Simiyu: Maafisa wa Serikali watuhumiwa kutumia gari la Ofisi ya Mkuu wa Mkoa kupora Wakulima kwa silaha za moto

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,308
5,462
Gari la Serikali la Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu lenye namba za usajili DFP. 9182 likitumiwa na Afisa Biashara Mkoa wa Simiyu, Mustafa Kimomwe (ambaye pia ni Afisa Ushirika) na maafisa wenzake, wamefanya unyang’anyi wa kutumia silaha za moto (bunduki) katika Ofisi za Vyama cha Kilimo na Masoko (AMCOS).

Waliingia wakiwa na lengo la kufanya ukaguzi wa mizani na kufuatilia ununuzi wa Pamba lakini wakamtisha Katibu wa Mwasita Amcos hiyo kisha wakapora shilingi milioni mbili.

Baada ya hapo wakaenda Amcos ya Mwadila wakapora shilingi 500,000, matukio yote hayo yametokea tarehe 31.07.2023.

Jana pia Agosti 1, 2023 wakajaribu kufanya tukio katika Amcos ya Mwamitumai lakini Kamati ya Ulinzi na Usalama chini ya Mkuu wa Wilaya wa Maswa, Aswege Kaminyoge wakawakurupusha kwa kushirikiana na Wananchi ambapo wakafanikiwa kutoroka na kwenda kulitelekeza gari katika Kituo cha Afya Muungano Mjini Bariadi.

Mustafa kwa sasa yuko Kituo cha Polisi Maswa amekamatwa tangu tarehe 1/08/2023.

==============

UPDATES…

MKUU WA WILAYA ATOA UFAFANUZI...

Mkuu wa Wilaya ya Maswa, Aswege Kaminyoge ameulizwa kuhusu tukio hilo amesema ni kweli kuna tuhuma hizo, mpaka sasa anayeshikiliwa ni Mustafa Kimomwe, wenzake wawili hawapo wanaendelea kutafutwa.

Amesema "Mustafa Atafikishwa Mahakamani, kwa sasa anashikiliwa Kituo cha Polisi, Mahakama ndio itakayoamua.

"Tuhuma zinaeleza kuwa katika AMCOS ya kwanza watuhumiwa walichukua shilingi milioni mbili, nyingine hatujapata taarifa rasmi ya kiwango cha fedha walichochukua, hiyo ya mwisho tuliyowawekea mtego, wakati wanazungumza ili kupata hizo fedha wakahisi kuna hatari wakakimbia, tukawakimbiza lakini wakafanikiwa kwenda kulitelekeza gari Bariadi.

"Kuhusu silaha za moto kutumika, mtu mmoja kati ya waliotoa hela baada ya kutishiwa, ametuambia alitishiwa kwa bastola, hivyo hatuji kama ni ya kweli au ni bandia."

UPDATES...
JESHI LA POLISI LAKANUSHA

Maafisa wa Serikali kudaiwa kutumia gari la RC kupora wakiwa na silaha, Kamanda wa Polisi Simiyu, Kamishna Msaidizi wa Polisi, ACP Edith Swebe anaeleza:
 
Wangechomwa hao kenge,bahati yao wamekimbia,
Gari la Serikali la Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu lenye namba za usajili DFP. 9182 likitumiwa na Afisa Biashara Mkoa wa Simiyu, Mustafa Kimomwe (ambaye pia ni Afisa Ushirika) na maafisa wenzake, wamefanya unyang’anyi wa kutumia silaha za moto (bunduki) katika Ofisi za Vyama cha Kilimo na Masoko (AMCOS).

Waliingia wakiwa na lengo la kufanya ukaguzi wa mizani na kufuatilia ununuzi wa Pamba lakini wakamtisha Katibu wa Mwasita Amcos hiyo kisha wakapora shilingi milioni mbili.

Baada ya hapo wakaenda Amcos ya Mwadila wakapora shilingi 500,000, matukio yote hayo yametokea tarehe 31.07.2023.

Jana pia Agosti 1, 2023 wakajaribu kufanya tukio katika Amcos ya Mwamitumai lakini Kamati ya Ulinzi na Usalama chini ya Mkuu wa Wilaya wa Maswa, Aswege Kaminyoge wakawakurupusha kwa kushirikiana na Wananchi ambapo wakafanikiwa kutoroka na kwenda kulitelekeza gari katika Kituo cha Afya Muungano Mjini Bariadi.

Mustafa kwa sasa yuko Kituo cha Polisi Maswa amekamatwa tangu tarehe 1/08/2023.

Taarifa zaidi zinafuata...
 
Back
Top Bottom