Silaha ya mlinzi wa Lissu imenitoa ushamba

Gluk

JF-Expert Member
Mar 23, 2017
1,763
2,000
Hiyo ni harpoon gun au Chusa kwa kiswahili
zipo zaidi ya aina 100 za harpoon gun (Chusa)
Broo hiyo kitu ukitandikwa nayo huponi na sijawahi kusikikia popote pale duniani mtu aliyetandikwa na harpoon gun akapona.
images.jpg
 

Black BackUp

JF-Expert Member
Aug 5, 2019
618
1,000
Baba huo ni Mshale wa Bomu Kama ile aliokua anatumia Rambo/ Chuck Nolis/ Van Damme kwenye Hard Target mwanzo kabisa inapoanza. Hebu chukua Muda kuperuzi utajua tu
 

zitto junior

JF-Expert Member
Oct 7, 2013
12,319
2,000
Hiyo ndiyo demokrasi na utawala wa sheria huo; hapo hajawa rais!
Would you suggest an alternative course of action?
Maana naona mnalaumu tu bila kuangalia situation. Watu wamepona kifo, polisi hawachukui hatua, gari halijaachiwa alafu unataka wafanyeje?
Siku kachukue fomu kwa tiketi ya upinzani nadhani ndio utaacha kuropoka mambo usiyofahamu.
 

Santos06

JF-Expert Member
Mar 11, 2019
728
500
Wakuu,

Nianze kwa kudeclare interest kwamba mimi sio mjuvi na sina utaalam wowote kuhusu masuala ya silaha.

Kilichonisukuma kupandisha huu uzi ni baada ya kutazama video hapa chini ikimuonyesha mlinzi wa Lissu akiwa na silaha ya ajabu ambayo nimeshindwa kuelewa ni silaha ya aina gani.

Kombora sio kombora, mkuki sio mkuki, upinde sio upinde, Rpg sio rpg

View attachment 1600189
. Hakika imenitoa ushamba sana.

Naomba mwenye kuijua anipe taarifa zake ili siku nikipata ukwasi wa kutosha na mimi nikainunue kwaajili ya ulinzi binafsi.
Asante.
picha
 

kawoli

JF-Expert Member
Feb 20, 2014
5,889
2,000
Huyu akiwa rahisi atayafunga ma flyover yote
Nimeshangaa Sana. Yaani raia wakose huduma ya kutumia barabara kisa interests zake? Halafu anadai abapambania haki za wanyonge, hapo amefeli. Sasa huyu akiwa president halafu mtu akaingilia maslahi yake binafsi atabaki salama kweli?
 

Saguda47

JF-Expert Member
May 1, 2016
8,052
2,000
mkuu zile ni Uzi gun tu wala zisikutishe sana. ni tofauti sana na hiyo harpoon gun. kwa lugha nyepesi ile ni bomu mshale
Hahhaaa! "Uzi gun tu Wala zisikutishe".... Kati ya hiyo harpoon na hizo Uzi guns + IWI Galilee zipi Ni bunduki za gharama na ufanisi?

Hiyo harpoon inalenga shabaha moja tu na haina quick reloading system Ni sawa na goboli tu.

Usilinganishe supersonic rifles za ulinzi wa Rais na Hilo goboli la karne ya 18 na 19 !
 

Mdaiwa-Sugu

Senior Member
Mar 8, 2020
189
500
Hiyo ni harpoon gun au Chusa kwa kiswahili
zipo zaidi ya aina 100 za harpoon gun (Chusa)
Broo hiyo kitu ukitandikwa nayo huponi na sijawahi kusikikia popote pale duniani mtu aliyetandikwa na harpoon gun akapona. View attachment 1602620
Mkuu nimesoma habari zake ni kweli inajulikana kwa hilo jina la harpoon gun. Google wanasema ni moja ya silaha hatari sana inayotumiwa kuulia samaki wakubwa kama vile papa na nyangumi ambao siyo rahisi kufa kwa mpigo wa risasi moja.
Nilichokosa ni jinsi gani inavyofanya kazi kama hutojali nipe elimu kidogo kuhusu utendaji kazi wake, upatikanaji wake, kibali chake na namna ya kuitumia
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom