DOKEZO Simiyu: Kuna uhaba mkubwa wa mafuta ya Petroli kwenye Wilaya ya Bariadi

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

BigTall

JF-Expert Member
Mar 9, 2022
422
1,049
Katika Mji wa Bariadi Makao makuu ya Mkoa wa Simiyu, mapema Leo Asubuhi kumekumbwa na Changamoto ya upatikanaji wa Mafuta ya Petroli.

Nimetembelea vituo vya Mafuta 8 ambavyo vimekuwa vikitoa huduma ya mafuta ambapo vituo vyote 7 havina Mafuta huku kituo kimoja tu Total Energies ndicho chenye mafuta.
Simi.jpg

Simii.jpg

Licha ya kukosekana kwa Petroli, Mafuta ya Dieseli yanapatikana kwenye vituo hicho na huduma kwa watumiaji wa Mafuta hayo ambao siyo wengi zinaendelea kutolewa.

Baadhi ya vituo, vimeweka matangazo yanayoelezea kuwa hakuna huduma ya mafuta ya Petroli, huku vingine vikibandika matangazo yenye ujumbe kuwa Petroli Hamna.

Waendesha Pikipiki za Abiria (Bodaboda) wamelalamikia Hali hiyo, wakidai kuwa wametembelea vituo vyote na hawajapata huduma.

" Toka Asubuhi Mji mzima wa Bariadi, Mafuta ni kama Dhahabu, kimebaki kituo kimoja tu Cha Total ndicho chenye mafuta, vituo vingine vyote havina Mafuta", Amesema mmoja wa Bodaboda.
Simiiiiii.jpg



Pia soma EWURA: Tuna mafuta ya kutosha Nchini, wenye vituo lazima wawe na mikataba na waagizaji
 
Back
Top Bottom