Simu za mezani Ikulu ya Chamwino hazipokelewi

Simu za mezani Ikulu ya Chamwino hazipokelewi

MzeeKipusa

JF-Expert Member
Joined
Feb 10, 2023
Posts
2,705
Reaction score
4,978
Kwema Ndugu zangu,

Hii sasa ni ya pata nusu mwaka, kila nikipiga namba zilizopo kwenye tovuti ya Rais Samia (www.ikulu.go.tz) hazipokelewi kabisa. Zinakua zinaita tu bila kupokelewa.

Ina maana ofisi ya Rais haina maPS? Na je kwanini namba hizo huwekwa kwenye nyaraka za Serikali ( Barua )?

Kwani kupokea simu inachukua muda gani Ndugu zangu wa hapo Chamwino Ikulu? Mbona mnaringa sana nyie watu? Mbona mnajisikia sana asee? Tutawapataje sasa, kama kupokea simu za ofisi hamtaki?

Kuna umaana gani sasa wa kuweka hizi namba za simu kwenye barua zenu kama kupokea simu inakua shida, asee hebu kuweni na utu hata kidogo basi.

Hizo ni ofisi tu Ndugu zangu na mtaziacha, msifikiri mtakaa humo milele. Utaratibu wa hovyo sana huo. Yaani watu wanawapigia simu, nyie mnakua mnaziangalia tu huku mkipiga story ofisini.

NAMBA ZA SIMU HIZI: 0262961500 na 0262961501 HAZIPOKELEWI KABISA HAPO CHAMWINO IKULU DODOMA.
 
Kwema Ndugu zangu,

Hii sasa ni ya pata nusu mwaka....kila nikipiga namba zilizopo kwenye tovuti ya Rais SAMIA ( www.ikulu.go.tz ) hazipokelewi kabisa.

Zinakua zinaita tu bila kupokelewa.

Ina maana ofisi ya Rais haina maPS? Na je kwanini namba hizo huwekwa kwenye nyaraka za Serikali ( Barua ) ?

Kwani kupokea simu inachukua muda gani Ndugu zangu wa hapo Chamwino IKULU? Mbona mnalinga sana nyie watu? Mbona mnajisikia sana asee? Tutawapataje sasa, kama kupokea simu za ofisi hamtaki??!!!

Kuna umaana gani sasa wa kuweka hizi namba za simu kwenye barua zenu kama kupokea simu inakua shida...asee...ebu kuweni na UTU hata kidogo. Hizo ni ofisi tu na mtaziacha, msifikiri mtakaa humo milele!..Utaratibu wa hovyo sana huo!!! Yani watu wanawapigia simu , nyie mnakua mnaziangalia tu huku mkipiga story za mapenzi ofisini + umbea

NAMBA ZA SIMU HIZI : 0262961500 na 0262961501 HAZIPOKELEWI KABISA HAPO CHAMWINO IKULU DODOMA.


Ova
Unaweza kuwalaumu Ikulu kumbe shida iko kwa mtoa huduma, usishangse ukiambiwa zinaishia TTCL Ikulu haziwafikii.
 
Dharau Kubwa Sana Mwananchi Anapiga Simu Lakini Inaitaaa Haipokelewi

Msemaji Wa Serikali Ama Kurugenzi Ya Mawasiliano Ikulu Ya Chamwino
Ije Hadharani Kutoa Ufafanuzi Laa Sivyo Number Hizo Zifutwe Kwenye Nyaraka Za Serikali
Wanajisikia sana hapo Chamwino IKULU.

Usikute kuna limtu limejaa mi UTI, limewaamrisha maPS wasipokee hizo simu, bila kujali wala kuwa na huruma Wananchi Kukosa huduma hiyo. Bure kabisa!!!

Nasemaje...hilo limtu litakufa soon na litaicha hiyo ofisi.
 
Unaweza kuwalaumu Ikulu kumbe shida iko kwa mtoa huduma, usishangse ukiambiwa zinaishia TTCL Ikulu haziwafikii.
Ikulu ni ofisi kubwa sana. Kuna watu wa Usalama+ kuna ma IT makini sana....kuna MaPs wasomi kabisa....sidhani kama haziiti huko ofisini kwao. Ni ujeuri tu ndio wanaoutumia. Kujisahau na kujiona wamefika,..kana kwamba watakua kwenye ofisi hiyo milele. #UkosefuWaAkili
 
Mambo ni mengi Wacha la dp world liishe kwanza pengine wako bize nalo
Wangekua wako busy nalo wasingesubhutu kwenda Mwanza. Hilo walishalimaliza kitambo sana...na walishajua nini kitatokea. Ndio maana unawaona wakiendelea kucheza draft.

KELELE ZA CHURA HAZIMZUII TEMBO KUNYWA MAJI
 
Back
Top Bottom