Unajua inauma sana kuona jamii yetu haibadiliki sijui kwanini. Kuna maneno ya kutiana moyo kama vile ndoa ndoano, vumilia au ndoa ndivyo zilivyo kitu ambacho si kweli ndoa haziko hivyo. Ziko ndoa nyingi tu watu wanaheshimiana na kuthaminiana na tena neno kukosa uaminifu halipo miongoni mwao. Unajua ni kama mtu anaeishi karibu na vilabu vya pombe au sehemu wanazopika pombe . Huyo ukimuuliza jamii yetu ikoje atakuambia watu wote walevi kumbe si kweli ni kwasababu yeye mlevi ndio maana anaona aonavyo.Mzima Ablessed? Nimefurahi kukuona maana busara na hekima zako tulizikosa hapa jamvini. Natumai kila kitu kiko bomba.
Unajua inauma sana kuona jamii yetu haibadiliki sijui kwanini. Kuna maneno ya kutiana moyo kama vile ndoa ndoano, vumilia au ndoa ndivyo zilivyo kitu ambacho si kweli ndoa haziko hivyo. Ziko ndoa nyingi tu watu wanaheshimiana na kuthaminiana na tena neno kukosa uaminifu halipo miongoni mwao. Unajua ni kama mtu anaeishi karibu na vilabu vya pombe au sehemu wanazopika pombe . Huyo ukimuuliza jamii yetu ikoje atakuambia watu wote walevi kumbe si kweli ni kwasababu yeye mlevi ndio maana anaona aonavyo.
Matokeo ya hii mitazamo ni mmoja wa wanandoa anaishi jela huku huyu mwingine anatanua kwa kigezo cha udhaifu. So namuonea huruma bidada
sala zAko ndo mkombozi wako
jiulize huyo mtu mzima ovyooo
kajiamini nini mpaka kakufata kukupa live?
je km ni muong?picha zipo hata za kuunganishA!
usikurupuke anza uspy taratibu
ukweli utaujua
mi mwenzio (natoa ushuhuda )niliona mme wangu hana uhuru na simu yake ikipgwa silence tena saa 6 usiku sikuuliza nikasubir kalala nikachuku a simu nkakuta 7misd call,3dialled calls,4 ricvd calls za mtu mmoja
nikachukua namba asubuh kaondoka nkapiga mdada kapokea nkauliza unamjua fulani akasema simju nkamwambia sasa umjue usimjue huyo mtu ana mke na ana watoto na mi ndo mkewe siondoki leo walA kesho
dada akaanza kujishauashaua pale nsamehe mi kaniAmbia hana mke il sijatembea nae
nkamwambia mi sjui mtembee mruke ujumbe umeupata tena mwambie mkeo kanipigia
akaomba msamaha
AM SORY STORY NDEFU ila nataka nkwambie km ni kweli huyo mmama anatoka nae
hao ndo wanaume na ktk dunia hii UKITAKA MKAMILIFU MUUMBE MWENYEWE
Yes......
Unahalalisha mwanaume kuchepuka?
Jamani nyie mumeo alivyokuja akasemaje...
Hii thread inaniskitisha
Nawasabahi wanaMMU.
Ni Jumapili kama hii wiki moja imepita nilipokea simu ambayo imebadilisha maisha yangu na mtazamo wangu kuhusu mahusiano. Well, nilipokea simu na upande wa pili nikasikia sauti ya mwanamke, na kwa sauti ni mtu mzima.
Aliongea mengi na mwisho akaniambia kama unataka kujua zaidi kuhusu mume wako nitafute. Basi Jumatatu, akanipigia tena na nilikuwa nasita kuonana naye, basi akaanza kuniambia wewe hauko serious.
Basi kama wazungu wanavyosema - Curiosity killed the cat, but satisfaction brought it back.
Imagine kumeet na mtu haumfahamu then mawazo ya tindikali na mambo mengi yakanijia kichwani, nikaanza safari kuonana naye huku nasali novena takatifu.
Well sikuamini nilipokutana naye - ni mama mtu mzima na age diff kama 18 - 20 years. Basi nikampa heshima na kukaa, nikamuuliza mama ishu ni nini na ana mahusiano gani na mume wangu (nikidhania ni biashara) Aisee, mapigo ya moyo yalisimama sekunde kadhaa aliponiambia wanamahusiano ya kimapenzi.
Na aliponiona kama nashangaa as in seriously, akaniambia nijuwe na yeye pia ana hamu na hajakuwa na mwanamume 4 years baada ya ndoa yake ya miaka 28 kuvunjika.
Akanitolea na picha kabisa na roho inamuuma kweli kuhusu mume wangu na anajitetea hakumwambia ana mke na watoto.
To cut a long story short, wamekuwa na mahusiano miezi 3 na anavyoongea alikuwa ameambiwa mahusiano yaishe lakini she was not happy na inamuuma sana. Mwisho akaniambia mi ndoa ya 28 years imevunjika sembuse ww wa miaka michache.
Basi angesubiri na mimi nifikishe hiyo 28 na ndo amshambulie huyu kiumbe dhaifu. I am so angry, not for me only but for all those men who cheat on good women na wanawake ambao wanavunja ndoa za watu kwa ajili hawana self control au basi watafute wa rika yao.
There are some battles worth fighting but this one am throwing in my towel. Hivi mtu akikuambia ni shetani - seriously miezi 3 ni yeye tu shetani anamwandama?
Kuna mambo magumu napitia wakati huu, everything is looking down but this put the last nail on my coffin.
Swali - Why would a man take the risk of losing a diamond to pick stones?
Nina uhakika maana kanionesha picha ya mume wangu, Rafiki wa mume wangu alikiri na yeye mwenyewe nilimuuliza kama anamfahamu (majina yake niliyapata kupitia namba yake ya simu), na akajibu ni changudoa - baadae akakubali na kusema ni shetani. Huyo mama alitaka nijue alivyoniumiza na alitaka nimuache. Alimpigia hata mama mkwe simu na vitisho...Yaani sijapata drama aina hii maishani, na anajua very deep personal things about me.
Vipi venereal diseases? Hiyo siyo concern?
Au mpaka mtu aanze kutoa usaha kwenye papuchi ndo ajue kwamba 'ahaaa'......kumbe nipo hatarini?
Kwa nn mme wako alienda nje ya ndoa?Rekebisha kasoro hizo then msamehe mmeo maana mpinzani wako hayupo tena na mmeo!
Acheni mambo haya yenu ya kizungu ya kumpimia mme round za kitandani bana!
Huwezi kumake excuses kwa ajili ya mwenza anaekucheat. NEVER! Na wewe mkeo akikucheat unajirekebisha ili aache? Once a cheater, always a cheater. Huyu dada mie nimesita kumshauri kwa sababu it seems kuwa mumewe anamdepress kwa muda sasa. Mwisho wa siku inabidi aamue anaishije na anaishi na nani.
ni kweli unapopata habari kama hiyo lazima ikuume!!!
kuna hii formula huwa naifataga sana na nahisi inanisaidia kama upo tayari na wewe ifate tangu nimeanza kutumia sijagombana na mpenzi wangu ng'ooo!!!!
1.nikikatiwa simu nasema labda yupo sehemu mbaya nitamcheki baadae!!!
2.kama asipopokea simu nasema labda yupo mbali na simu ngoja nimcheki tena baadae!!!
3.akichelewa kurudi nasema labda kazi zilikuwa nyingi leo + foleni za daladala!!!
4.akipanic nasema labda hayupo sawa ngoja nimwache kidogo!!
5.nikiletewa taarifa ana mchepuko nasema wao wabaya nia yao nini hasa ngoja nipotezeee!!!
I am not a saint, but ninaamini a sinner also learns not to repeat the same mistake twice. Fahamu kwamba huyu huyu amenifanya nitumie depression drugs kwa muda wa mwaka mmoja. Ameambiwa ataje mapungufu yangu ameshindwa...
#Theo , unayoona au kudhani ni dhahabu haiwi kweli kwa kila mtu. Mmeo mpaka kutoka nje kuna 7bu. If you care, tafiti kisha tenda kurekebisha.