Nawasabahi wanaMMU.
Ni Jumapili kama hii wiki moja imepita nilipokea simu ambayo imebadilisha maisha yangu na mtazamo wangu kuhusu mahusiano. Well, nilipokea simu na upande wa pili nikasikia sauti ya mwanamke, na kwa sauti ni mtu mzima.
Aliongea mengi na mwisho akaniambia kama unataka kujua zaidi kuhusu mume wako nitafute. Basi Jumatatu, akanipigia tena na nilikuwa nasita kuonana naye, basi akaanza kuniambia wewe hauko serious.
Basi kama wazungu wanavyosema - Curiosity killed the cat, but satisfaction brought it back.
Imagine kumeet na mtu haumfahamu then mawazo ya tindikali na mambo mengi yakanijia kichwani, nikaanza safari kuonana naye huku nasali novena takatifu.
Well sikuamini nilipokutana naye - ni mama mtu mzima na age diff kama 18 - 20 years. Basi nikampa heshima na kukaa, nikamuuliza mama ishu ni nini na ana mahusiano gani na mume wangu (nikidhania ni biashara) Aisee, mapigo ya moyo yalisimama sekunde kadhaa aliponiambia wanamahusiano ya kimapenzi.
Na aliponiona kama nashangaa as in seriously, akaniambia nijuwe na yeye pia ana hamu na hajakuwa na mwanamume 4 years baada ya ndoa yake ya miaka 28 kuvunjika.
Akanitolea na picha kabisa na roho inamuuma kweli kuhusu mume wangu na anajitetea hakumwambia ana mke na watoto.
To cut a long story short, wamekuwa na mahusiano miezi 3 na anavyoongea alikuwa ameambiwa mahusiano yaishe lakini she was not happy na inamuuma sana. Mwisho akaniambia mi ndoa ya 28 years imevunjika sembuse ww wa miaka michache.
Basi angesubiri na mimi nifikishe hiyo 28 na ndo amshambulie huyu kiumbe dhaifu. I am so angry, not for me only but for all those men who cheat on good women na wanawake ambao wanavunja ndoa za watu kwa ajili hawana self control au basi watafute wa rika yao.
There are some battles worth fighting but this one am throwing in my towel. Hivi mtu akikuambia ni shetani - seriously miezi 3 ni yeye tu shetani anamwandama?
Kuna mambo magumu napitia wakati huu, everything is looking down but this put the last nail on my coffin.
Swali - Why would a man take the risk of losing a diamond to pick stones?