyingi lakini bahti mbaya au nzuri, Wengine tukimpenda mtu, shida zake zinakuwa zako hivyo huoni shida kumsaidia maana unakuwa unaona kama ni shida zako vile vile.
 
Halafu utakuta jamii yake inaishi maisha ya kuunga unga halafu anahonga huku 1.4M kwa mwezi,ungekua mdogo wangu ungekula vitasa vya kutosha kurestore akili yake
[emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1]
 
Mama si ana mume wake anaempa
Huyo mumewe unadhani anao uwezo wa kumpa mkewe 1.4m per month,hata kama anao yeye kama mtoto mama yake anamuangalia vipi/anamjali vipi!...pia kama mwanafamilia huyu jamaa hana mtu wa kumsaidia hata kama kwao wote matajiri hana jirani mwenye shida?kumbuka ugomvi hapa sio kumpa mwanamke hela ugomvi ni kiasi anachompa angesema 300,000/= hakuna ambaye angeshangaa ila 1.4m huyu jamaa ni kuwakuchunguza.
 
kuna kitu umeficha hapa... from no where na msaada wote huo alete jeuri hiyo ? what 1.4m per month? kwani upo kwenye list ya makininikia ? long live jf, maisha ya mtanadoni na maisha ya kiuhalisia ni kama mafuta na maji kamwe haviwezi kulandana
 
Pole mkuu,ila naomba nikulize ki roho safi tuu,una muwaza kua nani atamsaidia tena baada yako,au bado kuna kijinafasi au vimazowea ume vi miss japo kua hana jipya,au ndio hayo mazowea yana tabu tabia zikilinga,au kuna mchezo mbaya wako hapendi amekubali kula bamia hataki mamilioni.
mwanamke kama ameamua kukujibu hivyo for sure yupo anaemtia jeuri, hiyo pesa nadhani kama still unataka kumsaidia wapo watu ukiwapa mwenyezi mungu atakulipa kheir zaidi na zaidi,wape wazee,peleka kwenye nyumba za ibada,wanunulie chakula watoto yatima,huyo hata hupati dhawabu zaidi ya thambi za Uzinzi...
 
Kuna huyu mdada single mother, ana watoto wawili. Nimekuwa naye for a while mwezi ujao tungefikisha miaka 2. Ukweli huyu dada nilimkuta na hali mbaya sana kiuchumi. Lakini uzuri wake uliweza kuonekana hata katika hiyo hali. Basi nikajitolea kumsaidia. Ana Degree na kazi ya kawaida, lakini alikopaga hela nyingi akaanza biashara ambayo haikumlipa ikafa. Hivyo Mshahara wake wote unakatwa. Anabaki na kama laki 3 tu kwa mwezi ambayo haimtoshi.

Basi nikawa na mlea na watoto wake. Ki ukweli toka tuanze nilikuwa nampa jumla ya tsh 1.4m kwa mwezi cash. Ikiwa ni nyumba laki 3, vicoba laki 2, matumizi laki 6, rejesho deni la vicoba laki 3. (Alikopa ada za watoto wake na some furniture).

Sasa cha ajabu huyu dada alianza kama kupoteza furaha na mimi, nikawa namuuliza nini shida anasema hakuna shida. Hali hiyo ikaendelea na akawa sasa hanitafuti wala kusalimia hadi mimi ndo nimuanze. Nikimuuliza anajibu tu kifupi kwamba hakuna shida yuko sawa, mara ya mwisho akanijibu kama unaona nimebadilika si uniache kwani umelazimishwa.

Kuanzia siku hiyo sijamtafuta wala hajanitafuta, ni mwezi sasa umepita. Ninachojiuliza huyu dada ana jeuri gani, anajiamini nini? Siamini kama ana mtu, ambaye anaweza kumuhudumia zaidi kuliko nilivyokuwa nafanya mimi. Kimsingi simuhitaji sana kwani alikuwa hana jipya zaidi ya kumzoea na kumpenda tu, ila namuonea huruma. Nimejikuta nawaza sana juu ya hatima ya maisha yake. Sijui ni kwanini. Naombeni ushauri.
1.4 kwa mwaka mzma ukichanga unajenga nyumba ya vyumba vitatu na unahamia! au bora hata usomeshe ndugu zako kumi watakusaidia bdae
 
Cjui Nani katuloga wanaume huyodada anakazi take na ulimkuta na maisha take sasa hizi 1.4m peleka kwa maskini au wale machangudoa sio unajigandisha gandisha tu hapo
 
Kibo cha ndesi!!!huyu mwanamke jinga sana watu na vibaru vyetu na hatufiki hiyo pesa kwa mwezi,, yeye anapiga teke roba LA almasi kweli??uwiiiiii nimechanganyikiwa
 
Back
Top Bottom