Siku ya Wanawake imeondoka na bibi yangu(RIP bibi yangu)

Siku ya Wanawake imeondoka na bibi yangu(RIP bibi yangu)

Dejane

JF-Expert Member
Joined
Jan 1, 2014
Posts
51,088
Reaction score
72,505
Leo watu wakisherehekea siku ya wanawake, napigiwa simu na mama yangu analia mama yake amefariki muda si mrefu, ntamkumbuka Kwa mambo mengi, vituko na wajukuu wake.

Alikuwa akisumbuliwa na uvimbe ndani ya kibofu cha mkojo, tulimpeleka hospitali lakini akakataa kufanyiwa upasuaji, pia presha ilipanda Kwa hiyo ikashindikana na kakataa kabisa akasema arudishwe nyumbani, ameugua kama mwaka hivi na ndipo leo kaaga dunia.

Nahisi sitaisahau hii siku ya leo na tarehe yake nitakumiss bibi yangu Mwanaloshinge upumzike Kwa amani nasi tupo njiani twaja siku yoyote.
RIP BIBI
 
Pole sana mamy
Naweza kuwa nimeelewa sababu za yeye kukataa kufaninyiwa op.
Alale kwa amani
 
Mwanaloshinge Pumzika Kazi Uliyotumwa Hapa Duniani Nina Imani Umeitimiza Rudisha Namba Nasi Tuko Nyuma Yako Vipi Mkuu Msiba Uko Wapi?
 
pole sana kwa msiba best yangu mie
Mungu awatie nguvu kwa kipindi hiki kigumu kwako na kwa familia
RIP bibi yetu
 
Back
Top Bottom