Hii nchi inawapumbavu wengi kuliko wajinga.
Yaani leo hii Yeriko anataka tuamini kuwa huu mradi ni wa manufaa kwetu kuliko kwa Mchina na mu Oman?.
Ni kweli tumekuwa wapumbavu kiasi hiki?
Mtu anakuambia atagharamia kila kitu wewe toa ardhi tu na rasilimali nyingine...halafu kutakuwa na chombo cha kukusanya mapato na si TRA ila TRA watachukua gawio kutoka kwa chombo hicho! Kweli?
Miongoni mwa viongozi wa hovyo nchi hii kwasasa ni Ndugai.
Ni mnafiki.
Ni tapeli.
Yaani hajui watu wanaakili kuliko yeye.
Tuna watu wa hovyo sana nchi hii.
Yaani tunatakiwa kuaminishwa leo kuwa mchina ni mkombozi wetu.
Eti Tanzania ifanywe kitovu cha uchumi wa dunia
. Dah. Yaani Yeriko umetudharau kiasi hicho?
Eti Dubai na Marekani sijui gani huko zigawane uchumi na Tanzania.
Eti mizigo yote Africa ipitie Bagamoyo!!
Eti leo Tanzania iwe na eneo linaloitwa Bagamoyo nchi zote Africa zije kuchukulia bidhaa zake hapo.
Ee Mungu tunusuru. Kama kuna mahali Mungu tumekukosea tusamehe tu jamani.
Yaani kuna kakikundi ka watu wanaamini wao ndo wanauwezo wa kufikiri kwaniaba ya Watanzania wote.
Tuacheni na vi miji vyetu na vibandari vyetu.
Narudia tena kusema....hii Username muimark.....kuna siku nitajitambulisha hadharani.
Ila wakati huo katika hali ambayo haitatarajiwa na wengi.
AMEN.