Simba na Azam zisipofanya vizuri ZICHEKWE

Muite

JF-Expert Member
Sep 10, 2013
2,363
4,889
Nguvu kubwa ya kumtoa Feisal kwa fitina pale Yanga na usajili mkubwa wa wachezaji wa nje basi tunategemea Azam kuchukuwa kombe la ligi kuu(NBC) , Kombe la Shirikisho la Azam .
Simba kwa usajili wa wachezaji wa nje walioufanya kwa vibe na mbwembwe na jinsi MNAVYOJIAPIZA KUWA HAKUNA KAMA SIMBA MSIMU HUU basi tunategemea timu ichukuwe makombe yote ya ndani na ifike mbali zaidi kwenye michuano ya CAF.

NIMEONA MWAKA HUU YANGA HAINA VIBE WALA MAJIGAMBO, HIVYO HUENDA ITAKUWA NI TIMU YA KU STRUGGLE MSIMU HUU NA KWENYE LIGI IKIWA YA 3 AU 4 HATUTASHANGAA.

SIMBA NA AZAM NI WA KUCHEKWA WASIPOCHUKUWA VIKOMBE VYA NDANI NA WASIPOVUKA ROBO FAINALI LIGI YA MABINGWA
 
Yanga imeshatoka kwenye level za mbwembwe za usajili,unavyodhani Yanga haijasajili mpaka sasa,hizo timu ulizizozitaja huu ndio wakati wa vibe ndio maana unaona hata wachezaji wanaowasajili msimu huu wanawatambulisha na jezi za msimu uliopita
 
Nguvu kubwa ya kumtoa Feisal kwa fitina pale Yanga na usajili mkubwa wa wachezaji wa nje basi tunategemea Azam kuchukuwa kombe la ligi kuu(NBC) , Kombe la Shirikisho la Azam na kufika nusu fainali ya ligi ya Mabingwa.
Kweli wewe utopolo yaani azam afike nusu fainali ligi ya mabingwa wakati hashiriki
 
Hata team Kama arsenal,Barca,man u,zishatoka level za usajil wa mbwembwe 🤣🤣mbaazi ikikosa maua husingizia jua,pyeee
Yanga imeshatoka kwenye level za mbwembwe za usajili,unavyodhani Yanga haijasajili mpaka sasa,hizo timu ulizizozitaja huu ndio wakati wa vibe ndio maana unaona hata wachezaji wanaowasajili msimu huu wanawatambulisha na jezi za msimu ulio
 
Kweli wewe utopolo yaani azam afike nusu fainali ligi ya mabingwa wakati hashiriki
Mimi Kolo mwenzako bwana. Basi tuseme makombe ya ndani. Hivi unajua Azam anaweza kushangaza watu kwa kumaliza ligi nafasi ya 4
 
Majigambo na ukimya nadhani inatokana mienendo ya usajili mpaka sasa. Ukimya wa Yanga unatokana na mashabiki kuwa na hofu ya kusambaratika timu iliyokuwa tayari inaonesha dira. Tayari benchi la ufundi limeshameguka bado wachezaji muhimu haijulikani hatima yake. Na ukijumlisha kuwa mashabiki walikuwa wameshazoshwa kujiamini kupitia Nabi sasa haijulikani nini kitajili mbeleni. Nyuso za mashabiki wa Yanga zitarudi baada ya kuangalia mechi kadhaa zitakazochezwa ili kujua uwezo wa benchi jipya.

Azam, wanachokifanya sio kigeni, walishafanya hivyo misimu kadhaa nyuma kuleta vyuma lakini ubingwa ni kupokezana kwa timu za Kariakoo, labda wabadiilike hivi sasa.

Simba ndio pekee ambao wanaweza kuwa na matumaini makubwa nyusoni mwao tofauti na Azam kwasababu Simba wanaimarisha kikosi chao. Kikosi cha Simba cha msimu uliopita ilikuwa ni kikosi bora cha wachezaji wanaonza ila mapungufu yalikuwa ni machache sana. Ndio timu iliyokuwa na Ukuta bora + safu bora ya ushambuliaji kwa Tanzania kwa msimu uliopita. Kiungo ndio ilikuwa sehemu kubwa yenye mapungufu. Kwa kuziba hayo mapungufu wanajawa na matumaini ya kufanya vizuri kwa kuzingatia kuwa kocha ni yule yule wa msimu uliopita.
 
Hata team Kama arsenal,Barca,man u,zishatoka level za usajil wa mbwembwe 🤣🤣mbaazi ikikosa maua husingizia jua,pyeee
So Yanga imemuacha morrison,kisinda perhaps kuna wachezaji wengine 3 wa kigeni ikaachana nao na wasisajili,kwa taarifa yako Yanga imesajili wachezaji 1 au 2 kutoka congo, m1 ivory coast na kuna m1 kutoka huko huko west africa,na wandani 2 au 3,Yanga aisajili kuunda timu inasajili kuboresha nafasi zilizokua na mapungufu last season,but makolo atuwashangai hata msimu uliopita mlida okrah ni pekee wa ndani kuitwa black star,kina sawadogo atusahau mbwembwe zao so hiki ndio kipindi chenu cha kujidai
 
Yanga imeshatoka kwenye level za mbwembwe za usajili,unavyodhani Yanga haijasajili mpaka sasa,hizo timu ulizizozitaja huu ndio wakati wa vibe ndio maana unaona hata wachezaji wanaowasajili msimu huu wanawatambulisha na jezi za msimu uliopita
Sasa utakuwa na mbwembwe gani wakati huna Cha kusajili

By the way namba 6 anasubiriwa. Hoi mbwembwe Ina mwezi sasa inatrend.
 
Back
Top Bottom