Simuelewi wifi yangu

Simuelewi wifi yangu

Huyo ni mtu mstaarabu sana sababu hapo ni kwako sasa akikurupuka mpaka jikoni wakati hajakaribishwa ungesema anakuingilia!!!!!!!
Either ways wewe siku ya tatu tu ushaanza mpaka ku post huku, je angekuja mgonjwa kukaa hapo mwezi mzima!!!????
Kwanza wewe mtu wa kazini so hushindi hapo kazi anafanya dada labda sasa wewe nini taabu yako!!!!???
Leo wkend kesho sikukuu muamshe mwambie mwende sokoni mkanunue vya kununua na mkija fikia naye jikoni mpe nyanya muombe akusaidie wakati wewe unafanya mengine then anzisha story kuwa uko happy kwa ujio wake sababu sikukuu mtapika vyakula mbalimbali kwa kushirikiana, mtamaliza mapema na ku enjoy.................


Sikuhukumu ila ni kama hupendi ndugu wa mume au una ghubu flani kama sio mvivu..........ungekuwa mke wangu ningekuchana live!!!!!




Dah!!!!!!
 
Kila binadamu ana mahitaji yake, maana wanawake wenzako wengi huwa hawapendi kuingiliwa jikoni na wengi hulalamika kwamba wifi yake anamwona kama hajui kupika ndio anaamua kuingia jikoni. Mpigishe story maana wakati mwingine labda na yeye ana lake la moyoni "ukute anajisemea wifi yangu sio "user friendly" maana hata haonyeshi uso wa tabasamu"
 
Yani mwalimu wa watu kaja likizo ya pasaka we unataka mfanya awe house gelo!

Nani alikua kungwi wako?
 
Kila binadamu ana mahitaji yake, maana wanawake wenzako wengi huwa hawapendi kuingiliwa jikoni na wengi hulalamika kwamba wifi yake planamwona kama hajui kupika ndio anaamua kuingia jikoni. Mpigishe story maana wakati mwingine labda na yeye ana lake la moyoni "ukute anajisemea wifi yangu sio "user friendly" maana hata haonyeshi uso wa tabasamu"

Kweli kabisa ndugu me nilikuwa course for sometimes kaka zangu wakawa wananiomba niende kwao nasema wananiomba coz wifi zangu nahisi wanna tabia za mleta thread so huwa siendi Nyumba Zao without justifiable reasons.Basi hawa mawifi kila mja kwa Nyumba yake wanapenda vitu vya supermarket.so nikifika watoto wanaanza kuomba niwapikie mostly chapati wao wamezoea za Azam au pilau kumbe bwana me nafikiri nasaidia watu roho zinawapasuka na ukizingatia nikipika watoto na baba wote wanasifia nikaja kupata maneno huko mbali lo tangu hapo nikilazimika kwenda nafua shuka nitakayolalia na sahani nitakayolia though I feel sorry for the babies.cjui tuna tatizo gani
 
Anzisha maongezi ya kiuwanawake huku ukimwonyesha kumchangamkia, ukiwa unaenda jikoni unamwita wifi njoo, huku mkiwa mnaendelea na maongezi unamwambia wifi leo nataka nionje mapishi yako, hebu pika nionje chakula cha wifi yangu ukionyesha hali ya kumchangamkia.

Ni bora umuambie kuliko kukaa na kitu moyoni, binadamu tunatofautiana - wengine hadi umfahamishe au umuelekeze ndio mipangilio inaenda sawa
 
Kweli kabisa ndugu me nilikuwa course for sometimes kaka zangu wakawa wananiomba niende kwao nasema wananiomba coz wifi zangu nahisi wanna tabia za mleta thread so huwa siendi Nyumba Zao without justifiable reasons.Basi hawa mawifi kila mja kwa Nyumba yake wanapenda vitu vya supermarket.so nikifika watoto wanaanza kuomba niwapikie mostly chapati wao wamezoea za Azam au pilau kumbe bwana me nafikiri nasaidia watu roho zinawapasuka na ukizingatia nikipika watoto na baba wote wanasifia nikaja kupata maneno huko mbali lo tangu hapo nikilazimika kwenda nafua shuka nitakayolalia na sahani nitakayolia though I feel sorry for the babies.cjui tuna tatizo gani

Halafu wakiitwa wachawi wanalia. Manina! Pole sana.
 
Duh...! Mleta mada kachanwachanwa humu hadi huruma maskini....inaonekana alikurupuka! ha ha aha aha aha ah ah aha!

cc. MamaBeata

aisee! Sio masihara. Dada wa watu kala za uso mpaka kaingia mitin nafikir anajuta kuleta uzi huu..... Mpaka anaionea aibu jf nzima hahahaa jf ina mambo kudadek! Ukija resi utarud umelowa hahahahaaa!
 
Last edited by a moderator:
Wifi yangu amekuja juzi. Ni dada wa mume wangu. Alipofika sikuwepo nilikua kazini. Nilipofika toka kazini nikamkuta amelala. Nikamsubiri alipoamka akaja tukatambulishana tukaendelea na maongezi.

Jana siku ya pili kaamka kaoga kawasha tv, akitoka anaenda kulala. Anaamka anakula anarudi kulala. Leo siku ya tatu ameamka mapema tu ameoga karudi tena kulala. Mwenzenu Simuelewi huyu mwanamke mwenzangu hata mlango wa jikoni haujui. Nimekua kama nina waume wawili. Kuolewa kuna shida wenzangu.

Du.. mwanamke wewe una majanga kweli, hilo ni jambo la kupost hapa kweli? Si mbaya sana umetusaidia kujua tabia yako kuwa hujafundika. u mwanamke wa kidijitali. Unataka wageni wakija kwako wawe watumishi wa ndani? yaelekea wewe ni mvivu saaana hata huko kazini usipojihadhari utagombana na boss wako.
 
Acha udhalilishaji wewe..walikufuta kamasi hao leo hii unawatukana hata haya huna.......kwa taarifa yako hakuna watu wenye busara na wanaojua kushi na watu kama walimu....shika adabu yako

mkuu ww ni mwlm nn! Mbona unakuj juu sana akisemwa mwlm kwa mabaya?!
 
Wifi tu unalalamika, je akija mkwe anaumwa, kapooza anahitaji kuogeshwa, kufuliwa na kufanyiwa kazi zote si ndo utamsimulia mtaa mzima? Angekuwa ndugu yako ungekuja kumsema huku?
Acha roho mbaya mwanamke. Ndugu wa mumeo ni wako pia. Unaonekana una majungu sana.

mkuu huyo mwanamke ni sehem ya tatizo. Anaonekana mchoyo sana....... Amekosea step huyu. Kwanaza kanyweaaa
 
MamaBeata unaweza kunipa contact za huyo wifi yako ..Hakika nimegundua kumbe mwanamke akisomea ualimu akauelewa anakuwa na uwezo mkubwa wa kuishi na wadada kama wewe MamaBeata tafadhali naomba mawasiliano yake..
 
MamaBeata unaweza kunipa contact za huyo wifi yako ..Hakika nimegundua kumbe mwanamke akisomea ualimu akauelewa anakuwa na uwezo mkubwa wa kuishi na wadada kama wewe MamaBeata tafadhali naomba mawasiliano yake..

Ama kweli akili unazo
 
Naona kama intrusion of privacy aisee.

Naanzaje kuingia kwa wenyewe jikoni naanza kupika. Ndio kujionyesha fundi au?

Wakiniomba sawa tena nitafurahia but azawais I keep off.

Mi nadhan hamjamuelewa huyu dada
 
Ndio sababu watu huambiwa wakaoe/olewa kwao kama ulikuwa hujagundua.


Kwa kifupi umekosea.
Umekosea mtazamo
Umeanza kwa mguu wa kushoto uhusiano wako na yeye

Mimi nilikokulia inategewa kila mgeni wa kike akija akae na wenyeji wake wa kike popote walipo. Nipoolewa nilipata shock sema nilishatijayarisha kisaikolojia kwa kufundwa, ndugu wa ikoo wa mume wangu tangu nilipokabidhiwa jiko, hawaruhusiwi kuliingia tena!!! ni taboo, na kuonyesha dharau kwangu eti.
Ilichukua muda ila niliwapenda sana nao walinipenda so kwa wao kujua nilikotokea huwa wananiambia nipeleke vitu vya kutayarisha eg karoti etc sehemu ingine wakasaidie. Wanoko wakiondoka basi na wao wanaingia jikoni.

Muite wifi yako, mkaribishe, mpe ruhusa, muelekeze mabo yako ya jikoni, mwombe msaada wa mawazo, kazi etc

U r the real definition of a wife
Hongera
 
Back
Top Bottom