Simu ya mwenza wako ya nini? Unajipa presha bure

Simu ya mwenza wako ya nini? Unajipa presha bure

Nimuamua kushare na nyie huu ujumbe nimekutana nao sehemu ili uwe na Amani ya moyo fanya hivi.

Kwa wanandoa na wenye wapenzi waaminifu.
uaminifu limekuwa ni jambo la msingi sana ili udumu na huyo uliyeingia naye kwenye ndoa, mjengee imani kuwa wewe ni wake na haitatokea siku ukamsaliti.

Lakini wakati ukweli ukiwa hivyo, kwenye baadhi ya ndoa kuna sarakasi nyingi sana. Katika ulimwengu wa sasa kumekuwa na tatizo kubwa la baadhi ya wanandoa kutibuana kila siku kisa kikiwa
ni kutokuaminiana kupitia simu zao. Kwa hili niseme tu kwamba, ni wanandoa wachache sana ambao wanaamini simu za wenza wao hazina madhambi, wengi wanahisi wanasalitiwa kupitia simu na ndiyo maana unaweza kukuta mke akishika simu ya mumewe tu inakuwa shida.

Si hivyo tu, wapo wake za watu nao hawataki kabisa simu zao zishikwe na waume zao, unajiuliza kwa nini iwe hivyo kama kila mtu anajiamini? Lakini sasa, leo naomba niwashauri kitu wale walioingia kwenye ndoa. Kuna mambo ambayo unatakiwa kuyapuuza laa sivyo huwezi kuwa na amani katika maisha yako. Kama kweli unampenda huyo uliyenaye, usimfikirie vibaya! Jenga imani kuwa,
hawezi kukusaliti.

Hii tabia kwamba simu ya mwenza wako ikiita tu unachungulia kujua nani kapiga, SMS ikiingia unafungua, ya nini kujipa presha? Hivi unadhani kweli unaweza kumzuia huyo mwenza wako asikusaliti kwa kutompa uhuru wa simu yake? Hili ni gumu hivyo unachotakiwa kufanya ni kumuacha na simu yake. Usijipe presha zisizo na msingi.

Unaweza kukurupuka, ukapokea simu ya mumeo, mara unakutana na sauti nyororo ya msichana, presha inakupanda bila kujua aliyepiga ni nani. Na yeye kwa kuwa aliyepokea siye aliyempigia, anakata. Wewe huko uliko unachanganyikiwa, unafikiri aliyepiga ni mchepuko. Kumbe aliyepiga labda ni mfanyakazi mwenzake
au rafiki yake wa kawaida tu. Wewe unakuja juu na kumwambia mumeo anakusaliti, kumbe hamna kitu kama hicho.

Au wewe mwanaume unaweza kuchukua simu ya mkeo, ukaenda kwenye sehemu ya meseji ukitaka kujua ni nani huwa anachati nao. Bahati mbaya unakutana na meseji ya kimahaba iliyotumwa na mwanaume ambaye alikosea namba. Wewe bila kuwa na uhakika na kile ulichoona unakimbilia kuhitimisha kuwa, mke si muaminifu.

Hili ni tatizo kubwa ndiyo maana leo hii nimeona niwakumbushe tu kwamba, simu ya mwenza wako achana nayo ili kujihakikishia amani ya moyo wako.
23c55d4648bf05f379c437ced765d0f5.jpg
Mimi ninachoamini nikwamba watu kuaminiana au kutoaminiana kunakuja baada ya kuchunguzana sasa sijui kwamba kuna ubaya gani mimi kushika simu ya mpenzi wangu au yeye kushika simu yangu, ila katika maisha nimeishi na watu aina nyingi nahua nimejifunza sana suala la saikologia za binadamu..

Binadamu hana jambo zuri la milele wala jambo baya la milele

Iko hivi:-

1) Ukimkuta mwanamke/mwanaume mwaminifu katika mahusiano yake atakuambia jambo lakushika simu ya mpenzi wako nikawaida na hakuna ubaya kwasababu yeye anajiamini.

2) Ukikuta mwanaume/mwanamke ambaye sio muaminifu atakuambia kushika simu ya mpenzi wako hakuna maana yoyote niujinga nikutoaminiana nk lakini nikwasababu hataki yake ishikwe na anajua akishika ya mwenzake nayake itashikwa.

Huo ndio ufahamu wangu ila ningependa nimalize kwa kusema "Asilimia kubwa ya wanaopinga waizi wasichomwe moto kama sio waizi basi wana ndugu au watoto wezi"

Neno langu sio sheria
 
Shunie niwe mkwel sana kutoka moyon leo umeongea jambo la maana sana, Simu yako simu yangu kila mtu ana yake bas full stop sio kila dakika unanipekua pekua utasema mie mwizi bwana
 
TUNACHOTAKIWA KUJUA WANAUME NI KWAMBA MWANAMKE ANAWINDWA NA WATU MBALIMBALI BILA HATA YEYE KUJUA HIVYO TUNATAKIWA KUWA WAELEWA NA KINGINE MADADA MUWE MUNAWASHIRIKISHA WAPENZI WENU KAMA KUNA MWANAUME ANAKUSUMBUA NA UMEMUAMBIA UNA MTU WAKO LAKINI BADO ANAKUSUMBUA HII ITASAIDIA KUJENGA UAMINIFU KWENYE MAPENZI
 
Asante
 
Asante kaka eddy tumekusikia tutakuwa tunawaambia tukisumbuliwa
 
Shunie niwe mkwel sana kutoka moyon leo umeongea jambo la maana sana, Simu yako simu yangu kila mtu ana yake bas full stop sio kila dakika unanipekua pekua utasema mie mwizi bwana
hivi siku nyingine naongeaga uongo eenh kila mtu abaki na simu yake jamani ili tuishi maisha marefu kupekuana sio kuzuri bado tunahitaji kuishi
 
Sina huo muda aisee moyo wangu nnavyoupenda sipend kuupa shida aisee kama siwez kumuacha ya nn nmchunguze?
umeona Bonny kama umemchoka mtu mnataka kuachana ndio muanze kuchunguzana ili umtafutie sababu
 
Back
Top Bottom