Sikumkimbia Dr. Slaa New Africa Hotel

Dr. Mwigulu Nchemba

JF-Expert Member
Feb 25, 2012
416
2,037
Kuna thread iliwekwa humu kuwa nilikuwa naongea na Nyakarungu na mara baada ya Dr Slaa kufika nilikimbia.

Taarifa hizi kuwa nilikimbia sio za kweli na sikuwa na sababu ya kufanya hivyo. Nina ratiba zangu na uhuru wa kuongea na mtu yeyote. Ni bahati nzuri hata Dr. Slaa mwenyewe sikumwona na sijui kama na yeye aliniona. Na nilikuwa njiani na kulikuwa na watu wengi tu na alipita bila attention ya watu.

Mimi naongea mambo kadha wa kadha na vijana wengi tu bila kujali vyama wakitaka kujua namna ya kuingia bila fedha kwenye siasa na kufanikiwa kama ilivyotokea kwangu, wakiomba ushauri kwa mambo ya shule na ujasiliamali.

Si jambo jema na sio afya kwa Taifa kwa vijana kuwaza fitna kila wakati.
 
Humu kuna vituko,sasa umkimbie kwani ana mapembe.
Ndiyo ,jamaa sio handsome kivile,hata kama anatisha(i mean muonekano)ndo kweli mtu amkimbie?
 
Nina ratiba zangu na uhuru wa kuongea na mtu yeyote. Ni bahati nzuri hata slaa mwenyewe sikumwona na sijui kama na yeye aliniona. Na nilikuwa njiani na kulikuwa na watu wengi tu na alipita bila attention ya watu.
Mwigulu,
Hapo kwenye nyekundu na blue mbona zinakinzana? Nikisoma between lines naona kama ulimuona Dr. Slaa (angalia kwenye blue), ndiyo maana unasema kulikuwa na watu wengi na hata attention hakupata. Wakati huo huo unasema (kwenye nyekundu) kwamba hukumwona Dr. Slaa. Pole sana kwa kujichanganya.
 
Mwigulu,mwenye akili alishajua kilichoongelewa kwenye ile thread issue ilikuwa babu kujitafutia ujiko.
 
Ungekuwa unawajibika kujibu hivi na kwenye mambo ya msingi labda tungekutofautisha kidogo na JK, lakini yale yale...mambo madogo madogo ndio mnayoyapata uzito. Mbona hujasema kitu kuhusu uhuni mliofanya bungeni kuzima hoja ya Mbatia, Matokeo mabaya ya Kidato cha 4 na kutoweka kwa amani huko Zanzibar na Geita? Nataka ujibu kama Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara)
 
Nchemba unaweza kuwa na maarifa na uzoefu wa kubadilishana au kufunza wengine juu ya siasa za kupandikiza na kueneza chuki lakini si mbinu za kuingia katika siasa bila kutumia pesa.

Unaweza kufundisha ujasiriamlo wa kisiasa na si ujasiriamali wa kutafuta mafanikio kihalali.

Anza kwa kutuweka wazi ni biashara gani umewahi kuifanikisha kijasiriamali kabla ya siasa chafu?
 
Ungekuwa unawajibika kujibu hivi na kwenye mambo ya msingi labda tungekutofautisha kidogo na JK, lakini yale yale...mambo madogo madogo ndio mnayoyapata uzito. Mbona hujasema kitu kuhusu uhuni mliofanya bungeni kuzima hoja ya Mbatia, Matokeo mabaya ya Kidato cha 4 na kutoweka kwa amani huko Zanzibar na Geita? Nataka ujibu kama Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara)

Mkuu SG8 nimeipenda hiyo. Very well said.
 
Mkuu naomba kuuliza kwani wewe na Dr.Slaa mna ugomvi hadi umkimbie? au nikuchafuana tu.
 
Back
Top Bottom