Sikulifuta Azimio la Arusha - Mwinyi

Sikulifuta Azimio la Arusha - Mwinyi

Mkuu jmushi1, nimeipenda sana signature yako, ""Our POVERTY is the EVIDENCE to the NEGLIGENCE of OURLEADERS" The facts speaks for themselves." Na kama alivyosema Rev Kishoka yaani uandishi wako umeongezeka katika kiwango kikubwa sana. Hongera sana Mkuu.
11582789.gif
 
- Bado ninasisistiza kwamba taifa linatakiwa kuongozwa na sheria, sio maa-Azimo flani hivi, haya maazimio ndiyo yamechangia sana kuturudisha nyuma katika utawala wa kuheshimu sheria, tujali sheria kwanza ndio tutasonga mbele.

Respect.

FMEs!

Sheria hutokana na sera na maazimio. Ndio maana sheria nyingi za haki za binadamu zinatokana na Azimio la Haki za Binadamu. Azimio la Arusha liliweka misingi ambayo ilipaswa kuingia kwenye sheria mfano. Sheria dhidi ya Ufisadi wa Viongozi wanaokiuka Maadili/Mwongozo, Sheria dhidi ya Umiliki wa Kifisadi wa Makampuni ya nje yanayochota madini yetu na kutuulia wananchi wetu, Sheria dhidi ya umiliki binafsi wa ardhi kubwa n.k.
 
Waberoya,

Mimi na wewe tunatofautiana kwenye msingi mmoja tu. Argument zako zimeegemea kuwa Azimio Halikuwa sheria wala Katiba. Mimi naungana na waliosema kuwa Azimio lilikuwa vision, lilikuwa roadmap. Sheria Nyingi zilitungwa ambazo hazikuwa azimio lenyewe bali kwa lengo la kufikia vision iliyomo kwenye Azimio.

Mzee Mwinyi na serikali yake hawakulipinga Azimio kama vision, ila walifanya mambo yaliyoashiria kuwa hawakubaliani na vision ile. Azimio la Zanzibar lilikuwa ni difiance against lile la Arusha na lilionesha wazi about turn kutoka mwelekeo wa kuelekea Azimio la Arusha.

Hakuna tukio jingine linaloonesha kulikataa azimio la Arusha kama azimio la Zanzibar. Mwinyi inabidi akiri kuwa leadership yake ilituondoa kwenye mwelekeo wa kuelekea AA. Alituelekeza wapi? Aseme.

Kusema kuwa hatu appreciate mazuri ya uongozi wa Mwinyi si sahihi. Tunajua kuwa mwinyi yako mambo aliyofanya kama uhuru wa kujieleza kuimalika, kuruhusu private enteprise ku flourish, n.k. Lakini Makosa yake yako wazi zaidi na sihitaji kuyarudia hapa.

Mwinyi alicho fanya ni BLAME GAME NA ESCAPISM alipokuwa akihutubia taifa kwenye ufunguzi wa benki ya Mkombozi. Ni makosa gani ambayo Mwinyi kwa maneno yake Mwenyewe ameshayakiri??
 
Wakuu zangu tutabishana hadi kesho kutwa ikiwa hatutazingatia hoja ya mada hii.. Kauli ya Mh. Mwinyi kuhusu yeye kutoliua Azimio la Arusha inatokana na hali halisi ya Ufisadi na Uongozi mbaya usokuwa na Uzalendo uliopo leo hii..Na ndio sababu kubwa ya hotuba ya Mwinyi kukana kwamba Azimio la Arusha halikufa! akiwa na maana bado lengo la kufikia Ujamaa na Kujitegemea lipo pale pale kama sababu ya kuepa matokeo ya Azimio la Arusha ktk joto la uongozi..

Na kama tutazungumzia mashirika ya Umma nadhani Ujamaa wa kisoshalist ulikufa siku mwalimu Nyerere alipokubali kuhsindwa Mai -June mwaka 1984 na kuingia Ubepari.. Hapo ilikuwa ruksa tosha ya Kibepari nchini tulipofungua milango ya kimfumo kuingia soko huria..hatukuhitaji Azimio la Zanzibar kwani tayari ruksa ilikuwepo..Ila Azimio la Zanzibar lilikuja kuwapa viongozi uwezo wa kumiliki mali na hakika uwezo wa kujiuzia mashirika na mali yote ya Umma iwe mikononi mwao..Ilipangwa hivyo toka awali na haya ndio matokeo wazi kabisa ya Azimio hilo na hayahitaji mjadala. Hakika hapakuwa na jipya ktk Azimio la Zanzibar isipokuwa kuwawezesha viongozi kujishughulisha na Biashara..

Sasa tuzungumzie malengo na yatokanayo na Azimio la Zanzibar - Kuwawezesha viongozi kufanya biashara ilikuwa ni hatua ya kwanza kuleta UBINAFSI..Pili, ilikuwa ni kuwawezesha wao VINGOZI kuyanunua ama kuyauza mashirika ya Umma ili wao wapate kuyamiliki. Azimio la Zanzibar halikuja na mfumo wowote wenye kulinufaisha Taifa ktk uuzaji wa mashirika ya Umma ila kuwawezesha viongozi kuyachukua wao. Haya ndio yalikuwa malengo ya Azimio hilo

Sasa tujiulize, ikiwa wao ndio waliokuwa viongozi wa mashirika haya haya wakayaua, leo tena yanauzwa kwa wale wale walioshindwa kuiyaongoza hapo awali..Tunategemea kitu gani?..Huko nyuma kuna mchangiaji kayataja mashirika mengi ambayo aliyaita Utitiri wa mashirika chini ya serikali kuu, kweli yalikuwepo lakini sijui kama mchangiaji anaweza kunambia ni mashirika mangapi kati ya hayo leo hii yanafanya kazi chini ya umiliki binafsi? Lengo ya kuyauza ni kuyawezesha mashirika yale au sio? vipi tena leo ndani ya Ubepari hatuna hadithi hata moja ya mafanikio ya mashirika yale yale tuliyoyabeza ndani ya Ujamaa?..
Mashirika haya waligawana ama kuyauza wao walioyaua ndani ya Ujamaa kuyabinafsisha! toka mkono wa serikali kwenda mkono wa viongozi....ama kweli Ubepari una mikakati ya ajabu. Hawa viongozi walichukua mashirika hayo wakahodhi ardhi (viwanja) ambavyo ndivyo vyenye thamani, leo hii wanaviuza viwanja kwa mabilioni kwa sababu hawakuwa na nia ya kufufua mashirika yale yaliyojiuzia..Tunayaona pia majumba ya NHC na Msajili, bustani za taifa, hifadhi za wanyama na kadhalika yaani mali yote ya Umma imekuwa ni mali ya viongozi ambao wanaamua wao kuuza kama mali zao BINAFSI na sidhani kama wanalipa hata kodi za uuzaji...Huu ndio Ubepari tuliouchukua sijui toka nchi za Magharibi zipi!

Wakuu zangu, matokeo ya hali mbaya ya kiuchumi leo hii inatokana sana na Azimio la Zanzibar, na kwa bahati mbaya lile gonjwa la UBINAFSI limefika ktk mizizi ya mti huu wa maendeleo ya Tanzania kiasi kwamba wakati wa Nyerere ilikuwa matawi tu (mashirika ya Umma) ya mti huu yalibakia gunzi tupu, leo hii mti mzima wa maendeleo ya Tanzania unaliwa na mchwa na imefikia hadi WATU na mazingira yake kulana wenyewe kwa wenyewe.. Hakika huo Ubinfsi at the best!.

Hivyo tunapozuingumzia Ubepari na pengine kuukejeri Ujamaa tujiulize, hivi kweli leo hii sisi Watanzania tunafuata mfumo wa Ubepari ama tunajiendelea tu bora liende tukidhani kwamba kuondoa mashirika chini ya Uongozi wa serikali ndio Ubepari wenyewe na hakuna miiko wala maadili yake..
Kisha jamani nitarudi nyuma tena kuwakumbusha kwamba WATU na MAZINGIRA ndio kioo cha upangaji mikakati yoyote ya nchi. Ubinafsi kinyume cha Ujamaa hauwezi kufanya kazi nchini kwetu kwa sababu sisi Watanzania hatuna utamaduni huo. Ubinafsi ni utamaduni mpya kabisa ktk jamii yetu na hakika ndio maana tunakwenda hovyo pasipo kujua malengo mazima ya ujenzi wa Taifa letu ni kupata kitu gani.
Huwezi kubadilisha mfumo wa maisha ya mchwa na kuyafanya yawe sawa na wadudu wenye asili moja..Sisi tulikuwa Wajamaa toka enzi kwa mana ya Ujamaa wa Kiafrika, tulijenga vijiji vyetu kama familia moja pamoja na kuwepo Ubinafsi wa koo lakini kwa Ujumla wake tulikuwa Wajamaa Kijamii na Mabepari kiuchumi, leo hii tunakuwa Mabepari kijamii na Madalali kiuchumi.. hatutafika!
 
By the way, kuna mtu anaweza kuweka analysis jinsi WB na IMF walivyoathiri nchi zetu, na je AD lingekuwa in effect lingeathiriwa na WB au lisingeathiriwa??-msaada jamani

Mzee Waberoya, heshima yako ndugu yangu. Ningependa kuchangia kidogo katika ombi lako la haya majinamizi ya WB, IMF na pengine WTO. Lakini kabla sijachangia, naomba elimu kidogo. Umeandika mahala katika mjadala huu kuwa Nyerere alikataa mawazo mazuri ya Mtei. Je ni yepi hayo? Unaweza kuniorodheshea unayoyajua na uzuri wake ni upi? Je, unatumia muzani gani kupima uzuri wa hayo mawazo. Hapa nina maana kwamba, unadhani ni mazuri kwa sababu yalitolewa na Mtei au kwa sababu yalikataliwa na Nyerere? Je inawezekana ni mazuri kwa sababu aliyatoa mahala pengine na yakakubaliwa na kuonyesha uzuri wake? Kama hivyo ndivyo, unaweza kunishirikisha mifano? Mzee nakusubiri kwa hamu kubwa. Si unajua hapa tunakuja kuchota busara na kuingia mitini!
 
Mzee Waberoya, heshima yako ndugu yangu. Ningependa kuchangia kidogo katika ombi lako la haya majinamizi ya WB, IMF na pengine WTO. Lakini kabla sijachangia, naomba elimu kidogo. Umeandika mahala katika mjadala huu kuwa Nyerere alikataa mawazo mazuri ya Mtei. Je ni yepi hayo? Unaweza kuniorodheshea unayoyajua na uzuri wake ni upi? Je, unatumia muzani gani kupima uzuri wa hayo mawazo. Hapa nina maana kwamba, unadhani ni mazuri kwa sababu yalitolewa na Mtei au kwa sababu yalikataliwa na Nyerere? Je inawezekana ni mazuri kwa sababu aliyatoa mahala pengine na yakakubaliwa na kuonyesha uzuri wake? Kama hivyo ndivyo, unaweza kunishirikisha mifano? Mzee nakusubiri kwa hamu kubwa. Si unajua hapa tunakuja kuchota busara na kuingia mitini!

umepotea muda mrefu kamanda, lakini pamoja na hayo, umeuliza maswali ya maana sana, ambayo ni raisi mno kujenga hoja za maana, na labda hilo swali lisingekaa zaidi kwa Mtei bali lingekuwa kwa yoyote ambaye alitoa mawazo ya maana na yakakataliwa na Nyerere ni bora yakawekwa hapa ili tupate kujenga hoja zenye balance
 
Sasa Wareboya na Pundamilia ( Mnyama Mpole, mtaratibu hope mwenye Busara pia)
Kuna Pepsi walikuwa wafanya biashara na hakuna share holding ya serikali, na ushindani ulikuwa kama hakuna, kuna Coca Cola, kuna Toyota Tanzania LTD, KJ motors, JV Group of Companies, Somaia Group, na mengineyo mengi tu, je kwanini hawapo mpaka leo au katika ili nguvu waliokuwa nayo mwanzo, na licha ya kupewa exmption za kila aina na wizi juu? tukaona new kids on the block kama marehemu gulamali, dewji kassim na nduguze yule wa pan african na yule wa simba sc sio huyu mo'dewji mbunge wa singida, afro cooling system imeishia wapi , haya makampuni ya kutengeneza mafuta ya kula ndio hayo tena, yanaenda kinyume nyume badala ya quality na prduction kuongezeka, kulikuwa na VOIL, na yale mafuta ya pamba wapo wapi nk nk.
maana kipindi kile cha imf/wb tulitekeleza kila kitu walicho kitaka je mafanikio yapoje? mimi nilitegemea shs yetu sasa ingekuwa atleast 1 to centi hamsini za kenya lakini utaona ndio tumezidi kuchwa mbali, wakati kenya ardhi iliyo na rutuba ni 1/3 sisi ni 3/4, mahindi s'wanga na kwingine yanalimwa na watu binafsi, shinyanga mchele kibao, lakini leo hii sehemu maskini ni hizo mbili au yenye miundo mbini mibovu, uje singida na alizetti yao, hivyo hivyo, tabora na tumbaku yao mambo ni hayo hayo.

Nadhani Tanzania tunahitaji wafanyibiashara wakubwa wasiozidi 10 tu hasa wale ambao ndiyo walipa kodi wakubwa. The rest wawekwe katika kundi la wafanyibiashara wa kati na wadogo. Sera zetu za kuleta madabidiliko ya uchumi yalenge katika kuimarisha uwezo wa kundi hili ambalo nadhani linaweza kuwa ndiyo moja ya mihimili mikuu ya uchumi wetu kwani lina rasilimali nyingi kuliko wafanyi biashara wakubwa.
Pili hayo makampuni uliyoyataja ya KJ Motors, VOIL, JV Group na mengine kama hayo yalimilikiwa na watu ambao walikuwa victims wa AD. Kwa hiyo walipoachiwa wafanye bila ya kuwepo ushindani kutoka kwa wazawa walihakikisha wanahamisha fedha zao Canada, UK na kwingineko. Wengi wao hawakuendeleza uwekezaji wao kwa wameshindwa kuhimili ushindani na mabadiliko ya kweli ya uchumi. Kwa mfano KJ Motors wakati ameshamiri hakukuwa na wazawa wanauza magari lakini sasa magari yanauzwa kila kona tena kwa bei na maelewano mazuri. Wapo wafanyibiashara wengi tu ambao walikuwa wanabiashara kubwa-kubwa lakini sasa hivi wanafanya biashara zinazolingana na mahitaji ya soko.
Tatu, biashara nyingi zilizokuwa zinamilikiwa na baadhi ya hao wafanyibiashara walikuwa wakichotewa fedha kutoka katika pesa zetu za kodi kwa kushirikiana na watumishi wa serkali ambao walikatazwa kufanya biashara ama kupokea vipato viwili, kwa hiyo baada ya mirija hiyo kukatika ni wazi mengi yao yatajifia. Lakini kubwa zaidi pesa zetu nyingi zilihamishwa nje na wale victims wa Azimio la Arusha.
 
- Kuzungumzia kifo cha Azimio bila kutaja faida zake kwa hili taifa ni kufukuza upepo, so far zimetajwa hasara nyingi za Azimio kuliko faida, maana yake ni moja kwamba Azimio halikuwa effective at all, sasa alaumiwe nani aliyelileta Mwalimu, au aliyeliua Mwinyi?

- Kwangu it does not matter, cha muhimu ni reconciliation na tusonge mbele, Azimio halitakuja kurudi tena hiyo ni fact, kulumbana kuhusu aliyelileta au aliyeliua ni waste of time, ni muhimu kujadili effective zake kwa taifa lakini in the process ya ku-move forward sio kutafutana uchawi.

- Bado ninasisistiza kwamba taifa linatakiwa kuongozwa na sheria, sio maa-Azimo flani hivi, haya maazimio ndiyo yamechangia sana kuturudisha nyuma katika utawala wa kuheshimu sheria, tujali sheria kwanza ndio tutasonga mbele.

Respect.

FMEs!

Ni kweli nchi inatakiwa kuongozwa kwa mujibu wa sheria na wala si maazimio.
Tukianza kuongelea maazimio kama msingi wa kuendesha tutakesha. Kuna maazimio mengi tu na hatujui kama yapo au yalikufa.
Azimio la Musoma,
Azimio la Iringa
So, why Azimio la Arusha?
rip AD!!!!
 
- Kuzungumzia kifo cha Azimio bila kutaja faida zake kwa hili taifa ni kufukuza upepo, so far zimetajwa hasara nyingi za Azimio kuliko faida, maana yake ni moja kwamba Azimio halikuwa effective at all, sasa alaumiwe nani aliyelileta Mwalimu, au aliyeliua Mwinyi?

- Kwangu it does not matter, cha muhimu ni reconciliation na tusonge mbele, Azimio halitakuja kurudi tena hiyo ni fact, kulumbana kuhusu aliyelileta au aliyeliua ni waste of time, ni muhimu kujadili effective zake kwa taifa lakini in the process ya ku-move forward sio kutafutana uchawi.

- Bado ninasisistiza kwamba taifa linatakiwa kuongozwa na sheria, sio maa-Azimo flani hivi, haya maazimio ndiyo yamechangia sana kuturudisha nyuma katika utawala wa kuheshimu sheria, tujali sheria kwanza ndio tutasonga mbele.

Respect.

FMEs!
Mimi siambiwi kitu kuhusu Azimio la Arusha. Nakaa nyumba ya NHC ilyotaifishwa baada ya Azimio hili; Nimesoma shule ya kanisa iliyotaifishwa baada ya Azimio hili; Nimefanya kazi kwenye mashirika ya umma ambayo ni matunda halisi ya Azimio hili; Nimezikuta maliasili zetu zote zikiwa "intact". Tumeanza kuzifakamia baada ya kuliua Azimio hili.
Tumekuwa na viongozi wazuri tu kimaadili wakati wa Azimio hili; kwa kweli manufaa ni mengi.
 
Mzee Mwanakijiji;854186]Hapa tutazungumzia magnitude ya kufanya hivyo; leo hii nchi za Kibepari zinaingilia kati umiliki wa uchumi na zimekuwa zikifanya hivyo kwa muda mrefu. Tusingeweza kuacha njia za uchumi zote ziwe mikononi mwa kikundi cha watu watu wachache. Tusingeweza kusubiri kama kina Obama miaka 40 baadaye kuona kuwa wananchi ni lazima wawe na interest katika kuendesha uchumi wao.

Kinachotakiwa kwa serikali ni kusimamia majukumu yake ya kuongoza nchi ikiwa ni pamoja na uweka mazingira mazuri ya kustawi kwa uchumi wa nchi, hii ni kazi ya serikali. Kwa hiyo kazi ya serikali si kufanya UCHUUZI kama ilivyokuwa ikifanywa hapo awali. Hata huko umarekani serikali haifanyi UCHUUZI inahokifanya ni kutimiza wajibu kama msimamizi wa sera za ustawi wa uchumi.


Kwenye hili la kuku inaonekana hujui lengo la shirika hilo lilikuwa ni nini. Sisi tulikuwa wafugani wa kuku wa mayai na wa nyama. Shirika la Kuku lilikuwa linafanya urahisi wa sisi wengine kwenda kununua vifaranga kutka katika matawi yake mbalimbali. Ulikuwa unaweka oda halafu unaenda kuchukua au wanakutumia maboxi yenye matobo matobo ya vifaranga. Ilikuwa inahakikisha chakula cha kuku kipo na chenye mchango wa lishe inayotakiwa.

Sisi wananchi tuliokuwa tunafanya shughuli hiyo hatukulazimika kwenda Zambia kutafuta vifaranga.

Hapa Mzee Mkjj huna hoja ya nguvu, hivi sasa Tanzania kuna wafanyibiashara wa kuku wangapi ukilinganisha na wakati huo? Je, wanapata wapi vifaranga? Kampuni ya kuku haikuwa na umuhimu wowote wa kumilikiwa na serikali. Serikali ilitakiwa kuwekeza katika vituo vya utafiti wa kuku na wanyama wengine na sio kufanya biashara. Vituo vya utafiti ndiyo vingetumika kutoa ushauri wa jinsi ya wafugaji wanaweza kuwekeza katika biashara ya kutotoa vifaranga, ubora wa chakula cha kuku, matibabu, nk. Resources muhimu ya kufanya mambo hayo zilipotezwa kwa kuanzisha na kuiendesha kampuni hiyo. Tukubali wazo halikuwa sahihi.


Serikali karibu zote duniani zinafanya aina fulani ya biashara. La maana ni kuchagua ni biashara gani na kwa kiasi gani. Fannie Mae na Fred Mac ni makampuni ya biashara ya serikali, leo hii GM na Chrysler ni makampuni binafsi lakini serikali ya Marekani ina hisa? why is that? Kwa sababu kuna mambo fulani kwenye uchumi uwezi kuachia tamaa za watu za fedha kuyafanya, matokeo yake ndiyo haya tunayoyaona.

Kama nilivyoeleza kazi za serikali sikuchuuza bali ni kubuni na kusimamia utekelezajiwa sera za kustawisha uchumi ambazo wananchi watazituma/watafaidika nazo katika kujiletea maendeleo yao. Kwa hiyo katika issue ya GM/ Chrysler/mabenki serikali ya umarekani ilichokifanya kutimiza kazi yake ya usimamizi (regulator mkuu wa uchumi) na wala si vinginevyo. Hali kama hiyo inaweza ikamkuta mtu yeyote yule anayefanya biashara pale ambapo biashara yake haiendi vizuri basi anaweza kuteuliwa maneja wa kuisimamia kampuni yako kwa maslahi ya wale wenye interest kwenye biashara yako kama vile wanahisa au wadogo au creditors.
Juu ya Fannie Mae na Fred Mac, haya makampuni yameanzishwa kwa malengo maalum na yana mfumo wa uendeshaji wa private mbali ya kwamba ni ya serikali. Mfumo kama huo ndiyo ambao umeanzishwa Tanzania - TASAF ambapo in the long run iwe inajiendesha yenyewe kama partner wa jamii. Kwa hiyo makampuni ya Sallie Mae na Fannie Mae hayapo kwa malengo ya kufanya biashara.
Amtrak ni shirika la reli la nchi ya kibepari zaidi; angalia hata matreni ya DC na NY




Nipe mfano wa nchi yoyote duniani yenye mfumo ambao hauusishi serikali kwa namna fulani hata kwa umiliki?

Swali lako linajibika kwa swali hili
Nipe mfumo ambao serikali inafanya UCHUUZI karibu katika kila jambo kuanzia Viatu, Nguo, Vyakula, Kuku, Ng'ombe, Maziwa, list ni ndefu

Hilo ni suluhisho potofu, suluhisho bora ni kuangalia jinsi gani unaweza kuyasaidia kuyafanya ya faida. Kuyauza tu hakutayafanya kuwa na faida. Kuuza mashirika hakutasababisha yawe na faida. Mtu mwenye hekima na utaalamu ni yule anayejiuliza jinsi ya kuyafanya mashirika hayo yawe bora na yenye faida.

Wewe ungeamua kugombea ubunge leo hii ningekunyima kura yangu. Nchi ilikuwa na makampuni ya serikali takribani 400 na mengi yao yanategemea ruzuku ya serikali ambayo inatokana na pesa za walipa kodi wa nchi nyingine, wanaokupa hizo pesa za kulipa mishahara ya walimu na polisi wanakuambia kuwa hatuwezi kubeba mzigo wa hasara zinazopatikana katika makampuni yako, wewe utaendelea kuwaambia kuwa nipeni tu? Busara unayoisema wewe ndiyo hiyo ambayo serikali ya Mwinyi na Mkapa iliifanya ya kuyarekebisha mashirika hayo kupitia Tume ya Rais ya Kurekebisha Mashirika ya Umma, ambapo yale yaliyokuwa mzigo na hayawezekani kurekebishwa yalipigwa chini ikiwemo Kampuni ya Kuku. Na mengine yaliuzwa. Na huo ndiyo ulikuwa uamuzi sahihi.

Hoja yako ya mwisho ina negate kabisa hoja nyingine. Kama serikali haifai kufanya biashara kwanini tena iwe na hisa badala ya kuacha sekta binafsi ifanye mambo yote? Unless unaamini upande mwingine kuwa serikali inaweza kushiriki katika biashara ya aina fulani.

Mimi siyo conservative kwa maana nikikataa hoja moja kwa ajili ya eneo fulani basi niihuishe na eneo jingine. Hoja imesimama vizuri na wala haina mushkeli mkuu. Kwa kumalizia serikali haitakiwi kufanya biashara isipokuwa inatakiwa kutengeneza mazingira muafaka kwa akina Ruge na Kusaga waweze kuwa wabunifu, Bakhresa na Gulam Dewji waweze kutumia uzoefu wao, Profesa J, Jide na Mwana FA waweze kutumia vipaji vyao, list ni ndefu inaendelea...
 
". . . The Arusha Declaration and the actions relating to public ownership which we took last week were all concerned with ensuring that we can build Socialism in our country. The nationalization and the taking of a controlling interest in many firms were a necessary part of our determination to organize our society in such a way that our efforts benefit all our people and that there is no exploitation of one man by another.'

a) Sikubaliani na serikali kumiliki njia kuu za uchumi kwani zinamuacha mwananchi asiweze kutumia uwezo wake katika kuweza kuzimiliki njia hizo kuu za uchumi. Matokeo yake serikali ilianzisha National Poultry Co. Ltd na nyinginezo ili ifuge kuku na badala ya kuwaachia wananchi wafanye biashara hiyo kwa ushindani zaidi.

b) Ningehakikisha kuwa serikali inajitoa katika kufanya biashara moja kwa moja na kuwaacha shughuli hizo zifanywe na wananchi ili wao ndiyo wawe ni mhimili wa kweli wa uchumi wa nchi hii. Ninatambua kuwa kujituma kw mtu mmoja mmoja ndiyo ndiyo njia nzuri ya kuifanya jamii izalishe na kutumia resources zake kwa mgawanyo unaotokana juhudi za uzalishaji.

Ningehakikisha kuwa mashirika yote ambayo ni mzigo kwa walipa kodi na hayachangiii katikapato la taifa ninayauza mara moja. Na yale mashirika mengine ambayo yanajimudu basi ningehakikisha yanabinafsishwa na wananchi wenye kupenda wananunua hisa humo. Ningehakikisha yale mashirika ambayo ni nyeti kama Reli, Bandari, Posta, Ndege na mengine machache kama hayo yanabinafsishwa na serikali inabakiza hisa chache kwa ajili ya interest ya watanzania wote.
Hivi pale NAPOCO kuna shughuli gani siku hizi?
 
Sheria hutokana na sera na maazimio. Ndio maana sheria nyingi za haki za binadamu zinatokana na Azimio la Haki za Binadamu. Azimio la Arusha liliweka misingi ambayo ilipaswa kuingia kwenye sheria mfano. Sheria dhidi ya Ufisadi wa Viongozi wanaokiuka Maadili/Mwongozo, Sheria dhidi ya Umiliki wa Kifisadi wa Makampuni ya nje yanayochota madini yetu na kutuulia wananchi wetu, Sheria dhidi ya umiliki binafsi wa ardhi kubwa n.k.

Companero,
Naamini hayo yote yako covered na sheria tulizonazo. Tatizo ni Walinzi na Watekelezaji wa sheria wamegeuzwa kuwa Wanasiasa, ngonjera nyingi kulinda maslahi yao na yale ya Mabwana zao.
 
Waberoya,
The problem I have with Mwinyi is that he has not even been able to come out and defend AZ.
At least angetuambia sababu zake za kuleta AZ ningemkubali. Sasa hivi anatupa lawama kwa wengine tu yeye anapeta. To me that is not leadership. Ni ubabaishaji.

You are right Jasusi; Hakuweza kulisimamia, kushawishi na hata halijulikani, sababu za kuleta azimio la Zzanzibar amelisema na kasema kabisa hakuua AD,

Lets assume kuwa leo hii AZ lingeleta matunda mazuri kabisa (positive kwa kila mtanzania) je tungekumbuka AD?

AZ was a roadmap according o Mwinyi, but it was worng map! kwa hiyo kuna possibility ya kuwa angetokea mtu ambaye angelimodofiy Azimio na kufanya vizuri zaidi! au sio?

So failure ya Mwinyi siyo kwa sababu hakulifuata AD, ila lake la AZ lilikuwa baya!
Waberoya,

Mimi na wewe tunatofautiana kwenye msingi mmoja tu. Argument zako zimeegemea kuwa Azimio Halikuwa sheria wala Katiba. Mimi naungana na waliosema kuwa Azimio lilikuwa vision, lilikuwa roadmap. Sheria Nyingi zilitungwa ambazo hazikuwa azimio lenyewe bali kwa lengo la kufikia vision iliyomo kwenye Azimio.

Mzee Mwinyi na serikali yake hawakulipinga Azimio kama vision, ila walifanya mambo yaliyoashiria kuwa hawakubaliani na vision ile. Azimio la Zanzibar lilikuwa ni difiance against lile la Arusha na lilionesha wazi about turn kutoka mwelekeo wa kuelekea Azimio la Arusha.

Hakuna tukio jingine linaloonesha kulikataa azimio la Arusha kama azimio la Zanzibar. Mwinyi inabidi akiri kuwa leadership yake ilituondoa kwenye mwelekeo wa kuelekea AA. Alituelekeza wapi? Aseme.

Kusema kuwa hatu appreciate mazuri ya uongozi wa Mwinyi si sahihi. Tunajua kuwa mwinyi yako mambo aliyofanya kama uhuru wa kujieleza kuimalika, kuruhusu private enteprise ku flourish, n.k. Lakini Makosa yake yako wazi zaidi na sihitaji kuyarudia hapa.

Mwinyi alicho fanya ni BLAME GAME NA ESCAPISM alipokuwa akihutubia taifa kwenye ufunguzi wa benki ya Mkombozi. Ni makosa gani ambayo Mwinyi kwa maneno yake Mwenyewe ameshayakiri??

Wala hata mimi simtetei Mwinyi ila nataka kuweka uhuru wa watanzania kuwa huru zaidi katika kufikiri na kuamua mambo yetu. Kama leo hii atatokea mtu atakayeleta Azimio bora zaidi ya AD anakaribishwa , lakini tusijifunge kuwa ndiyo the only roadmap! I agree with you Mwinyi did wrong, he did that because he was free man na hatukuwa na chombo cha kumlazimisha kulifuata Azimio!, leo hii tukiweka Azimio tuhakikishe linakuwa na nguvu, ukisema kuwa Azimio lilileta sheria; je wa kusimamia sheria hii ni nani? si jukumu letu sote? na lini alibadiisha sheria? Sheria hata leo zipo na hazitekelezwi sasa swala hapa si Mwinyi tena, we have anothe problems zinazoshiria hata lingekuwepo Azimio tusingelifuata!

Ndugu Kipima Pembe utaona pia katika maelezo yangu nimetilia mkazo wa free thinking na kufanya assignment zetu na sio lazima kurudi AD, na nimesema kuwa AD kwangu mimi nalikubali, ila we need modifications! tukisema tunataka modification then hatutakuwa tofauti na Mwinyi! Mwinyi lake la AZ likuwa na makosa mengi, (japo hutayaona kwenye document); sisi ad YETU tunayoitaka itakuwa na inpu zetu , ambazo kujua kuwa tumekosea au la ni paka liwe in action

Lets think mkuu! JKN was not a roadmap, he proposed good roadmap by that time then!

Kukuweka katika mstari mzuri, je Mwinyi aliapa kulinda Katiba au Azimio????


Mzee Waberoya, heshima yako ndugu yangu. Ningependa kuchangia kidogo katika ombi lako la haya majinamizi ya WB, IMF na pengine WTO. Lakini kabla sijachangia, naomba elimu kidogo. Umeandika mahala katika mjadala huu kuwa Nyerere alikataa mawazo mazuri ya Mtei. Je ni yepi hayo? Unaweza kuniorodheshea unayoyajua na uzuri wake ni upi? Je, unatumia muzani gani kupima uzuri wa hayo mawazo. Hapa nina maana kwamba, unadhani ni mazuri kwa sababu yalitolewa na Mtei au kwa sababu yalikataliwa na Nyerere? Je inawezekana ni mazuri kwa sababu aliyatoa mahala pengine na yakakubaliwa na kuonyesha uzuri wake? Kama hivyo ndivyo, unaweza kunishirikisha mifano? Mzee nakusubiri kwa hamu kubwa. Si unajua hapa tunakuja kuchota busara na kuingia mitini!

You are questions can be asily found in the links below, read and come back for discussion: Halafu kuna mengine umenisemea hapo, source ya kusema vile ni kuwa JKN alikuwa haambiliki na nikatoa mfano tu; so whether Mtei was right or wrong was not my argument! kuna post nimetaka wataalamu watueleze issue za hawa WB na IMF ni kwa jins gani wangeiathiri AD, that shows I have no clue in this very area!

http://www.dailynews.co.tz/home/?n=4834&cat=home
 
Mkuu kusonga mbele ni muhimu sana lakini hatuwezi kusonga mbele bila kuangalia kule tulikotoka na kuyatafakari mazuri na mabaya yote tuliyoyafanya hadi kufikia hapa tulipo leo. Hili litatuwezesha kuamua ni mazuri yepi ambayo yanafaa kuendelea nayo katika safari yetu na mabaya yapi tuliyoyafanya ili tuyaepuke kabisa katika kuweza kufanikisha safari yetu, vinginevyo tutajikuta tunayarudia makosa yale yale miaka nenda miaka rudi.

This is very area ambayo wengine hawalioni lets think with free mind; makosa, matatizo , mazuri yote ya AD, tugeukie kwenye AZ, tulichambue, nalo makosa mazuri na mabaya yote

Tuchuje na kuchukua mazuri in both cases;

Then lets add our inputs maana dunia imebadilika sana, globalisation au free market pekee ni ' ni tangazo la kifo kwa viwanda vya nchi za duni ya tatu'

Climate change na uharibifu wa mazingira...

Vyama vingi......

etc


We can not think of kilimo, wakati hatuna mvui na watu wameshakata miti....! (sijui ni kutokufuata azimio au la!)

Then tupange TUTATOKAJE...

Then tuingie mitaani tusisubiri serikali, waumini wengi wa AD, wanakuwa kama wana kifafa wanalikumbuka AD linapoongelewa tukishamaliza kujadili basi! tunataka Kikwete na serikali yake waanze kuhubiri Azimio!

Tukijua hizi historia kama anvyosema BAK ndiyo mwanzo mzuri wa kujua tunaeNda wapi

Nitamshangaa mtu akitokea na akasema AD was good for 100%, na AZ was bad for 100% ! na tunapoyasema haya maazimio ndiyo tunagusa waasisi wa haya maazimio, KUSEMA mabaya ya Nyerere siyo kumchuki au kumdharau JKN, na kusema mabaya ya Mwinyi siyo kumchukia wala kumdharau

Thanks BAK
 
Ni kweli nchi inatakiwa kuongozwa kwa mujibu wa sheria na wala si maazimio.
Tukianza kuongelea maazimio kama msingi wa kuendesha tutakesha. Kuna maazimio mengi tu na hatujui kama yapo au yalikufa.
Azimio la Musoma,
Azimio la Iringa
So, why Azimio la Arusha?
rip AD!!!!

-Kuna watu wanalizungumzia AD kwa kukumbuka hotuba za Nyerere na ile misisimko

-Kuna watu wanalizungumzia AD kama waamini wa Nyerere, yaani kwa AD ni dini na Nyerere ni mtume

-Kuna watu wanalizungumzia AD kama compass/dira ya kutupeleka mahali ambapo tunaamini no bora

-Kuna watu wanalizungumzi AD kwa sababu tu ya hali halisi ya sasa na siyokwa sababu ni waamini, wanajaribu kujiuliza tumekosea wapi

-Kuna watu wanalipenda AD kwa sababu mpaka leo wanaona GAP kuwa hakuna kiongozi yeyote aliyeweza kuwa kama JKN

-Kuna watu wanazungumzia AD kwa unafiki, AD has got nothing to with them, hawakliamini, hawaliishii na hawakuliewwa , hawa wako wengi sana,


-Ninamuamini mtu aliyeona uzuri wa AD mara tu baada ya AZ kuwa in effect!

-Pengine wengine ni matatizo ya kisaikolojia kama mimi ninavyokumbuka primary school!

Nina muheshimu mtu aliyetayari kusem turudi kwenye AD baada ya kufanya marekebisho fulani, simply kwa sababu watanzania bila maazimio hatuendi! yaani bila kushawishiwa na kuhamasishwa hatuendi!

Nina muheshimu zaidi mtu yeyote anayepinga AD kwa dhana ya kuwa, aweke Azimio lake lililotofauti na Nyerere, kama mtu huru, mwenye mawazo huru, na anayeishi duniani kuleta changes! na sio kudumazwa ubongo hata kukosa kufikiria uzuri wa uwezo wetu wanadamu kuwa we can do better than JKN leo hii, ikiwa tutaamua! ila tu ahakikiseh kuwa Azimio lake linalinda mambo ya msingi wa mwanadamu, uaswa, utaifa, umoja, na responsibility(ukikosa au ukiwa kazini)

Nitampa heshima ya juu kabisa ya mtu yeyote asiyezungumzia azimio lolote lile, kwa namna yoyote ile , ila akasimamia sheria zinazopendekezwa na wanaharakati, bunge na wananchi, akasimamia katiba tuliyojiwekea wenyewe, na akawa tayari kubadilika na kuwasikilza waanchi, This is real leadership and to qualify here we don,t need maazimio!

I will adore mtu ambaye leo hii atatoka na system yake ambayo si ujamaa wala ubepari iko somewhere I don,t know where, systems mbayo we a s third world tunahitaji , systems ambayo iko radhi kutupeleka kasi kwenye maendeleo, maana UKWELI HATUSHI KWENYE KARNE YA 21 we are living in 15th century!!, hatujaweza kufikia mapiunduzi ya viwanda , wakati wakoloni walikuja kuchukua malighafi karne ya 18, leo hii 2010 ya dunia ya 1510 ya Tanzania hatujaweza kufikia level hii!

I adore Nyerere simply because ujamaa wake ulikuwa wa tofauti ali-hybrid, siasa za ujamaa za nchi nyingi na kutaka tuufuate, Huyu mzee alisoma, alifikiri, aliumiza kichwa, aliwaza, akaandika, akasema, akatekeleza, simply because he was a real man who created to do something extraordinary!

sisi wengine we are lazy, hatusomi, hatufikiri, hatuwazi, wanafiki, wabinafsi, na hatujaumiza bongo zetu kufikiri kuweka system imara zaidi kwa taifa letu na KWA SABABU HIYO TUMESHINDWA KUWA kama Nyerere, we are simply falling back to Nyerere...wapi professors wa sociology leo hii, wapi professsors wa uchumi, wapi ..., wapi.. Nyerere he did that just with masters degree.... na ndiyo maana nikasema mnaotaka kumkumbuka huyu mzee , fanyeni something extraordinary ambayo mtaweza kwa sababu ya kuchukua Idea zake.

Kushinda kwenye matamasha ya kumkumbuka Nyerere ni sawa na kushinda kanisani kumuabudu Nyerere! na kujidhalilisha, you can only do better kwa kufanya something better, na ndio hao mkisema baya la Nyerere anaweza kukupiga ngumi, Nyerere haenziwi kwa maneno! watu wakikosea hapa itakuwa dini hii!

Leo akina David Ricardo, Hegel, Adam Smith tunawakumbuka kupitia Karl Marx,, karl max alizichukua idea zao, leo hii Karl max amezaa watoto wengi wa fikara zake!

In science, akina Newton walisimama kwa giants wengi sana wa sayansi kabla yake!

Leo hii we need Tanzanian who will take JKN idea and move foward sio kulilia kurudi nyuma, tutafute hawa walikosea wapi na tuchuke mazuri tusonge mbele! However, still anaweza akatokea mtu akafuta kila kitu cha JKN na kuweka kitu bora kabisa kwa mawazo yake , we are welcoming those. Lakini mtu asiseme hapa failure ya Mwinyi ni simply kutofuata AD!! hakuwa robot Mwinyi! kama mnataka fair judgement, mwekeni kando kama Mwinyi, chukunei AZ yake ahukumiwe kwa hiyo, still AD had many negative things!
 
OK, tupunguze urefu wa mjadala. Ni kweli kabisa tunahitaji kiongozi anayesimama na kufanya mambo anayoyaamini. Ayasimamie kama yeye na yakishindwa au kuleta matokeo mabaya awe tayari kusimama na kusema alikosea hapa. Kwa hili Mwinyi simply didn't do it, he did the opposite, simply blaming the Mchwas. AA lilishakufa na ni kweli halipo tena. Na Mwinyi alishiriki kuliua, ingawa anasema hakuliua.

Tunamjadili Mwinyi kwa kauli aliyoongea, si kwa vile tunavyofikiria. Vile vile siasa ya Ujamaa na kujitegemea haipo tena. CCM na uongozi uliofuata baada ya Mwalimu wameshindwa kuja mbele na kusema wanatuongoza kutuelekeza wapi! Ukweli ni kwamba wanatuongoza na wapo madarakani. Wanachokifanya kinatuathiri wewe na mimi na ni wajibu wetu kuwahoji, ikiwa misingi tuliyoielewa wameifuta; basi wasimame wakiri kuwa wameifuta ili tuwaulize baada ya kuifuta wameweka nini mahali pake?

Hakuna anayelazimisha tufuate ujamaa. Tumeshasema mara nyingi kuwa kinachofanyika sasa si ubepari vile vile kwani kwa wale wanaoelewa ubepari halisi (si ule wa chuki tulizopandikizwa huko nyuma) wanaelewa vile vile kuwa kinachoendelea sasa si ubepari. Tunataka viongozi waliopo madarakani wasimame mbele waseme wanatuongoza vipi ili watakapomaliza muda wao tuwahukumu kwa kile walichofanya. Siyo viongozi wakae madarakani halafu baada ya miaka kumi waje hapa na kusema hatukufanya chochote kwa sababu tulikuta nchi imeharibika.

Waberoya umesema mambo ambayo unafikiri yakifanyika itakuwa bora. Ni sawa. Lakini tusiishie hapo. Twende mbali tuwaulize hawa waliopo madarakani wanatuongozaje? Ni lazima watuambie, tena watuambie sasa! Hatutaki haya ya kuzuka "from no where" na kurushia madongo kwa wengine kwa yale ambayo wao walitakiwa wayafanye.

Viongozi wanabeba dhamana ya kile kinachotokea. Mafanikio yakipatikana viongozi ni wepesi kuchukua "credit". Lakini vile vile viongozi wawe tayari kuchukua lawama kwa failure. Kama taifa tupo wote tunashiriki katika uongozi wa nchi hii kwa hili na lile tunalolifanya katika maeneo yetu. Lakini vile vile tukubaliane kuwa kila mmoja ana majukumu tofauti na wengine. Jukumu la Rais ni tofauti na jukumu la Mwalimu, Mhandisi au daktari. Rais akishindwa tuseme rais ameshindwa siyo tuseme wameshindwa wahasibu, wahandisi, madaktari, n.k. waliokuwa chini yake, kwamba wameshindwa wote; si sahihi. Kazi ya kiongozi ni kutoa leadership matokeo ya kushindwa kwa leadership ni kutofanikiwa kwani siku zote binadamu tunafanya kazi kama team. Viongozi huipa jamii mwelekeo au huisambaratisha kwani wamekabidhiwa jukumu kubwa zaidi. Wakishindwa tuwaseme wameshindwa, ili wanaokuja waangalie pale. Haisaidii kuzua "utopia" ya kile tunachokitaka wakati tukikwepa hali halisi.

Napenda nifunge hoja zangu kwa hapa.
 
It is true that Mzee Mwinyi did not kill Arusha Declaration rather he abandoned every principle stated on Arusha Declaration!
 
You are questions can be asily found in the links below, read and come back for discussion: Halafu kuna mengine umenisemea hapo, source ya kusema vile ni kuwa JKN alikuwa haambiliki na nikatoa mfano tu; so whether Mtei was right or wrong was not my argument! kuna post nimetaka wataalamu watueleze issue za hawa WB na IMF ni kwa jins gani wangeiathiri AD, that shows I have no clue in this very area! http://www.dailynews.co.tz/home/?n=4834&cat=home

Mkuu Waberoya, heshima yako mkuu. Samahani kama sikueleweka, kwani najua maana iko kwa msomaji na siyo mwandishi. Sikukusudia kukuweka maneno mdomoni, ila nilitaka kudadisi kwa kutumia maswali. Hakika nilitaka kujua ulichoandika kuwa hayo mawazo mazuri ya Mtei yaliyokataliwa na Nyerere ni yepi na uzuri wake ni upi?

Link uliyonipa kwamba kuna majibu ya maswali yangu sikuyakuta. Nimekuta vitu viwili.

Mosi, nanukuu "Another issue that makes him happy at the moment he says, is the IMF's recent decisions which he used to push foward but were ignored when he was working at the Breton Wood institute. One of the things he proposed in the early 80's was that since poor nations paid their fees to IMF in gold, and the gold over time appreciated, the fund was supposed to give back some of the profits obtained from sell of gold to poor nations."

Hili wazo halihusiani na Nyerere. Mtei alipojiuzuru, aliajiriwa na IMF. Hapa anaongelea ushauri mzuri alioutoa kwa IMF ili kuziinua nchi masikini duniani kutokana na rasilimali za nchi hizo, lakini IMF wakaukataa. Ningeshangaa kama wangekubali kwa sababu IMF, WB na WTO hazikuundwa kuziinua nchi masikini. Katika hali ya anguko la uchumi wa dunia, ambapo dola imeshuka thamani na dhahabu imepanda thamani maradufu kwa kipindi kifupi, na baadhi ya nchi masikini zinatoa dhahabu kwa wingi, ningeshangaa kama IMF wasingekimbilia kuyatekeleza hayo mawazo kwa sababu hayazinufaishi nchi masikini. Hili nitalijadili katika kipengele tofauti kwa sababu halihusiani na maswali yangu. Hii ni Mtei na IMF siyo Mtei na Nyerere ambalo ni swali langu.

Pili, katika link uliyonipa nimekuta wazo jingine ambalo pia halijibu swali langu. Nanukuu "He says one of his 'friction' with Nyerere was that when the Ujamaa policy vividly failed in the late 70's he wanted to apply IMF's measures to rescue the situation. At independence we were neck in neck against Kenya and Uganda but we failed because we took too long to take actions after the fall of Ujamaa," he explained." Hapa hakuna mahala wanataja mawazo ya Mtei ni yepi na uzuri wake ni upi?

Katika link hiyo wanaongelea kitabu alichokiandika Mtei cha "From Goathed to Governor" kilichochapishwa mwaka jana - 2009 ambacho nimekisoma. Unless mtu anayaweka mawazo ya Mtei yaliyokataliwa na Nyerere katika maandishi, mimi nitaendelea kumuamini Mtei mwenyewe ambaye ameuweka ukweli huu katika kitabu chake. Katika kitabu chake, kuanzia ukurasa wa 146 mpaka 157, Mtei anaeleza kwa kinagaubaga Nyerere aliyakataa mawazo ya Bo Karlstrom kutoka IMF. Haya hayakuwa mawazo ya Mtei.

Anaeleza kuwa mara tu baada ya vita ya Kagera 1979, uchumi ulilegalega na ulihitaji dola milioni 375 ili kuukarabati. Anasema yeye kama Waziri wa Fedha alipewa jukumu la kuhusisha jopo la weledi ili kuukwamua uchumi dhidi ya madhara ya vita ya Kagera.

Na hili ni jambo la kawaida popote duniani. Mfano, 2008 Marekani ilikumbwa na anguko la uchumi kutokana na mchanganyiko wa sababu, mojawapo zikiwa ni madhara ya vita dhidi ya Iraq, mtikisiko wa soko la nyumba, kupanda kwa bei ya mafuta n.k. Hiyo ilisababisha baadhi ya viwanda na mabenki makubwa kufilisika na vingine kulegalega. Marais Bush na Obama, mara zote waliwataka Mawaziri wao wa Fedha kukaa na majopo ya weledi ili kubuni mbinu za kujikwamua.

Majopo yao ya weledi yaliamua kuwa baadhi ya benki (hata viwanda) ni kubwa kiasi kwamba hawawezi kuziachia kufa, na wala kuzimega katika vibaba. Walizigomboa kwa mitaji mikubwa ya kodi za wananchi, ambapo serikali inamiliki asilimia kubwa ya hisa mpaka hapo dhoruba litakapo pita na zikaanza kupata faida. IMF, WB na WTO hawaruhusiwi kunusa pua katika majopo ya Marekani ya kufufua uchumi.

Sasa turudi katika kitabu cha Mtei. Katika ukurasa wa 149, yeye aliamua kuwaalika weledi wa IMF wakiongozwa na Bo Karlstrom ili washirikiane na weledi wa Wizara ya Fedha kubuni program ya kufufua uchumi. Anasema katika jopo lao, IMF walikuwa tayari kutoa mkopo wa kufufua uchumi lakini kwa masharti matatu. Mtei ameyaorodhesha hayo masharti kuwa ni; Mosi, kushusha thamani ya shilingi, pili, kuleta wawekezaji kutoka nje ya nchi, na tatu, serikali iache kusaidia kifedha mashirika ya umma na viwanda, na badala yake iyabinafsishe. Anatoa mfano wa benki ya taifa ya biashara NBC, kuwa ilikuwa ni kubwa mno iliyotishia usalama wake yenyewe.

Mtei alirudi kumueleza Bo Karlstrom kuwa Nyerere ameyakataa masharti. Bo Karlstrom akamwambia Mtei kuwa ebu niwezeshe nionane naye hana kwa hana nitamlainisha na atayakubali. Tarehe 29 November 1979 alimkutanisha na Nyerere Msasani. Baada ya maongezi, Nyerere alimwambia Mtei kuwa awaambie warudi zao Washington kwani yeye hawezi kuruhusu nchi yake iendeshwe kwa amri kutoka Washington (Washington consensus). Kuwa Nyerere alimwambia "I will devalue the Shilling over my dead body". Na hiki ndicho kisa kilichopelekea Mtei Kujiuzulu/kuachishwa kazi.

Kwa maoni yangu, kikatiba, Rais anapomuomba Waziri mawazo katika suala muhimu, na Waziri akampeleka mtu mwingine na kumwambia Rais kuwa "msikilize huyu ndiye mwenye mawazo mazuri", haimaanishi kwamba yale ni mawazo ya Waziri. Ila inamaanisha kuwa Waziri alikuwa na mawazo yake na akayaona siyo mazuri kama ya mwenzake. Au inawezekana Waziri hakuwa na mawazo kabisa ndiyo maana akayaona ya yule mtu ni bora. Sijuhi katika issue ya Mtei ni lipi linaegemea kwake, ila katika kitabu chake, hakutaka ile ya "copy and paste" yaani kuyafanya mawazo ya IMF ni yake. Kama ambavyo hukujibu maswali yangu, na link uliyonipa haina majibu, basi nitaendelea kuamini maandishi ya Mtei mpaka hapo atakapojitokeza mdau wa kunielemisha kuhusu mawazo ya Mtei ni yapi na uzuri wake ni upi?
 
Back
Top Bottom