Mtanzanias
JF-Expert Member
- Jul 30, 2021
- 1,747
- 3,723
Nimeona baadhi ya mashabiki wa simba na wachambuzi wakiipongeza simba kuwa pamoja na kutolewa na whydad lakini wamejitahidi.
Ikumbukwe kwenye hatua ya robo fainali akunaga cha kujtahidi kinachoangaliwa ni kuvuka kwenda hatua inayofata ya nusu fainali aijalishi umevukaje, na mafanikio yako yatapimwa hapo na sio vinginevyo.
Haiwezekani kila msimu unaoingia robo fainali safari yako inakomea hapo hapo iyo inamaanisha uwezo wa timu yako mwisho wake ni huo!
Wachezaji ulionao wana uwezo wa kukusogeza mpaka robo fainali tu basi na biashara inaishia hapo, Wengi walitegemea whydad ingeshinda magoli mengi jana lakini mpira auko ivyo, mpira una njia zake, ni ngumu sana kuifungua timu ambayo inakaa nyuma ya mpira karibia wachezaji 9 wote wakijilinda na uku ukimwacha baleke akiwa kama mtumishi hewa uwanjani, kwa maana iyo walitafuta goli lao moja la kulipa deni kisha wakatumia uwanja wao wa nyumbani kuvuka hatua inayofata kupitia mikwaju ya penalti.
Simba walitolewa kwenye mechi ya kwanza baada ya kushindwa kutumia uwanja wao vizuri kilichokuwa kinafata ndio icho kukamilisha ratiba, simba angeondolewa mashindanoni kwa njia yoyote ile ilikuwa ni suala la muda tu, Hii ni mara ya tatu simba anaishia robo fainali na maneno yakiwa ni yale yale ''Tumetolewa lakini tumejitahidi'' Sidhani kama kuna tuzo ya kujitahidi kwenye hii michuano, Unapotupwa nje ya michuano iyo inakuwa imeisha na wewe unabaki kujifariji na neno ''Tumejitahidi'' ambalo aliwezi kukusaidia lolote.
Wydad kafuzu nusu fainali na malengo yao yametimia aijalishi wamevuka kwa staili ipi, Uwezi kuwa unawategemea kiba john boko na erasto nyoni ndio wakupeleke nusu fainali ni uongo uliotukuka.
Sasa rudini nyumbani mjipange kufanya usajili vinginevyo yanga anakuja kwa kasi ya kimbunga kuwaonyesha ya kuwa kuna jambo lake analitaka na anataka kuvunja rekodi zote ambazo ndio kilikuwa kichaka cha mashabiki wa simba kutamba mitaani!