Hakuna derby kati ya Azam na Simba au Azam na Yanga!

Dabil

JF-Expert Member
Sep 30, 2021
5,885
13,263
Sijui kwanini Azam media wanalazimisha timu yao ya Azam kwamba ni derby dhidhi ya wakongwe wa Kariakoo?

Kwanza ni timu ya juzi hakuna derby kati ya baba na mtoto,

Mafanikio ya mataji haiwezi kufika hata robo ya Simba na Yanga

Kwa mashabiki hata robo ya hizo timu Azam haifiki.

Sasa wanavyosema azam ni derby kwa Simba na Yanga ni derby kwenye nini hasa hawana umri sawa kuanzishwa,hawana mashabiki, wana kikombe kimoja tu cha ligi.

Kama wanaangalia timu ambazo zote zipo Dar basi Azam anafaa kuwa derby na KMC maana hata umri wanaendana kwa mbali.

Azam kuwa derby kwa Simba na Yanga ni kuzishusha hadhi Simba na Yanga.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Screenshot_20240206-213222.png
 
Azam wameubadili sana mpira wa TZ. Wameongeza ushindani. Mpira ni burudani. Wakifungwa Azam burudani itanoga sana. Kila la heri Simba Mnyama mkali.
Kaizer na Orlando ni derby, Mamelodi wanakimbiza kwenye ligi lakini derby ya Orlando na Kaizer imebaki palepale,Azam wafanikiwe kwanza kuishika ligi ya bongo kwa mataji back to back watapata mashabiki.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sijui kwanini Azam media wanalazimisha timu yao ya Azam kwamba ni derby dhidhi ya wakongwe wa Kariakoo?

Kwanza ni timu ya juzi hakuna derby kati ya baba na mtoto...
Mimi nikajua derby ni ikiwa teams zina makazi ndani ya mji mmoja kumbe sii hivyo tena!

Kwa hiyo Shalk 04 na Dortmund siyo derby?

Man U na Sandaland siyo Derby?
 
Derby ni mechi kati ya timu za mji mmoja.
Kuna London derby halafu kuna north London derby

London derby= arsenal VS chelsea
North London derby= arsenal VS Tottenham

Azam na simba ni Dar es Salaam derby
Simba vs Yanga ni Kariakoo derby

Kama ile timu ya African Lyon ingekuwa bado ipo ndio ingekuwa Mbagala derby kati ya Azam na African Lyon
 
Kaizer na Orlando ni derby, Mamelodi wanakimbiza kwenye ligi lakini derby ya Orlando na Kaizer imebaki palepale,Azam wafanikiwe kwanza kuishika ligi ya bongo kwa mataji back to back watapata mashabiki.

Sent using Jamii Forums mobile app
Upo sawa. Hichi wanachofanya ni kutengeneza attention na wanafanikiwa sababu mpaka sasa mechi ya Simba na Azam ina attention kuliko Simba na timu nyingine ukiwatoa Yanga.
 
Derby ni mechi kati ya timu za mji mmoja.
Kuna London derby halafu kuna north London derby

London derby= arsenal VS chelsea
North London derby= arsenal VS Tottenham

Azam na simba ni Dar es Salaam derby
Simba vs Yanga ni Kariakoo derby

Kama ile timu ya African Lyon ingekuwa bado ipo ndio ingekuwa Mbagala derby kati ya Azam na African Lyon
Kama ni timu zote zinazotoka sehemu moja kwahiyo KMC pia ni derby ya Simba,Yanga,Azam?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni wanatangaza biashara yao tu ikuwe ila ukizungumzia derby kama derby ;timu lazima zitoke kitongoji kimoja kwanza.
mji mmoja sio kitongoji kimoja, sema Derby ni ya timu mbili, haiwezi kuwa timu 3 ndani ya mji mmoja
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom