Jamani rejeeni hotuba ya Mwinyi ya kuleta Azimio la Zanzibar - ipo humu humu JF kwenye mjadala wa Azimio la Zanzibar, kwa kiasi fulani yuko sahihi hawakulifuta kabisa Azimio!
Mkuu Companero,
Ni kweli kabisa kwenye Hotuba wanasema hawakulifuta bali walikuwa wanaweka mazingira mazuri ili wana siasa waweze kushiriki kwenye shughuli za biashara.
Msingi wa Azimio la Arusha ni siasa ya Ujamaa na Kujitegemea, ambayo kwa sasa imebaki kwenye maandishi tu.
Nchi zilizoendelea mtu akiamua kuingia kwenye siasa, biashara zake anaziacha ili zisimamiwe na mtu mwingine kwa ajili ya kuepuka mgongano wa kimaslahi ama kutumia vibaya madaraka.
Tumeona akina Karamagi, Mkapa, Yona, Mramba na wengineo wengi jinsi walivyotumia vibaya ofisi zao kwa maslahi yao na tena kwa uwazi kabisa maana walikuwa wanajua hakuna sheria ya kuwabana. Ndiyo JK anapiga kelele sasa kwamba watunge sheria ya kutenganisha biashara na siasa, which is too late.
Kwa kifupi, Azimio la Zanzibar limezaa mafisadi wakubwa sana na ndiyo maana pengo kati ya tabaka la walalahoi na wenye nazo (wanasiasa) limezidi kuongezeka. Walipoleta Azimio la Arusha waliacha mianya ya wao kujitajirisha kwa haraka bila ya kuwa na sheria, kanuni, taratibu za kuwabana iwapo wangetumia vibaya madaraka yao.
Nenda kwenye vitalu vya uwindaji wamejaa wanasiasa, nenda kwenye migodi kuna mikono ya wana siasa, nenda kwenye vikampuni vya utalii wamejaa wao. Ukichunguza sana utakuta kila mwana siasa ana kikampuni uchwara kwa ajili ya fursa ya kukitumia pindi fursa ikitokea.