Niwafanye nini hawa watu..?

Niwafanye nini hawa watu..?

Too face

JF-Expert Member
Joined
Feb 9, 2015
Posts
243
Reaction score
226
Kwa muda mrefu nimekuwa nikimuhisi mwanamke mmoja kuwa na mahusiano na MUME wangu kutokana na charting zao ..na ubize WA simu WA MUME wangu..

Wiki iliyopita nikapata nafasi nzuri ya kukagua simu ya Mr hivyo ..nimethibitisha pasi na shaka kuwa wako katika mahusiano kutokana na majina ya kimapenzi wanayoitana,na MAWASILIANO ya mara kwa mara( karibu kila siku wanawasiliana asubuh,mchana Hadi usiku).

Nilichofanya niliscreenshot MESEJI zoote nikajitumia na sikuacha ushahidi wowote kama nilishika simu yake..MAISHA yanaendelea kama kawaida ...

Wote ni waajiriwa..Tuna miaka 10 ya ndoa(tulikubaliana kufunga ndoa ya serikali sisi wenyewe bila kushirikisha wazazi hivyo hata mashahidi hawakuwa ndugu zetu Wala rafiki zetu japo MAHARI ALITOA na taratibu zingine zilifuatwa. Hivyo tukaanza kuishi pamoja ili tukijipata tufunge ndoa ya kanisani) , ..but Hadi leo hatujafanikiwa kuwa na ndoa ya kanisani.

Tuna watoto 4( mmoja WA mama mwingine mkubwa kwa watoto wangu jhakuwahi kunieleza kabla ..niligundua baada ya kuanza kuishi pamoja... lakini MAISHA yaliendelea)

Sikuwa na tabia ya kumchunguza Mume wangu apo mwanzo Kilichonifanya nianze kumchunguza ni mabadiliko ya muda mrefu yaliyopo ndani( miaka kama 4 sasa )dharau ,MAPUUZA, kutokujali mambo..Kuna KIPINDI aliwahi kunipiga,kunifungia mlango nje Tena nikiwa na mtoto mdogo WA miezi(nilimuacha ndani) sikuwahi kusikia neno la Msamaha kutoka kwake aliona sawa tu...bado nilivumilia MAISHA yakaendelea ...ukikosea jambo anakua mkali kupita maelezo Tena kwa maneno makali ya kukera.Mwanzoni nilikua naumia sana na kulia.. badaye nilivyoona ni ujinga kumlilia mtu ambaye haoni thamani ya chozi lako na Wala hawezi kubadilika,na mimi nikaanza kupunguza upendo taratibu kwake nikahamishia mapenzi kwa watoto wangu,kazi na kuanzisha biashara zangu,...

Tendo la ndoa SIJAWAHI kumnyima japo sometimes mood inakata kabisa nikianza kufikiria matukio na kauli zake.. tunaweza kukaa hata wiki hatujagusana ...

Sasa kilichonifanya nije hapa...
Ni hiki.. kwa muda wote huo nilikua natafuta nafasi na chanzo kikuu Cha mabadiliko hayo...Nimeshakipata kama nilivyoeleza huko juu MAHUSIANO na mwanamke mwingine..na ushahidi ninao..

Sitaki kumuuliza WAla kuongea naye chochote juu ya hilo..

Nataka niondoke nikaanzishe MAISHA yangu nimuache na watoto ( kuhusu kuondoka na watoto hapa usinishauri))

....lakini kabla ya kuondoka, nataka AJUE KAMA NIMEJUA USALITI WAKE na nataka ATESEKE KISAIKOLOJIA alipie MAUMIVU yote niliyoyaishi kwa miaka yote hiyo..

Je NITUMIE MBINU GANI?.. Ikiwezekana nipe MBINU ya kumtesa na huyo mwanamke(iwe MENTALLY). Tena ikiwezekana kuwafanya wote wawili kila mmoja kwa wakati wake anipe hela Ndefu afu nijikatae ZANGU lengo ni kuwakomoa tu...wasinisahau..
SIMTAKI TENA!!
 
Dahh inasikitisha
downloadfile-20.png
 
Kama anakuhudumia wewe na wanao una shida gani ? Hakuna mwanaume wa kurizika na mbunye moja ....Sahau kabisa ! Zinakinaisha !

Alafu ukute wewe ni zile type jamaa akitaka mara nimechoka, ooh sijisikii vizuri ....ukimpa umemsusia .... Wewe ishi maisha yako, kama anaitambua na kuijali family yake [yenu] kaa kimya !

Alafu unashikaje simu ya mwanaume wako ? Utakufa kwa Kiroho.... mwanaume huwezi kumlinda yani, akienda hata bar anainamiwa chooni anapewa kimoja cha fasta
 
Chuki humuumiza aliyeibeba! Kama unasepa wewe sepa ila usijipe adhabu ya kutaka kuwaumiza waliokusaliti.

Ukiona watu wameachana kirafiki/kimapenzi halafu mmoja kila siku mapovu yanamtoka basi jua anayetokwa na mapovu ndio kaumizwa na alipendA sana.

Ukimove on, nenda mazima ujipe amani ya moyo. Hao wanaweza wasiteseke vilevile sababu Mungu hatoki kijijini kwenu.
 
Sijui nikushauri hapo uliposema hautaki ushauri? Nakushauri hivo hivo utajua mwenyewe.

Pole sana kwa changamoto hiyo sis, ila watoto wana umri gani? Ila kwa miaka kumi ya ndoa hao watoto itakuwa bado wadogo. Usiache watoto kama unaondoka. Hao watoto bado hawajaweza kujitegemea na usitegemee watapata malezi mazuri kwa mama wa kambo.

Una kazi , una biashara beba watoto uende. Ila pia fuatilia kuhusu taratibu za talaka. Achana na mambo ya kumfanya aumie au kulipa kisasi. Kuondoka kwako ndicho kisasi chenyewe.
 
Ndoa huiwezi ondoka.

huwezi kuwakomowa watu walio mapenzini kwa zaidi ya miaka minne.

Hao watoto mimi ndio walionifanya mpka nikoment hapa!.

Je una mpango gani wa malezi ya hao watoto baada ya kuondoka hapo???
Mazingira umeyatengeneza au unakurupuka kuondoka???
Hapo unaenda kuumiza viumbe visivyo na hatia.

Achaneni, lipiza kisasi lakini watoto hakikisha umeandaa mustakabali mzuri wa malezi yao...

NB;;
Mumeo ana pesa?? sio za kula na kuvaa!!!! ana miliki pesa nyingi ukwasi??? nijibu hapa nikupe ushauri.
 
Ili usiteseke huko unako enda, mashairi mvute mkopo mkubwa chukua chako ili tuendako usipange uanzie nyumbani kwako, ukipalamia Kodi za nyumba au chumba utajua haujui, ila jirizishe SAA zingine waweza kuta una nongwa Yako tu hamna inshu ya jamaa kuchepuka Wala nini
 
Pole sana Mkuu,
Huna haja ya kumfanya ajutie, maana utakuwa umehamishia hatia upande wako siku moja hasira zitapoa alafu utabaki kufeel guilty,
Kama umeamua kuachana nae basi jipange kwanza then mwambie straight kwamba haupo tayari kuendelea na hayo maisha yenu.
Kwa kiburi akisema uondoke, basi ondoka.
Kuacha watoto ni move nzuri mtatafutana baadae.
 
Hapo kwenye kukupiga huku ukiwa na mtoto mdogo na kukufungia nje huku mwanao mchanga akiwa ndani 🥹🥹🥹😭😭😭. Unaishi na muuaji dada,wanaokataga mapanga wake zao wanaanza hivi hivi. Yaani mtu anakupiga sio tu kukupiga huku ukiwa na kichanga?? Yaani hata ule ubinadamu wa kuigiza hana. Pole. Mi ningekuwa wewe hiyo ndoa ingekuwa ishakufa baada ya hiki kitendo cha kinyama,sijui kuhusu wewe na moyo wako.
 
Hivi ukiondoka unachokitaka utakipata nje au unaona single mother wanafaidi nje

Kaza mwanamke ndoa sio lele mama hivyo zungumza nae zaidi shirikisha mtu wa bus busara baina yenu mkae sawa
 
Hivi ukiondoka unachokitaka utakipata nje au unaona single mother wanafaidi nje

Kaza mwanamke ndoa sio lele mama hivyo zungumza nae zaidi shirikisha mtu wa bus busara baina yenu mkae sawa
Kwa maelezo hayo hakuna kitachobadilika hapo, ni aidha kila mtu aangalie upande sahihi kwa mustakabali wa maisha yao na familia yao kwa ujumla.
 
Huu sio ushauri, naandika tu nachokiwaza:

1) Kwanini binadamu anafikiri ana hati miliki ya binadamu mwengine? ? ? Like how? ? Who are you? ?

2) Utasema ni kwasababu alisema / alitoa kiapo kuwa utakuwa mali yake.

Watu husema mengi ambayo hawayamaanishi.

Wengine wanasindikiza maneno yao na matarumbeta na sherehe za bei ghali, lakini hawamaanishi walichokisema. Understand this.

Njia pekee ya kujua kuwa mtu kamaanisha alichokisema ni matendo yake, anayaishi maneno yake.

Kama mtu alisema nyeupe lakini anaishi nyeusi, wewe kukaa kung'ang'ana kumkumbusha kuwa alisema nyeupe, ni tatizo lako seriously. Rudia point namba 1.

3) Tungekuwa na imani juu ya MUNGU kama tulivyo na imani juu ya hawa wafanya mauzauza, maisha yangekuwa bora sana.

Unakuta mtu haamini MUNGU akisema ataleta Ufalme wake duniani, lakini kabaki kushikilia maneno ya kikaragosi kimoja kilichompiga fix kwa nderemo na vifijo, kabaki kuishi kwa sonona akishikilia imani kuwa siku moja kikaragosi hicho kitatimiza ahadi zake na maisha yatabadilika na kuwa mapya! ! !

Hata Abrahamu aliyekuwa tayari kumtoa Isaka hakuwa na imani ya namna hii!

Hata Noah aliyejenga safina wakati hakuwahi kuona mvua maisha yake yote hakuwa na imani ya namna hii!

Hata wanafunzi wa Yesu waliokubali kuuawa kumshuhudia Yesu hawakuwa na imani ya namna hii!
 
Back
Top Bottom