Siku za Paul Makonda kama RC wa Dar es salaam zinahesabika

Kama serikali yenyewe ilishasema kuwa wafanyakazi wake ni laki 4 tu,(kikwete akimjibu mgaya wa tucta kabla ya kampeni zake awamu ya pili).
Makonda ajiulize hiyo ni asilimia ngapi katika watu milioni 45 ya sensa ya mwisho?
Kwa hesabu rahisi ni asilimia 1 tu ndiyo wana ajira,na Dar ina watu zaidi ya milioni 4 karibu asilimia 10 ya watanzania wote wanaishi Dar.
Akishawajua wasioajiriwa na viwanda bado,atawapeleka wapi?na kutokuwa na ajira na ukosefu wa viwanda,nani anastahili lawama?
 
Sio kosa lake ni ulimbuken wa uongozi.. Uongozi una historia kutoka chini. Utasema yeye ndio Rais wa Tz. Lakin wahenga wanena. Ngoma ikilia sana mwishoe......???
 
Makonda watingishe tu, wavivu wamejaa wengiiiiii mji huu. Kutwa kulalamika huku wamekaa na kulala na kuibia watu
 
mhhhh naona anafuata falsafa ya bosi wake kwamba "UKIONA WANAKUCHUKIA UJUE UPO SAWA, NA UKIONA WANAKUSIFU JIJUE HAUPO SAWA"

Shkamoo falsafa za Mwendokasi !
 
1. Kila nyumba ipakwe rangi.
2. Omba omba wote marufuku jijini.
3. Kila nyumba iwekwe taa mbele na nyuma
4.kila mwenye silaha aisajili
5. Gereji bubu zote kiama kimefika
6. Hotel zitakuwa na mtaa wake, club zote mtaa mmoja, gereji mtaa mmoja nk.
7. Walimu kupanda mabasi bureeee.
8. Makonda ajitathmini
9. Kuondoa mashoga wote jijini..
10. Na sasa ni kukamata jobless..

Mm namuunga mkono koz kila kitu huletwa na uthubutu...lakini namshauri afanye analysisi yote alioyaplan lipi walau moja alofanikisha kwa asilimia 50....otherwise wakishamzoea kuwani mtu wa matamko atakuwa ameisha kabisaa koz hakuna jambo atakalokuja kuagiza likachukuliwa serious.....watu watasema aaaah huyo ndio zake achana nae.
 
Nimekuwa najiuliza mara kwa mara, hivi Mh. Rais haoni kwamba Makonda hana sifa za uongozi? Alipomteua kuwa RC nilikiwa na maahaka sana na kama angeweza kusimamia jiji la Dar, sass imedhihirika huyu kijana hata ile nafasi ya UDC labda Mh Meck Sadiki alikuwa anamsaidia sana.
Makonda hana hata sifa za kuwa mtendaji wa Kata. Ni wakati sasa Mh Rais aangakie upya uteuzi wa huyu RC maana anamharibia.
correction Makonda ana sifa ya uongozi na hilo aliliprove alivokuwa kinondoni,tatizo linakuja jiji linamzidi uwezo wake wakiuongozi........na jiji kuwa chini ya upinzani ni jambo linalomsumbua kiasi kwamba anapigana sana kushindana na upinzani katika utendaji badala ya kujenga uhusiano mzuri kupeleka jiji mbele....
 
nimeangalia kila post inamkashifu tu. hivi niulize ni kitu gani alichokifanya makonda kinachowaudhi hivo? siyo kukurupuka tu, kama kuna baya lolote la kufaa hizo kashifa tulione.
 
Wasiompenda Makonda ni Mafisadi chadema tu.



Lkn Wenye akili tuko na makonda na tumeyaona mabadiliko dar
 
Makonda watingishe tu, wavivu wamejaa wengiiiiii mji huu. Kutwa kulalamika huku wamekaa na kulala na kuibia watu
Makonda akomae tu.Awakamate ma-jobless wote awarudishe kijijini.Tuna hitaji nguvu lazi kubwa katika kilimo pale bush.#Hapa kaz tu
 
Loading ngoja jpm anamuangalia tu vituko vyake
Ameshamuona anatafuta sababu ya kumtumbua tu
Kufanya kazi kwa kiherehere bila kufuata JD, na hata bila kutaka kuongeza maarifa ya kazi, na kukurupuka vitamjutisha!. Angelikuwa mtu mwenye akili za kazi, angesoma JD yake kwa makini, akatafuta tafsiri kama kuna sehemu haelewi, aangalie sheria zinasemajie, ajipime yeye mwenyewe mapungufu na uwezo wake uko wapi (Self SWOT analysis), kisha aanza kazi kwa utaalamu huku akiongezea elimu pale anaona maarifa yamepungua. Kukurupuka kwakila kitu bila weledi, hakuwezi kufanikisha kila kitu. Alifanikisha tu hujuma za mijadala ya katiba na kumpiga Mzee Warioba, akadhani umafia unafanya kazi kila sehemu. Ajifunze yeye n awatu wa aina yake. Mtu ni utu.
 
Tulisema toka alipopewa u DC Makonda hafai hata u katibu kata lakini ndio kwanza akazidi kupaa, nafikiri makonda hana tatizo bali ni jamaa aliyempigia debe kumweka pale kishikaji
 
mimi naendelea kuusoma mchezo.nikimaliza ntarudi niwajuze baazi ya mambo
 
Siku zote ukifanya kazi kwa mihemuko ya kutaka kusifiwa matokeo yake ndio hivyo kutoa matamko yasiyokuwa na utafiti. Hovyo kabisa Magufuli tumbua huyu mtu haraka iwezekanavyo sifa zimemlevya.
 
Makonda watingishe tu, wavivu wamejaa wengiiiiii mji huu. Kutwa kulalamika huku wamekaa na kulala na kuibia watu
Kama hujui hao unaowaona ni wafanya biashara wakubwa ndio wapanga mipango ya wizi. Hao Vijana vibaka wadogo huwezi kuwamaliza kwa sasa hata ufanyeje
 
Kama hujui hao unaowaona ni wafanya biashara wakubwa ndio wapanga mipango ya wizi. Hao Vijana vibaka wadogo huwezi kuwamaliza kwa sasa hata ufanyeje
Ucha uvivu wa kufikiria mkuu, yani kitu brainstorming kwa wabongo ni msala?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom