Mwamini Bwana Yesu kuwa ni Mungu na kwamba aliacha utukufu wake Mbinguni na kukubali kuzaliwa kama mwanadamu ili afe na kuchukua adhabu ya dhambi zako. Huyu Yesu alifufuka na alirudi Mbinguni kwa babaye. Sasa, muombe atakujulisha inakupasa kufanya nini.
Naona umeanza kuleta hoja nyingine, okay tuendelee kukumbushana tu,
1. Mimi kwanza namuamini yesu (Issah) kama mtume aliyekuja kabla ya Mtume Muhammad (s.a.w) na sio mungu kwasababu hana sifa za kuwa mungu ila wewe kama unazo hizo sifa unaweza kunieleza,
2. Yesu hakuwahi kufa ila alipaa mbinguni na hapo baadae atarudi na moja ya lengo la kurudi ni kuja kubainisha kuwa yeye ni nani, ni mungu au alikuwa ni mtume kama mitume mingine tu.
3. Siamini kwamba mungu au mtume anaweza kuchukua dhambi za mtu, ila naamini kwamba kila mtu atalipwa kulingana na kile alichokitenda hapa duniani.
4. Mimi naamini kuwa wakuombwa ni Mungu mmoja tu, na sio Yesu (Issah) wala Mtume (S.A.W), hivyo mimi na wewe tunapaswa kumuomba mungu kupitia mafundisho ya hao mitume na sio kuwaomba wao.
5. Unasema yesu aliacha utukufu wake mbinguni na kukubali kuzaliwa kama mwanadamu ili afe na achukue dhambi zako alafu hapohapo unasema alipofufuka alirudi kwa baba yake (sio kwenye utukufu wake tena), okay. swali, kipindi mungu (yesu) amekufa (kabla hajafufuka) dunia ilikuwa inaendeshwa na mungu yupi?
NB; hatugombani ila ni kueleweshana tu. Ahsante.