Bora mh [MENTION]Nchemba [/MENTION]Ungekuja na mikakati ya nini kifanyike baada ya chama chako
1. Kuwagawa watanzania kupitia sera zenu za kusingizia udini kwa wapinzani wenu mfano, CUF waislam, Chadema kristo
2. Kufeli kwa watoto wetu 60% zeros na haya ni kwa mujibu wa sera zenu ccm kuwapuuza waalimu nk
3. Afya duni na ukosefu wa huduma bora kwa mujibu wa sera za ovyo za ccm
4. Mfumko wa bei, maisha bagum na hakuna chochote kuwapa nafuu watanzania kila leo afazari ya jana
5. Ukosefu wa ajira na kufa kwa viwanda vyetu ambako kungeinua uchumi wetu nk
6. Ukandamizaji wa demokrasia bungeni na kufutika hoja zenye tija mkibakia kufanya ushabiki.
Mh mwigulu, ungekuja na mjadala wenye changamoto kama hizo hapo juu, ungeleweka kutokana na nafasi yako kitaifa
katika chama chako ccm. unakuja kujiteta hapa na hoja dhaifu kabisa kiasi kwamba ni kuendeleza dhana ya viongozi
wengi wa ccm kutupuuza kama mfanyavo bungeni kila siku, kupuuza na kuzima hoja zenye tija kwa visingizio vya muda
lakini muda wa wa kuzipokea yanga na simba bungeni mnaupata. Mwigulu hujatutendea haki.