Simu ya mwenza wako ya nini? Unajipa presha bure

Shunie

JF-Expert Member
Aug 14, 2016
127,187
2,000
Nimuamua kushare na nyie huu ujumbe nimekutana nao sehemu ili uwe na Amani ya moyo fanya hivi;

Kwa wanandoa na wenye wapenzi waaminifu, uaminifu limekuwa ni jambo la msingi sana ili udumu na huyo uliyeingia naye kwenye ndoa, mjengee imani kuwa wewe ni wake na haitatokea siku ukamsaliti.

Lakini wakati ukweli ukiwa hivyo, kwenye baadhi ya ndoa kuna sarakasi nyingi sana. Katika ulimwengu wa sasa kumekuwa na tatizo kubwa la baadhi ya wanandoa kutibuana kila siku kisa kikiwa ni kutokuaminiana kupitia simu zao.

Kwa hili niseme tu kwamba, ni wanandoa wachache sana ambao wanaamini simu za wenza wao hazina madhambi, wengi wanahisi wanasalitiwa kupitia simu na ndiyo maana unaweza kukuta mke akishika simu ya mumewe tu inakuwa shida.

Si hivyo tu, wapo wake za watu nao hawataki kabisa simu zao zishikwe na waume zao, unajiuliza kwa nini iwe hivyo kama kila mtu anajiamini? Lakini sasa, leo naomba niwashauri kitu wale walioingia kwenye ndoa.

Kuna mambo ambayo unatakiwa kuyapuuza laa sivyo huwezi kuwa na amani katika maisha yako. Kama kweli unampenda huyo uliyenaye, usimfikirie vibaya! Jenga imani kuwa, hawezi kukusaliti.

Hii tabia kwamba simu ya mwenza wako ikiita tu unachungulia kujua nani kapiga, SMS ikiingia unafungua, ya nini kujipa presha? Hivi unadhani kweli unaweza kumzuia huyo mwenza wako asikusaliti kwa kutompa uhuru wa simu yake? Hili ni gumu hivyo unachotakiwa kufanya ni kumuacha na simu yake. Usijipe presha zisizo na msingi.

Unaweza kukurupuka, ukapokea simu ya mumeo, mara unakutana na sauti nyororo ya msichana, presha inakupanda bila kujua aliyepiga ni nani. Na yeye kwa kuwa aliyepokea siye aliyempigia, anakata.

Wewe huko uliko unachanganyikiwa, unafikiri aliyepiga ni mchepuko. Kumbe aliyepiga labda ni mfanyakazi mwenzake au rafiki yake wa kawaida tu. Wewe unakuja juu na kumwambia mumeo anakusaliti, kumbe hamna kitu kama hicho.

Au wewe mwanaume unaweza kuchukua simu ya mkeo, ukaenda kwenye sehemu ya meseji ukitaka kujua ni nani huwa anachati nao. Bahati mbaya unakutana na meseji ya kimahaba iliyotumwa na mwanaume ambaye alikosea namba. Wewe bila kuwa na uhakika na kile ulichoona unakimbilia kuhitimisha kuwa, mke si muaminifu.

Hili ni tatizo kubwa ndiyo maana leo hii nimeona niwakumbushe tu kwamba, simu ya mwenza wako achana nayo ili kujihakikishia amani ya moyo wako.
23c55d4648bf05f379c437ced765d0f5.jpg
 

Shunie

JF-Expert Member
Aug 14, 2016
127,187
2,000
Daah. Sitaki kukumbuka huo ugonjwa wangu wa zamani sababu nilitaka kubaki mifupa mana nilikuwa na mawazo hasi kila kukicha kumbe nilikuwa najimaliza mwenyewe.
basi tulikuwa wote ndugu mwanzoni nilikua napata shida sana jaman yaan nikiona simu yake hapo naitamani halaf mwisho ninayokutana nayo navimba nalia aisee ila sasa hivi aache simu yake hapo atakutana na missed calls zake na text
 

General Mangi

JF-Expert Member
Dec 21, 2013
14,972
2,000
basi tulikuwa wote ndugu mwanzoni nilikua napata shida sana jaman yaan nikiona simu yake hapo naitamani halaf mwisho ninayokutana nayo navimba nalia aisee ila sasa hivi aache simu yake hapo atakutana na missed calls zake na text
Wangu amekoma, nilimuonya mapema aachane na simu yangu.
Mbaya zaidi sijaweka password.

Hata iweje hashiki tena.
 

Shadeeya

JF-Expert Member
Mar 12, 2014
40,857
2,000
basi tulikuwa wote ndugu mwanzoni nilikua napata shida sana jaman yaan nikiona simu yake hapo naitamani halaf mwisho ninayokutana nayo navimba nalia aisee ila sasa hivi aache simu yake hapo atakutana na missed calls zake na text

Umeonaee japokuwa inachukua muda ila inapotokea kuzowea ile hali ya kuiacha wala haiwi shida tena na maisha yanakuwa mepesi kuliko kawaida.
 

Shunie

JF-Expert Member
Aug 14, 2016
127,187
2,000
Tatizo wivu unatofautiana hasa pale unapopenda na uyo MTU hauko tayari kumpoteza kwa MTU mwingine yoyote,...kuna watu wana wivu sio wa dunia ii,anahisi anataka kupasuka ,yaan anawashwa mda wote,...bwahahahaha
wivu lazima bana ujue
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom