Siku za Paul Makonda kama RC wa Dar es salaam zinahesabika

TL. Marandu

JF-Expert Member
Jul 12, 2015
3,625
5,810
Kabla Sijasema Nalotaka Kusema, Niseme swala dogo la Kihistoria, Natolea Mfano wa Utawala wa Uganda, Hii Ni orodha ya Marais wa Uganda, Kabla, Mara tu na Baada ya Vita vya Uganda na Tanzania.

1) Fredrick Edward Kabaka Mutessa II 1963-66
2) Dr. Milton Obote 1966-1971

3) Idi Amin Dada 1971-1979
4) Prof. Yusufu Kironde Lule 13 April 79 to 20 May 1979
5) Geodfrey Lukongwa Binaisa 1979 mpaka 1980
6) Paul Muwanga* one month May 1980

7) Dr. Milton Obote 1980-1985
8) Bazilio Okello* 2 Days July 1985
9) Maj. Tito Okelo 1985-1986

10) Yoweri Kaguta Museveni 1986 Mpaka Leo.

Orodha hii nimeiweka Kwa ajili ya Wanaopenda Historia lakini zaidi Lengo Langu Ni Kumzungumzia Mmoja Tu, Namba 4 au Prof. Yusufu Kironde Lule, Baada ya Kumalizika Vita, Kwa influence ya Mwalimu Lule alikabidhiwa Uongozi wa Uganda ili kuijenga Upya Nchi Lakini Kwa Muda Mfupi akaongoza Kwa Vituko na akasababisha Malalamiko, Kiasi cha Mwalimu Nyerere Kusema, "Lule mpumbavu, tulimpa ubatizo akashidwa Kipaimara" Mwisho wa Kunukuu.

Sasa Naona Wazi Kuwa Maneno haya Muda sio Mrefu sana yatamfaa Makonda ambaye Kama Baradhuli alidhani anaurefu wa maili 12 elfu, akazika Kichwa chake juu, juu kabisa mawinguni, huku akaanza kasi ya kufukuza Kivuli chake wala asione aendako, loo Ukingo wa bahari!

images
 
Kufanya kazi kwa kiherehere bila kufuata JD, na hata bila kutaka kuongeza maarifa ya kazi, na kukurupuka vitamjutisha!. Angelikuwa mtu mwenye akili za kazi, angesoma JD yake kwa makini, akatafuta tafsiri kama kuna sehemu haelewi, aangalie sheria zinasemajie, ajipime yeye mwenyewe mapungufu na uwezo wake uko wapi (Self SWOT analysis), kisha aanza kazi kwa utaalamu huku akiongezea elimu pale anaona maarifa yamepungua. Kukurupuka kwakila kitu bila weledi, hakuwezi kufanikisha kila kitu. Alifanikisha tu hujuma za mijadala ya katiba na kumpiga Mzee Warioba, akadhani umafia unafanya kazi kila sehemu. Ajifunze yeye n awatu wa aina yake. Mtu ni utu.

Kabla Sijasema Nalotaka Kusema, Niseme swala dogo la Kihistoria, Natolea Mfano wa Utawala wa Uganda, Hii Ni orodha ya Marais wa Uganda, Kabla, Mara tu na Baada ya Vita vya Uganda na Tanzania.

1) Fredrick Edward Kabaka Mutessa II 1963-66
2) Dr. Milton Obote 1966-1971

3) Idi Amin Dada 1971-1978
4) Prof. Yusufu Kironde Lule 13 April 79 to 20 May 1979
5) Geodfrey Lukongwa Binaisa 1979 mpaka 1980
6) Paul Muwanga* one month May 1980

7) Dr. Milton Obote 1980-1985
8) Bazilio Okello* 2 Days July 1985
9) Maj. Tito Okelo 1985-1986

10) Yoweri Kaguta Museveni 1986 Mpaka Leo.

Orodha hii nimeiweka Kwa ajili ya Wanaopenda Historia lakini zaidi Lengo Langu Ni Kumzungumzia Mmoja Tu, Namba 4 au Prof. Yusufu Kironde Lule, Baada ya Kumalizika Vita, Kwa influence ya Mwalimu Lule alikabidhiwa Uongozi wa Uganda ili kuijenga Upya Nchi Lakini Kwa Muda Mfupi akaongoza Kwa Vituko na akasababisha Malalamiko, Kiasi cha Mwalimu Nyerere Kusema, "Lule ********, tulimpa ubatizo akashidwa Kipaimara" Mwisho wa Kunukuu.

Sasa Naona Wazi Kuwa Maneno haya Muda sio Mrefu sana yatamfaa Makonda ambaye Kama Baradhuli alidhani anaurefu wa maili 12 elfu, akazika Kichwa chake juu, juu kabisa mawinguni, huku akaanza kasi ya kufukuza Kivuli chake wala asione aendako, loo Ukingo wa bahari!
 
Kabla Sijasema Nalotaka Kusema, Niseme swala dogo la Kihistoria, Natolea Mfano wa Utawala wa Uganda, Hii Ni orodha ya Marais wa Uganda, Kabla, Mara tu na Baada ya Vita vya Uganda na Tanzania.

1) Fredrick Edward Kabaka Mutessa II 1963-66
2) Dr. Milton Obote 1966-1971

3) Idi Amin Dada 1971-1979
4) Prof. Yusufu Kironde Lule 13 April 79 to 20 May 1979
5) Geodfrey Lukongwa Binaisa 1979 mpaka 1980
6) Paul Muwanga* one month May 1980

7) Dr. Milton Obote 1980-1985
8) Bazilio Okello* 2 Days July 1985
9) Maj. Tito Okelo 1985-1986

10) Yoweri Kaguta Museveni 1986 Mpaka Leo.

Orodha hii nimeiweka Kwa ajili ya Wanaopenda Historia lakini zaidi Lengo Langu Ni Kumzungumzia Mmoja Tu, Namba 4 au Prof. Yusufu Kironde Lule, Baada ya Kumalizika Vita, Kwa influence ya Mwalimu Lule alikabidhiwa Uongozi wa Uganda ili kuijenga Upya Nchi Lakini Kwa Muda Mfupi akaongoza Kwa Vituko na akasababisha Malalamiko, Kiasi cha Mwalimu Nyerere Kusema, "Lule ********, tulimpa ubatizo akashidwa Kipaimara" Mwisho wa Kunukuu.

Sasa Naona Wazi Kuwa Maneno haya Muda sio Mrefu sana yatamfaa Makonda ambaye Kama Baradhuli alidhani anaurefu wa maili 12 elfu, akazika Kichwa chake juu, juu kabisa mawinguni, huku akaanza kasi ya kufukuza Kivuli chake wala asione aendako, loo Ukingo wa bahari!
Anajiona yeye ndiye mteule wa ikulu,hakuna mwingine na sifa zina mlevya
 
Utasikia sik moja JPM anawauliza wananchi
"Nimtumbue nisimtumbue?"
Wananchi "Tumbuaaaaaaa!"
Msee Kalala Mbere na Mh Kitwanga (Rafiki yake) akampa Manakoz, Akampa Katibu Mkuu Kiongozi HE Sefue Manakoz akampa Bi Anne Malechela Manakoz, Wote watu wazito, Nini Kinawafanya watu wadhani atafikiri Mara Mbili Kumtembezea Makonda Manakoz!
 
Nimekuwa najiuliza mara kwa mara, hivi Mh. Rais haoni kwamba Makonda hana sifa za uongozi? Alipomteua kuwa RC nilikiwa na maahaka sana na kama angeweza kusimamia jiji la Dar, sass imedhihirika huyu kijana hata ile nafasi ya UDC labda Mh Meck Sadiki alikuwa anamsaidia sana.

Makonda hana hata sifa za kuwa mtendaji wa Kata. Ni wakati sasa Mh Rais aangakie upya uteuzi wa huyu RC maana anamharibia.
 
Tatizo aliye juu yake wanatofautiana kiweled?? Mm naona kopo na mfuniko sidhan kama hilo litatokea. Ukiangalia kwa umakini unaweza dhan ni mtu na baba yake.maamuz ya bira kutafakar wote sawa sawa. Mm namhesabu kama ndiye anayemfurahisha mkuu kuliko wote! Mkuu anapenda sifa huku huyu anafanya kaz kwa sifa japo anakosea 90%. Haya nasubir!!
 
Makonda badala ya kushirikiana na viongozi tuliowachagua wananchi kama wabunge na madiwani yeye anajenga uadui nao, sasa viongozi wa kisiasa wasipomuunga mkono ataweza kuongoza na kuleta maendeleo kweli, hajui hata maana ya total management, corporate management, team work etc
 
Makonda hana uwezo wa kiakili au kihekima kuwa kiongozi na bado utoto umejaa kichwani, kupenda kujipendekeza na sifa tuu.
Mkoa wa Dar kumuweka mtu wa aina hiyo ni kuyatafuta matatizo tuu.
Kitendo cha kutoa kauli za kuwadharau mameya wa jiji kuwa hawana kazi atakijutia yeye na chama chake siku zijazo kwani hao ndio wawakilishi wa wananchi
 
Kwani makonda huyu si ndio yule aliye nusulika kupewa kibano na madereva pale ubungo terminal akaokolewa na askari tena kwa kujificha miguuni mwa hao askari?au ni yupi huyo?
 
Makonda ajitathmini upya kwa mambo anayotamka.alianza na walimu kupanda daladala bule amefeli,kupaka rangi nyumba zote za Dar kafeli,kuondoa gerej mitaani kafeli,kuondoa maduka ya kuuza magar mitaani kafeli,kuondoa mashoga jijin Dar ameshfeli,sasa anakuja na wazo jingine la kufikirika;kukamata wasio na kaz mitaani,baada ya kuwakamata atawapa kaz ya kufanya??
Nasubiri mengi yatakuja katika nchi ya wafikirika....
 
Back
Top Bottom