Simbachawene asema wabunge wote ni sehemu ya mapungufu yanayotokea katika Serikali za Mitaa, apingwa vikali

Rare Sapphire

JF-Expert Member
Jul 24, 2021
576
1,625
Issa Mtemvu akiwa anachangia hoja amesema ana kauli mbiu inayosema Kumtenganisha Rais, kumtenganisha Rais na Wezi, akisema yuko tayari kutofautiana na kauli ya Olesendek alisema "Kuwatenganisha Mawaziri na Wezi" akisema,


Anaamini Makamisaa wamepelekwa kwenye Wizara ili wawasaidie Wabunge na Rais, lakini inapofika sehemu sasa waziri atengenishwe na mafisadi, eti maafisa fisadi waitwe ni maafisa masauli pamoja na wasaidizi wao, wao mawaziri wanakuwa wako wapi? Kama wamepewa dhana zote za kushughulika na afisa yoyote anaehujumu mali umma kwanini watenganishwe na ufisadi huo usiposhughulikiwa?

Akiwa anatoa taarifa kutokana na kauli hiyo Simbachawene amesema, kwanza watambue kwamba yeye anaijua vizuri na ni mtaalamu wa masuala ya serikali za mtaa, akisema kwa mujibu wa sheria za fedha za serikali ya mtaa, wote waliopo ndani (wabunge) ni wajumbe wa kamati ya fedha wa halmashauri ya serikali za mtaa na kwa hiyo mapungufu yote yanayotokea kule hata wao ni sehemu ya mapungufu hayo, akisema hawawezi kuwatenga wabunge kwa mapungufu hayo, wote wanatakiwa kuwajibika!

Ambapo mtevu amemjibu na kusema Madiwani ni sehemu ya maamuzi kwenye serikali ya mtaa lakini vipi upande wa serikali kuu? Nani anatakiwa ashughulike na hayo kama siyo mawaziri?

Olesendeka nae akatoa taarifa na kusema kwa ripoti iliyowasilishwa bungeni hakuna paliposema Madiwani wa Halmashauri fulani walilazimisha fedha ziende katika eneo jingine, hivyo kwa lugha nyepesi, wahalifu dhidi ya mali ya umma ni maafisa masuuli katika halmashauri zetu, na watendaji na maafisa masuuli katika wizara na mashirika ya umma ambayo mwenye dhamana ya kuwasimamia ni Mawaziri walioko katika hayo.



Hivyo ndio maana akasema ni vizuri Mawaziri wajitenge na wahalifu hao kwa kuwachukulia hatua walioko chini yao wakiwemo wakurugenzi maana madiwani sio mamlaka ya mwisho kwa wakurugenzi kwani wao wanapendekeza tu, na wanaweza wakahamishwa bila kuchukuliwa hatua yoyote. Na kuhitimisha kuwa Bunge sio sehemu ya uhalifu katika Ripoti ya CAG.
 
Back
Top Bottom