DOKEZO Wilaya ya Ngara hakuna petroli siku ya nne

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

Seth seth

Member
Jan 2, 2022
95
135
Moja kwa moja kwenye hoja kuu. Hapa wilayani Ngara mkoani kagera hakuna mafuta aina ya petrol Leo siku ya nne. Wilaya hii Ina vituo vya mafuta takriban vinane vya mafuta. Lakini Kati ya hivyo vitano vinamilikiwa na kampuni moja inaitwa ngara oil.

Kampuni hii imekuwa na tabia ya kusitisha kuuza mafuta hasa pale zinapotokea tetesi kuwa mafuta yatapanda Bei siku chache zijazo ili wapige faida zaidi pasipokujali raia wanaoteseka kwa KUKOSA huduma hiyo hasa wagonjwa wanaowahi mahospitalini.

Kwa mfano bunge lilipokuwa linajadili bajeti ya mwaka huu na kupendekeza nyongeza ya sh.100 kwa Lita moja ya petroli kuanzia tarehe 1 July, vituo vyote vya mafuta vinavyomilikiwa na ngara oil walisitisha kutoa huduma kwa kisingizio kwamba mafuta yameisha kumbe wanasubiri ifike tarehe moja July ili wapige hela.

Kweli bana ilipofika tarehe moja wakaanza kuuza mafuta kwa Bei mpya iliyotangazwa. Baada Kama ya wiki moja Kama mnavyofahamu mafuta yalishuka Bei tena. Hapo hapo ngaraoili wakasitisha kuuza mafuta kwa kisingizio kuwa yameisha.

Kituo kioja kilijitahidi kutoa huduma lakini mwisho kilizidiwa nguvu kwani mahitaji yalikuwa makubwa Sana kuliko uwezo wake. Sasa Leo ninsiku ya nne wilaya nzima haina mafuta. Vishoka wanauza Lita moja kwa sh 11,000 na bado hayapatikani.

Kwa ufupi Hali ni mbaya na madhara yake ni makubwa wagonjwa wanakosa usafiri wa kwenda hospitalini, wanafunzi hawana usafiri wa kwenda shule,wafanyakaz hawaend makazini, nauli zimepanda Karib Mara tatu kiufupi ni kero Kero kero.

Pia soma > Hali ya Mafuta ya Petroli Liwale ni tete kwa zaidi ya wiki sasa
Pia soma > Manyara: Upatikanaji wa Petroli Mbulu ni changamoto, Wananchi wanahaha kupata huduma
 
Dah!! Pesa ni mwanaharamu, mtu yuko radhi kutesa watu kisa faida maradufu sio kwamba akiuza hapati faida ila anasubiri yapamde ili apate faida maradufu.

Huko kuna viongozi wa serikali, usikute wanashindwa kumchukulia hatua pengine wa kijani mwenzao, wanapeana sana 10%.. ni vurugu mechi.
 
Hapo mtu anapiga hesabu za utofauti wa bei na hali ya demand, anaona kuliko apeleke Ngara bora auzie petrol yake Dodoma au Moro ambapo transport cost to Dar es salaam is cheap na mda wa kusafirisha ni mchache.

Hiyo ndo data driven decision.

Otherwise, wauzaji wa ngara watatengeneza shortage kama hiyo ili bei ipande kwenye black market, waweze kuuza mafuta yao kwa faida.

Overall, its a business
 
Mama anaupiga mwingi

Hilo sio tatizo la ngara tu takriban nchi nzima mafuta yanapatikana shida et wanaomgomo bei imeshuka sana mwezi huu na wanastock kubwa...

Mbona miez karibu mitatu mafuta yalikua yanapanda tu na wanapiga faida tu leo kushuka imekua jau kwao...

Rip Magunga mwamba
 
Kuna Watu Wana roho mbaya Sanaaa...n ndo shida ya monopoly hiyo.

Aje mwingine afungue sheli hukoo aone mziki wake
Monopoly ni mbaya sana ndo maana first class world huwa wanaipinga kwa nguvu zote!

Airbus walipokuwa wanatengeneza A380, engine manufacturer aliyeshinda tenda alikuwa ni Rolls Royce akitumia engine ya Trent 900. Baadaye Airbus waliona ni risk kuwa na engine supplier mmoja, wakawashauri Pratt & Whitney waungane na General Electric ili wawe second option kwenye engine supplier. Ndipo ilipozaliwa kampuni ya Engine Alliance wakaja na engine ya GP 7000.

Wasingechukua hatua hiyo, A380 ingefeli hatua za mwanzo kabisa.

Ngara Oil ana petrol station nyingi huko Ngara, akiamua kuzingua mji lazima uyumbe.
 
Monopoly ni mbaya sana ndo maana first class world huwa wanaipinga kwa nguvu zote!

Airbus walipokuwa wanatengeneza A380, engine manufacturer aliyeshinda tenda alikuwa ni Rolls Royce akitumia engine ya Trent 900. Baadaye Airbus waliona ni risk kuwa na engine supplier mmoja, wakawashauri Pratt & Whitney waungane na General Electric ili wawe second option kwenye engine supplier. Ndipo ilipozaliwa kampuni ya Engine Alliance wakaja na engine ya GP 7000.

Wasingechukua hatua hiyo, A380 ingefeli hatua za mwanzo kabisa.

Ngara Oil ana petrol station nyingi huko Ngara, akiamua kuzingua mji lazima uyumbe.
Anawatesa sanaaa...daahhh
 
Wadau, wananchi wanalalamikia kuhusu uwanja wa ndege wa Bukoba kuwa ni mdogo, hivyo inaleta tafrani kwa marubani wakati wa kutua. Hili swala limekaaje? Anayejua atoe ufafanuzi kwa kadri inavyowezekana.
 
Back
Top Bottom