Sasa je hata Kama wewe ukiona mpambano umekushinda kifuatacho[emoji125][emoji125]Tiger ana uwezo wa kupigana kwa kusimamia miguu ya nyuma wakati anatoa kichapo kwa adui.
Ni mnyama ambaye ni mwepesi mno na anashambulia kwa kasi kuliko simba!
Ana uwezo wa kujitupa na kujigeuza upande wowote wakati wa mapigano kwa kasi na kwa nguvu zote.
Bahati mbaya anachoka haraka tofauti na simba!
Simba anaweza asiwe na ufanisi wa mbinu za kupigana kama tiger lakini ana ujasiri na hachoki. Anapigana mpaka tone la mwisho la damu hata apigwe vipi hakimbii.
Tigers wana nguvu na ufanisi lakini ni wazembe. Anashambulia kwa kasi lakini akichoka anakimbia pambano!
Sent using Jamii Forums mobile app
Tiger wanapatikana India kiuwezo hawezi kimfikia Simba
Simba Ni habari nyingine
Daima toa bila kukumbuka na Pokea bila kusahau
Mnamo mwaka 1859 lilitajwa pambano lililodumu takribani dakika 10 mjini lonfon ambapo TIGER aliyefahamika kwa jina la GUNGA ambaye hapo awali alikua akimilikiwa na ufalme wa 'OUDE' aliua SIMBA wapatao 30Teh teh kweli mkuu me nipo upande wa simba kwa uzamini wa member hapa jukwaani nimeangali upande nimeona simba kawazi wote ndo maana kapewa uking
Kelele zote za hao mabwege kumbe tiger wao anahitaji apakwe mkongo..
Upuuzi kweliMnamo mwaka 1859 lilitajwa pambano lililodumu takribani dakika 10 mjini lonfon ambapo TIGER aliyefahamika kwa jina la GUNGA ambaye hapo awali alikua akimilikiwa na ufalme wa 'OUDE' aliua SIMBA wapatao 30
Tukio lingine lilitokea 2010 ambapo "BENGAL TIGER" katika zoo ya "ANKARA" alipita kwenye uwazi kutoka kwenye cage alipofungiwa hadi kwenye cage ya simba na kumuua kwa pigo moja tu
Habari hii ilikuja kuripotiwa mwaka 2011 nakuwekea link hapa kutoka BBC usome mwenyewe
Tiger kills lion in Turkish zoo
Mbwa mwitu c paka sababu wana mdomo mrefu ni jamii ya mbwa ambao nao pia wana magroup yao fox.hyena.wolf nkNimependa maelezo haya. Yamechambua vizuri nguvu na udhaifu wa kila mmoja katika aina hizi za paka. Ni kweli Simba hana mzaha linapokuja suala la kupambana. Huwezi ukamtoa nduki kama unavyoweza kufanya kwa Tiger and the like. Utamuua akijilinda huku akitafuta uwezekano wa kukumaliza na wewe
Ila nina swali moja mkuu. Umesema Simba ndio mnyama wa aina ya paka anaewinda kwa pamoja. Je mbwa mwitu hawako kwenye kundi hili maana wao haswaa ndio wawindaji kwa group
Sasa hapo unakua umeandika nini?Upuuzi kweli
Nilifikiri Clip ...kumbe malezo Mchwara
Tiger ni Mkubwa ...lkn si mkubwa kihivyo kumzidi Simba
Ama katika sifa ya mapigano
Simba huwa ni Shujaa asiekubali kushindwa katika maisha yake,ilihali Tiger ana sifa ya Uoga na hukimbia Vita
Simba atabaki kuwa Mfalme
Kwa meeengi sana
Kisha
Wapambe wa Tiger,mnatakiwa mfahamu
Ukubwa si sababu ya Ushindi kwa wenye akili
Bali ushujaa na kuthubutu,ndio kila kitu mbele ya Wanaume
Sent using Jamii Forums mobile app
Hello,habari za majukumu wadau,bila shaka mtakuwa mko vyema na mnaendelea kuchukua hatua na tahadhari dhidi ya hili gonjwa dharimu la Covid-19 linalosababishwa na virus hatari wa corona,Mungu awabariki sana!.
Niende moja kwa moja kwenye mada.
Kuna mjadala mahali fulani nimekutana nao kuhusu mnyama SIMBA na TIGER (Chui milia).
Kiukweli kama mnavyofahamu mijadala mizito mara nyingi huwa ina vuta nkuvute,kulingana na tafiti mbalimbali pamoja na Historia kadha wa kadha!,sasa kuna wengine waliosema ya kwamba SIMBA ni hatari zaidi ya Tiger na kuna wengine waliosema Tiger ni hatari zaidi ya Simba,na huo uhatari wao ni pale wanapokutana wao kwa wao.
Wapo waliosema SIMBA kwa uwezo wa nguvu,uwindaji,mapigano basi akikutana na Tiger atapokea kipondo kikali,lakini pia wapo vilevile waliosema kwamba Tiger kwa uwezo,minguvu,uwindaji na mapigano basi akikutana na Simba atampiga mpaka achakae kabisa,na si kuchakaa tu bali pia kuua kabisa.
Mtazamo wako wewe ni upi hapa,hebu lete facts za uhalisia,kiroho na kimwili pia unaweza kuhusisha!!
Tulia hivyo hivyo dawa ikuingie..[emoji382]
Nyumba za kale zinahusiana vipi kua simba ni ananguvu kuliko tiger?History
Inamtambua Simba kama Mfalme wa Pori,hii haina maana kipindi hicho,hapakuwa na Tiger kabisa Duniani
Someni History,tazameni nyumba za kale za kihistoria ...utajua ukweli
Sent using Jamii Forums mobile app
Asante saana mkuu kwa elimu hii,hakika umeniongezea maarifaMbwa mwitu c paka sababu wana mdomo mrefu ni jamii ya mbwa ambao nao pia wana magroup yao fox.hyena.wolf nk
ChiefSasa hapo unakua umeandika nini?
Aliyekudanganya Kutokubali kushindwa ni kigezo ambacho mwenye nguvu huwa nacho ni nani?
Pierre akiwa na sifa ya kutokubali kushindwa hiyo itamaanisha TYSON FURY atapigwa kwasababu chenye sifa ya kutokushindwa hakishindwi?
Hiyo link umeielewaje wewe?
Tiger angekua na sifa ya uoga angemvamia simba na kumuua tena kwa kipigo cha aibu kama kile?
Au mganga wako alikuambia kua una nyota ya simba na simba ni shujaa ndo maana unamtetea hapa tena bila references?
Sa si bora uwe na nyota ya nyani tu
Bado akili mgandoNyumba za kale zinahusiana vipi kua simba ni ananguvu kuliko tiger?
Simba sio tu kwamba anamuogopa TIGER bali hata mbwa mwitu simba anaufyata
Duuh!!Kelele zote za hao mabwege kumbe tiger wao anahitaji apakwe mkongo..
Tiger kama mwanaume wa kinondoni tu, mwili miubwa dakika 2 chali...
Lazima uelewe kwamba wanyama wanatofautiana tabia zao kulingana na mazingira waliyomo lakini pia kulingana na jinsi walivyo kwa asili yao.Sasa je hata Kama wewe ukiona mpambano umekushinda kifuatacho[emoji125][emoji125]
Kuna video niliona ng'ombe wanashindwanishwa nani zaidi kwenye kupigana bas huo mmoja alianza kwa makeke mengi watu wakawa wanamshangilia kumbe mwenzie anausoma mchezo
Alivyoona kachoka yule aliyekuwa anausoma mchezo akaanza alimla kichwa kimoja yule ng'ombe akawa Kama kapigwa butwaa Sasa yule mwingine akarudi nyuma akamfuata kwa spidi bas yule ng'ombe alikimbia akatoka nnje ya uwanja watu walizomea dah nikikumbukaga nacheka [emoji23][emoji23][emoji23]
Sent using Jamii Forums mobile app
Point Chief,na huu ndio uhalisiaLazima uelewe kwamba wanyama wanatofautiana tabia zao kulingana na mazingira waliyomo lakini pia kulingana na jinsi walivyo kwa asili yao.
Tiger ni mnyama anayeishi maisha ya upweke. Hivyo, kila anapowinda lazima awe na shabaha ya uhakika ya kukamata windo lake mara moja na kwa ufanisi bila kuchelewa maana hana kampani ya kumpa msaada.
Tabia hiyo ya kuwinda mwenyewe, imemfanya kuwa mnyama mwenye ufanisi na maguvu mengi kama matokeo ya natural evolution.
Ni mnyama ambaye ameundwa kuua na kupambana na adui kwa nguvu na kwa ufanisi uliotukuka. It is a killing machine. Akikushambulia ujue ndani ya dakika mbili ameshakutoa roho.
Simba ni mnyama aliyeundwa kwa mapigano. Ni mnyama anayefurahia bifu, kutawala na kuvamia himaya za wengine. Ni mnyama anayependa ubabe tu na udikteta japo hana ukatili wa kufanya mauaji ya haraka.
Ndio maana tiger na simba wakiwa wanapigana, yule tiger atamvamia simba kwa kasi kwa nia ya kutaka kummaliza kwa kichapo cha fasta fasta, lakini bahati mbaya simba anahimili na kurudisha mapigo bila kuchoka au kusalimu amri.
Tiger akishaona anapigana na adui ambaye hafi kwa urahisi, lazima aondoke maana hajaundwa kwa mapambano. Ameundwa kuua haraka na kujificha kwa sababu ni solitary hunter anahitaji kujilinda dhidi ya majeraha yoyote kwa kadiri inavyowezekana.
Tiger akipata jeraha anakufa njaa mana hana sapoti ya kuwindiwa na wenzake. Ni mnyama aliyeundwa kuua chap chap na kwa tahadhari ya hali ya juu kuepuka kujeruhiwa.
Hivyo anapopigana na simba anatoa dozi nzito kweli kweli za mwanzoni lakini anachoka na kukacha pambano maana simba harudi nyuma hata apigwe vipi.
Sent using Jamii Forums mobile app
Chui gani huyo?
Maelezo yako mbona kama unamzungumzia jibwa?
Hapa tunamzungumzia TIGER mwenye mabaka yake ambaye hata BBC wana CV yake
Tiger kills lion in Turkish zoo haya