Barabara za mitaa ya Kimara ni nyembamba mno, Serikali imelala

instagram

JF-Expert Member
May 27, 2014
2,091
4,716
Mitaa ya Mbezi Kimara, Kibamba hadi Goba inajengwa kwa kasi kubwa sana na serikali iko usingizini wakati watu wanajenga bila utaratibu. Barabara hazipitiki gari zinapishana kwa kuviziana.

Kila anayejenga badala ya kurudi nyuma hatua moja ya mpaka wake anaenda mbele hatua moja ya mpaka wake anajenga ukuta yani serikali imelala usingizi wa pono.

Huu ni ujinga wa hali ya juu kila mtu anawaza jinsi ya kupanua eneo la mpaka wake anamega barabara.
Mwisho wa siku tutakuwa na mji wa kipumbavu kabisa nyumba nzuri lakini mitaa haipitiki.

Imagine sasahv hakuna foleni miaka 20/30 ijayo kutakuwaje? Gari hazitapishana, ambulance hazitapita, Fire hawatapita, emergency responders watapata tabu sana.

Hivi kwanini tunashindwa kujifunza kwa miji ya wenzetu hata kama hatujafika Ulaya hata movies hatuoni?

Marekani unaona kabisa barabara zao za mitaa zilivyo pana na pavements na sehemu za wapita kwa miguu hadi mitaa ya watu maskini barabara zimepangika haswa inakuwaje sisi tunajenga hovyo hovyo na serikali ipo na kuna waziri wa ardhi na watu wa mipango miji na serikali za mitaa zipo hadi uchochoroni yani unakuta watu wa serikali za mtaa washamba yani wamekaa na matisheti yao ya chama unajiuliza hivi hawa watu wanajua hata kazi za serikali ya mtaa kweli?

Alafu sasa asilimia kubwa ya wamiliki wa hizi nyumba ni watumishi wa umma inashangaza sana, na usiombee ukutane na jirani ni mtu wa kaskazini yani hawafuati mipaka kabisa mtu anajenga hadi barabarani kwa kweli inaskitisha sana kama nchi.
 
tatizo sugu hili linaloshika kasi
ujue unaweza fika sehem, hakuna nyumba, lakini zile njia zinakukufanya kuamini gari linapita hapa bila wasiwasi
baada ya kila mtu kujenga sasa, unakuta njia nyembamba, maana kila mtu kazidi mbele, kona zumekuwa sharp hukati tena
Yani huku kuna mtu ana kieneo chake kidogo basi anajenga ukuta hata gari inapita kwa tabu nawaza siku ikija semi trailer itapitaje
 
tatizo sugu hili linaloshika kasi
ujue unaweza fika sehem, hakuna nyumba, lakini zile njia zinakukufanya kuamini gari linapita hapa bila wasiwasi
baada ya kila mtu kujenga sasa, unakuta njia nyembamba, maana kila mtu kazidi mbele, kona zumekuwa sharp hukati tena
Watu wanaigana akianzisha moja tu kutanua barabarani basi wote nao wanafatisha ukuta wao. Kuna barabara gari kupishana hadi moja aingie getini kwa mtu ndo mpishane sasa hivi kweli kuna serikali hapa?
 
Hiki jambo niliwahi kusema hapa Chanika ni Manzese ya baadaye ujenzi holela umeshamiri sana.

Kutakuja kuwa na bonge la uswazi miaka michache ijayo baadhi ya maeneo imeshaanza kuonekana
Yani unajenga nyumba yako safi linakuja jitu linajenga mabanda ya kupangisha barabarani mtaa ulikuwa wa kishua unakuwa uswazi,
 
Kweli kabisa...nyingine zinawekwa mpaka lami ila ni nyembamba kupishana ni kazi, juzi nimepita barabara inayotokea stopover, yan inabid uwe mpole maana kukwanguana muda wowote, na kuna barabara ya Msuguri na ya Matosa ujinga ni ule ule.
Hata sehemu ya wapita kwa miguu hamna.
Kuna muda unapita unakutana na lundo la wanafunzi wanafatisha barabara.
 
Back
Top Bottom