Komredi Shemsha Mohamed Akabidhi Gari la Wagonjwa lililotolewa na Serikali Katika Kituo cha Afya Mwanunda Wilaya ya Itilima, Simiyu.

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,900
944

Komredi Shemsha Mohamed Akabidhi Gari la Wagonjwa lililotolewa na Serikali litakalotumika Katika Kituo cha Afya Mwanunda Wilaya ya Itilima Mkoa wa Simiyu

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Simiyu, Shemsha Mohamed amekabidhi gari la wagonjwa lililotolewa na Serikali ambalo litatumika katika kituo cha Afya Mwanunda kilichoko katika Wilaya ya Itilima Mkoani humo.

Akikabidhi gari hilo mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Dkt. Yahaya Nawanda, Mwenyekiti huyo amesema gari hilo litasaidia kurahisisha utaoji wa huduma hususani kwa akina mama wajawazito na watoto.

Aidha, Hafla fupi ya makabidhiano hayo yamefanyika katika kituo hicho cha afya na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali Serikali na Chama cha Mapinduzi (CCM) wa mkoa wa Simiyu na wilaya ya Itilima pamoja na wananchi.

Mbunge wa Jimbo la Itilima Njalu Silanga ameipongeza serikali kwa kutoa gari hilo ambalo litahudumia wagonjwa.

Mganga Mkuu wa Wilaya hiyo Dk. Emmanuel Costantine amesema kupatikana kwa gari hilo kutarahisisha utoaji wa huduma katika kituo cha Afya Mwanhunda.

''Ujio wa gari hili unaends kuongeza ufanisi katika kuokoa mama na mtoto, ilitulazimu kutoa gari hospitali ya wilaya kufuata wakinamama Longambogo, Makomelo kilometa 50, lakini sasa tutawafuata kilometa 17...kilometa 60 kwenda vijiji vya Ndoleleji, Nkuyu na Mwaswale, lakini sasa itakuwa kilometa 30, tunamshukuru Dk. Samia Suluhu Hassan'' amesema.
 

Attachments

  • WhatsApp Image 2023-11-26 at 01.24.27(1).jpeg
    WhatsApp Image 2023-11-26 at 01.24.27(1).jpeg
    39.9 KB · Views: 1
  • WhatsApp Image 2023-11-26 at 01.24.27.jpeg
    WhatsApp Image 2023-11-26 at 01.24.27.jpeg
    37.5 KB · Views: 2
  • WhatsApp Image 2023-11-26 at 01.24.28.jpeg
    WhatsApp Image 2023-11-26 at 01.24.28.jpeg
    47.5 KB · Views: 1
  • WhatsApp Image 2023-11-26 at 01.24.28(1).jpeg
    WhatsApp Image 2023-11-26 at 01.24.28(1).jpeg
    28 KB · Views: 1
  • WhatsApp Image 2023-11-26 at 01.24.28(2).jpeg
    WhatsApp Image 2023-11-26 at 01.24.28(2).jpeg
    46 KB · Views: 1
Back
Top Bottom