Je, huyu mlinzi wa Tundu Lissu anauwezo wa kumlinda dhidi ya jaribio lolote endapo litatokea?

othuman dan fodio

JF-Expert Member
Jan 2, 2018
5,668
9,055
Bila shaka wengi wetu kwa siku za hivi karibuni tumeona nyuma ya Tundu Lissu kuna mtu anasimama kama Bodyguard katika kila sehemu anapokuwa mfano mzuri pia ni leo alikuwepo naye katika mkutano wa ACT Wazalendo.

Ni kipande kimoja cha mtu huwa kinapiga miwani yake nyeusi na muda mwingi huwa hacheki ( uso wa kauzu) kwa inavoonekana ndiye mlinzi wa undu Lissu kwa sasa.

Swali linakuja, je hicho kipande cha mtu anaaminika kulinda usalama wa Lissu hasa katika kipindi hiki tunachoelekea kwenye mikiki mikiki ya kampeni?

Chama kinapaswa kutambua kwamba Lissu amenusurika kuuawa na watu wasiojulikana, lakini kwa ujasiri alionao amerudi nchini na chama kimemteua agombee nafasi ya Urais.

Lakini mmeona na kusikia tangu Lisu arudi kutoka Ng'ambo amekuwa mwiba mkali na kurusha makombora hatari hasa upande ule na hususani kumuhusu namba moja.

Wote tunafahamu kwamba namba moja sio mvumilivu sana kwenye siasa za ushindani hasa kwa hasimu wake Tundu Lissu, yamkini kuna second attempt to attack Tundu Lissu

So huyu Bodyguard ambaye anaambatana na Lissu yupo makini kiasi gani kuhakikisha this time around hawafanikiwa kuchomoa manati zao na kumshambulia tena?

Angalizo umakini uongezwe juu ya ulinzi kwa Lissu, ilikusudi aendeshe kampeni zake akiwa salama salmin.
 
Sidhani kama hayo na ni matumizi sahihi ya neno ,,credible'' kulingana na maudhui yako, nafikiri ulitaka kumaanisha kama huyo Bodyguard anaaminika kwenye kumulinda huyo Masia wenu, kama ni hivyo sidhani kama hilo neno sahihi kutumika hapo, ...
 
Sidhani kama hayo na ni matumizi sahihi ya neno ,,credible'' kulingana na maudhui yako, nafikiri ulitaka kumaanisha kama huyo Bodyguard anaaminika kwenye kumulinda huyo Masia wenu, kama ni hivyo sidhani kama hilo neno sahihi kutumika hapo, ...

kumulinda ni nini?
...wewe mwenyewe hujui hata kuandika, umebaki kusema tu unadhani, mara unafikiri!
Umeandika takataka!
 
Maaduwi wake.. ndiwo anashinda nao kila siku.. huyo naye anawapa yale anafanya.. hivi dereva wapi siku hizi?

Kikulacho ki.....
 
kumulinda ni nini?
...wewe mwenyewe hujui hata kuandika, umebaki kusema tu unadhani, mara unafikiri!
Umeandika takataka!


Sawa, lkn hilo neno ,,credible'' ni sawa kutumika hapo kulingana na maudhui yake?
 
Kama wewe unaona si sawa ni mtazamo wako!
Mwingine ataelewa zaidi yako ama tofauti na wewe! Neno moja linaweza kuwa na tafsiri nyingi tu linapotumika!


Ni matumizi sahihi ya hilo neno au siyo? ndiyo/hapana/haujui?
 
Naomba kuuliza..hiyo mbavu bodiguard anaweza kusimama wima akipigwa sindano ya hicho? Au Ni mbwembwe tu za kutinisha misuli
 
Back
Top Bottom