Simuelewi wifi yangu

Simuelewi wifi yangu

Wifi tu unalalamika, je akija mkwe anaumwa, kapooza anahitaji kuogeshwa, kufuliwa na kufanyiwa kazi zote si ndo utamsimulia mtaa mzima? Angekuwa ndugu yako ungekuja kumsema huku?
Acha roho mbaya mwanamke. Ndugu wa mumeo ni wako pia. Unaonekana una majungu sana.
 
Ni nyumbani kwako,sehemu ya utawala wako...jambo halikuridhishi-lirekebishe papo hapo kabla ya kuja kuanzisha uzi huku.

A phenomenal woman rules her home strictly but politely.

*epuka majungu....mapema mno kumuhukumu wifi.
 
Ushauri tele chukua ule mzuri halafu rudi hapa na majibu sasa nikiamini wote hamtakuwa vikwazo kama ambavyo mwenye nyumba ulitaka kufanya.
 
Mi kwa kweli jikoni kwangu ndiko ufalme Wang ulipo.naamini hivyo hats nikienda kwa mtu.
Unless uniambie njoo tupike.
Kila nyumba na kila mwanamke ana namna yake ya upishi.
Sitegemei mdada analilia mtu kuingia jikoni kwake.

Kupika utapika mwenyewe, hata kuoshewa sahani nako kutakuwa na formula? Labda tu mtoa mada ametoa upande wa jiko kama kiwakilishi, si mgeni angevunga hata kupiga deki? Mimi kwa kweli ugenini huwa najistukia kukaa bure wakati wenye nyumba wanachacharika, labda na wao wajidai kukataa msaada.
 
ni mapema mno kumhukumu, yaani wifi kukaa siku 3 tu umeshasema kuolewa ni kazi! acha roho mbaya dada, watu tunaishi na mamamkwe mwaka wa 11 na tupo pouwa kabisa. ingekuw wewe si ungehama nyumba! mama mkwe humtumi yy ndio anakutuma upo?
 
....unabahati kupata wifi mstaarabu kama huyu,maana anazingatia mipaka yake. hajui kaka anapenda kula nini, saa ngapi,chakula kipikwe vipi,chimvi kiasi gani au hatumii chumvi. wakati mwingine wanaume tunapenda chakula kipikwe na wake zetu n.k. Mtazamo wangu naona tatizo lipo kwako tayari una mtazamo hasi juu yake. jaribu kumwambia taratibu za nyumbani kwako kama atashindwa ndo umlaumu,vinginevyo sioni tatizo lolote. yeye ameaga anakuja kupumzika kwa kakayake kama unataka akusaidie mwambie....
 
Huyo ni mtu mstaarabu sana sababu hapo ni kwako sasa akikurupuka mpaka jikoni wakati hajakaribishwa ungesema anakuingilia!!!!!!!
Either ways wewe siku ya tatu tu ushaanza mpaka ku post huku, je angekuja mgonjwa kukaa hapo mwezi mzima!!!????
Kwanza wewe mtu wa kazini so hushindi hapo kazi anafanya dada labda sasa wewe nini taabu yako!!!!???
Leo wkend kesho sikukuu muamshe mwambie mwende sokoni mkanunue vya kununua na mkija fikia naye jikoni mpe nyanya muombe akusaidie wakati wewe unafanya mengine then anzisha story kuwa uko happy kwa ujio wake sababu sikukuu mtapika vyakula mbalimbali kwa kushirikiana, mtamaliza mapema na ku enjoy.................


Sikuhukumu ila ni kama hupendi ndugu wa mume au una ghubu flani kama sio mvivu..........ungekuwa mke wangu ningekuchana live!!!!!
OLESAIDIMU pokea like 1000!Umenena kwa busara,safi sana!
 
Last edited by a moderator:
....unabahati kupata wifi mstaarabu kama huyu,maana anazingatia mipaka yake. hajui kaka anapenda kula nini, saa ngapi,chakula kipikwe vipi,chimvi kiasi gani au hatumii chumvi. wakati mwingine wanaume tunapenda chakula kipikwe na wake zetu n.k. Mtazamo wangu naona tatizo lipo kwako tayari una mtazamo hasi juu yake. jaribu kumwambia taratibu za nyumbani kwako kama atashindwa ndo umlaumu,vinginevyo sioni tatizo lolote. yeye ameaga anakuja kupumzika kwa kakayake kama unataka akusaidie mwambie....

Kaka Gefu nilikuwa nakusalimu!!!!!!
 
Last edited by a moderator:
Mama beata hasira za humu usije ukaenda kuzihamishia kwa wifi yako!!

Ukileta ujuaji humu utanyooshwa tu!
 
Kwani kaja kupika acha mawazo yakijinga kumuhudumia wifi yako sisababu yakuhoji kama umeolewa na watu wawili huow niuswahili nawanaokudanganya hawaitakii mema ndoa yako

Angekuwa baba mkwe kaja angesema hivyo?
 
Back
Top Bottom