Silaha za Masafa Marefu Zinazomilikiwa na JWTZ

Kichuguu

Platinum Member
Oct 11, 2006
15,485
19,319
Nin wasiwasi sana na silaha za masafa marefu tulizo nazo ndani ya majeshi yetu ya ulinzi. Miaka ya 2000 kuna zile zilizokuwa zinalipuka zenyewe kule Mbagala. Na ninavyokumbuka Tanzania tuliwahi kununua vifaru vingi na Gun Howitzers nyingi sana wakati wa utawala wa Nyerere kutokea Urusi. Silaha zile ndizo kwa kiasi kikubwa sana zinazotumika sasa hivi vitani huko Ukraine.

Urusi inazitumia na Ukraine pia inazitumia. Jambo linalojitokeza ni kuwa mizinga inayotumika katika Howitzers na vifaru hivyo haipatikani tena. Urusi haizitengenezi tena, na Ukraine imekusanya mizinga karibu yote iliyokuwa kwenye nchi za Warsaw pact na haitoshi kwani mizinga mingine imekuwa hailipuki; hiyo imetokea kwenye pande zote mbili za magogoro huo.

Sijaona Tanzania ikitupa vifaru vya zamani na kuleta vipya, na sijui kama Tanzania itapata tena mzinga ya kutumia kwenye vifaru hivyo kama siyo vya shoo tu. Vifaru kama hivyo leo hii vimekuwa scrap zilizosambaa kwenye ardhi ya ukraine.

Ninajua kuwa zamani shirika la Mzinga liliundwa ili kuwa linatengeza mizinga hiyo, ila sasa baada ya kutokuwa na matumizi ya mizinga hiyo kwa muda mrefu sijui tuko wapi. Ila vita hii ya Ukraine tuichukulie kama funzo kuwa utegemezi wa silaha za urusi siyo jawabu la usalama na ulinzi wetu tena. Urusi imeshapitwa na wakati sana kwenye teknolojia ya vita.

1652213551874.png
1652213578377.png
1652213668825.png
 
Umeandika mada inayofikirisha Sana. Naamini wahusija JW wanaelewa hasa nini cha kufanya. Pia naamini kama kweli Russia hatengenezi tena mizinga hiyo kutakuwa na another alternative. Kwa kuwa ingawa hatupigani vita lakini huwa wanafanya manunuzi ya vifaa vita.
 
Kwenye modern wafare ni mwehu tu anayetegemea vifaru vitani ... Vifaru vimebak kama magar ya msafara w kijeshi kipind cha Amani , kiufupi vita ya kutegemea vifaru ishapitwa na wakati, Ila ukijidai utegemee vifaru kwenye active battle zone ujue unawatoa kafara askari ....!! Vita ya sa hv ni propaganda , technology na Airforce , kama huna uwezo kwenye maeneo hayo omba maridhiano mapema.... Askari wenu wanaopasua tofali uwanja wa mkapa wanawadanganya
 
kwa levo za nch zetu nahic tuko vzur kuna sku zlkua znapta zana za kijesh mepgwa chata za UN kuelekea lugalo na kule ununio asee watakao omba batle na sie wajpange na izo n kwa darslam bado iyo mikoa ya mipakan ambayo ndio ua na silaha nzto zaid kimsng hakuna taifa ambalo halijajiwekeza ki usalama hata kama hakuna machafuko

Sent from my Infinix X650B using JamiiForums mobile app
 
Una maana Urusi hawana silaha walizotengeneza toka enzi hizo, tokea sisi tunaagiza toka kwao?

Na haya makombora yanayokwenda spidi ya G5, na kuwa na uwezo wa kuepa kinga dhidi yake, nayo ni teknologia ya zamani?
Makombora hayo ya high tech (cruise missiles) siyo mengi; hata urusi yenyewe na hata Marekani for that case hawana mengi ya ya kuwatosha hadi kuuza nje.

Hata kama wangependa kuyauza nje huwa ni vigumu kwa vile guns zake ni maalum sana hazipatikani kokote kwani nyingi wamezijengea ama kwenye meli zao za kivita au kwenye ndege maalumu za kivita.

Siamini kama Tanzania tayari tunazo hizo guns za cruise missles. Ukitafuta silaha kutoka urusi utauziwa zile za zamani. Miaka michache iliyopita walitangaza vifaru vipya vya aina ya T-4 Armata kuwa ni vya hali ya juu sana, lakini walipovijaribu vitani huko Syria na huko Donbas Ukraine kabla ya vitaa hii inayeondelea, vikaonekana kuwa weak sana wakaacha kabisa kuvitangza tena ingawa huwa vinaoenaka kwenye magwaride yao. Zaidi ya hapo, vifaru vyote kutoka Urusi ni design zilzoachwa na USSR.
 
Kwamba Urusi ishapitwa na wakati kwenye technolojia ya vita..

Ngoja nicheke kwanza 😄😄😄
wamepitwa sana mzee; Usitishwe na hayo makombora ya hypersonic au isobaric. Hizo siyo silaha za kushindia vita kwani jeshi haliwezi kuwa nazo nyingi kiasi hicho, na in fact kiwanda cha silaha hizo sasa hivi kimeshindwa kuendelea na kazi kutokana na vikwazo.
 
Wamagharibi wenyewe wanasema Urusi anatumia silaha za zamani tu mpya hajatoa hata kidogo zaidi ya yale makombora yasiyozuilika.

Hata US/NATO hakuna anaempa Ukraine silaha mpya zote ni za zamani tu.

Yaani kwa operation ya Ukraine Urusi ni kama anasafisha stoo tu..
 
Nin wasiwasi sana na silaha za masafa merfu tulizo nazo ndani ya majeshi yetu ya ulinzi. Miaka ya 200 kuna zile zilizokuwa zinarupuka zenyewe kule mbagala. Na ninavyokumkb uka Tanzania tuliwahi kununua vifaru vingi na Gun Howitzers nyingi sana wakati wa utawala wa Nyerere kutokea Urusi. Silha azile ndizo kwa kiasis kikubwa sana zinazutumika sasa hivi vitani huko Ukraine...
Kuna mwanajeshi aliyepo upande wa Ukraine alituhumu US kuwa imefanya vita ya Ukraine na Russia kama sehemu ya kuteketeza siraha zake za zaman! Mizinga waliyopeleka sometime hailipuki wamepeleka siraha za zaman!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwenye modern wafare ni mwehu tu anayetegemea vifaru vitani ... Vifaru vimebak kama magar ya msafara w kijeshi kipind cha Amani , kiufupi vita ya kutegemea vifaru ishapitwa na wakati, Ila ukijidai utegemee vifaru kwenye active battle zone ujue unawatoa kafara askari ....!! Vita ya sa hv ni propaganda , technology na Airforce , kama huna uwezo kwenye maeneo hayo omba maridhiano mapema.... Askari wenu wanaopasua tofali uwanja wa mkapa wanawadanganya
Boots on the ground bado ndiyo main part ya vita. Hivyo vyote ulivyoelezea ni msaada kwa askari wa miguu.
 
Makombora hayo ya high tech (cruise missiles) siyo mengi; hata urusi yenyewe na hata Marekani for that case hawana mengi ya ya kuwatosha hadi kuuza nje. Hata kama wangependa kuyauza nje huwa ni vigumu kwa vile guns zake ni maalum sana hazipatikani kokote kwani nyingi wamezijengea ama kwenye meli zao za kivita au kwenye ndege maalumu za kivita. Siamini kama Tanzania tayari tunazo hizo guns za cruise missles. Ukitafuta silaha kutoka urusi utauziwa zile za zamani. Miaka michache iliyopita walitangaza vifaru vipya vya aina ya T-4 Armata kuwa ni vya hali ya juu sana, lakini walipovijaribu vitani huko Syria na huko Donbas Ukraine kabla ya vitaa hii inayeondelea, vikaonekana kuwa weak sana wakaacha kabisa kuvitangza tena ingawa huwa vinaoenaka kwenye magwaride yao. Zaidi ya hapo, vifaru vyote kutoka Urusi ni design zilzoachwa na USSR.
Acha uongo T-4 haijawahi kutumika kwenye vita yeyote.
 
Makombora hayo ya high tech (cruise missiles) siyo mengi; hata urusi yenyewe na hata Marekani for that case hawana mengi ya ya kuwatosha hadi kuuza nje. Hata kama wangependa kuyauza nje huwa ni vigumu...
Armata kimetumika wapi?
 
Mkuu, Marekani hadi sasa hawana hayo makombora, kama hujui. Wanajaribu kutengeneza, lakini bado hawajafanikiwa.

Ironically. yule kiduku wa Korea Kaskazini tayari anayo!
Kuna makombora ya na mbili hapo: thermobaric na hypersonic. Thermobaric ni makombora ya kawaida sana ambayo yapo siku nyingi sana tangu mabomu ya Hydrogen yaliopoanza kutengezwa zaidi ya miaka 60 iliypoita. Kama Nyuklia, yanapigwa vita kwa sababu ni WMD; yanakamua oxygyen yote na kuua kila kiumbe kilichopo.

Tatizo labda ni hayo makombora ya hypersonic, ambayo Marekani haijatangaza kuwa nayo kwa sababu kadhaa. Hata Urusi inayatangaza lakini inayotangaza siyo Hypersonic kweli. Makombora ya hypersonic yanatakiwa kurushwa kutokana na chanzo ambacho tayari kinakaribia supersonic speed. Hakuna kombora linaloweza kurushwa kutoka stationary launcher ardhini halafu likafikia spidi ya hyepersonic kwenye hii atmospheric space. Aerodynamic principles haziruhusu kabisa kitu hiyo. Njia inayotumia kuwapata hypersonic speed ni kuyarusha makombora hayo kwa kutumia rocket ya kawaida hadi kwenye orbit fulani ambako yanaaculumate spid kufuikia kiwango kuwa yakiachiwa yanaccelerate hadi kufikia hypersonic.

Mabomu aliyotangaza Putin kuwa ni Hypesronic siyo kweli ingawa kweli yana spidi kubwa kutokana na uijazo wake wa rocket fuel lakini huwa hayafikii hypersonic speed. Mabomu ya spidi kubwa kutokana na wingi wa fuel yake kama hiyo yapo Marekani pia lakini hawayatangazi kama hyepersonic.
 
Kwenye modern wafare ni mwehu tu anayetegemea vifaru vitani ... Vifaru vimebak kama magar ya msafara w kijeshi kipind cha Amani , kiufupi vita ya kutegemea vifaru ishapitwa na wakati, Ila ukijidai utegemee vifaru kwenye active battle zone ujue unawatoa kafara askari ....!! Vita ya sa hv ni propaganda , technology na Airforce , kama huna uwezo kwenye maeneo hayo omba maridhiano mapema.... Askari wenu wanaopasua tofali uwanja wa mkapa wanawadanganya
Kama havina msaada mbona kila siku raisi wa Ukraine amekuwa akiviomba?
 
Back
Top Bottom