Simba Bob Junior wa Serengeti apinduliwa na kuuawa

Gang Chomba

JF-Expert Member
Feb 29, 2008
20,301
4,681
SAD NEWS…

Taarifa ya kifo cha Simba maarufu huko Serengeti ajulikanae kama Bob imezistua Nyoyo za Watu wengi Duniani ambao walifanikiwa kumuona Simba huyo ambae alikuwa kipenzi cha Watu kwa kuwa hakuwa na tabia za kujificha wala kukwepa Camera.

Bob alikutwa na umauti baada ya kundi la Simba Watatu kumvamia na kutimiza Lengo lao la muda mrefu la kuuangusha utawala wa Bob na kusimika ufalme wao porini hapo.

Simba hao Watatu ambao Bob aliwalea tangu wakiwa wachanga inasemekana walishafanya mapinduzi mara kadhaa ya kutaka kuuangusha utawala wa Bob lakini mara zote walikutana na upinzani mkali na hata kukimbizwa maeneo hayo.

Bob ambae alikuwa mtemi na mtawala wa eneo la Namiri aliongoza Simba wa eneo hilo kwa kipindi kirefu sana na alikwepa mapinduzi ya aina mbalimbali kwa vipindi tofauti huko Mashariki ya Serengeti.

Utawala wa Bob ulikuja baada ya kumpindua na kumuua Baba yake ambae alikuwa maarufu pia kwa Watalii Duniani ambae alifahamika kama C-Boy.

Umauti ulimkuta C-Boy mwendo wa Jioni pembezoni mwa Mto Ngare Nanyuki ambapo wakiwa wawili tu Bob alifanikiwa kufanya mapinduzi hayo tukufu na kuumaliza utawala wa Baba yake.

Pumzika kwa amani Bob.
Vita ulivipigana na mwendo umeumaliza.

simba.jpg


 
Mie sipendi kuona wakimuua pundamilia, yule mnyama namuonaga ndio pisi ya porini....ananiuma akiliwa
Mi niliacha kuangalia kipindicha wanyama sababu ya simba kumla twigana pundamilia ,na nyati
Roho ikawa inaniuma sana nikaona niachane nayo, kweli Twiga wapole hawana shida walitakiwa watengwe na simba kabisa ,viswala vikikamatwa sasa hadi watoto nikaona nitachizika huyu bwana bob afe tu makatili wakubwa
 
Mi niliacha kuangalia kipindicha wanyama sababu ya simba kumla twigana pundamilia ,na nyati
Roho ikawa inaniuma sana nikaona niachane nayo ,kweli Twiga wapole hawana shida walitakiwa watengwe na simba kabisa ,viswala vikikamatwa sasa hadi watoto nikaona nitachizika huyu bwana bob afe tu makatili wakubwa
Mi napenda sana kuangalia animals....nat geo wild my fav
 
Back
Top Bottom