Simuelewi wifi yangu

Simuelewi wifi yangu

Mbona huyo ndio bonge la wifi? Wanawake hatuna jema, angekuja akapita kila mahali huko jikoni ungesema anaharibu bajeti. Mie wifi zangu tunapendana kweli. Manake nikienda kwa kakangu nachangia stori na kuangalia tv! Na mgeni anaekaa tu hanipunguzii wala kuniongezea. Unaingia kwa watu unajipeleka jikoni unapika kuku, kumbe kuku wao kwenye friza anapikwa jumapili tu! Si ugomvi huo!

cha kufanya bi shosti asubuhi muulize wifi unajiskia kula nini? Kama hakipo muombe mumeo, muambie wifi ana hamu na kuku, naomba hela. Mbona utapendwa kote kote? Mnashindwa ndoa wenyewe!

Hivi dada,yule kibopa alikupiga kibuti kwasababu ya nini kweli?
 
Ndio sababu watu huambiwa wakaoe/olewa kwao kama ulikuwa hujagundua.


Kwa kifupi umekosea.
Umekosea mtazamo
Umeanza kwa mguu wa kushoto uhusiano wako na yeye

Mimi nilikokulia inategewa kila mgeni wa kike akija akae na wenyeji wake wa kike popote walipo. Nipoolewa nilipata shock sema nilishatijayarisha kisaikolojia kwa kufundwa, ndugu wa ikoo wa mume wangu tangu nilipokabidhiwa jiko, hawaruhusiwi kuliingia tena!!! ni taboo, na kuonyesha dharau kwangu eti.
Ilichukua muda ila niliwapenda sana nao walinipenda so kwa wao kujua nilikotokea huwa wananiambia nipeleke vitu vya kutayarisha eg karoti etc sehemu ingine wakasaidie. Wanoko wakiondoka basi na wao wanaingia jikoni.

Muite wifi yako, mkaribishe, mpe ruhusa, muelekeze mabo yako ya jikoni, mwombe msaada wa mawazo, kazi etc
 
Wifi yako labda ana jetlagged, mpe uhuru apoze moyo wake na akili yake.
Maisha yana mengi
 
Tatizo wapo wachache na waoaji tupo wengi!!

Hapo maombi yanashindana,ukipewa galasa ulie na moyo wako!

Ndoa ni kazi ngumu ila lazima tuifanye!!

Kaka sababu nao wanachagua basi we hakikisha una vigezo husika tu......mbona watakuchagua tu halafu utachagua uzao mwema kwa raha zako!!!!

Inafanyika hiyo kazi kaka umakini tu !!!!!
 
Wee usitafute ugomvi nae mwache tu akae, mwisho atajistukia mwenyewe ataondoke ama ataanza kufanya kazi!

Sio rahisi mkuu
But nadhani anapaswa kuongea na mumewe maana asijeambiwa "WiFi ana gubu lol"
 
kikawaida mgeni ni siku tatu....ikifika siku ya 4 sio mgeni tena....toka mwanzo sio mgeni ila ni sahihi kumpa siku tatu za mapumziko...siku ya 4 jaribu kutumia Hikma....unaweza kumuuliza wifi eti we mwenzangu chakula gani unakipatia vizuri kukipika? atakujbu ikesha utakitafuta chakula hicho ataazakupika....na hapo utaandaaa mazingira ya kuasiadiana nae...na hapo ndo itakua mwanzo...jenga nae urafiki mpaka uweze kuuteka moyo wake.....au umesahahu ule usemi "Don't fight with them wins their Heart"
 
Wewe ndio umekosea
Kawaida mgeni akifika kwako siku ya kwanza tu unampa utaratibu wa nyumba yako

Pili unatakiwa kujua anakaa muda gani

Ikifika siku ya tatu unampa majukumu

Anyway unasema wifi yako umetambulishwa, ina maana ulijua humjui? Ammmh asije akawa wiiiiiifyiiiiiiii badala ya wifi (joking.....)

Ila seriously dawa ni kuzungumza nae na kumpa majukumu
Sio kila mtu ana mshipa wa aibu aanze kujishughulisha halafu ukizingatia ni mgeni mara ya kwanza, hawezi kukurupuka na kuingia jikoni bila kumshika mkono
Awazoee
Aizoee nyumba
Ajue mnaishije
 
Mi kwa kweli jikoni kwangu ndiko ufalme Wang ulipo.naamini hivyo hats nikienda kwa mtu.
Unless uniambie njoo tupike.
Kila nyumba na kila mwanamke ana namna yake ya upishi.
Sitegemei mdada analilia mtu kuingia jikoni kwake.

Haswaaa
Ukifika kwa mtu jikoni shurti ukaribishwe

Sio uamke uingie jikoni ukiitwa mroho je?
Lazima usome mazingira

Ila wifi nae si angekua anashinda na wenzie
 
Dah kuoa shida sana mawifi,mashemeji mara mwanandoa wenyewe vurugu tupu.
 
Back
Top Bottom