Simu za mezani Ikulu ya Chamwino hazipokelewi

Simu za mezani Ikulu ya Chamwino hazipokelewi

Ok ,..niliwahi kumsikia dk.Mpango akiwaonya watumishi wasiwasiliane kwà njia ya WHATSAPP....

Kwahiyo kumbe Serikali hii ina mawasiliano mengine ya WhatsApp ambayo Wananchi hawana taarifa nayo?
 
Naomba namba yake au email address yake.

Halafu , mbona wakati wa Hayati Magufuli au Marehemu Kikwete zilikua zinapokelewa tu? Kulikoni sasa hivi kwenye huu Uongozi wa huyu Mama?
Tukikuomba ushahidi wa haya utatuonyesha? Kwamba kweli kwa mwaka ulipiga namba hazipokelewi na wakati wa awamu zilizopita zilikuwa zinapokelewa?
 
Kwema Ndugu zangu,

Hii sasa ni ya pata nusu mwaka, kila nikipiga namba zilizopo kwenye tovuti ya Rais Samia (www.ikulu.go.tz) hazipokelewi kabisa. Zinakua zinaita tu bila kupokelewa.

Ina maana ofisi ya Rais haina maPS? Na je kwanini namba hizo huwekwa kwenye nyaraka za Serikali ( Barua )?

Kwani kupokea simu inachukua muda gani Ndugu zangu wa hapo Chamwino Ikulu? Mbona mnaringa sana nyie watu? Mbona mnajisikia sana asee? Tutawapataje sasa, kama kupokea simu za ofisi hamtaki?

Kuna umaana gani sasa wa kuweka hizi namba za simu kwenye barua zenu kama kupokea simu inakua shida, asee hebu kuweni na utu hata kidogo basi.

Hizo ni ofisi tu Ndugu zangu na mtaziacha, msifikiri mtakaa humo milele. Utaratibu wa hovyo sana huo. Yaani watu wanawapigia simu, nyie mnakua mnaziangalia tu huku mkipiga story ofisini.

NAMBA ZA SIMU HIZI: 0262961500 na 0262961501 HAZIPOKELEWI KABISA HAPO CHAMWINO IKULU DODOMA.
Unawaonea tu, watumishi wa umma nchi hii wao wanajua kuvaa na kwenda ofisini kusaini posho za vikao,hayo mengine ni ziada tu.Mimi mwenyewe nimetuma barua ya malalamiko ofisi ya Katibu Mkuu Kiongozi tangu mwezi wa pili mpaka leo sijajibiwa!
 
Tukikuomba ushahidi wa haya utatuonyesha? Kwamba kweli kwa mwaka ulipiga namba hazipokelewi na wakati wa awamu zilizopita zilikuwa zinapokelewa?
Ndiyo. Nitathibitisha.

Ikulu ya Dar, simu zilikua zinapokelewa vizuri sana....ukisikilizwa....then kama issue yako ni nyepesi na inaeleweka...unajibiwa palepale....na kama huyo aliyepokea simu hana taarifa za kutosha...basi anakwambia subiri...then utasikia inapokelewa na mtu mwingine.
 
Tupo kwa muda wacha waringe life is a circle hawajui mtaani kuna siku watu watakua wanahadithia watu usimuone hivyo huyo mzee kafanya kazi ikulu huyo
 
Acha kupotosha bwana mbona mi nimepiga ijumaa na imepokelewa vzr na kupewa ushirikiano mzuri sana
 
Unataka ujue jina ili iweje?jua cm zinapokelewa Rais haondoki na ofisi ikulu ina maelfu ya wafanyakazi
 
Jamaa hawapokei , tangu Jumatatu nawapigia hadi leo, hawapokei tu.
 
Back
Top Bottom